Tuesday, February 19, 2013

Wanaoshikiliwa na nguvu za kaburi wataachiliwa By Rev Florian Katunzi

Rev Florian J Katunzi
KARIBU katika makala haya yanayoandaliwa na Mchungaji Florian J. Katunzi, wa Kanisa la EAGT City Centre,lenye makao yake viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam. Somo la wiki hii ni Maombi ndani mwa Maombi, katika kipengele kinachosema…“Wanaoshikiliwa na nguvu za kaburi wataachiliwa.”
Endelea….


Maombi yetu sasa, yanalenga kuwakomboa wale waliokamatwa na nguvu ya kaburi na mauti waachwe huru toka makaburini, tunakusudia kuwarejesha katika hali zao za kawaida kwa jina la Yesu. Yote haya yatawezekana kwa njia ya maombi.


Yesu Kristo alipokwisha kupaza sauti yake, alipokwisha kuomba kwa nguvu, maombi yake yalitetemesha falme na mamlaka za mauti na kaburi, Pazia la hekalu lilipasuka, nchi ilitetemeka miamba ilipasuka makaburi yakafunuka ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala. (Mathayo 27:50-53).Hata sasa maombi yetu tuliompokea Kristo kuwa BWANA na Mwokozi wa maisha yetu, tukaamua kutembea katika njia zake, yatafunua makaburi na waliofungwa humo wataachiliwa huru.
Makaburi yaliyofunga biashara yako yatafunuka na biashara yako inayokufa itafufuka, ndani mwa maombi katika jina la Yesu aliye hai.


Kaburi walimozika ndoa yako, walimokufunga ili usiolewe,lazima lifunuke na nafsi yako itoke humo na utakwenda kuolewa sasa.
Kaburi lililozika afya yako litafunuka leo na afya yakitarejeshwa upya, ndani mwa maombi.
Katika Biblia kitabu cha Yeremia 30:17 BWANA anasema: “Maana nitakurudishia afya nami nitakuponya jeraha zako asema BWANA…”
Kaburi lillilomeza mali zako ili usistawi litafunuka sasa na mali zako zitainuka tena, kazi yako itainuka tena.
Katika kitabu cha Ayubu 20:15, andiko linatuambia:  “Amemeza mali naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake.”
Kaburi la uchawi na hirizi walimozika nafsi yako,walimozika, watoto wako, litafunuka sasa na kuwatoa watoto wako; litakutoa nafsi yako iliyokamatwa na nguvu ya kuzimu.
Nakwambia hivyo kwa uhakika kwa kuwa BWANA anasema:“Tazama, mimi ni kinyume cha HIRIZI zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa
katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege. Na leso zenu nazo nitazirarua na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa
katika mkono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.” (Ezekiel 13:20-21).
Watu wengi wamefungwa kimaagano ya kimadhabahu kupitia hirizi, kwa maana hirizi ni kitu chochote ambacho mwanadamu anaweza kukitumia kuwa kinga yake badala ya Mungu
aliye hai.
Wakristo wengi kwa kupuuza maombi, wamejikuta wanategemea vitu viitwavyo vya upako, badala ya uweza wa kimungu kwa jinsi ya Roho maana Mungu ni Roho.
Kuacha kuomba na kutegemea kitu badala ya Mungu ni hirizi tu mbele za Muumba. Kumbuka Mungu ni Roho, si kitu cha kushikika.
Maandiko yafuatayo yanadhihirisha kuwa Mungu wetu si vitu vya kushikika: “Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa  Mungu,haitupasi kudhani ya kuwa uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi wa akili za wanadamu.” (Mdo. 17:29)
Tukisoma maandiko matakatifu katika kitabu cha Ezekiel sura ya 13, tunaona jinsi vitu vilivyotengezwa kwa mikono ya wanadamu kama leso, vilitumika kunasa nafsi za watu.
Kanisa la Kristo Yesu tumeachiwa maombi:
    • Sio mafuta ya upako
    • Sio chumvi za upako
    • Sio vitambaa (leso) za upako
    • Sio sabuni za upako
    • Sio maji ya upako.
Maombi Luka 22:39-46; imani sasa inapepetwa, Wakristo wengi wanajiunganisha na miungu ya wanadamu kupitia vitu hivi,matokeo yake nafsi zao zimo kaburini. Nguvu ya mkristo haitokani na kupakwa kitu, bali kwa kujazwa nguvu ya Roho Mtakatifu ndani mwa maombi Yesu Kristo anasema.“Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na katika Uyahudi wote na Samaria na hata mwisho wa nchi. (Mdo 1:8).
Angalia Yesu Kristo mwenyewe alijazwa nguvu ya Roho Mtakatifu ndani mwa maombi, sio kwa kupakwa;
 • Mafuta ya mzeituni
 • Chumvi ya upako
 • Sabuni ya upako
 • Maji ya upako
 • Kupewa leso ya upako
Katika Luka 3:21-22, Neno linasema: “Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni,wewe ndiwe mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.”
Maisha ya Yesu Kristo yalijaa maombi, yalijengwa ndani mwa maombi, sio nje. “Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani, ili kuomba; akakesha usiku kucha katika
kumwomba Mungu. (Luka 6:12).
Na uweza wa kimungu ulikuwa ukimtoka na kuponya watu na wale waliosumbuliwa na pepo wachafu waliponywa.Makaburi ya nguvu za giza yaliachia watu kwa uweza wa nguvu zake, (Mungu aliye hai). Na uweza huu unapatikana ndani mwa maombi.
“Lakini yeye alikuwa akijiengua; akaenda mahali pasipo kuwa na watu, akaomba.” (Luka 5:16).
Kanisa; fungu letu ni maombi, pasipo kukoma, maombi yakikoma yatazidisha kushindwa vita vya kiroho.(Kutoka 17:8-16). Nguvu ya kaburi itakomeshwa na miili ya watakatifu watainuka
tena. Kazi zao za mikono zilizoezekwa kwa kupitia nyota zao zitafufuka na kuinuka tena.
  • Wamezika maisha yako
• Wamezika ndoa yako
• Wamezika watoto wako
• Wamezika mafanikio yako,
• Wamezika utajiri wako,
• Wamezika mikono yako,
• Wamezika jina lako.
 BWANA anasema: “Tazama nitafunua makaburi yenu; na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu enyi watu wangu…
Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA,nitakapoyafunua makaburi yenu na kuwatoa ninyi, enyi watu wangu. Nami nitatia roho yangu ndani yenu; nanyi mtaishi name nitawawekeni katika nchi yenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi BWANA nimesema hayo na kuyatimiza, asema BWANA.”
Makaburi lazima yafunuke kwa jina la Yesu Kristo, yatoe kila kilichozikwa cha maisha yako upate kustawishwa.Kaburi la magonjwa likutoe na upate uzima tena.
Kaburi la dhambi likuachie ufunuke utoke huko uokoke.
• Kaburi la ulevi
• Kaburi la zinaa
• Kaburi la wizi
• Kaburi la usengenyaji
• Kaburi la utapeli
• Kaburi la ushoga
• Kaburi la usagaji
Baa ni kaburi la walevi toka huko uokoke Yeremia 31: 9 “Watakuja kwa kulia, na kwa maombi; nitawaongoza nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia iliyonyooka katika njia hiyo hawatajikwaa…”Pia katika Ezra 8:21-23 Neno linasema:“Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka;
• Kwa ajili yetu sisi na
• Kwa ajili ya watoto wetu
• Kwa ajili ya mali zetu……….”Lazima tuinue kazi zetu za mikono mbele za BWANA; kwa
maombi, achana na imani tegemezi mwendee Yesu Kristo aliye jiwe kuu la pembeni sio mawe ya upako tena.“Na itakuwa kwamba mtu awaye yote atakayeliita ina la BWANA ataponywa,…” ( Yoeli 2:32).
Silaha za vita vyetu si mwili bali ni za Roho.Ukisoma vyema katika Biblia vitabu vya; 2Kor. 10:34; Kutoka 17:8-16; utaona kuwa pamoja na vikuki kuwepo,Israeli hakushinda vita pasipo maombi. Maombi yanaleta mtiririko wa nguvu za ki-Mungu kwa mwombaji.Yesu alipopaza sauti yake akaomba makaburi yalifunuka nchi ilitetemeka miamba ikapasuka.
Nami nitaomba kwake nchi iliyomeza maisha yako italimika.Mwamba ulioficha baraka zako na ustawi utatetemeshwa.Na makaburi yaliyozika maisha yako kwa ujumla yatafunuka,nawe utainuka kwa uwezo na nguvu.“Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti ewe mauti, ya wapi mapigo yako,…” (Hosea 13:14).Yesu Kristo ndiye mkombozi wetu dhidi ya nguvu ya maadui na kaburi.
Usiogope, hapana tena makaburi yakayokamata maisha yako;watoto wako na mali zako.

Itaendelea


 

6 comments:

  1. Hey there! I just want to give you a big thumbs up for the excellent info you have here on this post.
    I am returning to your web site for more soon.


    Stop by my blog - daytime Tv

    ReplyDelete
  2. Asking questions are truly good thing if you are not understanding anything entirely,
    but this piece of writing offers pleasant understanding even.


    Also visit my site :: http://www.fonax.com/moodle/blog/index.php?postid=14089

    ReplyDelete
  3. Very good info. Lucky me I discovered your blog by chance (stumbleupon).

    I've book-marked it for later!

    My webpage: www.soheit.Com

    ReplyDelete
  4. Hi there to every , since I am actually keen of reading this blog's post to be updated regularly. It contains pleasant data.

    Here is my web site; wheatgrass juicers

    ReplyDelete
  5. Very great post. I just stumbled upon your blog and wished to mention that I have really enjoyed browsing
    your blog posts. In any case I will be subscribing for your
    rss feed and I'm hoping you write once more soon!

    Also visit my homepage :: sasqa.org

    ReplyDelete
  6. This design is incredible! You certainly know how to keep a reader
    amused. Between your wit and your videos, I was almost moved to start my own blog
    (well, almost...HaHa!) Fantastic job. I really enjoyed what you had to say,
    and more than that, how you presented it. Too cool!

    My website - http://petrock.ru/index.php?do=/blog/6075/best-juicers-on-the-marketplace

    ReplyDelete