Wednesday, March 29, 2017

CITY HARVEST CHURCH WELCOMED TO TEGETA TAG SECTION

City Harvest Church welcomed to TAG Tegeta Section last Sunday after moving from Mabibo Garage (Magomeni Section) last December. Among many who witnessed the event is the Overseer for Tegeta Section, Rev. Urassa and Bishop Magila of Dodoma South, who is a part of a partneship in Mpwapwa church planting mission together with City Harvest and Ubungo TAG Church
Reverend Urassa, TAG Tegeta Section Overseer preaching at City Harvest
Mr & Mrs Chris Dondo marking birthdays and anniversaries with a cake
Bishop Magila, from Dodoma South, a partner in Mpwapwa church planting mission
Voice of Victory Choir from TAG Boko Basihaya singing at City Harvest
Voice of Victory Choir from TAG Boko Basihaya singing at City Harvest
Voice of Victory Choir from TAG Boko Basihaya singing at City Harvest
WWK City Harvest giving recognition award to Tegeta Section WWK Director
WWK City Harvest giving recognition award to Tegeta Section Overseer
WWK City Harvest leaders welcoming the visitors
William Vitalis receiving a certificate upon graduating Spiritual Maturity Class
Mary Mallya receiving a certificate upon graduating Spiritual Maturity Class
Sosthenes Mallya receiving a certificate upon graduating Spiritual Maturity Class
Lilian Kityege receiving a certificate upon graduating Spiritual Maturity Class
Ester Kaniki receiving a certificate upon graduating Spiritual Maturity Class
Edwin Ndibalema receiving a certificate upon graduating Spiritual Maturity Class
Joseph Buchoti receiving a certificate upon graduating Spiritual Maturity Class
Anna Kimaro receiving a certificate upon graduating Spiritual Maturity Class
Alexander Mtweve receiving a certificate upon graduating Spiritual Maturity Class
Abednego Mhagama receiving a certificate upon graduating Spiritual Maturity Class
George Nzowa receiving a certificate upon graduating Spiritual Maturity Class
Pastor Samwel Mwangu, the Spiritual Maturity Class Program Organiser

CITY HARVEST HOME COMING WORSHIP CONCERT THIS FRIDAY

This Friday... Most Welcome

Tuesday, March 21, 2017

A GLORIOUS CITY HARVEST CAMPUS SUNDAY


Esther Bernard with City Shakers International and Campus Students leading Praise
Pastoral Team during Praise and Worship session
We do it like this....
Show me the dance....
Let the music praise His Holy Name
Drumming praise to jesus
Give Him praise
Praise ON
City Shakers International and Campus Students leading Praise
Alexander with City Shakers International and Campus Students leading Praise
Mighty Warriors Children Class presenting a special song
Mighty Warriors Children Class presenting memory verses
Mighty Warriors Children Class presenting memory verses
Students presenting a drama
Attentively following the drama my Campus Students
Students presenting a drama
In attendance

MENTORSHIP PROGRAM - ANZISHA NA KUZA BIASHARA


Mahusiano Kuelekea Ndoa - 7

Na Sir Azgard Stephen

Sir Azgard Stephen
Shalom shalom wana wa Mungu. Hatimaye leo tunamalizia swali la 6 katika makala yetu ya mahusiano, swali lilihoji njia sahihi ya kuchumbia (proposing). Wengi wetu humu hili linaweza lisiwe la kwetu, lakini likawe msaada kwa wadogo zetu na jamii inayotuzungumza. Kwa yote niliyozunguka, ni dhahili mtu kujua cha kufanya mpaka sasa, hasa kwenye swali la #3 na #4 nilipozungumza juu ya kukataliwa.

Leo nizungumze majumuisho katika hili, ili kwa namna flani itusaidie angalau kutokukosea, angalau.

Kuna tofauti kati ya kutongoza (seducing) na kuchumbia (proposing). Mtu yeyote anaweza akatongoza, kwa madhumuni yoyote yale, ila kuchumbia mtu anahitajika kuwa na uzatiti (commitment). Kutongoza ni kitendo (action), kuchumbia ni mchakato (process).

Mambo kadhaa ni muhimu kuyajua unapoamua kuchumbia:
  • Ni muhimu kuanza mchakato huu ukiwa uko tayari kuoa leo, yaani ukiwa una utayari na uwezo wa kuoa sasa. Nimeeleza sana juu ya hili, nisirudie tena.
  • Kuwa na uhakika kuwa huyo unayetaka kumchumbia unampenda na anakupenda pia. Hii ni muhimu kuliko unavyoweza kafikiri. Nimezungumza sana juu ya upendo. Kukaa ndani na mtu ambaye huna affection naye ni mzigo mkubwa, kama unaweza kuepuka hilo basi fanya hivyo. Nasema hivi kwasababu nyingi. Mojawapo ni kwamba, unaweza "ukajikuta" kwenye mahusiano kwa bahati mbaya. Yaani mmekuwa tu marafiki, mkawa mnakubaliana sana katika mambo mengi, na ukawa mhitaji na huyo dada naye akawa mhitaji, ukafikiri kwasababu tu mnakubaliana katika mambo mengi basi huyo anafaa kuwa mkeo. Ni kweli uchumba mzuri huanzia kwenye urafiki, lakini si kila urafiki lazima uishie kwenye uchumba na ndoa. Test your feelings on that girl, na wala huhitaji kipimo cha kisayansi hapa. Kuna vile moyo unashtuka ukimuona, kuna vile unapoteza control. Pamoja na uchunguzi wote na vipimo vyote, lakini kipimo cha mwisho katika maamuzi haya ni upendo.
  • Kuwa na mtazamo wa miaka ya uzeeni. Hapa ndio kipimo cha utu uzima. Utu wa nje unachakaa, utu wa ndani hudumu milele. Kuutazama uzee ni kwamba, wakati utafika huyo mrembo atakuwa kibogoyo. Ni kitu gani kitakuwa kivutio cha upendo wako kwake? Ni utu wa ndani pekee, character, ndio utakuwa asali yako. No matter how beautiful she is, don't skip her character. Uzuri wa ndani huuzidi wa nje, na humfanya asiyevutia avutie. Kwahiyo, pamoja na uzuri wote alio nao mtu, lakini kama utu wa ndani umeoza please don't.
  • Usidhani utambadilisha mtu. Huu ni uongo tunaojidanganya, kwamba ana tabia hii mbaya lakini tukiingia kwenye ndoa nitambadilisha. That is a very risk gamble, si kazi rahisi kumbadilisha mtu. Mtu anaweza kuamua kubadilika, lakini huwezi kumbadilisha kwa lazima. Wapo watu waliingia wakitegemea kuwabadilisha wenzi wao, it never happened. Lakini pia kuna watu waliingia kwenye mahusiano na watu wenye tabia mbaya na wakabadilika. Ukiwahoji, watakwambia waliamua wenyewe kubadilika, na si kwamba waume zao waliwabadilisha. Inaweza ikatokea ukambadilisha, but it is the risk gamble. Kwa ushauri wangu, usijaribu hii.
  • Pita kwenye mchakato nilioeleza kwenye swali la 3. Jenga ukaribu na mawasiliano, win her heart, muoneshe unampenda, kisha chukua hatua. Kwa ushauri wangu, hata kama Mungu amekuonesha katika ndoto kuwa huyo ndiye, usiende na kumshuhudia kama njia ya kumpata. She need to see your love, show it.

Katika mambo yote haya, mipango ni ya mwanadamu lakini jawabu latoka kwa Bwana. Hatuingii kwenye mahusiano sahihi kwa umalidadi wetu, bali kwasababu ni kusudi la Bwana.

Mungu ametupa akili, tunafanya mpaka pale upeo wetu unapoishia. Mambo tusiyoyajua ni ya Bwana,na kwa neema yake anatuvusha katika mengi.

BONDE LA KUKATA MANENO! NAAM!

Niwatakie baraka za Bwana

Sunday, March 19, 2017

Mahusiano Kuelekea Ndoa - 6

Na Sir Azgard Stephen

Shalom wana wa Mungu. Katika kuendeleza kujibu maswali niliyoweka hapa, leo nizungumzie swali la 4, swali ambalo lilihoji juu ya kuvunjika kwa mahusiano, shida ni nini?

Ukifuatilia tangu maelezo ya swali la kwanza, juu ya upendo, unaweza ukaelewa ni kwa nini watu wanakaa katika mahusiano na wakafanikiwa kuingia kwenye ndoa, lakini wengine wanaishia njiani.

Nianze kwa kusema, kuvunjika kwa mahusiano sio jambo zuri, linaumiza na kujeruhi. Lakini pia ikibidi kuvunja mahusiano ni bora kuliko kuja kuvunja ndoa au kuishi na msalaba milele.

Nimeeleza katika swali la tatu, juu ya kukataliwa na kuishi katika mahusiano katika hali ya sintofahamu. Tungependa watu waingie kwenye mahusiano, na mahusiano hayo yapelekee ndoa, hii ndio furaha yetu, na kwa kweli ndio mpango wa Mungu. Kwa bahati nzuri maandiko yanatupa kisa kimoja tu cha mahusiano yaliyotetereka, na Mungu akaingilia kati. Ni pale Yusufu alipotaka kumuacha Mariamu kwa siri kisa Mariamu ni mjamzito, Mungu akamfafanulia Yusufu na hatimaye Yusufu akaahirisha mpango wake. Kimsingi, mahusiano yakianza na kufikia lengo inapendeza.

Zipo sababu nyingi za mahusiano kuvunjika, mimi niweke hapa chache kati ya hizo:

1. Sababu za wawili hao kuingia kwenye mahusiano hazikuwa dhahiri. Yaani hapa unaingia na mtu kwenye mahusiano ukiwa huna sababu za kuingia kwenye mahusiano. Unakuta watu wako kwenye mahusiano hawana vision, they are just in relationship. Mtu anaona kuliko kuwa peke yake ni afadhali niwe na mtu wa kwenda naye “out”, na kuchat naye usiku kucha. Wawili hawa wakiwa kwenye safari hiyo, mmoja atazinduka usingizini, na kugundua kuwa anatakiwa awe kwenye serious relationship. Anamtafakari aliye naye kwenye mahusiano, hafai kuwa mke/mume. Kinachofuata hapo unaelewa, kuna mtu ataachwa, na mahusiano ndio yanakuwa yameishia hapo. Hii ni very premature, lakini ni common practice kwa vijana wengi hasa walio kwenye umri wa kati, yaani 22 mpaka 26. Bahati mbaya sasa kwa upande wa wadada, akiachwa hapa ana-panic, na anaweza akachukua maamuzi ya kumkomoa huyo mwenzake kwa kuingia kwenye mahusiano mengine ya ghafla. Huwa na yenyewe haina mwisho mzuri.

2. Kukaa kwenye mahusiano muda mrefu. Ukimchunguza sana bata humli. Baadhi yetu tunafikiri kukaa kwenye mahusiano muda mrefu ndio kuchunguzana vizuri. Watu wanakaa kwenye mahusiano miaka 5, na hawana sababu za msingi. Yaani uwezo wa kuoana wanao, lakini wanakaa tu kwenye mahusiano, hoja yao wafahamiane. Ni jambo zuri kufahamiana kabla ya kufunga ndoa, lakini kwa kweli kufahamiana hakuji kwa kukaa muda mrefu kupita kiasi.

Kuna sababu za kukaa muda mrefu, ikiwa haziepukiki, lakini mimi nashauri tu kuwa sio afya, ina risks nyingi. Kama mna mahusiano yenye dira, basi chukueni hatua msonge mbele badala ya kuendelea kuchunguzana.

3. Kuingia kwenye mahusiano mkiwa hamna uwezo wa kuoana. Hii inarejea kule kule kwa jana, lakini hoja yangu ya msingi hapa ni hii, unaingia kwenye mahusiano na mdada ilhali hauko tayari kuoa leo. Mfano, wewe ni mwanafunzi au “graduate”, huna kipato na unaishi kwenu au kwa mshkaji, halafu unaongezea na mahusiano juu. Unakaa muda wa kutosha tu na huyo dadajusi, ukimpa ahadi kedekede juu ya kesho yenu. Muda haugandi, time inasogea. Baada ya miaka 4 unapata kazi, lakini unagundua huyo dadajusi sio type yako, unaanza kufanya maombi ya kuachana kwa amani. My brother hakunaga kuachana kwa amani katika hiyo situation, utamjeruhi tu huyo mdada. Upande wa pili nao unahusika.

Hapa naomba nikazie, ingia kwenye mahusiano pale unapokuwa na uhakika wa kuoa kesho, na mdada ingia kwenye mahusiano na mkaka ambaye yuko tayari kuoa leo/kesho. “I don’t mean you become materialistic, I mean be realistic. Don’t misquote me by leaving your man with a vision for a man with television, you will end-up seeing the man with vision in your husband's television.”

I mean, go into relationship when you both ready for it, usiingie kwenye mahusiano kwa sababu wakaka wataisha.

Hapa nakumbuka wakati natoka chuo nikaambiwa kama huna relationship utapata tabu sana kupata mtu mtaani kwani ni wachache, eti kule chuo ni wengi

Nijuavyo mimi, sioi kwa sababu ni wengi, nimeoa kwa sababu wangu yupo.

Mdada mmoja, was my college young-sister, alimaliza chuo pale UDOM akiwa single. Nakumbuka akiwa mwaka wa tatu nilimuuliza kama yuko na mahusiano, akaniambia hana. Nikamuuliza kwa nini, akaniambia sentensi ambayo kamwe siisahau, "Mama ameniambia nisome, nijiweke vizuri, niwe wife material. Wakati ukifika nikitaka kuolewa mtu anaye-derseve kunioa atakuja." This was so powerful to me, na huyu dada hakuwa mpendwa.

Changamoto ya kuwa kwenye mahusiano na Serengeti Boy ni kwamba, unakuwa occupied na kwa hiyo unakuwa busy na mtu ambaye sio muoaji. Huchukui muda wa kutosha kujiandaa kuwa wife material kwasababu tayari "unaye" (ambaye siye). Na waoaji wanakosa nafasi kwa sababu kila wakija uko occupied. Umri unaenda, na huyo uliyenaye analiona hilo. Ikifika wakati yuko tayari kuoa, anagundua wewe sio wife material, anakuacha. Hii ni mbaya sana, lakini sasa inatokea na watu wanaumia, very bad.

4. Kuonja pembeni. Hili nimelizungumza kule kwa wadada. Zinaa huleta uharibifu, dawa yake ni toba tu. Mkiingia kwenye mahusiano halafu mkajihusisha na ngono, ni sababu kubwa ya mahusiano kuvunjika. Jambo la kwanza, hii inaondoa kabisa uwepo wa Mungu, mnaenda wenyewe. Lakini pili, maziwa yale yanayokufanya ufuge ng'ombe sasa unayapata dukani, why keep a cow! Ni muhimu kujizuia, ili iwape nafasi ya kumsogelea Mungu kwa sala na maombi, lakini pia iwape sababu ya kwenda huko kwa shauku. Nilisema sana katika hili, nisirudie. Jambo la msingi ni kwamba, mkishirikiana ngono inawapunguzia credit, value, na hivyo kuonana wa kawaida. Kuna tofauti ya ngono na tendo la ndoa; ngono huleta aibu, tendo la ndoa huleta utukufu.

5. Tabia zisizo za adili. Hii nimeiweka hivi kwa sababu kuna tabia ambazo mimi naziita si nzuri kuzi-practice kwenye mahusiano.

↘Tabia ya kuomba hela. Ni kweli huyu ni mchumba wako, lakini kwa kweli sio tiketi ya yeye kutatua shida zako zote. Hii ni kwa pande zote. Dada mmoja alimuacha kakajusi wake kwa sababu tu huyo kakajusi alikwenda kuchukua gari ya dadajusi na kukaa nayo, kupigia misele. Dadajusi akaona huyu ni “Mario” akaachana naye. Si jambo baya mkaka kutumia gari ya dadajusi wake, lakini pale inapolazimu, sio kupigia misele.

↘Kueleza matatizo ya kwenu. Yaani kabla sijaingia kwenye ndoa na wewe najua kuwa kwenye familia yenu uchawi umeweka makao. Ni advantage ya kakajusi kujua anakoingia, lakini sasa wewe usimtangazie. Sasa kama umemwambia kwenu wachawi, akikukimbia utamlaumu? Ni kazi yake kuchunguza kwenu kukoje, akijua atachagua kusuka au kunyoa, akikuuliza mwambie ndio kuna hiyo shida, ila mimi nimetengwa nayo na damu ya Yesu. Let your problems not to be problems.

↘Kuelezea changamoto za mahusiano yako ya nyuma. Wengi hapa watasema, kuwa muwazi, usiifiche historia yako. Mimi nasema burry the past, live your today. Kama atataka kujua huko nyuma mahusiano yako yalikuwaje, mwache achimbe, akijua akikuuliza mwambie ndio yalitokea, lakini hiyo ni historia. Simaanishi umfiche kuwa hujawahi kuwa na mahusiano, akikuuliza mwambie, asipokuuliza usimwambie. Hivi kwani ukimwambia inaongeza nini katika mahusiano yenu? Sasa wewe unaingia kwenye mahusiano leo, kesho unaitisha outing ya kumwambia changamoto za mahusiano yako yaliyopita, in the name of transparency. My dear, you are digging ur own grave, achana na hiyo kitu. Yazungumzie pale tu kunapokuwa na strings ambazo unaona zinaweza kuhatarisha mahusiano yenu ya sasa, otherwise don’t talk about. I know I swim up-stream in this, lakini sijawahi kuona manufaa ya jambo hili.

↘Kuigiza. Unaishi maisha yasiyo halisi. Unaazima gari la mshkaji utoke out na mchumba wako. Kila anachoomba mpaka unakopa umtimizie. Be you, because the day she/he realise the real you, she/he will dump you definitely. Unavaa sketi ndefu ilhali unajua kabisa huwa sketi zako ni za magotini. Vaa sketi zako, akupende nazo hizo. Siku mojamoja onana naye ukiwa hujapaka poda, auone uso wako halisi. Usihofie kuachwa, ila afadhali akuache mapema kuliko akikuacha mwezi mmoja kabla ya ndoa baada ya kukutembelea ukiwa unaamka by surprise. Be you.

↘Kujipendekeza kwa ndugu wa kakajusi/dadajusi. Ni jambo zuri kufahamika ukweni, ila usijipeleke. Ni jambo la staha mkaka kwenda ukweni, ila ni jambo la aibu mdada kujipendekeza ukweni. Acha akupeleke, na kama unataka kwenda mwambie akupeleke. Sio unachukua namba ya dada yake na kuanza kujitambulisha, this is bad.

↘Kukagua simu ya kakajusi/dadajusi wako. Another up-stream swimming. Una uhuru na haki ya kuperuzi simu ya mchumba wako, lakini sio tabia nzuri. Huwa ina connotation mbaya, humuamini. Leave his/her phone alone, mind yours. Simu ni private property, kupekenyua humo ni kujivusha mipaka ya umiliki. Mkiingia kwenye ndoa mtayaamua, lakini katika mahusiano sio tabia nzuri.

↘Kutokuwa nadhifu. Pamoja na kwamba umeshampata na ni wako, lakini sio tiketi ya kuwa rafu. Kila mtu anapenda kilichopendeza, pendeza my friend. Unaenda kuonana na kakajusi/dadajusi wako, vunja sanduku lako japo kidogo. Usiende kuvunja la rafiki, vunja lako. Be real, and be smart.

Kwa hayo machache niwatakie siku njema.

Saturday, March 18, 2017

UZINDUZI WA ALBAMU YA NENO YA FRIDA FELIX

Uzinduzi wa Audio Album kufanyika tarehe 26 Machi 2017
katika kanisa la TAG City Harvest Bahari Beach
Kwa Mawasiliano zaidi piga +255 712 093 696

Mahusiano Kuelekea Ndoa - 5

Na Sir Azgard Stephen

Sir Azgard & mkewe
Shalom wana wa Mungu. Leo niendelee kidogo pale nilipoishia jana, hasa nizungumze sababu kadhaa za wadada kukaa kwenye mahusiano muda mrefu bila kuwa na uhakika wa hatma ya mahusiano hayo. Moja ya vitu vigumu duniani ni kukaa katika sintofahamu. Kukaa katika hali ambayo hujui nini kitatokea kesho.

Katika maisha ya mahusiano, kukaa katika mahusiano na sintofahamu ni miongoni mwa changamoto ya moyo.

Unaingia kwenye mahusiano na mkaka, mwaka wa kwanza unapita, mwaka wa pili, na kuendelea, na hujui ni lini huyo kakajusi atakuoa, zaidi sana huna uhakika kama atakuoa au la. Hii hupelekea vidonda vya tumbo kwa sababu ya mawazo.

Nitoe sababu kadhaa za jambo hili kutokea:

1. Kuingia kwenye mahusiano na mtu ambaye hayuko tayari kuoa. Utayari hapa namaanisha uhitaji. "Demand" ina "components" mbili muhimu, ability and willingness. Mtu anaweza akawa willing lakini hana uwezo. Hapa naweza kutupiwa mawe, lakini ni ukweli dhahiri kwamba hii ni miongoni mwa sababu. Nitoe mfano, mkaka amekuchumbia akiwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu. Hana uhakika wa wapi atakuwa na atafanya nini. Anakuja kupata kazi miaka 4 baadaye, wakati huo mmekaa kwenye uhusiano miaka mitano. Alikuchumbia ukiwa na miaka 24, sasa hivi una miaka 29. Kinachotokea ni yeye kujiuliza swali hili, hivi nimuoe kweli au nitafute mdada mdogo! Hii inakutengenezea probability, na likely unaweza kujikuta unaachika. Ni "nature" tu, kuwa mdada huwa anakuwa kwenye "peak" akiwa kati ya 22 na 27, mara nyingi (sio mara zote) mdada akifikisha 30 inakuwa ni changamoto kwake, wadada mnanielewa. Hii si katika roho, ni katika mwili, naomba nieleweke hapa.

Huwa nasema, ingia katika mahusiano na mkaka ambaye yuko tayari kuoa kesho, nikiwa na maana ana uwezo (demand) ya kukuoa hata kama ndoa ingewezekana kufanyika kesho. Sasa kuna watu wameingia kwenye mahusiano wakiwa wanafunzi, na wengine wakakaa kwenye uhusiano miaka 7 na zaidi, na wakaoana, na wako fresh kabisa,wapo. Ila ninachokisema hapa ni kwamba,kwa wengi hii imekuwa sababu ya sintofahamu.

2. Kuingia kwenye mahusiano bila malengo. Kwa lugha rahisi hii tunaita mahusiano butu. Yaani uko kwenye mahusiano na mtu, lakini hamjui hata mnaelekea wapi na lini kitatokea nini. Huyo kakajusi mnajuana ninyi tu, hakuna hata ndugu yako/yake anayejua. Hii ni "risk," kwani siku akiwaza vinginevyo hakuna anayejua, anasepa kimyakimya. Mkiwa kwenye mahusiano shaurianeni kuwafahamisha watu kadhaa, hasa watu wa karibu ikiwamo ndugu wachache wa karibu. Kuna wakati tufani inavuma, hawa ndio watawasaidia kushika makasia.

3. Kushikishana matatizo yooote. Yaani wewe uko kwenye mahusiano na kakajusi, anajua mpaka mshahara wa baba yako kuwa ni mdogo. Unamweleza kila kitu, na changamoto ikitokea home fasta ushamwambia na unataka akusaidie. Sifundishi roho mbaya, lakini kwa kweli kipindi cha uchumba kinajengwa zaidi na habari nzuri kuliko habari mbaya. Mshirikishe huyo kakajusi shida zako au za familia yako pale inapolazimu, tena si kwa kumuomba msaada bali kumshirikisha akusaidie kuomba. On the way akiona vyema kukusaidia itokee, lakini usimwambie. Hii inaweza kuwa ngumu kumeza,lakini naturally wakaka hawapendi kuombwa hela. Kuomba hela kwa mkaka ina connotation fulani sio nzuri. Anaweza asiseme, upendo hufunika wingi wa dhambi, lakini kwenye Medula Oblangata, kule kwenye subconscious mind kuna kitu inapandikiza ambacho si kizuri, kitachangia kwenye maamuzi ya kukuacha. Matatizo sio fedha tu, matatizo yoyote. Yafanye matatizo yako kuwa yako,japo kwa kipindi hiki tu,mkishaoana ndio yatakuwa yenu.

4. Kutokuwa wewe. Huwa nashauri, don't disguise. Be you. Tabia ni ngozi huwa haijifichi milele. Kuwa wewe from the beginning, ili huyu kaka asiwe na tabia mpya za kuzoea muwapo safarini. Kama kila siku kuna kitu kipya kinaunfold huyu kakajusi anachkua muda mwingi kutafakari kama ataweza kukibeba, akimaliza hiki kinajitokeza kingine. Akujue tu kuwa wewe uko hivi, ili muwepo pamoja achukue muda kukuzoea au hata kukushape. Hii itasaidia mbivu na mbichi kujulikana mapema.

5. Kuwa king'ang'anizi. Ni vizuri kupigania kilicho chako mpaka dakika ya mwisho, fight to the last minute, lakini sio vizuri kuwa king'ang'anizi. Yaani unaona kuna dalili zote kuwa huyo kakajusi haku-feel, hakupendi, lakini wewe unaendelea tu kumng'ang'ania. Kuna wakaka hawana "courage" ya kukwambia it is over, watafanya matendo tu. Ukiona hivyo, futa pumzi jua ni kwanini hakufeel, kama unaweza kurekebisha fanya hivyo, kama huwezi muite weka kila kitu kweupe. Tell him why don't you feel/love me. Asiposema tell him anaweza kuamua vinginevyo just in case. Kama anakupenda mtaendelea, kama ilikuwa kweli hakupendi "atasepa".

Huwa inaumiza, lakini ni heri kutokuwa nacho kuliko kuwa na ambacho sio chako.

6. Kuonja pembeni. Yaani kushirikiana tendo la ndoa. Ni kweli kuoa/kuolewa ni wajibu na utume katika nyumba ya Bwana, lakini pia kuna need of sex. Hii wapendwa wengi hatuikubali, lakini kwa kweli ndio hivyo. I married my wife, together with other things, because I am in need of sex. Sasa ukimpa huyo kakajusi, atachuchumilia nini? Atakuwa hana haraka kwasababu kile ambacho anaharakisha kukipata anakipata. My dear you will be in that relationship for 7 years. Mwisho wa siku anakuchoka na anakuacha. Si kila ambao wameonja pembeni wameishia kutokuoana, lakini sio kitu kizuri kufanya hivi. Haimpi Mungu utukufu, lakini pia itawavuruga.

Basi kwa hayo machache nikutakie siku njema

Sir Azgard

Friday, March 17, 2017

SEMINA YA UINJILISTI - SINZA BAPTIST

Mahusiano Kuelekea Ndoa - 4

Na Sir Azgard Stephen

Azgard na mkewe
Shalom wana wa Asafu. Leo nataka nizungumzie swali la 3 linalohusu kukataliwa, au kibuti kama wahusika wanavyoita.

Hili ni miongoni mwa mambo mabaya kwa vijana, kupeleka proposal kisha kukataliwa.
Nianze kwa kusema, kibuti ni ishara ya "premature proposal." Kunaweza kukawa na sababu nyingine, lakini kwa kweli hii ndio main.

'Premature proposal, ni pale unapopeleka hoja kwa mdada bila kumuandaa vya kutosha.
Yaani unamuona mdada, unampenda, unatamani awe mkeo baadae. Unachofanya unafanya unachokiita uchunguzi, kisha ukijiridhisha unaenda kuomba. Unamkamata kwenye ulimwengu wa Roho, unajiwekea na ishara huko. Eti nikienda kumwambia aseme ndio, akisema hapana au nipe muda huyo sio wangu!!! Unaenda dada anakutolea macho, hakuelewi. Unamuona shetani mkuuubwa.

Well, sikosoi juhudi za watu katika hilo, kama nilivyosema awali kuomba ni muhimu tena sana kuliko ambavyo wengi tunafanya, lakini nasisitiza kutumia njia sahihi.

Proposing is an art, sio kupelekeana vitisho na mistari. Kuna mpendwa mmoja, kaoa sasa, alimkuta huyo dada yuko kwenye mahusiano. Akamtisha huyo dada kuwa yuko kwenye wrong relationship, yule dada akamuacha kaka wake, ndio wakaoana na huyo mpendwa. Sorry but to me this is intimidation. Inaweza kuwa kweli yule dada alikuwa kwenye wrong relationship, lakini njia aliyotumia kwa mtazamo wangu haikuwa nzuri. However, sometimes the end justifies the means.

Nikirejea kwenye mada, vibuti vingi vinatokea kwa sababu kaka hakujipanga. Najaribu kukaa kwenye nafasi ya mdada. Kwa mfano, Baraka (sorry kukutumia hapa, just example) unakuja kwangu nakuita kaka, unaniamsha kila siku 11 niende prayers, na kunihimiza fellowship. Nakuheshimu tu kama baba Jemadari, kwa miezi miwili uliyochukua namba yangu ya simu. All of a sudden unaniambia una maongezi nami, tukutane Talma cafeteria. Mimi najiandaa, naweka na kabiblia kangu kwenye pochi, nakuja nikijua kuna vitu unataka unielekeze nikue kiroho zaidi (kumbuka kuhimiza fellowship na maombi). Nafika unaleta vistori viwili vya uwongo, alafu unadondosha agenda unataka niwe mkeo

In actual sense, nitakutolea macho, "because I didnt expect that, it was very premature." "I mean how" nikuelewe, sijawahi hata siku moja kuwaza utatokea upande huo. Kwa akili zangu, na "understanding" yangu, nitakumwaga tu

'Guys' nilishawahi kufanya hii 'mistake', nilim-propose mdada very prematurely, nikamuweka kwenye 'hard time' sana. When I came to realize nikamwambia awe na amani, like it never happened. Alikuwa ananiheshimu sana, na maamuzi sahihi ilikuwa ni kunimwaga. Lakini sasa anawaza akinimwaga atakuwa kanikosea heshima na akinikubali atakuwa hajajitendea haki, she don't feel me. Akawa "so down", akakosa amani sana. Ikabidi ni-withdraw proposal yangu. It was real embarrassing.

Katika hili nashauri yafuatayo;

1. Establish a relationship with a person, communicate. Huyu dada akujue, akuzoee, akufahamu japo kwa uchache. Yaani "don't be formal, but casual." Hii haimaanishi uwe comedian, lakini kuwe na casual relationship between you.

2. Win her heart. Hapa ndio kuna shughuli hapa, winning someone's heart. This will stay forever. Sasa you dont win her heart by money or gifts, but by affections. Ukiamka asubuhi wish her good morning. Usiku don't go to sleep without telling good night. Siku moja moja mtegee uone kama una-win kwa yeye kukutafuta. Akiwa na tukio show concern, be there if possible. Sio unatuma maandiko tu. Maandiko yana-win Roho, ila kinachopenda ni moyo
Wish her happy birthday, send her a birthday card. Hivi vyoote ni vya kawaida tu, anyone can do to anybody, lakini ile "frequency" ya kuvifanya vinamfanya huyu dada akuwaze, akufikirie, na akuone kila wakati. Hapa ndio utaskia "yule kaka ana care". When u hear that, somehow u have won somebody's heart. She dont want to see how intelligent and God fearing you are, she want to see how much you care!

3. Muoneshe kuwa unampenda. Sijasema mwambie, nimesema muoneshe! Yaani huyu dada kabla hata hujamwambia kuwa unampenda, anatakiwa ajue unampenda, angalau awe na hiyo "clue". Katika hatua hii, fanya vitu vichache vinavyoonesha u-special kwake, na ajue kuwa that is special for her. Kama hakupendi, basi utaona ata-retreat. Ikitokea hiyo ama urudi kwenye #2 hapo juu au usepe, ukijua kuwa hii "mission" haina matunda. Hii itaepusha "embarassment" za kibuti, mtaachana mkiwa hamjaambiana.

Ukifanya hiyo #2 vizuri, hii ya #3 itakuja vizuri sana. Kabla hata hujaanza kumuonesha unampenda utaona response yake, badala ya wewe kumtafuta sana utaona mnatafutana. Ukiingiza #3 hapo utaona tu mambo yanaweka tick ✅

Jambo la msingi hapa ni kwamba, huyu dada akikukubali hapo #2 basi chukua hatua umuoneshe unampenda, mfanyie vitu ambavyo bila chenga atajua huyu kaka ananipenda. Mara nyingi hapa wadada wanashindwa kujizuia, usipomwambia atakwambia. Hii itakuwa na maana umeremba sana mwandiko mpaka peni ikatapika.

4. Sasa njia nyeupe, kupeleka proposal au kukimbia mission. Hii ina maana, kama #1 imekuruhusu kwenda #2, na #2 imetengeneza njia ya #3 vizuri, basi njia ni nyeupe kwenda kuweka hoja, na wala hutakuwa na wasiwasi kwasababu unajua matokeo, Chelsea vs Yanga

Kama nilivyosema awali, proposing is an art, kwahiyo ukicheza vizuri hapa kamwe hutakaa ukione kibuti kinafananaje.

Pamoja na ufundi wote huu, ni muhimu SANA kuomba in the process, kwani hii sio guarantee ya kupata mke mwema. Kumbuka, sikuwa nazungumzia jinsi ya kupata mke mwema, bali nazungumzia how to do it right.

Kuna watu wamepishana na wake zao kwa kufanya proposal zao vibaya, very bad. Yaani ukweli ni kwamba mdada ni mzuri (right), na wewe ni mzuri, na together you can make good couple. Lakini kwa sababu tu hukumu-affect (love is affection), mnapishana. Maskini hajui kwamba you are the right guy for her, wewe unajua she is the right girl for you, mnapishana. It is your responsibility to let her know, by process.

Nitoe "caution" hapa, mkaka ukimu-entertain mdada yeyote katika njia hiyo she will fall in the trap, na kama huna mpango naye utamuumiza sana.

Kwa kumalizia niseme tu kuwa, your wife is going to be your best friend, a soul-mate. Hiyo "process" hapo ni muhimu sana kumfanya awe hivyo. Yaani mke wako lazima akutofautishe wewe na kaka zake. Na wewe lazima umtofautishe na dada zako. It is not by responsibility, but by affection. Yaani kuna vile mke wangu akitokea moyo unaruka, tofauti kabisa na mdada yeyote. Na kuna vile namuona mke wangu nikiwepo, I am the only person no matter how many are in the place. Hii haitokei "naturally", inatengenezwa.

I had to propose to my wife 2 months before plan kwa sababu niliona nisipofanya hivyo she will break the ice, na wengine hatupendi wadada ndio watuambie wame-fall.

Love surpass all, upendo ndio humfanya mtu ku-move mountains. What makes your woman to choose u instead of her job (sometimes), you instead of her relatives, you instead of the movie superstars, you instead of high profile MPs, etc, is how much you invested in her heart. Maandiko yanasema, palipo na mapendo vinono vinakaa pembeni, mboga ya majani inatosha kabisaa.

Nimezungumza sana upande wa wakaka, ikimpendeza Mungu nitazungumza upande wa wadada, hasa kwanini wanakaa kwenye relationship muda mrefu bila kuwa na uhakika kama huyo kaka atamuoa au la

Mungu awabariki

Sir Azgard

Thursday, March 16, 2017

Siku ya Wanawake yafana City Harvest

WWK katika picha ya pamoja na Wachungaji
Maadhimisho ya siku ya wanawake katika kanisa la City Harvest lililopo Bahari Beach jijini Dar es Salaam yamekuwa na mvuto wa kipekee. Idara ya wanawake kanisani hapo (WWK) ambayo ndiyo iliongoza maandalizi ya maadhimisho ya siku hiyo, ilikuwa na mengi ya kuwasilisha ikiwa ni kuonyesha mchango wa wanawake katika kulijenga kanisa na kuujenga Ufalme wa Mungu kwa ujumla.

Mhubiri wa jumapili hiyo alikuwa Mchunagji Rose Mavika ambaye alisisitiza juu ya uchaji Mungu kama sifa kuu ya mwanamke katika kanisa. Neno kuu la siku ya wanawake mwaka huu lilitoka kitabu cha Mithali 31:30 “Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.”

Mama Rosemary Mavika akihubiri City Harvest siku ya Wanawake

Mchungaji Mavika aliendelea kusisitiza kuwa anayemcha Bwana ni wa tofauti, ana Roho njema kutoka kwa Bwana, na ikiwa mwanamke atakuwa mcha Mungu, basi familia, jamii na taifa zima litaambukizwa kumcha Bwana, kama ilivyokuwa ushuhuda kwa maisha yake.



Katika kuendelea kumcha Bwana, Mchungaji Mavika alitaja mambo makuu matano ya kuendelea kuyashika, ambayo ni Maombi, Neno la Bwana, Utoaji, Kukusanyika pamoja na Kushuhudia.

Katika maombi, mwanamke ni lazima kuibeba familia na jamii yake, na kuacha kufuata watu kama mke wa Ayubu (Ayubu 2:9), Safira mke wa Anania (Matendo 5), na pia Delila, ambao kutoka kwao hatujifunzi mambo mema.

Maombezi yakiongozwa na Mchungaji Mavika
Katika maombi ni muhimu kujitakasa kwani kufanya hivyo ni kama binti anayejiandaa kumpokea mchumba wake.

Vilevile Mchungaji Mavika alisisitiza kuhusu kusoma na kujifunza Neno la Bwana (Joshua 1:1-9; Wakolosai 3:16) ili kuendelea kusikia kutoka kwa Mungu.

Pamoja na hayo, msisitizo ulikuwepo kwenye utoaji sadaka na zaka (Malaki 3:7-10; Malaki 1:6-14; Kutoka 25) Kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25) kwenye ibada za pamoja kanisani, welcome groups na kusanyiko la nyumbani.


Mchungaji wa kanisa Matilda na Mchungaji Kiongozi
Yared Dondo wakikata keki kuadhimisha siku ya wanawake
Wanawake pia wanapaswa kuwa washuhudiaji, wahubiri wa Injili. Lakini juu ya yote, uhitaji wa kujazwa na nguvu ya Roho Mtakatifu wa Mungu afanyaye kazi ndani yetu (Luka 24:49; Matendo 1:8)

Katika shughuli nyingine, wanawake walithamini mchango wa watu mbalimbali katika huduma yao ikiwemo Wachungaji na viongozi wao kwa kuwapa zawadi kama sehemu ya kuwashukuru na vilevile kuchangia gharama ya ununuzi wa samani kwa ajili ya ofisi ya Mchungaji wa kanisa la City Harvest ambalo limehamia katika jengo lake jipya Bahari Beach

Wanawake wa City Harvest pia waliongoza ibada ya siku hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na nyimbo maalumu, shairi na igizo kama sehemu ya maadhimisho hayo muhimu ya kila mwaka.
Mchungaji wa WWK Dk. Bertha Kipilimba akikabidhi zawadi
kwa Mchungaji Kiongozi Architect Yared Dondo
Mstari wa mwaka kwa WWK: Mithali 31:30 “Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.”