Tuesday, January 10, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 10

SIKU YA 10 - 10/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

1 Wafalme 15:4 Walakini kwa ajili ya Daudi, Bwana, Mungu wake, akampa taa humo Yerusalemu, amwinue mwanawe baada yake, na kuufanya imara Yerusalemu;

Isaya 62:7 wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imaraYerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani.

Kwanini MIJI YETU TULIYOPO ifanywe imara? Yeremia 29:7 Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa Bwana; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani. AMANI YA MJI WAKO NI AMANI YAKO.. MAFANIKIO YA MJI WAKO YANAWEZA KU-AFFECT biashara zako, familia yako, kazi zako kwa njia moja au nyingine…Zaburi 122:6 Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao NDIVYO TUTAKAVYOFANYA KWENYE MIJI YETU

OMBEA MJI ULIOPO KWA SASA………………. OMBEA MIFUMO YA BIASHARA, ELIMU, DINI, STAREHE, VYOMBO VYA HABARI, SERIKALI NA SIASA, FAMILIA NA MASWALA YA KIJAMII….. MUNGU AKUPE NAFASI KWENYE SEKTA ULIYOPO NDANI YA MJI HUO
Apostle Shemeji Melayeki

GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES

PHONE: +255 714 548 565

We are the Standards! 2017

Monday, January 9, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 9

SIKU YA 09 - 09/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

SIKU YA 9… Danieli 11:14 Na zamani zile watu wengi watasimama ili kumpinga mfalme wa kusini; pia, wenye jeuri miongoni mwa watu wako watajiinua ili kuyathibitisha maono; lakini wataanguka.

MAONO YANAWEZA KUWA ESTABLISHED.. KAMA NI YA MUNGU HAITAANGUKA.. WALA SISI TUNAOTHIBITISHA TUTANG’AA NA KUWA WAKUU.. Danieli 11:32 … lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu.

MUNGU ATA-ESTABLISH MAONO YETU…

Endelea kujiombea………………na kuombea wengine…….HASA WALE AMBAO UNAWAFAHAMU WANAHITAJI NEEMA YA KRISTO

Apostle Shemeji Melayeki

GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES

PHONE: +255 714 548 565

We are the Standards! 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 8

SIKU YA 08 - 08/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA
Zaburi 99:4 Nguvu za mfalme nazo zapenda hukumu; Wewe ndiwe uliyeithibitisha adili; Ulifanya hukumu na haki katika Yakobo.

Zaburi 7:9 Ubaya wao wasio haki na ukome, Lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na viuno Ndiye Mungu aliye mwenye haki.

Amosi 5:15 Yachukieni mabaya; yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni; yamkini kwamba Bwana, Mungu wa majeshi, atawafanyia fadhili mabaki ya Yusufu.

Warumi 10:3 Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.

MUNGU NDIYE ATUPAYE HAKI YETU… NDIYO MAANA TUNASEMA Zaburi 71:2 Kwa haki yako uniponye, uniopoe, Unitegee sikio lako, uniokoe NA IKIWA TULIANGUKA KATIKA MAKOSA NI VYEMA KUOMBA BWANA AKURUDI KWA HAKI YAKE NA SIYO KWA MATENDO YAKO Yeremia 10:24 Ee Bwana, unirudi kwa haki; si kwa hasira yako, usije ukaniangamiza Zaburi 143:11 Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni;

UKITUMIA MATENDO YAKO KUJIHESABIA HAKI NA KUONA KUWA UNASTAHILI… UNAWEZA USIIONE NEEMA YA MUNGU MAISHANI MWAKO HATA SIKU MOJA…

Yakobo 3:18 Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao Amani…

NDIYO MAANA Waebrania 12:14 IMEANDIKWA Tafuteni KWA BIDII kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;

MUNGU AKUPE HAKI NA ADILI, UISHI VYEMA KATIKA DUNIA, UPENDEZWE NA UAMINIFU, UFANYE KAZI ZAKO KWA FURAHA BILA KUWA NA UCHUNGU WALA KUJIHUKUMU PAMOJA NA HOFU YA MABAYA YOYOTE… UWE NA AMANI NA WATU WOTE, MUNGU AKUPONYE KWA HAKI YAKE KWANI KWA MATENDO YAKO NA MBINU ZAKO ULISHINDWA KUJIOKOA NA HILA ZA ZA ADUI.. Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni, Ee Bwana, unirudi kwa haki; si kwa hasira yako, usije ukaniangamiza, Kwa haki yako uniponye, uniopoe, Unitegee sikio lako, uniokoe*

Endelea kujiombea………………na kuombea wengine…….HASA WALE AMBAO UNAWAFAHAMU WANAHITAJI NEEMA YA KRISTO
Apostle Shemeji Melayeki

GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES

PHONE: +255 714 548 565

We are the Standards! 2017


2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 7

SIKU YA 07 - 07/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

Zaburi 90:17 Na uzuri wa Bwana, Mungu wetu, uwe juu yetu, Na kazi ya mikono yetu utufanyie thabiti, Naam, kazi ya mikono yetu uithibitishe.

Waebrania 1:10 Na tena, Wewe,Bwana, hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, Na mbingu nikazi za mikono yako;

KAMA MBINGU NI KAZI YA MIKONO YA BWANA MUNGU WETU SISI UZAO WAKO NI LAZIMA TUWE NA KAZI ZA MIKONO YETU…. Uzuri ni kwamba Mungu anataka kuifanya thabiti/kuimarisha kazi ya mikono yetu…

KAZI YA MIKONO YANGU IWE ESTABLISHED…Uzuri wa Bwana, Mungu wangu, uwe juu yangu, Na kazi ya mikono yangu unifanyie thabiti, Naam, kazi ya mikono yangu uithibitishe.

MWAKA 2017, NITAJENGA BIASHARA ILIYOTHIBITISHWA, KAMA MBINGU KAZI YA MIKONO YA BABA YETU INADUMU HATA SASA, NAKATAA BIASHARA YANGU KUFA KUFA, KIPAJI CHANGU HAKITAPOTEA, DUKA LANGU HALITAPATA HASARA NA KUFUNGWA TENA, HUDUMA YANGU HAITAHARIBIKA, FAMILIA YANGU HAITAVUNJIKA, MUME WANGU HATANIACHA WALA WATOTO WANGU HAWATAKUWA KIZAZI CHA UKAIDI.

NATAMKA NA KUAMURU…. UTHABITI KATIKA KAMPUNI YANGU, UTHABITI KATIKA KAZI YANGU, KATIKA KILIMO CHANGU, BENKI YANGU, SACCOS YANGU,

NATAMKA UTHABITI KATIKA MIFUMO INAYOSHIKILIA SUSTAINABILITY YANGU…

KAMA KAZI YA BABA YANGU ALIYENIUMBA BADO INAPETA NA MIMI NINA SPIRITUAL DNA YA MUNGU…. NDIVYO ITAKAVYOKUWA KATIKA KAZI ZANGU…. Sasa na hata milele amina..

Zaburi 72:7 Siku zake yeye, mtumwenye hakiatasitawi, Na wingi wa amani hata mwezi utakapokom USIOGOPE HALI YA UCHUMI WA NCHI MAANA Mithali 10:25 Kisulisuli kikiisha pita asiye haki hayuko tena; Bali mwenye haki ni msingi wa milele.

HUTAONDOSHWA KATIKA JINA LA YESU………………..

Endelea kujiombea………………na kuombea hizo kazi za mikono…….

Apostle Shemeji Melayeki

GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES

PHONE: +255 714 548 565

We are the Standards! 2017


2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 6

SIKU YA 06 - 06/01/2017
Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA


Zaburi 89:4 Wazao wako nitawafanya imara milele, Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.

Neno lililotumika hapa WAZAO ni SEED (English), ZERA (Hebrews) ambapo ina maanisha fruit, plant, sowing time, posterity, child, fruitful Huu uzao ni zaidi ya watoto… hii inaitwa mbegu iliyootoka kwako/matunda yako…

Isaya 65:21 Nao watajenga nyumba, nakukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake. Mbali na kwamba utajenga na kula matunda yake…

Yohana 15:16…… nami nikawaweka mwende mkazae matunda; namatunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.

Mungu akupe uwezo wa kuzaa matunda, kuleta matokeo, na matokeo hayo yaweze kuwa na uwezo wa kustahimili majira na nyakati baada yako.. Yaani LEGACY au impact inayodumu baada yako.

IBRAHIM ALIAMBIWA NA MUNGU…

Mwanzo 17:6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako

LAKINI KUHUSU SISI…

Wagalatia 3:14ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya Imani

BARAKA YA IBRAHIMU ISINGEWEZA KUJA KWA MATAIFA BILA KURUHUSIWA NA TRANSACTIONAL ABILITY YA ROHO MTAKATIFU…

NDIYO MAANA ROHO MTAKATIFU NI MUHIMU NDANI YA KILA MKRISTO….

Tumshukuru Mungu kwamba Baraka ya Ibrahimu imetujilia…. Tutafanywa tuwe na uzaomwingi sana, tutafanywa kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwetu

UZAO WAKO UWE ESTABLISHED MILELE…

Endelea kujiombea……………

Apostle Shemeji Melayeki

GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES

PHONE: +255 714 548 565

We are the Standards! 2017

Thursday, January 5, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 5

SIKU YA 05 - 05/01/2017

Zaburi 40:2Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

2 Samweli 7:12…. nitainua mzao wako nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako, nami nitaufanya imara ufalme wake. 1 Mambo ya Nyakati 28:7 Na ufalme wake nitauweka imara milele, akijitia kwa bidii kuzitenda amri zangu na hukumu zangu, kama hivi leo.
1 Wafalme 2:4ili Bwana afanyeimara neno lake alilonena kwa habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli.

Kila mtu amepewa na Mungu eneo analotakiwa kutawala na kumiliki.. inaweza ikawa eneo la mazingira (nchi/mkoa/…), eneo la kibiashara, eneo la kipawa/kipaji, eneo la career, eneo la cheo, n.k.. NI MPANGO WA MUNGU KILA MTU AWE NA KITU ANACHO-DOMINATE TANGU MWANZO…

Mwanzo 1:28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Je, wewe unatawala eneo gani? Mwalimu? Mfanyabiashara? Mkulima? Mhubiri? Mfanyakazi?

Mungu aimarishe kila eneo ambalo umepewa kulimiliki katika jina la Yesu… UFANYE KWA UAMINIFU KWA KUIZIDISHA IZAE MATUNDA ZAIDI… KATIKA JINA LA YESU..
Luka 19:17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.

NGUVU YA KUMILIKI HUSABABISHWA NA NGUVU YA UZIDISHO Katika jina la Yesu Kristo, Mwaka 2017 uanze kuzidiha vipawa vyako ili upanuke katika umiliki wako.. Katika jina la Yesu….

KUFANYWA KUWA IMARA NA KUTHIBITISHWA.. UFALME WAKO… ENEO LAKO LA UTAWALA LIIMARISHWE 2017.

Endelea kuomba na kujiombea……………

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017


2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 4

SIKU YA 04 - 04/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

1 Samweli 1:23 ….. Bwana na alithibitishe neno lake tu. Basi yule mwanamke akangoja, akamnyonyesha mtoto wake, hata akamwachisha maziwa.

Baada ya Hana kuingia katika maombi mazito ya kumuomba Mungu ampe mtoto, kuna mambo kadhaa nataka  uone ikusaidie kupokea majibu maombi yako..
ANGALIA 1 Samweli 1:13-15

Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa.
Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako.
Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za Bwana

ELI ALIYEKUWA KUHANI AKAMJIBU MANENO HAYA…
1 Samweli 1:17 Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.

ANGALIA RESPONSE/MWITIKIO WA HANA BAADA YA MAOMBI…
1 Samweli 1:18 Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana tena.

Umewahi kuingia kwenye maombi hadi lugha ya kuomba inakuishia? USIACHE KUOMBA Hata kama jambo limekutia uchungu kiasi gani. OMBA HATA KWA MACHOZI, BWANA ATASIKIA MPAKA ALIVYOMJIBU HANA

Mungu anasikia pia kilio chako….. Mwanzo 16:11 Malaika wa Bwana akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana Bwana amesikia kilio cha mateso yako

Kutoka 2:23 Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.
Kutoka 3:7 Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;

Kutoka 3:9 Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa

LAKINI MUNGU TU HAKUWATOA KWENYE DHIKI KWA SABABU WALILIA LA! HASHA…. ILA MUNGU ALIKUWA NENO LA KUTHIBITISHWA JUU YA UHURU WAO…

Mwanzo 15:13 Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.

KILIO CHAO KIMEZIDI MIAKA MIA NNE ILISHAPITA… (ILIFIKA 430) Kutoka 12:41 Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, ya kwamba majeshi yote ya Bwana yalitoka nchi ya Misri.

NI NINI  KIMETOKEA?  MUNGU SI ALISEMA 400? NDIYO… KUNA WATU WALITAKIWA WAOMBE NA KUAMURU LILE NENO LITHIBITIKE LAKINI MUSA ALIKIMBILIA KWA WAMIDIANI…

ANGALIA DANIEL ALIPOONA NENO LA BWANA ALIINGIA KWENYE MAOMBI NA KU-CLAIM LITHIBITISHWE Danieli 9:2-3 “Katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.”

JE, UNAJUA KUNA MAMBO MENGI MUNGU AMESEMA JUU YA MAISHA YAKO NA UNATAKIWA KUONA UTHIBITISHO WAKE?

KWENYE
Afya yako
Ndoa yako
Biashara yako
Huduma yako
Familia yako
Kazi zako


CLAIM TODAY… OMBA LIWE HALISI… LITHIBITISHWE… MUNGU ANASIKIA NA YUKO TAYARI… 

“GOD DOES NOTHING EXCEPT IN ANSWER TO PRAYER” - John Wesley

MUNGU ATHIBITISHE NENO LAKE ALILOLISEMA KATIKA MAISHA YETU KUPITIA NENO LAKE… 


Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017