Pages

Thursday, December 20, 2012

Amini kwamba wengine wanaweza


Kutoka katika Meza ya Rejoice and Rejoice blog ...........



Mara nyingi watu wenye nyadhifa au majukumu mbalimbali katika makanisa,majumbani,ofisini,vyuoni,au mashuleni huwa wanakuwa na shida moja ya kutowaamini watu wengine na majukumu wanayoyafanya.

Kama nyumbani utakuta baba au mama anashidwa kuwaamini vijana wake wakubwa tu kwamba wanaweza kupewa jukumu Fulani na kufanya bila tatizo,tena mara nyingine wanaweza kufanya vizuri ya wazazi wao.

Sasa hii inamfanya mzazi awe anajichosha sana na majukumu mengi,utakuta sehemu ambayo alitakiwa amtume kijana wake anaenda yeye tena anakuwa ameacha kazi zake za maana sana.

Kuna kijana mmoja alikuwa analalamika kwamba baba yake haruhusu mtu yoyote aguse gari yake kabisaaaaaa yani it is strictly prohibited,sasa nikajiuliza sasa kwa mfano siku moja huyo baba amebaki nyumbani na kijana wake peke yao halafu from nowhere baba akapata shida au ugonjwa ambao anahitaji mtu  amkimbize hospital je atakodi Tax au watapanda daladala? Sisemi kwamba wazazi wawe Laissez-faire kwa watoto wao la hasha,lazima kuwe na taratibu lakini nyumba isije ikageuzwa kuwa kambi ya Jeshi jamani.

Mara nyingine vijana wanalalamika kwamba wazazi wanashindwa kuwaamini hata wanavyokuwa wanapanga mipango mbalimbali ya familia,au kama katika familia kuna sherehe Fulani baba anataka afanye yeye kila kitu maana anaona vijana wake hawawezi,sasa matokeo yake anaweza kuweka vitu ambavyo enzi zao ndio vilikuwa vizuri lakini kwa kipindi hiki labda jamii haivikubali sana,sasa hapo ndio mahusiano na watoto yanakuwa yakuburuzana,na watoto wanakususia maana wanajua hawaaminiki,halafu mzazi unajizidishia stress maana umri nao uliofika hutakiwa kujichosha sana na mambo madogo madogo,jamani wazazi wenzangu tumuombe Mungu atusaidie tuwaamini watoto wetu na tuwawezeshe kufanya majukumu mbalimbali ili na sisi tuweze kujikita katika mambo mazito zaidi,Amen!

Tabia hii pia iko makanisani,unakuta mchungaji anashindwa kuwaamini wasaidizi wake,sasa kila siku yeye ndio anaongoza sifa,maombi,anahubiri yeye,anabatiza yeye,yaaani ni yeye siku nzima,sasa mwanadamu ana tabia ya kuboreka,ni vizuri kuwaamini kwamba watu wa chini yangu nao wameumbwa na Mungu huyuhuyu aliyeniumba mimi,kwahiyo wanaweza wazungu wanasema Trust them…na kukiwa na watu tofauti tofauti wanafanya vitu mbalimbali kanisani kunakuwa na taste nzuri maana unakuwa umegusa makundi karibu yote.

Wamama pia tuna tabia hiyo kutowaamini watu tunaoishi nao kama wanaweza,matokeo yake mama analisha familia yake chakula saa 6 za usiku maaana ilibidi wasipike mpaka atoke kwenye shughuli zake usiku,amini na wafundishe jinsi unavyopenda ili ukichelewa waendelee watu wale ontime na kupumzika,Halleluyaaaaaaaa

Maofisini ndio usiseme,kama wewe ni Boss una wafanyakazi wako hebu waamini kama wanaweza maana wamesoma na wanajifunza kama wewe ulivyojifunza,waamini ili siku ukiwa haupo kazi za watu zisilale mpendwa halafu usiwe na hofu surbodinates wako wakijua kazi zako si lazima sana wachukue hiyo kazi yako Mungu ni mwaminifu atawafungulia mlango au atakufungulia mlango sehemu nyingine,Amen!

Hata kama una duka au chochote wewe amini tu wale wa chini yako wana kitu tofauti na ulicho nacho kwahiyo wanaweza,wawezeshe ili ikipunguzie na wewe kazi ufanye mambo mengine.

 

Faida za kuwaamini wengine kama wanaweza ni kama ifuatavyo:

1.       Inakupa wewe fursa ya kuweka mtazamo wako katika mambo yenye manufaa

2.       Kuwajengea uwezo watu wa chini yako kama watoto,wasaidizi kanisani na wafanyakazi katika ofisi

3.       Inakupa uwezo wa kuongeza ujuzi zaidi katika kile unachofanya pale unapokuwa unamfundhisha mtu na wewe unajifunza

4.       Ukiwaamini watoto,wasaidizi kanisania,watu wa chini yako ofisini inawaamasisha kufanya vizuri zaidi na kuwafanya wajitoe kikamilifu katika kila kazi uliyowapa,Aaaamen!


Kwa leo ndio ujumbe wangu……Kama una laziada maana na mimi sio kama najua kila kitu naomba maoni yako…KARIBU
 

Mungu akubariki sana unapojiandaa na sikukuu zilizo mbele yetu

 

 

No comments:

Post a Comment