Pages

Monday, January 14, 2013

Kutana na Joshua Ngoy Ngoy mwimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania

SANY4121 copy 2.jpg
Joshua Ngoy Ngoy
 
 

Blogger: Naomba majina yako kamili,na je unatumia Jina tofauti la kisanii? Tungependa kulijua pia ili jamii iweze kukutambua kwa urahisi.

Joshua Ngoy Ngoy

Blogger:Umeokoka? na unaabudu wapi

Nimeokoka;Ninaabudu katika Kanisa la Rehoboth Victory Church-Arusha-Mianzini

Blogger: Historia yako kwa Kifupi ya kuimba,yaani ulianzaje na wapi?

Nilianza kuimba tangu nikiwa darasa la tano mkoani Singida kama Kiongozi wa Sifa na mpaka sasa naendelea vizuri kwa uwezo wa Mungu.

joe.jpg


Blogger:Katika kuimba kwako je umeshatoa Album au single yoyote? Itaje ina nyimbo ngapi

Nimeshatoa Album moja na ina nyimbo nane(8) inajulikana kwa jina la BABA NAKUSIFU

Blogger: Wimbo unaoupenda katika nyimbo zako

Napenda nyimbo zote ila zaidi ni 'BABA NAKUSIFU'

Blogger:Ni kwanini unaupenda huo wimbo/nyimbo

Napenda saana kumsifu Mungu kwa mambo mengi alionitendea hasa kwa familia yetu

Blogger:Kuna mafanikio gani umeyapata katika kuimba kwako nyimbo za Injili
Mafanikio niliyopata uimbaji uninisaidia kufahamika kwa haraka sana na nimezunguka Tanzania hii na njeya Tanzania pia nimepata marafiki wengi Waimbaji/Wachungaji na Watumishi mbali mbali,

Blogger:Umekutana na changamoto gani katika safari yako ya kuimba
Changamoto zipo nyingi tu ,unakuta nimealikwa sehemu kwa makubaliano maalum lakini ukifika hapo eneo husika na baada yakumaliza icho ulichoitiwa unaachwa hewani bila kudhaminiwa tena na makubaliano yanavunjwa bila kutarajia

Blogger:Unaonaje Music wa Injili hapa Tanzania?
Kwa kweli Music wa Injili hapa Tanzania kwa sasa uko vizuri tofauti kabisa na kipindi cha nyuma. Unapendwa sana na Watu wa hapa (yaani wazawa) hata nchi jirani pia wameukubali sana Music wa Tanzania.

Blogger:Na Unatoa Ujumbe gani kwa waimbaji wa Nyimbo za Injili ambao kwa njia moja au nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia hii
Maoni yangu ni kwamba wakumbuke kusudi la Mungu kwao maana wengi wanatamani kuwa kama wao lakini hawakupata Neema hiyo kuwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili. Wawe makini maana Biblia inasema tutafute ufalme wa Mungu kwanza na haki yake na mengine yote tutazidishiwa.


Blogger:Zaidi ya kuimba ni kitu gani kingine unachofanya
Mwana chuo         

Blogger:Je kimaisha je uko wapi? Umeoa au Hujaoa bado
Naishi na wazazi. Sijaoa
Blogger:Una Ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa Tanzania
Nawasihi sana tuwe na Umoja/Upendo/Mshikamano pia,tukubali mtu akifanya vizuri apongezwe sio kunafikiana sisi kwa sisi.

Blogger: Una Ujumbe gani kwa Jamii inayoburidishwa na nyimbo za Injili
Nawaomba sana kutusapoti kwa kununua kazi zetu na hata tunapowaita kwa matamasha mbali mbali wasiache kuja kujumuika nasi

Mtumishi wa Mungu Josh Ngoy nakupongeza sana sana kwa Kazi Nzuri ya uimbaji unayoifanya ,Mungu akuinue na kukubariki katika utumishi wako.

Kama wale waohitaji album yake na kumsupport naweza kuwapa contacts zake kwa mawasiliano,tuwainue jamani watumishi hawa wa Mungu.

 

MBARIKIWE SANAAAA

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment