Pages

Monday, March 11, 2013

MOYO WA MWANAMKE 2013:Wanawake wapokea urejesho wa mioyo yao

 
Mchungaji Lilian Ndegi
 Siku tatu za Kongomano la "Moyo wa Mwanamke" linaloongozwa na Mchungaji Lilian Ndegi wa Kanisa la Makuti Kawe lilimalizika siku ya jumapili,huku likiwaacha wanawake wengi wakiwa wamepokea urejesho wa mioyo yao.
Katika Kongomano hilo kulikuwa na walimu mbalimbali wakiongozwa na Mchungaji Lilian Ndegi ambaye ni mbeba maono,Mchungaji Naomi Mhamba na Mchungaji Grace Kapswara kutoka Zimbambwe.

Mchungaji Lilian Ndegi akisisitiza wanawake waamue kubadilika jinsi wanavyoongea,waongea vitu vinavyompa Mungu utukufu

Mchungaji Lilian Ndegi katika maombi
Maombi yakiendelea

Kwakweli kongomano lilikuwa limefunikwa na uvuvio wa Roho Mtakatifu,wanawake waliweza kuhudumia kwa kadri utayari wa moyo wao ulivyokuwa.
Wanawake walijifunza masomo muhimu sana ya kuwajenga na kuwawezesha kusimama katika nafasi zao ambazo Mungu amekusudia wawepo.

Mchungaji Lilian Ndegi akifundisha
 
Wanawake wakisikiliza kwa makini


Wachungaji kutoka Zimbambwe wakitafsiriwa,kutoka kushoto ni Pastor Grace na Katikati ni mume wake Pastor Kapswara

Mchungaji Lilian Ndegi alianza na Somo la "Nguvu ya Maneno ya Kinywa Changu" wanawake walifundisha jinsi kinywa kinavyoweza kujenga au kubomoa,kuua au kuhuisha hali za maisha yao.Alikwenda mbele zaidi akisema kwamba vile ulivyo ni matunda ya unachokiongea,somo lilikuwa refu na mifano na uzoefu na shuhuda kwakweli alifundisha kutoka ndani kabisaa na kweli alitumiwa na Roho Mtakatifu kufikisha ujumbe.Vinywa vyetu wamama kwakweli vilipokea uponyaji katika Jina la Yesu.
Mchungaji Naomi Mhamba

Mwalimu Naomi Mhamba alifundisha somo muhimu sana pia la "Malezi ya Watoto:Watoto Wetu warithi wa Uzazi wetu"yaani ni somo lenye nguvu sana. Maana wanawake tulijifunza jinsi ambavyo tunayo nafasi kubwa ya kuwapeleka watoto na vizazi vyetu katika ahadi Mungu alizowaahidi. Na kwamba watu wengi wamekosea malezi kwasababu wanafanya kwa akili zao wenyewe. Swala la malezi ni la kumkabishi Mungu kwa kuhakikisha kwamba kile kitu cha Ki-Mungu kinakaa ndani ya watoto wetu tangia wakiwa tumboni. Na hata kama mtu hajaolewa anaanza katika ulimwengu wa Roho.Mpendwa somo hili lilitufungua macho sana jinsi ya kumkabili Ibilisi ambaye sasa anatumia technologia kuwateka watoto maana anapitisha mambo mengi katika technologia.Hatutaweza kushindana na watoto lakini tukimkabidhi Mungu tutaweza kuwasaidia wafike katika Hatima yao Mungu aliyowakusudia.

Watu wakipokea urejesho unaweza kujua Blogger sikuwa katika bloggin tu nilipokea portion yangu haswaaaaa

 

Pastor Grace Kapswara na mtafisiri wake mama mchungaji Tina

Kulikuwa na Mchungaji pia kutoka Zimbambwe,Pastor Grace yaani huyu mama alifanya watu wasimame na kujiachilia kwa Mungu bila kujali nani amekaa pembeni yake. Alifundisha habari za Yule mwanamke aliyeandikwa katika Kitabu cha Waamuzi 9:50-53,ambaye alichoshwa na mateso ya Abimeleck alivyokuwa anawatesa watu,akapanga mkakati akaweza kumuua Abimeleck.Mwanamke umepewa nguvu,sio nguvu ya kuharibu mahusiano ya watu,au umbea umepewa Nguvu ya kuleta suluhisho katika jamii yako,taifa lako,na katika familia yako. Usione mambo yanakwenda vibaya ukaanza tu kulalamika unacho cha kufanya mwanamke panga mkakati mwangamize adui anayetesa watu wanaokuzunguka.Na alitoa vitu kadhaa vitakavyokusiadia iliuweze kumwangamiza Abimeleck wako,Upendo,Kujua Neno la Mungu na Maombi.

Pastor Grace alisisitiza sana wanawake kuchoka kuishi maisha yaleyale kila siku,kuwa na maisha ambayo hayana matunda kuamua kuchukua hatua ya kuviondoa vyote vinavyokwamisha kuwa na hatima Mungu aliyotuwekea

Pastor Grace Kapswara,jamani huyu ni mtanzania aliyekulia Zimbabwe kwakweli sijui nisemeje Mungu anamtumia sana huyu mtumishi
Watu wakisiliza neno

Mchungaji Onesmo Ndegi ndie alikuwa mgeni rasmi nayeye aligusia kuhusu Malezi,kwakweli alitupa ukweli sana wanawake na tuliweza kujifunza huku tukicheka sana.Aliongea mambo yanayowaangusha wanawake hadi wanashindwa kusimama katika nafasi zao ambazo Mungu anataka wasimame.Lilikuwa ni somo Zuri sana.Kwakweli Mungu anakwenda kufanya kitu kikubwa sana katika taifa hili maana ukimbadilisha mama umebadilisha Taifa,Halleluyaaa

Zaidi ya Kujifunza pia wanawake walipata nafasi nzuri kumsifu na kumwabudu Mungu.Kulikuwa na waimbaji mbalimbali wa Nyimbo za Injili.

Upendo Nkone akiimba




Madam Ruth naye alikuwepo


Wanawake wakimsifu Bwana na kumwinua na kucheza kwa furaha maana hakika hatima ya Abimeleki imefika,Halleluya

Praise and Worshi Team ya Kawe

Wanawake wa Wafalme wa Kawe


5 comments:

  1. Kwakweli hili Kongomano sijui hata nisemeje mimi...Nakushuru sana Bwana Yesu

    ReplyDelete
  2. Sana mtumishi sana sanaa sana ukitaka kujua limenifanyia nini kutana na Henry

    ReplyDelete
  3. This is because in relationship student loans. The First Step to Generating Your Own MLM
    Network student loans LeadsStart creating and
    publishing videos.

    Also visit my blog post ... Private Student Loans for People

    ReplyDelete