Pages

Wednesday, March 27, 2013

Rev Florian Katunzi:Maombi ya Ulinzi,Mawe Matano ya Ulinzi yenye kuleta Ushindi


Rev Florian Katunzi
Karibuni katika makala haya yanayofundishwa na Mchungaji Florian Katunzi wa Kanisa la EAGT City Centre lililopo katika viwanja vya Sabasaba.

Endelea........
*1Samweli 17: 39-50

*“ Daudi akaichukua fimbo yake mkononi, akajichagulia mawe laini matano katika kijiti cha maji, akayatia katika mfuko wa kichungaji aliokuwa nao, maana ni mkoba wake na kombeo lake alilokuwa nalo mkononi mwake”.
Daudi anamshinda Goliathi, sauli na majeshi yake walishindwa kumpiga Goliathi, maandiko yanathibitisha silaha za daudi ni kama ifuatavyo.

1. Fimbo
2. Mawe matano


- Fimbo kiblia inawakilisha mamlaka katika mfufulizo wa mateso yetu, nataka nikufundishe juu ya mawe matano.Daudi aliyoyaweka  kwenye kifuko chake cha kichungaji kabla ya kumpiga Goliathi, pia kwa nini yawe mawe matano na si sita wala saba. Katika maisha ya kiimani lazima kuwepo msingi wake ndipo mtu wa Mungu anapoweza akajenga anayotaka kujenga.
- Jiwe la kwanza la kumfanya mtu wa Mungu ajijenge ili pate kutokutikisika kama vile Daudi ambavyo  hakuyumba wala kuogopa, maana alijua alicho nacho ndani ya mfuko wake kina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome za adui shetani katika ulimwengu wa roho.

-JIWE LA KWANZA: *NI NENO
*Yohana 1:1-5 * “ Hapo mwanzo kuliwako neno naye neno alikuwako kwa Mungu, naye ni neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu, vyote vilifanyika kwa huyo wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru ya ng’aa gizani, wala giza halikuiweza.”

- Nataka tujifunze na tuione jinsi ambavyo jiwe hili la kwanza ambalo ni NENO lilivyo na nguvu ya kuangusha kila silaha za adui, hivyo ushindi wa Daudi ulitegemea mawe matano kuwa ndani ya mfuko wake, pasipo NENO hakuna kilichofanyika wala kitachofanyika katika maisha yetu ya kiimani. NENO la Mungu linaleta uzima kwake yeye atayeliamini , kabla ya yote palikuwapo  NENO na yote yakawepo tunayoyaona ya mbinguni na duniani.

- A.  NENO LINAUMBA.* Zaburi 33 : 6 – 9 “Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake maana yeye alisema ikawa nay eye aliamuru ikasimama.”

* Waibrania 11: 3 “ Kwa Imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa Neno la Mungu, hata vitu vinayoonekana, havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.”

-Lazima mtu wa Mungu ufahamu kabisa pasipo kulishika Neno, kulitimiza Neno, kulikamata Neno na kulitii Neno la Mungu uto weza kushinda vita vya kiroho wala kuziona baraka za Mungu zilizomo katika Neno lake, kabla ya mambo yote kwanza ujue neno la Mungu.

-B. NENO HUTAKASA.* Yohana 15 : 3 “ Ninyi mmekuwa safi kwasababu ya Neno nililowaambia.”

- C.  NENO LA MUNGU NI TAA YA TUMAINI. * Zaburi 119: 105 “ Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu.”
-D. NENO NI NURU.  Kwa yeyote atakayelishika hatawenda gizani, * Zaburi 119:130 “Kufafannusha maneno yako kwatia nuru, na kumfahamisha mjinga.”

-E. NENO LA MUNGU NI UPANGA WA ROHO * Waefeso 6:17 “ Tena ipokeeni chepeo ya wakovu na upanga wa roho ambao ni neno la Mungu”

Upanga wa Roho ni silaha ya muumini (mkristo) ambayo anapaswa kuitumia kwenye vita vya kiroho dhidi ya silaha za uovu za shetani. Lakini pia ujasiri wetu humo katika neno tunaona Yesu kristo alivyotumia upanga wa roho kumshinda shetani. Hili ni jiwe la muhimu sana katika maisha ya watu waliokoka yaliyojaa vita.

Ukisoma katika kitabu cha Luka 4:1-13, utaona pamoja na kuwa Yesu alikuwa amejaa Roho Mtakatifu bado shetani alimjaribu kwa kupanga vita mbele yake kwa kutumia jiwe la neno na Yesu pia alitumia jiwe hilohilo kumnshinda shetani.

Hivyo kama mkristo aliyeokoka anapaswa kuwa makini na maneno yote yanayokuwa yanatamkwa kinyume  dhidi yake kwa kuyabatilisha au kuyatengua kwa jina la Yesu. Ukiangalia kwa undani zaidi utagundua kuwa wakristo wengi wananaswa na mitego ya shetani kwa kutokujua neno la Mungu na uweza wake.

1Samweli 17:1-58, inaonesha kuwa wakati Sauli anamwambia Daudi kuwa hawezi kumshinda Goriathi kwasababu ni mtu wa vita tangu siku nyingi, katika hali halisi ya nje Daudi asingeweza kupigana na Goliathi lakini Daudi alijua neno la Mungu na ndilo lililomsaidia.

Yoshua 1:5, “Hapatakuwa na mtu yoyote atakayeweza kusimama mbele yako, siku zote za maisha yako kama nilivyokuwa na Musa ndivyo nikatavyokuwa pamoja na wewe, sitapungukia wala sitakuacha”

Wakati mfalme anatetemekea na kuangalia ukuu wa Goliathi, Daudi yeye anaangalia ukuu wake Yehova mwenye nguvu. Lakini pia wakati watu wanatazama mapungufu ya mwanadamu Mungu yeye hutazama uwezo wake mwanadamu huyo katika kumtumikia.

Wafilipi 4:13, “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”

2Wakoritho 10:3-4, “Maana ingawa tunaenenda katika mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili , maana silaha za vita vyetu si za mwili bali zinauwezo katika Mungu hata kuangusha ngome”

F. NENO LA MUNGU NI HAI TENA LINA NGUVU KATIKA MUNGU.
Waebrania 4;12-13, “ Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu , tena lina ukali kuliko upanga likatalo kuwili , tena linachoma kuzigawanya nafsi na Roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake , tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake; lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”
Tunajifunza kuwa neno la Mungu ni muhimu sana hasa katika imani na hata tunapoomba maombi ya ulinzi lazima kwanza mtu ajue neno la Mungu. Mwanafunzi mzuri wa Yesu Kristo lazima akae katika neno la Mungu.
Yohana 8:31-32, “ Ninyi mkikaa katika neno la Mungu mmekuwa wanafunzi wangu kwelikweli tena mtaifahamu kweli itawaweka huru”
Kweli ya Mungu imo ndani ya neno lake , lakini wakristo wengi wa leo wanadanganywa na watu wanaotumia mapepo ya utambuzi au roho za utambuzi wakidhani ni manabii.Hali hii inapelekea kanisa kudanganywa katika kiwango kikubwa.
Habari za mapepo ya uaguzi zinapatikana katika kitabu cha 1samweli 28:4-25, ambapo inaonyesha jinsi mfalme Sauli alipoacha kushika neno na kulifuata , akaanza kufuata njia za uganga maana Mungu hakuwa amemjibu maombi yake.  Ukiendelea kusoma utagundua jinsi nguvu ya utambuzi  ilivyomsaidia mfalme Sauli kupata majibu aliyoyataka maana shetani alijigeuza kuwa malaika wa nuru.
Wakristo wengi wametekwa na Roho zidanganyazo ili mradi wameelezwa habari zao za siri ambazo hata hizo zinafanyika v ilevile kwa waganga wa kienyeji.
Kumbukumbu 12:1-11, katika sura hii biblia inaelezea kwa ndani zaidi kuzuka kwa manabii wengi wa uongo na waotaji ndoto , wakitolea ishara ya mambo yajayo. Hivyo wakristo wanapaswa kuwa na misimamo na kuacha kushawishika na hao waota ndoto na ishara zao kwani jambo ambalo lin aweza kuleta mahusiano mazuri baina ya Mungu na mwanadamu si katika ishara na maajabu.
1Yohana 4:1, “ Wapenzi msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho , kwamba zimetokana na Mungu kwasababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”
Watu wa namna hii wanaweza wakazungumza katika upako wa kipepo na ukadhani ni wa kimungu , watatabiri kwa usahihi mambo yajayo  na kutenda miujiza na maajabu yakatenda, maandiko hayajasema hawatatenda (ishara) Yesu kristo anasema;

Mathayo 24:11, “na manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi”
Marko 13: 22, “ Kwa maana wataondoka makristo wengi wa uongo , na manabii wa uongo watatoa ishara na maajabu wapate kuwadanganya kama yamkini hata wao wateule”
Yesu kristo analionya kanisa  kuwa macho na wapotoshaji wa kweli ya Mungu. Na kulitahadharisha kuwa pasipo kujua kweli ya Mungu waklristo wengi watanaswa na roho hizi zipotoshazo.
Mathayo  7:15-17”Jiadhari na manabii wa uongo , watu wanaowajia wavaa mavazi ya kondoo walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali. Mtawatambua kwa matendo yao , Je, watu huchuma dhabibu katika miiba  au tini katika mibamiti vivyo hivyo mti mwem ahuzaa matunda mazuri na mti mwovu huzaa matunda mabaya”.
Yesu anasema wazi kuwa pasipo kujua neno basi itakuwa ngumu sana kwa mkristo kuzishinda hila za mwovu shetani. Anaongeza kwa kuonya kuwa,
Mathayo 7:21-23, “Si kila aniambiaye BWANABWANA atakanyaga katika ufalme wa mbinguni bali yeye afanyaye mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni wengi wataniambia siku ile BWANABWANA hatukufanya unabii kwa jina lako , kutoa pepo kwa jina lako, kufanya miujiza mingi kwa jina lako, ndipo nitawaaambia dhahiri sikuwajua ninyi kamwe , ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu”
Wakisto wengi katika maisha ya sasa wamekuwa wakipenda zaidi miujiza na hata kupelekea kukimbilia katika ibada za watu wafanyao miujiza, hata hivyo bado maisha ya wakristo wengi ni machafu kwani mlevi,mzinzi,mchawi, na hata wavaa hirizi nao pia wanataka miujiza. Lakini ukweli ni kuwa hakuna muujiza kwa mtu ambaye ameambatana na uovu katika maisha yake.

Zaburi 103: 3-5, “Akusamehe maovu yako, akuponya magonjwa yako yote, atakomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhili na rehema, akushibisha mema uzee na maisha yako yote.

Mambo haya yote yatakuwea juu ya mwanadamu pindi atakapotubu dhambi na kuziacha.

Isaya 3:10-11, “ Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maaana watakula matunda ya matendo yao. Ole wake mtu mbaya , shari itakuwa kwake kwa maana atapewa ijara ya mikono yake”

Dhambi ni kikwazo kikuukwa mtu yoyote ambaye anahitaji msaada wa kimungu ndio maana wapo wakristo wengi ambao wanashida mbalimbali na wanazunguka katika makanisa mbalimbali wakitafuta maombezi lakini hawafunguliwi kutokana na mizigo ya dhambi waliyonayo.

Kutii neno kwafaa sana maana huondoa magonjwa na vifungo mbalimbali ambapo katika neno la uponyaji na ulinzi Kutoka 23:22-26, “ Lakini ukilisikiza sauti yake kweli na kuyatenda yote ninenayo mimi, ndipo mimi na mtesi wa hao wakutosao kwa kuwa malaika wangu atakutangulia mbele yako, nanyi mtamtumikia Bwana Mungu wenu , naye atawabarikia chakula chako  na maji yako, nami nitakuondolea ugonjwa kati yako, hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba wala aliye tasa katika nchi yako na hesabu ya siku zako zitazitimiza”

Kutii neno pia kunaleta ulizi na baraka Matendo 28:1-14

Pasipo kutii neno la Mungu hauwezi kubarikiwa  Mithali 12:11, “ Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele bali afuataye mambo ya upuuzi hana ufahamu”

Mitahali 10:14, “ Atendaye mambo kwa mkono legevu huwa masikini, bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha”

Mithali 19:15, “ Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito na nafsi yake mvivu itaona njaa”

Mithali 20:13, “ Usipende usingizi usije ukawa masikini”

Kimsingi umasikini hauwezi kuondoka kwa maombi peke yake bali kwa kujituma kwa bidii sambamba na kulifuata neno.

No comments:

Post a Comment