Pages

Tuesday, April 23, 2013

Mjue Frida Brown muimbaji wa Nyimbo za Injili anayechipukia Tanzania


Frida Brown Muimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania
 
Blogger: Naomba majina yako kamili,na je unatumia Jina tofauti la kisanii? Tungependa kulijua pia ili jamii iweze kukutambua kwa urahisi.

Naitwa FRIDA BROWN LEKEY, lakini huwa napenda kutumia majina mawili ya kwanza yaani FRIDA BROWN

Blogger:Umeokoka na unaabudu wapi

Nimeokoka, Yesu ni Bwana katika maisha yangu..Naabudu Kanisa la Imani Hai (a.k.a Winners Chapel) Ukonga – Banana, Dar es salaam

Blogger: Historia yako kwa Kifupi ya kuimba,yaani ulianzaje na wapi?

Nimeanza kuimba tangu Sunday School pale Kurasini Lutheran Church, Then nimeendelea hivyo nikiwa Ukwata (A-Level), Praise team pale Chuo cha Uhasibu Arusha. Na mara nyingi nikiwa nyumbani, Kazini uwa napenda sana kuimba.

Blogger:Katika kuimba kwako je umeshatoa Album au single yoyote? Itaje ina nyimbo ngapi?

Naamshukuru Mungu kwakunifanikisha kutoa Album ya kwanza katika kuimba kwangu yenye nyimbo nane(8). Jina la Album ni TEMBEA NA YESU


Blogger:Amen Hongera sana Frida, ni wimbo gani unaoupenda katika nyimbo zako?

Mmh nazipenda nyimbo zote kwakweli,. zaidi sana Eligibo Mungu Mwenye Nguvu..

Blogger:Ni kwanini unaupenda huo wimbo/nyimbo

Eligibo ni wimbo unaoeleza Majina ya Mungu kwa Lugha ya biblia na maana zake,.Ni wimbo wakuabudu na ninapoimba unanisogeza karibu na uwepo wa Mungu. Hakika Mungu wetu ni Eligibo

Blogger: Nani anasambaza kazi zako? Je anakusaidia vizuri?

 Kwasasa sina msambazaji, nauza CD mwenyewe ila nafikiria kutafuta msambazaji wa hii kazi

Blogger: Kuna mafanikio gani umeyapata katika kuimba kwako nyimbo za Injili

Mmh mafanikio yapo ndani ya Roho yangu na Maisha yangu ya Wokovu.. Album hii imekuwa mlinzi wa Maisha yangu kwamaana inanikumbusha ‘’Usiwahubirie wengine alafu wewe ukakataliwa’’. Kwakifupi inanifanya nisonge mbele

Blogger: Umekutana na changamoto gani katika safari yako ya kuimba

Changamoto kwakweli zipo unapopiga hatua yoyote ya mafanikio maishani lakini kwa upande wangu Kibali cha Mungu kilinifunika toka nimeanza kurecord mpaka sasa,kwakweli namshangaa sana Mungu wangu..To him be all thy Glory

Blogger: Amen, Unaonaje Music wa Injili hapa Tanzania?

Kwakweli Umekuwa sana kwa maana yakuwa na wasikilizaji wengi.

Blogger:Na Unatoa Ujumbe gani kwa waimbaji wa Nyimbo za Injili ambao kwa njia moja au nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia hii

Kila muimbaji aifanye Album yake kama Mlinzi wake kwamaana yakufananisha anachoimba na matendo yake. Mwisho wasiku Nimaombi yangu Mungu atusaidie sana kutenda sawasawa na Neno lake.

Blogger: Zaidi ya kuimba ni kitu gani kingine unachofanya

Nimeajiriwa kama Mhasibu katika kampuni ya Mtu Binafsi.

Blogger: Hongera sana Frida,kumbe unaweza kumtumikia Mungu hata kama unafanya kazi,unafundisha jamii kitu hapa maana wengine wanatingwa na kazi tu hawafanyi chochote kwa ajili ya Mungu,enhee tuendelee…Je kimaisha je uko wapi? Umeolewa au bado? Watoto wangapi?

Naishi Mikocheni B - Dar es salaam, Sijaolewa

Blogger: Una Ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa Tanzania

Tuombeane, na kila mmoja awiwe ndani yake kumsaidia, Kumwinua mwingine kwa namna moja au nyingine. Uimbaji wetu sisi sio wamashindano bali ni katika kuujenga mwili wa Kristo hivyo basi Tufanye uimbaji Huduma na si vinginevyo

Blogger: Amina,Una Ujumbe gani kwa Jamii inayoburidishwa na nyimbo za Injili

Kwakweli nawashauri wasiwe wasikilizaji wa Nyimbo tu bali watendaji wa jumbe mbalimbali wanazozisikia.

 

Blogger:Asante sana kwa Muda wako,Mungu akubariki na kukuinua unavyoendelea kumtumikia kwa uaminifu.Amen

 

Ukihitaji CD ya Frida Brown,tuwasiliane nitaweza kukupa mawasiliano yake.

 

20 comments:

  1. To God be all thy Glory....Congratulation Frida,.MUNGU wa mbinguni akuinue zaidi na zaidi,.

    ReplyDelete
  2. Nimependa sana majibu ya mtumishi huyu. Mungu azidi kumtumia kwa unyenyekevu sawa na majibu yake. MUNGU AKUBARIKI FRIDA.

    ReplyDelete
  3. Nilivyoisikiliza CD yako na wewe alivyo ni jambo ambalo mungu amekutendea maajabu katika uimbaji wako.Uokovu wako usirudi nyuma "hongera sana Frida mungu aendelee kukuongoza na kukubariki Amina"

    ReplyDelete
  4. Ubarikiwe sana mdogo wangu mungu aendelee kukupa upako wa kipaji hicho cha uimbaji... by GEORGE.

    ReplyDelete
  5. Hongera sana mwanangu!
    Maneno yamejaa hekima.
    Mungu akuongoze daima.
    Mungu wa Oyedepo na akutunuku kibali.
    Charls

    ReplyDelete
  6. Hongera dada yangu mungu azidi kukuinua ubariwe sana by Haika Lekey

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ameeen Mdogo wangu... kwa MUNGU kila kitu kinawezekana...

      Delete
  7. Mungu awabariki wote...Aminaaa Pst.Charls,. nitazidi kunyenyekea kwa yeye aliyeianzisha safari hii nikijua atanikweza kwa wakati wake, Tuzidi kuombeana tu....by Frida Brown

    ReplyDelete
  8. Yani sitaacha kusema kila nipatapo nafasi..Frida album yako inanibariki sana. Yani ndo CD yangu kwenye gari na mara nyingine huwa natamani hata nisimame humo ndani na mara nyingine napiga hata makofi. Kwakweli ubarikiwe sana na Mungu azidi kukuinua. Colle

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana dada yangu Colle..namshukuru Mungu sana kwa muujiza huu,.Endelea kuniombea Mungu azidi kunitumia kama apendavyo kwa utukufu wake..

      Delete
  9. Hongera sana Frida mungu akubariki by Dorothy UK

    ReplyDelete
  10. Hongera sana Frida mungu akubariki by Dorothy UK

    ReplyDelete
  11. Hongera sana Frida mungu akubariki by Dorothy UK

    ReplyDelete
  12. HONGERA sana my dear.. CD yako nzuri sana imenibariki...Mungu azidi kukuinua.
    its me MARIEDO

    ReplyDelete
    Replies
    1. Thx sanaa mdada..Glory to GOD

      Delete
  13. Hongera sana Frida, Nyimbo zina mafundisho mazuri sana. Mungu akuzidishie neena kwa kazi nzuri unayofanya.

    J.P.

    ReplyDelete
  14. An unexpected blessing
    is always the best gift!
    Congratulations
    by fa2 MDC

    ReplyDelete
  15. UPENDO UWE NGAO YAKO!!
    MUNGU AKUSIMAMIE MDADA,
    NAFARIJIKA MNO,NAOMBA CD 15 IJUMAA
    BEI YAKE NI SHILINGI NGAPI?
    MAMA BONY (FTR)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni shilling 5,000 tu mama Bony,.my No 0715 889271 psee ni sms.. Mungu akubariki

      Delete