Pages

Friday, June 21, 2013

Ambele Chapanyota amewataka waimbaji wa Nyimbo za Injili nchini Tanzania kusimama katika msimamo wa Neno la Mungu


Ambele Chapanyota muimbaji wa Nyimbo za Injili anayevuma na wimbo wa Salama Kwa Yesu
 
Ambele Chapanyota  mwimbaji wa Nyimbo za Injili ambaye anavuma kwa wimbo wa Salama Kwa Yesu amewataka waimbaji wa Nyimbo za Injili kusimama katika msimamo wa Neno la Mungu.

Maneno hayo aliyasema Ambele katika mahojiano aliyoyafanya na Rejoice and Rejoice blog,alipoulizwa anaonaje uimbaji wa Nyimbo za Injili hapa nchini Tanzania.

Ambele Chapanyota amesikika sana kupitia albamu yake ya kwanza ya Salama kwa Yesu ambayo ina nyimbo nane ambazo ni;


          Salama

          Yesu ndie Baraka

          Nakushuru Mungu

          Unaweza Yesu

          Nitakuabudu Bwana

          Nakupenda Yesu

          Wewe ni Mungu wangu

          Baba Mungu

 
Kwasasa Ambele ana Album mbili,zote zimetoka  ya pili imebeba jina la Kubali Matokeo yenye nyimbo nane ambayo ni mpya.

Ziko katika video na audio,
 

Yeye anabarikiwa sana na wimbo wa Salama kwa Yesu,nikiimba unagusa watu na unanigusa sana mimi mwenyewe.

Ambele amesema kwamba uimbaji wa Nyimbo za Injili umebadilika sana hapa karibuni na wengi wameufanya  wa kibiashara zaidi tofauti na jinsi Mungu alivyokusudia.

Katika nchi zingine uimbaji wa Injili uko katika Worship na Praise, na ndio maana unakuwa unabadilisha watu na hiyo ndio maana halisi ya kuwepo kwa uimbaji wa Injili.

Amewataka waimbaji wa Injili Kusimama katika msimamo wa neno la Mungu,tusiyumbishwe na dunia maana sisi ni wahubiri,tufanye kile Mungu anachotuitia.Tukifanya kitu kizuri jamii itabadilika.

Pia amewataka waimbaji tuwe wabunifu na kufanya kazi  katika ubora.

Zaidi ya kuimba ni mfanyakazi wa Manispaa Mbeya,anampango wa kufungua bucha na pia ni mwinjilisti.

Ambele anaabudu katika kanisa la Mito ya Baraka akiwa Dar es Salaam na akiwa Mbeya ni EAGT Sabasaba.

 

 

No comments:

Post a Comment