Pages

Tuesday, August 13, 2013

Mkutano Mkubwa wa Injili Dar es Salaam na Mwinjilisti wa Kimataifa Reinhard Bonnke

Mwinjilisti wa Kimataifa Reinhard Bonnke
 
 
Mwinjilisti wa Kimataifa Reinhard Bonnke anategemewa kufanya mkutano mkubwa wa Injili jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Mkutano huo umeandaliwa na umoja wa makanisa ya Kipentekoste Dar es Salaam.

Mkutano huo utafanyika kuanzia tarehe 21 hadi 25 mwezi wa nane 2013.

Mkutano huo mkubwa wa Injili utafanyika  Katika Viwanja vilivyo nyuma ya Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam, wilaya ya Temeke.

Mwinjilisti Reinhard Bonnke kwa kifupi ni muasisi wa shirika la kihuduma la kimataifa lijulikanalo kwa jina la Christ for All Nation (CfAN) na anajulikana kuwa mwinjilisti aliyejitoa sana kwa kazi ya Uinjilisti na Umisheni katika bara la Afrika.


Unakaribishwa sana katika mkutano,walete wenye shida mbalimbali.



MUNGU AKUBARIKI NA AKUTANE NA HAJA YA MOYO WAKO! Amen

No comments:

Post a Comment