Pages

Thursday, September 26, 2013

John Lisu kufanya Tamasha Kubwa la Kusifu na Kuabudu na DVD Live Recording ya "Uko Hapa"



Live recording ya DVD ya UKO HAPA (Albamu) ya mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Tanzania John Lisu inategemewa kufanyika tarehe 6 October 2013.


Tukio hilo litakuwa ni Tamasha la Sifa na Kuabudu ambalo litakuwa la tofauti kabisa na matamasha yote ya John Lisu ambayo umewahi kuhudhuria na si tamasha tu bali ni ibada ya kumwita Mungu na kila mmoja ategemee kukutana na Mungu siku hiyo.

Tamasha hilo litafanyika katika ukumbi wa Kanisa la CCC UPANGA ( Opposite Mzumbe University) .

Linategemewa kusindikizwa na waimbaji mbalimbali kama vile Christina Shusho, Neema Gospel Choir, Paul Clement, Bomby Jonson, Pastor Safari na wengine wengi.

Kiingilio cha 20,000/= VIP, 10,000/= KAWAIDA na 3,000/=WATOTO

Usipange kukosa na Mungu Akubariki

 

No comments:

Post a Comment