Pages

Wednesday, September 4, 2013

Uchumba hadi Ndoa: Mjadili mngependa kuwa na watoto wangapi




Karibu Katika Somo letu la Uchumba hadi Ndoa, katika mtiririko wa vitu muhimu vya kuangalia unapojiandaa kuwa na mwezi wako wa maisha. Leo tutaangalia jambo ambalo ni muhimu japo watu wengine wanaweza kulisahau halafu baadae linakuja kuleta matatizo.

Mnapokuwa katika kipindi cha uchumba ni vizuri mkazungumza idadi ya watoto ambao mtapenda kuwa nao katika ndoa yenu, najua mtu anaweza kusema kama je hatutapata watoto? Au unampangia Mungu? Haya ni maswala ya Imani lazima twende kwa Imani hivyohivyo maana kwanza sio wachumba wote lazima waje waoane kwa hiyo kama mnavyokuwa katika Imani kwamba mtafunga ndoa ndivyo hivyohivyo mnatakiwa kumwamini Mungu kwamba atawabariki na watoto.

Kubalianeni idadi maana isije ikawa mwingine labda hataki mtoto kabisa na mwenzi wake anataka watoto watano sasa hapo unafikiri wakifunga ndoa itakuwaje huko ndani. Nilishapata ushuhuda kuna mkaka alikuwa anataka watoto wanne lakini mwenzi wake alikuwa anataka aolewe na mtu ambaye wataishi bila kuwa na mtoto. Kwasababu walijadili kabla ya ndoa na kila mtu akajua mahitaji ya mwenzake kwenye jambo hilo, ilibidi wazungumze na kushauriana na mwisho wakakubaliana namba fulani. Hebu fikiria wasingejadili ingekuwaje mtu wa Mungu.

Mungu akusaidie uweze kufanya maamuzi sahihi maana kwakweli bora tu uchumba uvunjike lakini sio ndoa maana ndoa zetu sisi tunajua ni za milele ni Kifo tu kinazitenganisha.

 

Endelea Kutembelea Rejoice and Rejoice, Mambo mazuri yanakuja yatakuinua, kukubariki na kubadilisha kabisa maisha yako najua kuna mahali tunaelekea, Amen


2 comments:

  1. Habari, nimelipenda sana somo lako. Limenibariki na linanhusu sana kwakua niko kwenye uchumba natarajia kuingia kwenye ndoa mwishoni mwa mwezi wa kumi.

    Naomba kuuliza maswali yafuatayo kwa faida ya wengi:

    1. Kuna njia gani salama za kupanga uzazi zinazoshauriwa kwa watu tuliookoka?
    2. Je ni sawa wanandoa kupanga kwa imani juu ya jinsia za watoto jinsi wanavyotaka? Je kuna hatua gani za vitendo kuitimiza imani yao? Nauliza hivi kwasababu nimesikia kuna uwezekano wanandoa kuamua wapate mtoto wa kike au kiume.
    3. Je ni umri gani unashauriwa watoto kupishana ili kuzingatia afya yao na ya mama yao?

    Asante, ni hayo tu kwa sasa.

    Mbarikiwa.

    ReplyDelete
  2. Asante sana kwa Feedback, Karibu sana Rejoice and Rejoice
    Maswali yako:
    1.Njia Salama ni Calender,pia kuna mtumishi alinipa ushuhuda alimuomba Mungu kwa kumshukuru kwamba basi na kweli ikaishia hapo.

    2. Kwa mtazamo wangu ndio neno linasema tupeleke haja zetu lakini usije ukamsimamia kidete Mungu kwamba lazima wakwanza wa Kike wa pili Kiume,acha tu Mungu atake control usiwe mwilini sana na amini aina yoyote ya mtoto atakayokupa ni Baraka, mimi nina watatu wote wa kike na baba yao ni Rafiki yao Mkubwa.

    3. Hapo kwakweli naweza kusema inategemea na malengo yenu na uwezo wenu wa afya na kimaisha. Maana wengine wanakubaliana kuwa na gap la miaka mitano, wengine mwaka tu, siku hizi naona kama kupishana kumekuwa kufupi zaidi sijui nini kinatokea ila inasaidia maana uanwakuza kwa pamoja nasema hivyo maana na mimi nimo katika mkondo huo, wengine wanapishanisha sana wanaona ndio inawabariki kubalianeni mnataka ipi na Dr atawashauri jinsi ya kuhandle.
    KARIBU SANA NAKUTAKIA HARUSI NJEMA YENYE BARAKA TELE

    ReplyDelete