Pages

Wednesday, April 9, 2014

Nilichojifunza kuelekea Maadhimisho ya Miaka 75 ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God(TAG)


Kanisa la Tanzania Assemblies of God liko katika maandalizi ya kusherekea miaka 75 tangia kuanzishwa kwake. Kanisa hilo lilianzishwa mwaka 1939 na Mmishenari aitwaye Paul Deer ambaye alitokea katika uamsho wa Kipentekoste wa Azusa uliotokea kule Los Angeles, California nchini Marekani miaka ya 1906 hadi 1915.


Askofu Emmanuel Lazaro, Askofu wa Kwanza wa Kanisa la TAG


Paul Deer alifikia mkoani Mbeya ndipo akaanzisha Kanisa la TAG akishiriakiana na watu wengine.

Maadhimisho hayo yamesaidia tukaweza kujua mambo muhimu sana ambayo Wakristo wenzetu waliyafanya ili kuhakikisha kanisa linakuwepo na kuenea duniani.

Jambo kumbwa sana lililonifanya nijifikirie mara mbilimbili juu ya maisha yangu ya Ukristo ni jinsi wamishenari hao walivyotembea miles 120 ili tu kuhakikisha sehemu mbalimbali za Afrika zinapata Injili ya Kweli ya Yesu Kristo.
 
Askofu Dr Barnabas Mtokambali, Askofu Mkuu wa sasa wa Kanisa la TAG

Sasa nikiangalia kizazi cha sasa tulivyozoea kupanda bajaji, pikipiki na tax katika umbali mfupi ilimradi tu tusitembee maana ni wavivu watoto wa dotcom, je kweli tunaweze kutembea mpaka Tandahimba kupeleka Injili ya Yesu Kristo? Kwani hao waliotutangulia walisukumwa na nini hasa? Na sisi tutafanyaje basi ndugu yangu ili tuweze kuacha historia ya Injili hapa duniani.

Tujue kwamba kule Mbinguni kutakuwa na taji je kwa unavyojiangalia utavikwa taji kwa jambo gani hasa ulilolifanya la KUJITOA HASWAA kwa ajili ya Injili………….Tujichunguze na kumuomba Mungu atusaidie ni wapi anataka tumtumikie ili na sisi tubaki katika Historia kwamba tulifanya a,b,c kwa ajili ya Injili.

Kwa kifupi Maadhimisho yatafikia Kilele mwezi wa saba kule Mbeya.

 

Endelea kutembelea Rejoice and Rejoice Blog mambo mazuri yanakuja

 

Ubarikiwe na Bwana Yesu Kristo, Amen

No comments:

Post a Comment