Pages

Monday, May 19, 2014

Kongomano la Mwanamke wa Thamani lawa Baraka kwa Wanawake wa Moshi


Kongomano la Mwanamke wa Thamani lililofanyika Moshi mjini, lilimalizika wiki iliyopita likiwaacha wanawake wengi wakiwa wamepata maarifa ya Neno la Mungu na kufunguliwa.


Pastor Neema Shoo mwandaaji wa Kongomano la Mwanamke wa Thamani akifungua rasmi Kongomano hilo
Upendo Kilahiro alikuwepo akimsifu na kumwabudu Bwana Yesu

Watu wakisifu na Kuabudu
 
 
Kongomano hilo liliandaliwa na Pastor Neema Shoo ambaye alifungua na utangulizi kutoka  Mithali 31:1 alisema mwanamke au mke mwema nani awezaye kumuona nikaonyesha kipo kitu ndani ya mwanamke ambacho ni cha thamani 

Mambo manne yaliyofichika ndani ya Mwanamke             

1. Hekima Ayubu 28:18b naam Kima cha Hekima chapita marijani, Kama hekima inapita marijani basi na Mithali 31:1 inasema mwanamke mwema uthamani wake unapita marijani basi hicho cha thamani ndani ya mwanamke ni Hekima       Mithali 14:1 inaonyesha ukiwa na hekima unajenga nyumba yako bali mpumbavu anaibomoa                                                                   

2. Ufahamu kilichofichika ndani ya mwanamke ni ufahamu Ufahamu ni uwezo wa kupambanua jema/baya.  Ufahamu ni Akili Mwanamke mpumbavu asiye na akili hubomoa nyumba kwa mikono yake ukiwa na Akili utajenga utajua nini nifanye wapi na saa ngapi kwalugha nyepesi Utajitambua.                                         



Pastor Neema akitambulisha Mchungaji wake na Baba na Mama wa kiroho Pastor Dickson Mtalitinya na Mke wake pia alifundish​a

 
3. Adabu Mithali 11:16 Mwanamke wa Adabu hueshimiwa daima mwanamke ukiwa na adabu/ tabia njema utapata heshima kwa wakubwa na wadogo tabia njema ktk kuongea kukaa kwetu majumbani mwetu, Takwimu zinaonyesha wanawake kwasiku tunaongea maneno meeengi kuliko wanaume unaongea nini je ni umbea, magomvi, kuvunja nyumba za watu? Lazima tuwe na Adabu tuache kua na maneno ya kuumiza natuache tabia mbaya Mungu tusaidie.

Biblia inasema katika 1 Petro 3:1-6

“Kadhalika ninyi wake, jinyenyekezeni chini ya waume zenu, ili kama wako wasioliamini neno, wapate kuamini kwa kuvutiwa na mwenendo wa wake zao. Hawatahitaji kuambiwa neno 2 kwa sababu wataona maisha yenu safi na ya kumcha Mungu.

3 Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje, yaani: kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu na kuvaa mavazi maridadi. 4 Bali kujipamba kwenu kuwe katika utu wa ndani wa moyoni, kwa uzuri usioharibika, wa roho ya upole na utulivu. Uzuri wa namna hii ni wa thamani sana mbele za Mungu. 5 Maana ndivyo walivyojipamba wanawake wata katifu wa zamani, waliomtumaini Mungu na kuwa wanyenyekevu kwa waume zao. 6 Kama Sara alivyomtii mumewe Ibrahimu, akamwita ‘bwana’. Ninyi sasa ni binti zake Sara kama mkitenda mema pasipo kuogopa tishio lo lote.”

Wanawake tuwe na Utiii, utii ni hali ya kunyenyekea Adabu ni pamoja na Unyenyekevu Ili kama umeolewa na mume asiye amini ambaye hajaokoka avutwe na mwenendo wako wa kutii wa Adabu leo hii tumewazuia wanaume wengi wokovu sababu mwenendo wetu ni mibovu  mstari 4 unaonyesha tunavyopaswa kua na Roho ya upole, utulivu, ulio wa Thamani kubwa KUMBUKA KICHWA CHA SOMO MWANAMKE WA THAMANI sifa hizi biblia inasema zina thamani kuu Mbele ZA MUNGU Inasema hivi ndivyo walivyo jipamba wanawake wa takatifu wa zamani waliomtumaini Mungu na kuwatii Waume zao, kama Sara alivyotii akamuita mume wake Bwana. MSTARI WA 10 Unahusu Mdomo Maneno Yetu Atakaye Penda Maisha Na Kuona Siku Njema Auzuie Ulimi Wake Usinene Mabaya Wanawake Mabinti Tuzuie Ulimi Wetu Usinenee Mabaya                                                     
Wachungaji Mbalimbali waliofundisha katika Kongomano hilo, Kutoka Kushoto Mchungaji Lilian Ndegi, Mchungaji Dickson Dickson Mtalitinya na Pastor Neema wa mwisho kabisa ambaye ndio mwandaaji wa Kongomano
4. Kumcha Bwana (Kumpenda Mungu) Anasema ukinipenda utazishika Amri zangu yaani sheria ya Mungu Lugha nyepesi WOKOVU Mithali 31:30 UPENDELEO HUDANGANYA, NA UZURI NI UBATILI BALI MWANAMKE AMCHAYE BWANA NDIYE ATAKAYE SIFIWA. Mwanamke mwenye hofu ya Mungu atasifiwa mwanamke aliyeokoka ndiye atakaye sifiwa

AYUBU 28:28 Kisha Akamwambia Mwanadamu Tazama, Kumcha Bwana Ndiyo Hekima Kumbuka

1. Nilisema Ni Hekima Sasa Maana Ya Hekima Ni Kumcha Bwana, B. Na Kujitenga Na Uovu Ndiyo Ufahamu. Kumbuka Nilisema

2. Kilicho Fichika Kwa Mwanamke Ni Ufahamu So Another Definition Ya Ufahamu Ni Kujitenga Na Uovu Saa Imefika Binti Na Wamama( Mwanamke) Kufahamu Neno Linasema Nini Tulitende Tuinuke Kwaajili Ya Familia Zetu Ndoa Zetu Na Jamii Kwa Ujumla Uponyaji Uko Kwetu Tuinuke Soma Yeremia 9:17-21





Katika Kongomano hilo la Mwanamke wa Thamani pia Mchungaji Lilian Ndegi kutoka Living Water Kawe alifundisha na kufanya maombezi.


 

Na hii ndio kamati ya Maandalizi ya Kongomano la Mwanamke wa Thamani Moshi, Hongereni sana kwa kazi Nzuri. Naamini wanawake wa Moshi wamepata kitu tofauti


 

No comments:

Post a Comment