Pages

Tuesday, August 5, 2014

USALAMA NA UBORA WA NAFSI YAKO UNAVYOHUSIANA NA UHAI WA KANISA na Mwl Samwel Mkumbo -Sehemu ya Kwanza

Karibuni katika makala haya yanayoletwa kwani na Mwalimu Samwel Mkumbo
 
Mwalimu Samwel Mkumbo

Uhai wa kitu chochote kile unategemea namna au jinsi mwenye huo uhai au aliyekabidhiwa dhamana yuko katika hali gani, unaweza kulaumu juu ya uharibifu wa jambo au mambo Fulani lakini kabla ya kulaumu angalia kwanza yeye aliyeharibu au aliyekabidhiwa mikononi mwake yuko katika hali gani.

MATENDO 20:28 inasema hivi;

Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

Sasa kabla sijaendelea Zaidi nataka niseme jambo la msingi sana hapa, kichwa cha Somo letu kinatuhitaji tuwe na ufahamu wa kuhakikisha kwamba kila tunachokiongea katika somo hili ni mambo makubwa mawili, NAFSI YAKO NA KANISA LAKO. Wewe ni nafsi moja katika kanisa, Je unayo kazi gani wewe kama Nafsi?

Unaweza usijue wala usiliangalie kwa uzito, lakini inapasa kuelewa tafsiri hii;

KANISA ni Nafsi za watu zilizounganishwa kwa kunia mamoja katika Imani yao na hiyo Imani wameijenga katika msingi wa YESU KRISTO, hivyo kanisa bila ya nafsi zilizokubaliana za watu wengi wa aina mbalimbali si kanisa maana ili wawe kanisa lazima nafsi zao ziungane kwa kunia mamoja na kuwa na Imani moja ambayo hiyo Imani ndiyo inatengeneza nia moja.

TAZAMA NAMI:

Ili kanisa liwe na Nguvu na likae katika mstari unaotakiwa ni lazima nafsi za watu ndani ya Kanisa ziwe ziko salama kabisa, yaani ziwe zimetunzwa katika hali ambayo uhakika wa kundi kuishi kwa Amani utakuwepo kwa uhakika.

Labda tuunganishe vipande viwili vya huo mstari wetu wa msingi ili uone jambo la msingi kidogo….. Jitunzeni nafsi zenu,,.,.. mpate kulilisha kanisa lake Mungu,.,.,..

Mfano wa Mtumwa Mwaminifu

Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo. Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini (LUKA 12:42-46)

Sasa hapo ninataka nikufundishe jambo ambalo kimsingi ambalo halipo kwenye Mistari hiyo hapo juu, na lenyewe ni juu ya adhabu aliyopewa huyo wakili. Ona mtari huu;,..,.. akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, AKILA NA KUNYWA NA KULEWA;,.,….

Maana suala sio kusema bwana wake anachelewa ila baada kuona bwana wake anachelewa alifanya nini? Na wala sio kuwapiga watumwa ila baada ya kuwapiga watumwa alifanya nini? Yeye alichokifanya ni KULA NA KUNYWA NA KULEWA,..,..

Biblia inaposema yeye ALIKULA NA KUNYWA NA KULEWA, maana yake aliacha kufanya alichotakiwa kufanya lakini pia aliiharibu nafsi yake kwa MVINYO yaani kwa Ulevi. Maana suala si kula na kunywa kwa sababu hayo ni mahitaji ya mwili wa kila mtu, lakini suala ni KULEWA na biblia inasema KILEO HUDHIHAKI,. Na pia HUPOTOA HUKUMU ZA HAKI.


MAANDIKO KADHAA:

1 YOHANA 5:20-21 inasema hivi;

Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele. Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.

Sasa ninatamani tuangalie jambo zuri kidogo katika mstari huo hapo, ya kwamba msisitizo wa maneno ya mtume Yohana juu ya hayo aliyoandika haupo kwenye kutaka kuwaeleza habari ya Kuthibitisha kuwa YESU AMEKWISHAKUJA, wala pia si juu ya Habari ya kutaka kuwaeleza kuwa WAO WALIOAMINI WAKO NDANI YA YESU AMBAYE NI KWELI NA MUNGU WA KWELI, lakini hayo yote aliyasema ili kuipa nguvu sentensi yake ya mwisho ya kuwaambia JILINDENI NAFSI ZENU SANAMU.

TAZAMA NAMI:

Sasa tukianza kuangalia maneno ya Yohana kabla hajatoa msisitizo wa kuilinda nafsi zetu dhidi ya Sanamu, maneno yaliyotangulia kuna mahali yanatuelekeza;

Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele………

Sasa kwenye huo mstari nataka kwanza Ninyofoke na lile neno Nasi TWAJUA.,.. ikiwa na maana kwamba hayo yatakayofuata au atakayoyasema YANATOKA KWENYE UFAHAMU au ni UJUZI alionao juu ya Mungu, na Yesu Kristo mwana wake wa pekee.

Kwa hiyo Yohana anaposema kule mwishoni ya kwamba JILINDENI NAFSI ZENU NA SANAMU, maana yake JILINDENI NAFSI ZENU NA UJUZI AMBAO HAUTAELEZA JUU

YA HAYO ALIYOELEZA, kila KUJUA kusikokuonesha wewe ni nani mbele za MUNGU ni wa kujilinda nao, ujuzi usiokuwambia habari ya dhambi zako, ni wa Kujilinda nao, Ujuzi usiokuwambia ya kwamba dhambi zako zinaweza kusamehewa kwa Damu ya YESU iliyomwagika pale Msalabani huo Ujuzi ni wa Kujitenga nao, Ujuzi wowote usiokwambia kwamba unahitaji utakatifu kwa kiwango cha juu, na uache dhambi zako, uache kukaa na wenye dhambi kama si suala la kuwahubiria injili, ujuzi usiokwambia usikae mahali wanauza pombe, usiangalie dansi, usiangalie watu watendao mambo ya aibu, usiweke chaneli mbaya zinazoweza kuharibu watoto ujuzi usikwambia hivyo ni wa KUJITENGA NAO.

TAZAMA NAMI:

Ujuzi wowote unaokuja kwako unakuja kwa malengo makubwa yafuatayo, na ambayo ni lazima mtu ujiulize kwa undani sana ili upate kuona ni nini iko nyuma yake…,..,.

Kupima namna unavyojua au ujuzi wako au

ufahamu wako juu ya jambo Fulani.

Mwanzo 3:1 inasema hivi:

Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?

Ukitazama msingi wa hilo swali kwa undani utagundua shetani alikuwa na majibu ya swali alilouliza au alikuwa hana uhakika na majibu aliyokuwa nayo juu ya swali alilouliza au alikuwa anataka kulinganisha majibu yake na ya Hawa kuhusu kile anachofahamu juu ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kwa hiyo ALIKUWA ANAPIMA HAWA ANAJUA NINI JUU YA MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA.

Basi Yesu akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka. Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja. Basi Wayahudi wakasemezana, Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati! Atakwenda kwa Utawanyiko wa Wayunani, na kuwafundisha Wayunani? (YOHANA 7:33-35)

Ukitazama namna swali la Wayahudi limekaa katika mtindo ambao wanajaribu kupima ufahamu wa YESU kwa kuangalia ufahamu walionao wao, yaani ya kwamba YESU ana uhakika na hicho anachokisema hapo.

Itaendelea…….

No comments:

Post a Comment