Pages

Thursday, March 26, 2015

Mshukuru Mungu kwa kila jambo

Bwana asifiwe wapendwa, jana nilienda Kwenye mazishi ya Shemeji yangu, nilipenda sana mahubiri Mtumishi wa Mungu alitoa somo kutoka 1Watesalonike 5:17 " shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu."
Akasema watu wengi wanamkumbukaga Mungu wakiwa na shida, kama ugonjwa, mateso mbalimbali lakini mambo yao yakiwa mazuri wala hawamkumbuki Mungu.
Lakini pia anaendelea kusema watu wengi wanakwenda kumshukuru Mungu wakipata watoto, wenzi wa maisha, Gari, Nyumba nk, lakini watu hawamshukuru Mungu wakipatwa na taabu, mapito, vilio, misiba, majanga mbalimbali wakati neno hapo juu linatutaka kumshukuru Mungu kwa kila jambo.

Mahubiri yalikuwa mazuri nilifurahi sana yule mtumishi alikuwa ananikumbusha jambo hilo muhimu.
Kuonyesha kwamba NENO Hilo lilikuwa la kinabii baadae nilikutana na rafiki yangu ambaye miezi michache iliyopita alipatwa na janga kubwa sana yeye na familia yake lakini aliniambia jinsi alivyomshukuru Mungu na ameona Mungu akimtetea na kuendelea muonekania na anakuja kugundua haikutokea kwasababu labda Mungu hampendi bali Mungu analo kusudi jema kwa familia yake na ni kwa utukufu wa Mungu yote hayo yanatokea.
Kwahiyo ndugu yangu hebu muombe Mungu akupe Moyo wa Shukrani kwa lolote unalopitia yamkini ni Gumu sana linakuliza linakuacha huna raha, huna tumaini hebu tu mshukuru Mungu yeye anajua kwanini ameruhusu hayo ilimradi hujamkosea basi   mshukuru
Mungu akubariki na uwe na siku yenye ushindi

No comments:

Post a Comment