Pages

Wednesday, December 7, 2016

KANUNI ZA KIROHO ZA KUMPATA MWENZI

NA MCHUNGAJI JOEL HAMULI

Mwanzo 24

1.  Kupata mwenzi miongoni mwa WAAMINI. Mwanzo 24:1-4
-  Abrahimu alimtaka mtumishi wake kumtwalia Isaka mke kutoka kwa "jamii yake"
-  1Wakorintho 15:15-16 huwezi kujiunganisha na "makahaba" au kufanyika mwili mmoja na wasioamini

2.  Chochote ukitakacho kwa Bwana unakipata kwa IMANI.

-  Mwanzo 24:6-7 Mungu alimuapia Ibrahimu kumpa uzao wake nchi hiyo. Hivyo alimwamini Mungu na akamwambia mtumishi wake kwa imani kwamba Mungu angemtuma malaika wake kumwongoza kupata mke.
-  Filemoni 6:4 msisumbuke kwa neno lolote bali ktk kila jambo kwa kuomba na kushukuru. Badala ya kujishughulisha na kujisumbua sana kutafuta mke/mume, mwambie Mungu kasha endelea kuamini.

3.  Lazima kuwe na MAANDALIZI. Mwanzo 24:10-11

-  Maandalizi stahiki kadri ya taratibu zinazokubalika ni muhimu.
-  Luka 14:28 Kabla ya kujenga, kaa chini hesabu gharama
-  Jiandae kiroho, kimwili, kisaikolojia, nk
-  Ikiwa wamtaka kutoka kwa Mungu, timiza mapenzi yote ya Mungu. Matendo 20:27

4.  Fanya MAOMBI. Mwanzo 24:12-14

-  Ombea jambo hili na ujue mapenzi ya Mungu kulihusu.
-  Usiwe mgumu kubadilika na kulazimisha mapenzi yako, unaweza kuwa na vigezo vyako, lakini si lazima Mungu ajibu hivyo. Ila waweza kuomba ili kupata uthibitisho wa ki-Mungu

5.  Chukua HATUA

-  Kwa tamaduni nyingi mwanaume ndiye huanzisha mchakato kwa kwenda kuomba uchumba. Mwanamke anaweza pia Biblia haijakataza, lakini zingatia matokeo yake. Kwa kuwa upendo unaoshikilia ndoa ni wa mwanaume, inabidi yeye ndio ashawishike zaidi juu ya msichana. Ndiyo maana yeye anaagizwa kupenda na mwanamke kutii.

6.  Kuhusisha watu WENGINE. Mwanzo 24:28-31, 50

-  Yafaa kueleza familia. Zamani familia zilibeba jukumu la kijamii na kiroho
-  Kwa sasa majukumu ya kiroho yapo kwa kanisa, kwa hiyo waambie viongozi wako wa kiroho wakuongoze, hata kabla ya kwenda kwa wazazi

7.  Msichana KUKUBALI. Mwanzo 24:57-58

-  Msichana inabidi kwa utashi wake mwenyewe aamue kumkubali na kuolewa na mwanamume husika.
1Wakorinthi 7:39 inaongelea juu ya mwanamke kuolewa na mwanamme “amtakaye”. Kuingia kwenye ndoa kwa kulazimishwa si mapenzi ya Mungu.

Makala hii ni sehemu ya semina ya Mahusiano na Ndoa iliyofundishwa kanisani City Harvest na ni sehemu ya kitabu kilicho njiani.

No comments:

Post a Comment