Pages

Tuesday, January 10, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 10

SIKU YA 10 - 10/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

1 Wafalme 15:4 Walakini kwa ajili ya Daudi, Bwana, Mungu wake, akampa taa humo Yerusalemu, amwinue mwanawe baada yake, na kuufanya imara Yerusalemu;

Isaya 62:7 wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imaraYerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani.

Kwanini MIJI YETU TULIYOPO ifanywe imara? Yeremia 29:7 Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa Bwana; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani. AMANI YA MJI WAKO NI AMANI YAKO.. MAFANIKIO YA MJI WAKO YANAWEZA KU-AFFECT biashara zako, familia yako, kazi zako kwa njia moja au nyingine…Zaburi 122:6 Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao NDIVYO TUTAKAVYOFANYA KWENYE MIJI YETU

OMBEA MJI ULIOPO KWA SASA………………. OMBEA MIFUMO YA BIASHARA, ELIMU, DINI, STAREHE, VYOMBO VYA HABARI, SERIKALI NA SIASA, FAMILIA NA MASWALA YA KIJAMII….. MUNGU AKUPE NAFASI KWENYE SEKTA ULIYOPO NDANI YA MJI HUO
Apostle Shemeji Melayeki

GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES

PHONE: +255 714 548 565

We are the Standards! 2017

No comments:

Post a Comment