Pages

Monday, January 23, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 22

SIKU YA 22 - 22/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

KUSHINDWA AU KUACHA KUOMBA/ OVERCOMING PRAYERLESSNESS


Kuna sababu nyingine za watu kuacha kuomba… lakini napenda uangalie kidogo sababu chache kwa nini tunatakiwa kuomba….

KUNA MAMBO MABAYA YANAWEZA KUTOKEA TUSIPOOMBA, KUNA MAJIRA YATATUPA SHIDA, KUNA MAJARIBU TUNAWEZA KUINGIA…

Mathayo 24:20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. Luka 22:40 Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni.

YESU ALIKUWA NA KAWAIDA YA KUOMBA AKIMALIZA HUDUMA YAKE… NA NDIVYO ILIVYO KWETU KABISA…

Marko 6:46 Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kuomba.

1 Wathesalonike 5:17 ombeni bila kukoma; 1 Samweli 1:12 Ikawa, hapo alipodumu kuomba mbele za Bwana, Eli akamwangalia kinywa chake.

MAOMBI SIYO TUKIO LA BAADHI YA SIKU BALI TUNADUMU KATIKA MAOMBI…

Wakolosai 4:2 Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;

HATA KAMA MUNGU ANAJUA MAHITAJI YETU - ANATAKA TUJIZOEZE KUOMBA KWAKE… UHUSIANO NI MUHIMU… ANAPENDA… TUSEMEZANE NAYE.. Ufunuo wa Yohana 5:8 ……….. kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu. 2 Mambo ya Nyakati 1:7 Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe.

MAOMBI YANA-ENERGIZE MALAIKA WANAOYUHUDUMIA HASA TUNAPOOMBA MUDA MREFU…

Danieli 9:21 naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni. Kutoka 17:11 Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.

MAOMBI YA ANA NA MZEE SIMEONI YALIACHILIA MALAIKA KIPINDI CHA KUZALIWA YESU…
 Luka 2:34 Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Luka 2:26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.

Luka 2:36-38 Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.

Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.

KUNA VITU HAVITASOGEA BILA MAOMBI

Marko 9:29 Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba.

WAKATI MWINGINE MUNGU HUTUPA MAONO TUKIWA KWENYE MAOMBI… FIKIRIA KAMA PETRO ASINGEKUWA NA TABIA YA KUOMBA..

Matendo ya Mitume 10:9-12 Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana; akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia, akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi; ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani.

MUNGU ANATAKA KUSIKIA HAJA ZETU KABLA YA KUANZA KUWAAMBIA WATU WENGINE… YEYE NI BABA YETU… ANA NJIA BORA KABISA YA KUTUFANIKISHA...

Wafilipi 4:6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

JE, NI NINI KINACHOKUPINGA USIOMBE??

Maombolezo 3:8 Naam, nikilia na kuomba msaada, Huyapinga maombi yangu.

Warumi 8:26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

KUOMBA VIBAYA (KUTOKUJUA) SIYO DHAMBI HUO UDHAIFU ROHO MTAKATIFU ATAKUSAIDIA… ILA USIACHE KUOMBA…


JIFUNZE KUONGEA NA MUNGU MAMBO MBALIMBALI UTAONA FAIDA YAKE…. ACHA KUYABEBA PEKE YAKO… LIWE ZURI, RAHISI, GUMU, JEPESI, MFADHAIKO, MAUMIVU N.K.. 1 Petro 5:7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu ZOTE, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu…… fadhaa zenu ZOTE NA SIYO baadhi……

BABA NAKUOMBA KWA ROHO MTAKATIFU WAKO, NIRUDISHIE TENA KIU YA KUOMBA, KIU YA KUWA NA USHIRIKA NA WEWE, NINAPINGA KATIKA JINA LA YESU KILA KINACHONIPINGA NISIOMBE, NINAONDOA KWENYE MAISHA YANGU KITU CHOCHOTE KINACHONIONDOA UJASIRI WA KUKISOGELEA KITI CHA REHEMA

NA IWE KWANGU KATIKA JINA LA YESU

MWAKA 2017 SITAACHA KUOMBA KATIKA JINA LA YESU

NB: JIFUNZE ZAIDI JUU YA MAOMBI NA TAMANI KUWA NA UHUSIANO BINAFSI NA HUYU MUNGU ANAYEKUPENDA SANA…

Mungu atakujalia hayo utakayoyaomba katika jina la Yesu

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

No comments:

Post a Comment