Pages

Tuesday, January 3, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 3

SIKU YA TATU - 3/1/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.


KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

SIKU YA 3…. Hesabu 30:13 Kila nadhiri, na kila kiapo kifungacho, ili kuitaabisha nafsi ya mwanamke mumewe aweza kuthibitisha, au mumewe aweza kutangua

KUTHIBITISHA VITU VIZURI NA NADHIRI TULIZOZIWEKA NA KUZITANGUA YOTE YALIYONENWA JUU YETU… KILA KITU AMBACHO KINACHOITAABISHA NAFSI YAKO ITATANGULIWA KABISA… Kama mume wa mtu anaweza kuitangua, mtumishi wa Mungu anaweza kuitangua, kama mtumishi anaweza kuitangua, ina maana lipo neno linaloagiza… na wewe Mwenye Roho Mtakatifu unaweza kutangua pia… 

Wakati fulani Yoshua alitamka maneno magumu juu ya Yeriko Yoshua 6:26 "Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo"

MANENO YALE HAYAKUDONDOKA CHINI… 
1 Wafalme 16:34 "Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni."

Isaya 54:17 "……na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa." Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.

NI VIZURI KUUVIKA WEMA MWAKA 2017 KWA MANENO YETU… MABAYA YASITUPATE BALI MEMA Zaburi 65:11 "Umeuvika mwaka taji ya wema wako; Mapito yako yadondoza unono*"

TUMIA MANENO YAKO VIZURI KWA SABABU …. MUNGU ANATUMIA PIA UKIRI WETU KUTUPA MATOKEO TUNAYOYATAKA Hesabu 14:28 "Waambieni, Kama niishivyo, asema Bwana, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi"

USIPINGANE NA UNACHOAMINI.. Warumi 10:10 "Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu." BAADA YA KUAMINI UNAPOKEA ILA USIPOKIRI SAWA SAWA UNAPOTEZA… 

2 Wakorintho 4:13 Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, "Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena"

Marko 11:23… baada ya KUIMARISHWA KATIKA IMANI…..kifuatacho ni KUIMARISHWA KATIKA USEMI… Mwaka 2017 hatutakiri mapooza..udhaifu, kushindwa, kuonewa, kumilikiwa… BALI tutakiri… ushindi, kuinuliwa, kufanikiwa, afya, maendeleo, kumiliki…  Zaburi 45:1 Moyo wangu umefurika kwa neno jema, Mimi nasema niliyomfanyizia mfalme; Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi.

2017 SITAKUWA NA MISIBA, SITAONEWA NA ADUI, SITALAZWA KWA UGONJWA WOWOTE, SITASIKIA HABARI MBAYA, SITAINGIA KUUGUZWA, MAHUSIANO YANGU YATAKUWA YA AMANI, FURAHA NA UPENDO, NITAISHI KATIKA AMANI TELE, NITAIMARISHWA KATIKA KILA ENEO KATIKA JINA LA YESU….

ANDIKA VIZURI 2017 KWA KUTUMIA ULIMI WAKO

 Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565

We are the Standards! 2017


No comments:

Post a Comment