Pages

Tuesday, March 21, 2017

Mahusiano Kuelekea Ndoa - 7

Na Sir Azgard Stephen

Sir Azgard Stephen
Shalom shalom wana wa Mungu. Hatimaye leo tunamalizia swali la 6 katika makala yetu ya mahusiano, swali lilihoji njia sahihi ya kuchumbia (proposing). Wengi wetu humu hili linaweza lisiwe la kwetu, lakini likawe msaada kwa wadogo zetu na jamii inayotuzungumza. Kwa yote niliyozunguka, ni dhahili mtu kujua cha kufanya mpaka sasa, hasa kwenye swali la #3 na #4 nilipozungumza juu ya kukataliwa.

Leo nizungumze majumuisho katika hili, ili kwa namna flani itusaidie angalau kutokukosea, angalau.

Kuna tofauti kati ya kutongoza (seducing) na kuchumbia (proposing). Mtu yeyote anaweza akatongoza, kwa madhumuni yoyote yale, ila kuchumbia mtu anahitajika kuwa na uzatiti (commitment). Kutongoza ni kitendo (action), kuchumbia ni mchakato (process).

Mambo kadhaa ni muhimu kuyajua unapoamua kuchumbia:
  • Ni muhimu kuanza mchakato huu ukiwa uko tayari kuoa leo, yaani ukiwa una utayari na uwezo wa kuoa sasa. Nimeeleza sana juu ya hili, nisirudie tena.
  • Kuwa na uhakika kuwa huyo unayetaka kumchumbia unampenda na anakupenda pia. Hii ni muhimu kuliko unavyoweza kafikiri. Nimezungumza sana juu ya upendo. Kukaa ndani na mtu ambaye huna affection naye ni mzigo mkubwa, kama unaweza kuepuka hilo basi fanya hivyo. Nasema hivi kwasababu nyingi. Mojawapo ni kwamba, unaweza "ukajikuta" kwenye mahusiano kwa bahati mbaya. Yaani mmekuwa tu marafiki, mkawa mnakubaliana sana katika mambo mengi, na ukawa mhitaji na huyo dada naye akawa mhitaji, ukafikiri kwasababu tu mnakubaliana katika mambo mengi basi huyo anafaa kuwa mkeo. Ni kweli uchumba mzuri huanzia kwenye urafiki, lakini si kila urafiki lazima uishie kwenye uchumba na ndoa. Test your feelings on that girl, na wala huhitaji kipimo cha kisayansi hapa. Kuna vile moyo unashtuka ukimuona, kuna vile unapoteza control. Pamoja na uchunguzi wote na vipimo vyote, lakini kipimo cha mwisho katika maamuzi haya ni upendo.
  • Kuwa na mtazamo wa miaka ya uzeeni. Hapa ndio kipimo cha utu uzima. Utu wa nje unachakaa, utu wa ndani hudumu milele. Kuutazama uzee ni kwamba, wakati utafika huyo mrembo atakuwa kibogoyo. Ni kitu gani kitakuwa kivutio cha upendo wako kwake? Ni utu wa ndani pekee, character, ndio utakuwa asali yako. No matter how beautiful she is, don't skip her character. Uzuri wa ndani huuzidi wa nje, na humfanya asiyevutia avutie. Kwahiyo, pamoja na uzuri wote alio nao mtu, lakini kama utu wa ndani umeoza please don't.
  • Usidhani utambadilisha mtu. Huu ni uongo tunaojidanganya, kwamba ana tabia hii mbaya lakini tukiingia kwenye ndoa nitambadilisha. That is a very risk gamble, si kazi rahisi kumbadilisha mtu. Mtu anaweza kuamua kubadilika, lakini huwezi kumbadilisha kwa lazima. Wapo watu waliingia wakitegemea kuwabadilisha wenzi wao, it never happened. Lakini pia kuna watu waliingia kwenye mahusiano na watu wenye tabia mbaya na wakabadilika. Ukiwahoji, watakwambia waliamua wenyewe kubadilika, na si kwamba waume zao waliwabadilisha. Inaweza ikatokea ukambadilisha, but it is the risk gamble. Kwa ushauri wangu, usijaribu hii.
  • Pita kwenye mchakato nilioeleza kwenye swali la 3. Jenga ukaribu na mawasiliano, win her heart, muoneshe unampenda, kisha chukua hatua. Kwa ushauri wangu, hata kama Mungu amekuonesha katika ndoto kuwa huyo ndiye, usiende na kumshuhudia kama njia ya kumpata. She need to see your love, show it.

Katika mambo yote haya, mipango ni ya mwanadamu lakini jawabu latoka kwa Bwana. Hatuingii kwenye mahusiano sahihi kwa umalidadi wetu, bali kwasababu ni kusudi la Bwana.

Mungu ametupa akili, tunafanya mpaka pale upeo wetu unapoishia. Mambo tusiyoyajua ni ya Bwana,na kwa neema yake anatuvusha katika mengi.

BONDE LA KUKATA MANENO! NAAM!

Niwatakie baraka za Bwana

No comments:

Post a Comment