Pages

Friday, March 15, 2013

Tina Marego muimbaji wa Nyimbo za Injili anayetamba na Albamu ya "Bwana ni Nuru"....fuatana nami...


Tina Marego muimbaji mahiri wa Nyimbo za Injili
 
Blogger: Naomba majina yako kamili,na je unatumia Jina tofauti la kisanii? Tungependa kulijua pia ili jamii iweze kukutambua kwa urahisi.

Majina yangu kamili naitwa Justina Mwita Marego

Na katika uimbaji natumia Tina Marego

 Blogger:Umeokoka na unaabudu wapi

Minimeokoka nanina abudu EAGT Tabata Kimanga,nasali kwa baba yangu yeye ni mchungaji hapo

Blogger: Historia yako kwa Kifupi ya kuimba,yaani ulianzaje na wapi?

Nilianza kuimba nikiwa naumri wamiaka kumi na miwili nikiwa kanisani kwenye Sunday School kanisa la EAGT Urafiki chini ya Passtor John Zakaria ambae kwasasa ni Askofu wa jimbo

Tina Marego katika Pozi

Blogger:Katika kuimba kwako je umeshatoa Album au single yoyote? Itaje ina nyimbo ngapi?

Katika kuimba kwangu namshukuru Mungu nimetoa album inaitwa Bwana ni Nuru,yenye nyimbo nane nazo ni:

1.      BWANA NI NURU.

2.      UUMBAJI WA MUNGU

3.      SASA WOTE

4.      KIMBILIO LETU

5.      TUAMKE

6.      UNAHUZUNI

7.      NISHUJAA

8.      MSIFU

Blogger: Wimbo unaoupenda katika nyimbo zako

Wimbo ninaoupenda kati yahizi nihuu wa Kimbilio Letu
Albamu ya Bwana ni Nuru

Blogger:Ni kwanini unaupenda huo wimbo/nyimbo

Huwa unanifariji sana kwakweli nikikumbuka bila huyu Yesu mi ningekuwa wapi leo hii na ndio maana nikaupa jina Kimbilio Letu

Blogger:Nani anasambaza kazi zako? Je anakusaidia vizuri?

Kwakweli sina msambazaji wahii kazi yangu ila nimetoa copy kadhaa nikialikwa uwa naenda nazo

Blogger:Kuna mafanikio gani umeyapata katika kuimba kwako nyimbo za Injili

Mafanikio niliyoyapata nimejuana nawatu wengi nakujulikana pia kwa wengi kuna watu wengine sikutegemea ipo siku tutakaa nao nakubadilishana mawazo nao lakini kupitia hii huduma yangu nimeweza kukaa nao meza moja namshukuru Mungu kwa hilo

Blogger:Umekutana na changamoto gani katika safari yako ya kuimba

Changamoto zipo nyingi kwakweli labda mojawapo kugongana kwaratiba studio yani kupangiwa muda mmoja zaidi ya mtu mmoja pia producer anakwambia uje asubuhi lakini yeye anachelewa inashusha kwakweli mudi yakuimba maana umekua umekwazika

Blogger:Unaonaje Music wa Injili hapa Tanzania?

Kwakweli kwa hapa Tanzania Music wa Injili umekua sana tofauti na hapo nyuma kwasasa waimbaji n iwengi mno.

Blogger:Na Unatoa Ujumbe gani kwa waimbaji wa Nyimbo za Injili ambao kwa njia moja au nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia hii

Miningependa kuwashauri wachague moja sababu Mungu wetu hapendi michanganyo,kama umeamua kuwa kwa Mungu kaa kwakwe nakama umeamua huko Duniani baki huko ili tujue moja sikukaa mguu pande hueleweki,chagua moja,waswahili wanakwambia mtaka mawili moja humponyoka!
Tina kama kawaida
 
Blogger: Amina Tina Ujumbe una nguvu sana huo,Zaidi ya kuimba ni kitu gani kingine unachofanya

Zaidi nakuimba huwa nawasaidia watu nyimbo zao kama backvocal katika Chorus tunaelewana tu!

Blogger:Je kimaisha je uko wapi? Umeoa au Hujaoa bado? Watoto wangapi?

Kimaisha mimi bado nipo nyumbani,sijaolewa wala sina mtoto

Blogger:Una Ujumbe gani kwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili hapa Tanzania

Ujumbe wangu kwao tuwe na ushirikiano yaani umoja na moyo wa upendo kwa wote

Blogger: Una Ujumbe gani kwa Jamii inayoburidishwa,kuinuliwa na kubadilishwa na nyimbo za Injili
Napenda kuwaambia wapende nyimbo zawaimbaji pia wawasupport katika huduma zao ilii tuweze kumtukuza Mungu pamoja

 
Tina Marego Rejoice and Rejoice blog inakushukuru sana kwa kuwa  nasi na kwa muda wako,Mungu akubariki na kukuinua unavyoendelea kumtumikia kwa uaminifu.Amen

 

4 comments:

  1. Hongera sana Tina Mungu aendelee kikutumia

    ReplyDelete
  2. Mungu wa mbinguni akubariki. Na akuwezeshe kumtukuza kwa njia ya nyimbo za sifa na kuabudu.
    Martha Macha Msale

    ReplyDelete
  3. I nеed to to thank you for this very goοd read!
    ! I absοlutely enjoyed еvеry bit οf it.
    I have got you saνеd as a favorіte to look at new stuff you poѕt…

    Also viѕit my blоg post instant loans
    Also see my web site - instant loans

    ReplyDelete
  4. Awesome blog! Is your theme custom made or did you download it from somewhere?
    A design like yours with a few simple tweeks would really make my blog jump out.
    Please let me know where you got your design.
    Thanks

    Look into my blog - Ohio Moving

    ReplyDelete