Pages

Monday, March 18, 2013

Vitu muhimu vya kuangalia unapohitaji au kujiandaa kupata mwenzi wa wa Maisha


Watarajiwa hao in courtesy of stockpics


Watu wengi inapofika katika swala la kutafuta mwenzi wa maisha,nikiwa na maana mume au mke huwa inakuwa ngumu sana. Maana wanakuwa hawajui wafanye nini ili waweze kupata ubavu ambao ndio Mungu amekusudia na sio kuchukua ubavu wa wenzao. Ni jambo la maana sana unapotafuta au kujiandaa kuwa na mwenzi wa maisha kujua mambo muhimu yatakayo kusaidia kuepusha kukutana na mwenzi sahihi kutoka kwa Mungu.

Leo nitaelezea mambo muhimu matatu tu japo hii itakuwa series ambapo tutaendelea kueleza zaidi na zaidi juu ya vitu muhimu tunavyoendelea huko mbele.

Mambo hayo ni;
1.      Maombi
Maombi ni muhimu sana na yanakufanya uwe na ushirika na Mungu,na unapoomba ni ishara ya kumwambia Mungu kwamba bila wewe Mungu wangu siwezi. Kuna mchungaji mmoja alitufundisha ni muhimu kufanya maombi pale ambapo huna picha yoyote kichwani,maana tatizo la watu wengi ni kwamba wanakwenda kuomba Mungu huku ana picha ya mtu Fulani,au mwingine anamwambia Mungu ooh Mungu nipe huyu,nataka kukumbia rafiki hiyo sio njia nzuri.

Wewe muombe Mungu akupe mwenzi,halafu kama neno lake linavyosema kwamba tukiomba tuamini kwamba ametupatia na kwamba Mungu si dhalimu maana yeye ni baba atatupa kitu chema,basi tuamini hivyo.Ukishaomba na kuamini kwamba umepata hata kama katika hali halisi huoni anza kumshukuru Mungu kwa mwenzi mzuri kutoka kwake.

Mtumishi mwingine alifundisha unaweza kusema huyo mtu awe na haiba gani n.k,lakini ujue kwamba Mungu yuko juu ya vyote atakaye kupa ndio sahihi kuliko akili yako inavyohitaji au kudhani.

Maombi ni eneo muhimu sana ni vizuri ukawa na mtu ambaye mnaelewana na kiimani mko katika level moja au yeye amekuzidi mkawa mnaliombea hilo pamoja na mambo mengine yanayowazunguka,maana neno lake linasema palipo wawili watatu yeye yupo katikati yao,upako wa uwingi nao una umuhimu sana.

Unapukuwa katika maombi ni vizuri pia ukatubu maana unaweza ukawa na vitu vinavyozuia mawasiliano yako na Mungu. Tubu kwa chochote ambacho umefanya kwa kujua au kutojua maana Mungu wetu ni mtakatifu uende mbele zake ukiwa mweupe,Amen

2.      Je wewe ni mtu sahihi au unayefaa kuoa au kuolewa

Kitu kingine cha kuangalia nafikiri ni vizuri kujifanyia utafiti wewe mwenyewe,kujichunguza hivi kweli mimi kweli nina tabia gani ya kufaa kuishi na mtu mwingine. Hivi kweli mimi ninazo tabia za mke au mume mwema kweli ? Hivi mimi ni mtu ambaye watu wanaweza kumwamini na kumpa moyo wake kweli?

Ni kwanini nataka kuolewa au kuoa? Nataka kuolewa au kuoa  kwasababu mama au baba yangu anahitaji hivyo,au kwa vile rika langu wote wameolewa? Jamii inanionaje kwanza?

Ukijitafiti utagundua kwa njia moja au nyingine kuna mtu alishakupa mrudisho nyuma juu ya tabia zako mbaya,je kwa hizo tabia kweli bila kuzibadilisha kuna mtu anaweza kuishi na wewe? Jiulize peke yako wala usimuulize mtu,utapata majibu hayo utashangaa ambavyo unahitaji ujishughulikie kwanza. Watu wengi wanalia katika maombi oooh Mungu baba Jehova,naomba unipe mtu anayefaa kuwa mume au mke wangu lakini wao wanasahau hivi mimi Mungu ananionaje,kweli maisha yangu yanampa Mungu utukufu. Unaweza ukawa na vitabia ambavyo unaona kwamba si vibaya kumbe hivyo hivyo vyaweza kusimama kama kizingiti cha Baraka zako.

Ukishajua tatizo liko wapi badilika,saa nyingine kuna watu wanakuja na nia ya kuwa wenzi halafu wanaingia mitini basi ukijikagua unaona inawezekana tabia hii ndio imemkimbiza,basin i vizuri kufanyia kazi na sio kukaa na kulia. Kwakweli ni heri umlilie Mungu atakurehemu kuliko huyo aliyekukimbia maana akishaamua ndio ameamua na kama sio ubavu wako basi acha aende kwa ubavu wake,amen

3.      Uhusiano na Mungu
Unapokuwa unahitaji Mungu akupe mwenzi wako wa maisha pia ni vizuri kujichunguza juu ya uhusiano wako na Mungu. Je ushirika wako na Mungu uko vipi? Isije ikawa unakwenda tu kanisani kwasababu unataka Mungu akupe mwenza na wakati hujakaa sawasawa na huyo Mungu. Hakikisha unajitoa sana kumpenda Mungu na kujishughulisha na kazi yake yaani utashangaa jinsi mambo yako yatakavyokwenda bila kuchoka.

Ukijishughulisha sana na mambo ya Mungu na Mungu naye atajishughulisha na mambo yako.

Kwahiyo mpendwa chukua hatua leo ya kujitoa kwa Mungu kiujumla sit u kwasababu unataka mwenzi bali kwa vile umeamua kumpenda Mungu.

 

Endelea kututembealea maana ndio kwanza tumeanza,karibu kila wiki kutakuwa na kitu kipya cha kukusaidia.

 


Barikiwa unavyoweka haya katika matendo na tutaomba shuhuda kwa wale mliobarikiwa na somo hili.

 

3 comments:

  1. Point nzuri! Point namba nne mabinti wasiangalie hela hasa bongo.

    ReplyDelete
  2. point nyingine: kuwa mwenye bidii kwa kila ufanyacho (halali na venye kumpendeza Mungu) kama dent piga sana shule, kama employee piga sana kazi. hatutaki wachumba au wenza wavivu, wasiojishughulisha wenye visingizio kibao....

    ReplyDelete
  3. Points! Nimepata fundisho zaidi, na nadhani kama isha ni cost

    ReplyDelete