|
Watarajiwa hao |
Leo
tutaendelea na somo letu la uchumba hadi ndoa,tunaendelea kuangalia vitu muhimu
ambavyo mtu anatakiwa kuangalia au kuvifanya anapojindaa kupata mwenzi wa
maisha.
Katika
somo lililopita tuliangalia vitu ambavyo mtu anatakiwa kujifanyia mwenyewe,na
tuliangalia vitu muhimu vitatu ambavyo ni maombi,kuangalia kama wewe ni mtu
sahihi ambaye kweli unaweza kuishi na mtu mwingine na uhusiano wako binafsi na
Mungu ukoje.
Kabla
sijaendelea mbele naomba kukolezea katika swala la uhusiano wako na Mungu,mara nyingi
nimeona na kusikia wadada au wakaka wanataka wapate watu ambao wana uhusiano
mzuri na Mungu wakati wao they are far from
it,yaani hawana uhusiano mzuri na Mungu .
Uhusiano
ninaosema hapa sio kwenda kanisani wapendwa au kwenye tamasha,au kuwa na
urafiki na waimbaji wakubwa au watumishi,ninamaanisha ule ushirika wako na
Mungu umekaaje? Je Mungu ni rafiki yako? Je ni baba yako? je unawasiliana nae
kwa kiasi gani,ukipata crisis tu au wakati ukienda kanisani tu? Kama uko katika
kundi mojawapo hapo juu nakusihi kwa Neema ya Mungu ubadilishe mtazamo wako
mpendwa maana uhusiano wako na Mungu ni muhimu sana kukupeleka katika
mustakabali wako ambao Mungu amekuwekea hapa duniani.
Lakini
kama utakuwa na mahusiano hafifu na Mungu kwakweli mpendwa mambo yako mengi
hayatakwenda sawa,matokea yake utaweza kuchukia wokovu kumbe wewe mwenyewe ndio
mchawi wa maisha yako.Anza leo soma neno,omba,abudu na jishughulishe na mambo
yake nayeye atajishugulisha na mambo yake.
Hilo
jambo la mahusiano ni jambo ambalo lilinifanya niweze kufikia mustakabali na
kweli naweza kusema yeye ni Ebeneza na hata ninao wengi ninawajua wamefanikisha
kuwa katika mahusiano Mungu aliyekusudia kwasababu walikazana sana kumkaribia
Mungu,na Mungu aliweza kuwaepusha na mitego mibaya akawakutanisha na wenzi
aliowakusudia kwao.
Katika
somo lililopita nilizungumza juu ya kuwa na mtu mmoja wa karibu unayemwamini
awe prayer partner wako ni muhimu sana maana hata neno linasema Katika Mathayo 18:20 “Walipo wawili au watatu kwa
jina langu ,nami nipo katikati yao”. Katika Kiswahili kuna msemo unasema kwamba
umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Ukiomba na mwenzako unapata
nguvu,mnatiana moyo wa kuendelea mbele zaidi na zaidi,kupeana shuhuda,kwa
kifupi hutachoka na utaona Mungu akijibu maombi kwa njia ambayo utamshangaa si
katika swala na mwenzi wa maisha tu mambo yote.