Wednesday, August 16, 2017

Kanisa ni Nini? - Mch. Yared Dondo, Kanisa la City Harvest Bahari Beach

Matendo ya Mitume 2:41-47

Kristo alilipenda kanisa Akajitoa kwa ajili yake. Lakini kanisa ni nini na linapaswa kuwa nini? Maana rasmi kujibu swali hilo ni kuwa, kanisa ni jumuiya ya waamini walioitwa na waliounganishwa pamoja kwa ajili ya ibada, maombi, kujifunza Neno la Mungu, kushika maagizo, ushirika, kutangaza Neno na huduma yoyote ambayo Bwana ataitaka. Ikiwa kanisa letu au kanisa lolote liweze kuifikia maana hii, kuna tabia tatu linapaswa kuwa nazo – Mfanano, Jumuiya na Mawasiliano. Kushindwa katika maeneo haya ni kulidhoofisha kanisa na kulifanya kushindwa kuwa kanisa ambalo Kristo angependa liwe.


I. KUNAPASWA KUWA NA MFANANO

Waefeso 4:4-6 “Mwili mmoja, na Roho mmoja…”

A. Kuna wokovu wa namna moja – Wokovu kwa njia ya neema ya Kristo pekee

1. Matendo 2:41 

2. Wokovu ni kwa kupokea neema ya Mungu pekee, nje ya matendo, kaida za kidini, au aina yoyote ya bidii ya kibinadamu

3. Waefeso 2:8-9 

B. Kuna ramani ya pamoja - Biblia, Neno la Mungu lililohuishwa

1. Matendo 2:42 "... Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume..."

2. Maandiko ya Agano la Kale na Jipya, yakiwa yamepuliziwa pumzi na Mungu, yanatosheleza kabisa na ni kanuni ya imani na matendo tu, na kuhukumu mizozo

3. 2 Timotheo 3:16-17 

C. Kuna lengo la pamoja – kumtukuza Kristo

1. Matendo 2:47 inatuambia kuwa kanisa lilikuwa “likimsifu Mungu” siku zote

2. Waefeso 3:20-21 

3. Kusudi la Kanisa ni kumtukuza Mungu kwa kufanana naye tukiwa duniani, kuishi duniani kama Kristo alivyoishi, kuruhusu maisha yake kupitia mwili wake, Kanisa. Kama Kristo alivyopewa umisheni mmoja na Baba, yeye pia ametoa umisheni mmoja kwa Kanisa Lake. Kanisa lipo duniani kwa kusudi kuu lile lile ambalo Kristo alijia duniani – kuufunua utukufu wa Mungu kwa watu wote.

D. Kuna muunganiko mmoja

1. Matendo 2:44, 46a

2. 1 Wakorintho 12:12-13 

Kuna mtu amepata kuandika, "Tunaitwa Mwili wa Kristo, siyo mkusanyiko wa viungo vya mwili wa Kristo."

E. Kuna Ujumbe mmoja – Injili ya neema ya Mungu

1. Matendo 2:47 " Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.."

2. Kanisa lazima lihubiri ujumbe sahihi – ujumbe wa wokovu kwa njia ya imani katika Kristo

3. Ujumbe wa hali ya asili ya uharibifu wa dhambi, Eze. 18:4; Rum. 6:23. Inamuonya mdhambi kuziacha njia zake za dhambini.

4. Utangazaji wa ukuu na mamlaka pekee ya Mungu. Mungu ndiye Muanzishaji na Mmalizaji wa wokovu. Yona 2:9

5. Ujumbe kwamba wale waliookolewa wanapaswa kuishi kwa kumtii Bwana.

6 "Swali ambalo watu wamekuwa wakijiuliza mioyoni mwao kwa akrne nyingi limekuwa, ‘Nini nifanye kuweza kuokolewa?’ Wengine wanadhani ni kwa Kukidhi vigezo; Mungu anasema ni kwa Upatanisho. Wengine wanatangaza ni kwa tabia; Mungu anasema ni kwa njia ya Msalaba. Wengine wanasema ni kwa ujasiri; Mungu anasema ni kwa Kristo. Wengine wanadai ni kujaribu; Mungu anasema ni kwa kuamini. Jibu la Yesu liko dhahiri kabisa: ‘Lazima uzaliwe mara ya pili’ - imenukuliwa


II. LAZIMA KUWE NA JUMUIYA

A. Ndani ya mwili wa Kristo kunapaswa kuwe na Kujali na Huruma kama damu ilivyonunua, damu ilivyoosha mwili.

B. Matendo 2:42 inatuambia kuwa kanisa la kwanza lilidumu katika ushirika

C. Matendo 2:46 inasema “kwa moyo mmoja.”

D. Matendo 4:32 inasema “walikuwa na moyo mmoja na roho moja.”

E. Kanisa linalojikusanya pamoja, kukutana na mahitaji ya kila mmoja, linalosimama kwa ajili ya kila mmoja na siyo kila mmoja dhidi ya mwenziwe.

F. Yohana 13:34 "Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo."

G. Yohana 15:12 "Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi."

H. Yesu anapozungumza kuhusu upendo, huwa ni aina maalumu ya upendo, upendo usio wa kibinafsi, kupendana kwa manufaa ya mwingine pasipo kutegemea chochote kwa ajili yako.

I. Kulingana na Wagalatia 5:13 ni kupitia upendo tunapaswa kuwa katika kifungo kwa kila mmoja; kwa maneno mengine. Tunapaswa kuacha upendo wa agape utufunge kwenye kutumikia wengine na kutokeza matendo ya utumishi wa kifungo hicho

J. Warumi 14, Mathayo 18, Mathayo 5 na Wagalatia 6 zote zinagusia njia sahihi ya kushughulika na wale ndugu walio dhaifu katika imani na namna ya kushughulikia migogoro katika mwili wa Kristo pale inapoibuka. Lakini ikiwa migogoro inatokea, upendo wa agape lazima uinuke juu katika roho ya unyenyekevu na huruma.

K. "Kadri huruma inavyopungua, ukosoaji huongezeka. Kadri hruma inavyoongezeka, ukosoaji hupungua." - Kent Crockett

L. Mungu anatutarajia tutii sheria yake ya upendo, kupenda kama Kristo alivyotupenda.

M. Yohana 13:35 "Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi”


III. LAZIMA KUWE NA MAWASILIANO

A. Ya Ndani – ndani ya mwili

1. Matendo 2:44-45 " Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja."

2. Kunapaswa kuwepo Mawasiliano ya mahitaji ya kimwili na kiroho.

a. Wagalatia 6:2 "Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo."

b. Yakobo 5:16 "Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, …."

3. Kanisa linahitaji kuwa tayari kuombeana katika kila hali ambayo Mungu anatuweka.

4. Waebrania 10:25 inatuambia kwamba tusikose kukutanika, kama ambavyo wengine wamejenga tabia, Lakini tukutanike kutiana moyo. Tunahitaji kufanya hivyo hata zaidi kwa sasa kama tuonavyo siku ya Kristo kuja tena inakuja.

5. Kama kanisa, mawasiliano baina yetu ni muhimu. Hii inamaanisha kushirikishana kile Mungu anafanya kwenye maisha yetu, na kujengana kupitia ushirika wa kiujumla na kwa mawasiliano sahihi.

6. Waefeso 4:29 "Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, ………" -

7. Warumi 14:19 "Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana..."


B. Kwa Nje – nje ya mwili

1. 2 Wakorintho 5:19 inatuambia Kristo amelipa Kanisa lake “ujumbe wa upatanisho

2. Kama ilivyo shauku ya Mungu kwamba kanisa lake litangaze Utukufu wake, Mungu pia ana shauku kwamba kanisa lake lilete utukufu kwenye maisha ya watu wenigne kwa kuwafanya wanafunzi kupitia mawasiliano kwea ulimwengu juu ya kweli za Nneo Lake (Mat. 28:18-20)

3. Lengo letu linapaswa kuwa kutangaza Habari Njema za Yesu Kristo. Injili, habari njema za neema hutoa ujumbe pekee wa kweli kwa tiba ya kiroho na uhuru kwenye maisha ya sasa na yajayo kutoka katika ulimwengu uliopotea.

Kulingana na Matendo 2:47, kanisa la kwanza lilpata kibali kwa watu na mawasiliano yako yaliaminiwa na kupokelewa. Sababu ilikuwa maisha yao kama mwili wa Kristo yaliendana na maneno yao.

TESTIMONY TALE - SEASON 5