Pages

Friday, May 31, 2013

Vitu muhimu vya kuangalia unapojiandaa kuwa au kutafuta mwenzi wa Maisha-Part V


 
Watarajiwa......

Leo tunaendelea na somo letu la tano juu ya vitu muhimu vya kuangalia unapotafuta au kijuandaa kuwa na mwenzi wa maisha.

Tunapoendelea na somo hili ambalo ni pan asana,tumelichambua vizuri sana tukiangalia vitu muhimu ambavyo mhusika anayetegemea kupata au kutafuta mwenzi anatakiwa ahakikishe anavifanyia kazi,halafu tuliendelea kuangalia sasa vitu gani muhimu uangalie kwa huyo anategemea kuwa mwenzi wako.

Hivi vipengele ni muhimu sana kwa wewe ambaye unategemea kuingia kwenye ndoa na pia hata kwa mwanandoa maana vitakusaidia kutengeneza kwa upya juu ya ndoa yako.

Ni maombi yangu somo hili likawe Baraka na kukupeleka katika lile kusudi ambalo Mungu analo juu yako juu ya mambo ya ndoa.


Tuendelee..

3.         Je huyo mtu anakupenda kwa dhati

Ni muhimu sana kuwa na uhakika wa kiasi cha  upendo alichonacho mtarajiwa wako. Mwingine anaweza kuwa na wewe kwasababu tu labda amevutiwa na umbile au vitu ulivyo navyo.

Kuna mpendwa mmoja aliingia kwenye uhusiano akifikiri kwamba huyo mtarajiwa anampenda,basin a yeye akajitoa san asana kwake,kumbe yule mtarajiwa alikuwa tu anapenda kuwa na yule mpendwa   kwasababu alikuwa ana uwezo wa kifedha. Sasa hii ilikwenda hivyo ila kitu kizuri ni kwamba yule mpendwa alikuwa na mahusiano mazuri na Mungu wake,basi akawa anaendelea kumuomba Mungu juu ya ule uhusiano ndipo siku akaja kugundua kwamba yule mpendwa ana mahusiano na mtu mwingine ambaye sasa ndio anayempenda ila yeye alikuwa anamtumia tu kwasababu ana hela. Ashukuriwe Mungu maana hakuruhusu waingine katika ndoa,maana angeteseka sana huyo mpendwa kuwa na mahusiano na mke au mume ambaye hakupendi.

Nimetoa ushuhuda huu kukupa tahadhari na kukuonyesha umuhimu wa kuwa na mahusiano na Mungu kama nilivyokwisha kutoa somo hapo Nyuma.

Upendo utasaidia mambo yafuatayo katika ndoa;


a.         Kuweza kuchuliana katika madhaifu
Unatakiwa ujue kwamba hakuna mwanadamu aliyekamilika hapa duniani kila mtu ana madhaifu yake,sasa kama mtu hana upendo wa kweli itakuwa ngumu sana kwake kumchukulia mwenzake.

Maneno ya Mungu katika Waraka wa Kwanza wa Petro 4:8 inasema “Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi”

Mtu akiwa na upendo ataweza kuvumilia pale mwenzake anapokosea na akamsamehe kabisa,lakini akiwa hana upendo hatamsamehe.

Upendo utakuwezesha usimuhumu mwenzako kwa historia yake ya nyuma kama alikuwekea wazi,kwa mfano kama mtu kabla ya kuanza mahusinao akamwambia mwenzake kwamba nina mtoto au huko nyuma nilikuwa na a,b,c,ukiwa na upendo utamsamehe lakini wengine ndio kwanza anakukimbia na anakuwa na kazi moja tu ya kukutangaza labda kwenye kanisa ooh mnamuona yule yukom hivi na vile ooh unajua ana watoto watano tena baba tofauti ooh unamuona yule alikuwaga na mahusiano a,b,c ,unamuona yule alishavutaga bangi. Hapo utakachokuwa unakifanya ni kumuumiza mwenzako na sio kumsaidia,lakini ukiwa na upendo utamuombea na utamtia moyo wa kusimama Imara na Yesu.

Au kuna ushuhuda mwingine naujua huyo mtu alioa mdada ana mtoto wakaishi vizuri kipindi cha mwanzoni ,yule mama alivyopata watoto wengine wa yule baba, yule baba akaanza kuwabagua yaani mwisho alimkataa kabisa yule mtoto wa yule mama. Hapo ina maanisha hakuwa na upendo wa kweli na yule mama ndio maana akashindwa kumchukulia na mambo yake.

Kwahiyo mpendwa kuwa makini na huyo mtarajiwa msome vizuri sana asije akawa anakubali vitu vyako kumbe tu anataka aingie tu kwenye ndoa.

 b.         Utawafanya wanandoa wawe wamoja

Upendo unawaunganisha kuwa na mamoja na kuwa na nia moja.

Pasipokuwa na upendo hata umoja wa wanandoa unakuwa haupo. Utakuta mtu hata hajui mwenzi wake kaenda wapi au ana tatizo gani.

Katika ndoa ni vyema kushirikiana na kujua hata changamoto ambazo mwenzako anazipitia na kumuombea,yaani kuichukua shida mwenzako kama yako.

 c.         Mtakuwa mmetekelezaa Sheria ya Mungu

Maneno ya Mungu katika Kitabu cha Warumi 13:8 “Msiwe na deni kwa mtu yeyote, isipokuwa tu deni la kupendana. Ampendaye jirani yake ameitekeleza Sheria”

Upendo ni amri kutoka kwa Mungu,kwahiyo hakikisha unampendwa mtarajiwa au mwenzi wako.

 d.         Mtakuwa mmemshinda shetani

Mkiwa na Upendo,mtakuwa mnaomba pamoja na kusoma neno pamoja

Na Mungu atakuwa pamoja nanyi na kwa umoja wenu mtamshinda Ibilisi na hila zake,maana Ibilisi anapenda mafarakano ili apitishe mambo yake.

Chukua hatua kama unaona huna upendo wa dhati kwa mtarajiwa wako jiangalie kwa upya na pia kama mtarajiwa wako hana upendo wa dhati na wewe yakupasa kukaa chini na kufikiria kwa Upya.

 Leo ngoja niishie hapa,Tukutane tena katika masomo haya ya Uchumba hadi Ndoa,najua mpaka yaishe kuna mtu anakwenda kupona na hata ndoa zinakwenda kuwa kama Mungu alivyokusudia.

Jina la Bwana libarikiwe.

 

1 comment:

  1. ushauri mzuri sitalikosa hili somo kila siku asanteni sana

    ReplyDelete