Pages

Tuesday, April 29, 2014

Waimbaji wa Nyimbo za Injili wa Kundi la Double E Sisters watoa albamu mpya kali



Double E Sisters, Eve kushoto na Esther kulia
 
Kundi la Double E Sisters wamefanikiwa kutoa albamu mpya yenye jina la Tumeuona Mkono wa Bwana
 

Albamu hiyo ina nyimbo nane nzuri , nilipowauliza kwanini wameamua kuipa Albamu hiyo Jina la Tumeuona Mkono wa Bwana na kuimba huo wimbo walisema “Ni kwasababu wameuona Bwana Yesu katika safari yao ya Kihuduma na Maisha kwa ujumla. Bwana Yesu amefanya vingi sana, Mungu ni Mwema” .
 

 

 
Sasahivi wako kwenye maandalizi ya Video ambayo inategemewa kuwa sokoni kaunzia mwezi wa sita.

 

Kundi hili la Double E Sisters linaudwa na wadada wawili ambao ni ndugu wa damu Eve na Esther

Double E Sistes katika pozi
 

Wako Tayari kuhudumia na mialiko mbalimbali,

 

Email yao double@gmail.com

 

Double E Sisters mnafanya kazi nzuri sana , Mungu awabariki na kuwainua hatua hadi hatua

 

No comments:

Post a Comment