Pages

Wednesday, April 30, 2014

Uchumba hadi Ndoa: Jihadhari na matarajio potofu kuhusu Ndoa




Habari ya leo mpendwa wangu, Karibu sana katika Makala haya ya Uchumba hadi Ndoa yanayoletwa kwako na Mshauri wako kila wiki.

 
Leo tutazungumzia kipengele muhimu cha Kujihadhari na matarajio potofu kuhusu Ndoa, au yaliyojengwa kuhusu Ndoa.

Matarajio potofu ni ile hali ya kuamini kwamba kuna vitu fulani vitatokea au vitakuwa hivi halafu wala havitatokea na wala haviko hivyo unavyotarajia.

Matarajio potofu kuhusu ndoa yako sana katika jamii zetu sio za Kiafrika tu hata mabara ya Ulaya, yako katika jamii za dini mbalimbali, kabila na mila mbalimbali

Najua hata wewe kuna matarajio potofu kuhusu Ndoa ambayo utakuwa umeyaamini kwasababu ulizaliwa katika jamii ambayo yaligeuka kuwa sehemu ya hiyo jamii.
 
Katika jamii zetu na mazingira yanayotuzunguka matarajio potofu yanaweza kuwa na sehemu kubwa inayofanya Ndoa nyingi ziwe katika shida ambazo zimekuwa nazo leo.

Kitu kibaya ni kwamba hata sisi Wakristo tumeyaamini na tunayakiri maratajio hayo matarijio potofu, ndio maana leo nimekuja kukuambia kwamba hayo ni potofu labda ulikuwa hujui.

 

Tuangalie Aina Tano za Matarajio Potofu kuhusu Ndoa;

1.      Ndoa Ndoano au Ndoa si Lelemama

Mara nyingi kwenye sherehe mbalimbali za Harusi utakuta pande mbili ya Bibi Harusi na Bwana Harusi wanapewa nafasi ya kutoa nasaha sasa hapo ndio utasikia haya maneno yakisemwa katika nasaha na tena cha kushangaza utakuta watu ukumbini wananapiga makofi.

Sasa wewe mzazi au mlezi mwenzangu unaposubiri ile sherehe pale ndio uje kumwambia mtoto Ndoa si Lelemama au Ndoa ni Ndoano kwanini umechelewa si ungemkataza au ungekataa mahari jamani, Ili basi kumuepusha na hiyo lelemama unafikiri ipo.

Maana kwa kusema pale ina maana unakiri kabisa kwa mdomo wako Mwanangu Ndoa Ndoano au si Lelemama kwahiyo ukavumilie, pale unamfanya huyo mratajiwa awe na hofu kubwa kwahiyo atakaa kimtegomtego ili tu akiona tu kaugomvi kidogo anakumbukaa anhaa hii ndio ileee lelemama niliambiwa na baba au mama siku ile pale Kibada Skyline Hall…Ohh mwisho wa siku anaanza tu kuhesabu makosa siku anakurudia na mizigo ooh Baba na Mama ile Lelemama yangu anhaa hukuwahi kuiona imekuwa lelemama kwelikweli Nimeshindwa na Nimerudi, Utajibu nini mzazi mwenzangu au mlezi mwenzangu.

 
Haimaanishi kwamba kama wewe mzazi au mlezi ulipata shida katika Ndoa yako na mtoto wako lazima apitie ulichopita, hata kidogo , na jaribu ulilopitia je umetafuta Kusudi maana nimejifunza kila Jaribu ulilopitia katika maisha lina kusudi sasa kwasababu tunashikilia sana Uchungu inakuwa Ngumu kuliona Lile Kusudi ambalo ndilo hasa Mungu anataka tulifanye, Haleluyaaaaaaaaa

Sasa na wewe kijana au binti haya na wewe hata hujaolewa unaanza kukaa barazani ooh unajua Bwana wanaume siku hizi wasanii tuu Ndoa hamna, hakuna zote Ndoa Ndoano, unajua kinachotokea katika Ulimwengu wa Roho, tusome pamoja Mithali 18: 21 “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”

Haya kijana na Binti yangu umeona Maneno ya Mungu yanavyosema,kuwa makini unaongea nini wewe ni mtoto wa Mfalme wa Wafalme usiishi kama watu wa mataifa ambao hawana Tumaini,badili Maneno ya Kinywa chako leo, Sema mimi ndoa yangu itakuwa nzuri itabariki watu, itasimama kama Ushuhuda na utapata hicho unachokisema.Aminaaaaaa





2.      Ndoa ni 50/50

Hapa wanamaanisha usijitoe mzima mzima kwenye Ndoa, mwenzako asije akakujua sanaa. Hayo ni maneno tena hata wazazi wanafundisha watoto wao hivyo.

Unajua Mungu anataka moyo safi,Ndoa ili iwe Ndoa nakwambia ni kujitoa 100/100 asilimia katika maeneo ya kifikira, kimwili na kiakili nakadhalika.

Ukikaa nusu nusu na ndoa yetu ya Kikriso ni ya milele yaani kifo tu ndio kinatenganisha si utaumia sana mpendwa wangu maana utaishi maisha fake maisha yako yote.

Mungu ndio alianzisha Ndoa na kama Mungu ndio mwanzilishi alijua tu kwamba itakuwa nzuri ila tufuate kanuni zake, kila siku kujikana na kuhakikisha uko katika mstari Mungu anaotaka

 

3.      Ndoa ni sehemu ya kupunguzia matatizo

Wengine  wameoa au wameolewa ili kupunguza matatizo waliokuwa nayo kabla, labda mmoja ana kipato kidogo sasa anajua akiolewa na mwenye kipato kikubwa atakuwa amepata suluhisho,

Nakwambia ni kosa kubwa kuolewa na mtazamo huo, kwasababu kama ni hivyo matatizo yako yatazidi mara mia maana sasa unaweza kukuta mwenzako labda ana vitu vingine anavipa kipaumbele na sio kutapanya hela kama ulivyofikiri, maana mwingine anaolewa au kuoa anafikiri kila wiki atakuwa anapelekwa Sychells au Dubai kumbe mwenzako ana malengo mengine ya maendeleo, sasa hapo unajikuta unakuwa frustrated ooh hanipendi , kumbe wewe ndio unatakiwa kujua ndoa si sehemu ya kusolve matatizo yako ila inabidi ubadilike ili uweze kuishi vizuri na mwenzako, Halleluyaaa, Bado mnanipenda kweli jamani……..

 

4.      Mwanamke aliyesoma sana hafai kuwa mke

Nimekutana na hili swali mara nyingi jamani mama mimi nina Masters au PHD nitaolewa kweli, ni kutokana na jamii ambavyo imetufanya tuone kwamba sio sahihi.

Wengine wanasema ukitaka kuoa Bwana nenda zako kijijini wakutafutie mchumba mwenye elimu ya chini sana au hana kabisa ili niweze kumtawala hawa wasomi wana maswali sana sitawaweza,nani kakuambia Ndugu yangu wewe unafuata kanuni gani ya Ndoa ya Dunia inavyosema au Mungu. Je hujui kama unaweza kumchukua wa kijijini akitakata tuu anakuwa tatizo mpaka unajuta, achana na hilo tarajio potofu kama Mungu amekukutanisha na mdada ana PHD au Masters yeye Mungu huyohuyo atampa huyo dada hekima ya kuishi na wewe na wewe hivyohivyo.

Ukimuamini Mungu kwamba yeye ndio anakupa wa kufanana nae na ukaamini kabisa kwamba huyu amefanana nami chochote alicho nacho hakimkoseshi sifa za kuwa mke, huo mtazamo utafanya uwe na Ndoa yenye Amani sana.

 

 

5.      Kuishi pamoja, kinyumba kwanza ili kuona kama tunaendana

Eti kuna mtu ameniambia kwamba siku hizi kuna mtindo umeibuka Bwana, watu kwasababu wanajua Ndoa ni Lelemama ni Ndoano basi wamevumbua njia zao wenyewe kwamba sasa ili kumsoma mwenzangu kama anafaa kunioa au kumuoa nitest kuishi naye, yaani hiyo ni ajabu na kweli.

Hiyo si sawa kabisa maana nikipekua Biblia yangu sioni popote kinyumba kimeruhusiwa na Mungu, lazima tufuate manual ya aliyetuumba ili tuwe salama.

Ndoa ni mpango Kamili wa Mungu ukiingia ujue uko katika mpango wake uache hofu na Mashaka, uwe na Imani kwasababu maisha yetu ya Ukiristo ni maisha ya Imani.

 

Amini kwamba ukiingia katika Ndoa utashinda majaribu yooote maana kwakweli lazima yaje, wala siko mahali hapa kukuambia kwamba Majaribu hayatakuja yatakuja mpendwa wangu ila kama Neno linavyosema katika Warumi 8 : 37 ”Lakini katika mambo yote haya sisi ni washi ndi, naam, na zaidi ya washindi, tukiwa ndani yake yeye aliyetu penda.” TUJUE UTASHINDA NA UTAKUWA NA NDOA YENYE USHUHUDA, Aminaaaaaaa

 

Haya Mpendwa karibu tena Wiki ijayo Masomo yanaendelea , tuendelee kuombeane Mungu ashushe vile anataka tule watoto wake maana na mimi nafundishwa hapa, Amen

 

Barikiwa mpendwa wangu , weka maoni yako hapo chini ili kutiana moyo basi mnakaa kimya sana jamani ili nijue siongea peke yangu, Ameen

 

 

5 comments:

  1. Asante kwa kutuelewesha jinsi ya kuanza uchumba mpaka kufikia ndoa maana mawazo ya wengi tunaamini ukisha oa au kuolewa matatizo yameisha kabisa kumbe unatakiwa kupambanua mambo yaja. Barikiwa sana mtumishi wa Mungu kwa mafundisho mazuri Mungu akupe maona mazuri zaidi ili uzi kutufumbua macho ktk hili.

    ReplyDelete
  2. This sounds great mummy I like it. Iam a long time married lady but it has just revive my marriage life.. very useful teachings

    ReplyDelete
  3. barikiwa sana mtumishi huduma yako inatujenga sana vijana.

    ReplyDelete
  4. Ubarikiwe mtumishi wa Mungu kwa maundisho yenye baraka. Ni mara yangu ya kwanza kuisoma blog yako. Ni kweli tuishi kwa kulifuata neno la Mungu siyo ulimwengu. Tusiache kuombeana ili shetan asifanikiwe ktk ndoa za wana wa MUNGU.

    ReplyDelete