Pages

Monday, January 2, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 1

SIKU YA KWANZA - 1/1/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA



2 Nyakati 20:20 Mwaminini Bwana Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa 


1 Wathesalonike 3:2 Tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu katika Injili ya Kristo, ili kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa habari ya imani yenu; 
Warumi 1:11 Kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapa karama ya rohoni, ili mfanywe imara;


TUTHIBITISHWE/TUFANYWE IMARA SISI KWANZA….

Kuthibitishwa kunaanza kabla ya kufanikiwa ESTABLISHMENT NI KUTENGENEZA SYSTEM ITAKAYOKUSAIDIA KUFANIKIWA…

NGUZO KUU HAPA NI KUIMARISHWA KATIKA IMANI YETU KWA MUNGU HATUWEZI KUANZA KUMWOMBA MUNGU KABLA YA KUMWAMINI (Waebrania 11:6) 



Waebrania 11:1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.


Marko 11:24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. 

Luka 17:5 Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani. Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza (Mungu); kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Eee Bwana naomba kufanywa imara katika Imani yangu, Imani yangu juu yako, n.k. ninaomba uniongezee Imani katika jina la Yesu.. 

MAMBO MAKUBWA TUNAYOYAONA NA KUYAOMBA MWAKA 2017 TUTAPOKEA KWA MKONO WA IMANI (Waebrania 11:1, 6)



Apostle Shemeji Melayeki

GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES

We are the Standards! 2017

No comments:

Post a Comment