Pages

Wednesday, December 28, 2016

CITY HARVEST YAHAMIA JENGO JIPYA - BAHARI BEACH

City Harvest, Bahari Beach
Sehemu ya mbele ya jengo jipya la City Harvest
Disemba 25, 2016 ilikuwa siku ambayo itabakia kuwa ushuhuda kwa kanisa la TAG City Harvest baada ya kufanya ibada ya kwanza katika jengo lake jipya lililopo Bahari Beach wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Uhalisia wa kusanyiko wa ibada ya kwanza ambayo ilikuwa siku ya Krismas unaonyesha kuwa Ukuu wa Mungu na saburi ya watu wa City Harvest katika kuuongoja hatimaye kuupokea muujiza huo.

City Harvest imeweza kuhamia kwenye jengo la kisasa la kufurahisha lilojengwa na wataaaluma waliyobobea katika ufanisi na uhandisi wa majengo.

Kanisa hili limeweza kwa nguvu za Mungu kujenga nyumba ya ibada ikiwa bado ni changa ndani ya kipindi cha miaka minne tangu lianzishwe, kitu ambacho ni ushuhuda mkuu kanisani hapo wa yale Bwana ametenda.

Mchungaji kiongozi wa City Harvest, Architect Yared Dondo alielezea kwa furaha na ushuhuda kwa safari ndefu ya changamoto ilipelekea kupata makazi ya kudumu kwenye uwanja mkubwa wa ekari tano.


“Tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuhamia katika eneo la letu ambapo ni makazi yetu ya kudumu,” alisema.

City Harvest ilianza kufanya ibada zake miaka michache iliyopita katika ukumbi wa sinema uliyopo Mlimani City ambapo Mungu alikuwa anawezesha kulipa kodi ya Sh.900,000 kila ibada kwa kipindi cha mwaka moja na nusu kabla kuhamia Mabibo gereji.

Jengo la Bahari Beach lina uwezo wa kubeba watu 1,000 walioketi na ujenzi unaendelea mpaka hapo utakapokamilika kwa ajili ya ufunguzi rasmi mapema mwaka 2017.

Kanisa jipya la City Harvest lina ukumbi wa sinema ambayo unachukua watu takribani 200, ukumbi wa watoto, sehemu ya wakina mama ambazo zimejengwa kwa kiwango cha kimataifa.

Kwa upande mwingine eneo hilo lina maegesho ya magari zaidi ya 100, vifaa vya kuchezea watoto, viwanja vya michezo, na shughuli za kijamii kama shule ambayo itajengwa hapo.

City Harvest kama kanisa linalokua wanafurahia namna  Mungu amefungua milango kwa njia ya kipeke, hatua itakayotoa nafasi  kukamilisha maono ya kumtumia Mungu.

Nguzo za chuma zilizoshikilia jengo hilo ziliagizwa kutoka nchini marekani na kufanya kanisa hilo kupata jengo kabla hata ya kupata kiwanja cha kujenga.
Mfumo wa kisasa wa kuunda majengo kwa nguzo za chuma unaofahamika kama “pre-fabrication” ndiyo uliwezesha City Harvest kuweza kumiliki jengo huko muujiza wa kiwanja ukifuatia.

Ibada ya kwanza


Siku ya Krismasi mwaka huu ndiyo ilikuwa ibada ya kwanza ya City Harvest katika jengo hilo jipya, na wageni kutoka maeneo mbalimbali walifanikiwa kufika ikiwemo mhubiri na Mtumishi wa siku nyingi, Askofu Titus Mkama

Mchungaji huyo ndiye aliyealikwa kutoa ujumbe wa Neno la Mungu ambapo alihubiri kuhusu Kuishindania Imani akiongozwa na andiko kutoka kitabu cha Yuda 1:3 na kusisitiza kuwa yeye atakayeshindana na kushinda, ndiye atapewa taji stahili

Historia fupi

Umisheni

City Harvest kama ilivyo na moyo wa kuhudumia na kuwafikia watu hasa vijana wanataaluma na maeneo mbalimbali yasiofikiwa, katika jingo hilo jipya kutakuwepo ofisi maalumu za umisheni na uinjilisti, ikiwemo vyumba kwajili ya maombi na kambi za vijana ambazo zitakuwa wazi kwa saa 24 kila siku.

Kanisa hili limejikita zaidi kwenye huduma za kiinjilisti na kila mwaka hushirikiana na vyama vya wanafunzi wakristo vilivyopo vyuo vikuu kwenye kupeleka injili sehemu mbalimbali nchini.

Kwa mwaka huu unaoisha; City Harvest limeweza kufanya kazi ya umisheni sehemu mbalimbali ikiwemo Mpwapwa mkoa wa Dodoma, Lindi, Bagamoyo, Kibaha na Mkuranga kutoka Mkoa wa Pwani.

Mpaka sasa Kanisa limeshirikiana na wanafunzi na wamishenari wa hapo kanisani na nje ya nchi kupeleka Injili ya uwokovu zaidi ya wilaya 20 nchini na nchi za
Sudani Kusini na Msumbiji, na mipango ikiwepo kufika nchi nyingine zaidi.
  
Watoto

CityHarvest huthamini sana watoto na kuwalea katika misingi ya mafundisho Mungu kwa ajili ya kukua kiroho na kimwili.

Watoto wa City Harvest hupewa nafasi za kuhuduma ndani ya kanisa pia katika shughuli za kijamii nje kanisa ikiwa kufikia watoto wenzao. Katika jengo hilo jipya, watoto wana sehemu maalum kwajili kuendesha ibada zao pamoja na sehemu za michezo ya watoto.

Vijana


Kanisa la City Harvest ambalo limelenga kuinua vijana wana taaluma ambao wamejizatiti kwenye ubora na maono yao, limelenga kuboresha na kutumia taaluma zao kwa ajili ya majukumu ya Ufalme kwa mafanikio kupitia
uadilifu, ubunifu na ubora kama mabalozi waaminifu wa Kristo.

Waefeso 2:21-22


Katika yeye, jengo loye linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho

No comments:

Post a Comment