Pages

Thursday, January 5, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 4

SIKU YA 04 - 04/01/2017

Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

1 Samweli 1:23 ….. Bwana na alithibitishe neno lake tu. Basi yule mwanamke akangoja, akamnyonyesha mtoto wake, hata akamwachisha maziwa.

Baada ya Hana kuingia katika maombi mazito ya kumuomba Mungu ampe mtoto, kuna mambo kadhaa nataka  uone ikusaidie kupokea majibu maombi yako..
ANGALIA 1 Samweli 1:13-15

Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa.
Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako.
Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za Bwana

ELI ALIYEKUWA KUHANI AKAMJIBU MANENO HAYA…
1 Samweli 1:17 Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.

ANGALIA RESPONSE/MWITIKIO WA HANA BAADA YA MAOMBI…
1 Samweli 1:18 Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana tena.

Umewahi kuingia kwenye maombi hadi lugha ya kuomba inakuishia? USIACHE KUOMBA Hata kama jambo limekutia uchungu kiasi gani. OMBA HATA KWA MACHOZI, BWANA ATASIKIA MPAKA ALIVYOMJIBU HANA

Mungu anasikia pia kilio chako….. Mwanzo 16:11 Malaika wa Bwana akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana Bwana amesikia kilio cha mateso yako

Kutoka 2:23 Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.
Kutoka 3:7 Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;

Kutoka 3:9 Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa

LAKINI MUNGU TU HAKUWATOA KWENYE DHIKI KWA SABABU WALILIA LA! HASHA…. ILA MUNGU ALIKUWA NENO LA KUTHIBITISHWA JUU YA UHURU WAO…

Mwanzo 15:13 Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.

KILIO CHAO KIMEZIDI MIAKA MIA NNE ILISHAPITA… (ILIFIKA 430) Kutoka 12:41 Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, ya kwamba majeshi yote ya Bwana yalitoka nchi ya Misri.

NI NINI  KIMETOKEA?  MUNGU SI ALISEMA 400? NDIYO… KUNA WATU WALITAKIWA WAOMBE NA KUAMURU LILE NENO LITHIBITIKE LAKINI MUSA ALIKIMBILIA KWA WAMIDIANI…

ANGALIA DANIEL ALIPOONA NENO LA BWANA ALIINGIA KWENYE MAOMBI NA KU-CLAIM LITHIBITISHWE Danieli 9:2-3 “Katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.”

JE, UNAJUA KUNA MAMBO MENGI MUNGU AMESEMA JUU YA MAISHA YAKO NA UNATAKIWA KUONA UTHIBITISHO WAKE?

KWENYE
Afya yako
Ndoa yako
Biashara yako
Huduma yako
Familia yako
Kazi zako


CLAIM TODAY… OMBA LIWE HALISI… LITHIBITISHWE… MUNGU ANASIKIA NA YUKO TAYARI… 

“GOD DOES NOTHING EXCEPT IN ANSWER TO PRAYER” - John Wesley

MUNGU ATHIBITISHE NENO LAKE ALILOLISEMA KATIKA MAISHA YETU KUPITIA NENO LAKE… 


Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017

No comments:

Post a Comment