Pages

Thursday, January 5, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 5

SIKU YA 05 - 05/01/2017

Zaburi 40:2Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA

2 Samweli 7:12…. nitainua mzao wako nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako, nami nitaufanya imara ufalme wake. 1 Mambo ya Nyakati 28:7 Na ufalme wake nitauweka imara milele, akijitia kwa bidii kuzitenda amri zangu na hukumu zangu, kama hivi leo.
1 Wafalme 2:4ili Bwana afanyeimara neno lake alilonena kwa habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli.

Kila mtu amepewa na Mungu eneo analotakiwa kutawala na kumiliki.. inaweza ikawa eneo la mazingira (nchi/mkoa/…), eneo la kibiashara, eneo la kipawa/kipaji, eneo la career, eneo la cheo, n.k.. NI MPANGO WA MUNGU KILA MTU AWE NA KITU ANACHO-DOMINATE TANGU MWANZO…

Mwanzo 1:28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Je, wewe unatawala eneo gani? Mwalimu? Mfanyabiashara? Mkulima? Mhubiri? Mfanyakazi?

Mungu aimarishe kila eneo ambalo umepewa kulimiliki katika jina la Yesu… UFANYE KWA UAMINIFU KWA KUIZIDISHA IZAE MATUNDA ZAIDI… KATIKA JINA LA YESU..
Luka 19:17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.

NGUVU YA KUMILIKI HUSABABISHWA NA NGUVU YA UZIDISHO Katika jina la Yesu Kristo, Mwaka 2017 uanze kuzidiha vipawa vyako ili upanuke katika umiliki wako.. Katika jina la Yesu….

KUFANYWA KUWA IMARA NA KUTHIBITISHWA.. UFALME WAKO… ENEO LAKO LA UTAWALA LIIMARISHWE 2017.

Endelea kuomba na kujiombea……………

Apostle Shemeji Melayeki
GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES
PHONE: +255 714 548 565
We are the Standards! 2017


No comments:

Post a Comment