Pages

Monday, January 9, 2017

2017 MWAKA WA KUTHIBITIKA - 6

SIKU YA 06 - 06/01/2017
Zaburi 40:2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

KUWA ESTABLISHED/KUIMARISHWA/KUTHIBITIKA


Zaburi 89:4 Wazao wako nitawafanya imara milele, Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.

Neno lililotumika hapa WAZAO ni SEED (English), ZERA (Hebrews) ambapo ina maanisha fruit, plant, sowing time, posterity, child, fruitful Huu uzao ni zaidi ya watoto… hii inaitwa mbegu iliyootoka kwako/matunda yako…

Isaya 65:21 Nao watajenga nyumba, nakukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake. Mbali na kwamba utajenga na kula matunda yake…

Yohana 15:16…… nami nikawaweka mwende mkazae matunda; namatunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.

Mungu akupe uwezo wa kuzaa matunda, kuleta matokeo, na matokeo hayo yaweze kuwa na uwezo wa kustahimili majira na nyakati baada yako.. Yaani LEGACY au impact inayodumu baada yako.

IBRAHIM ALIAMBIWA NA MUNGU…

Mwanzo 17:6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako

LAKINI KUHUSU SISI…

Wagalatia 3:14ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya Imani

BARAKA YA IBRAHIMU ISINGEWEZA KUJA KWA MATAIFA BILA KURUHUSIWA NA TRANSACTIONAL ABILITY YA ROHO MTAKATIFU…

NDIYO MAANA ROHO MTAKATIFU NI MUHIMU NDANI YA KILA MKRISTO….

Tumshukuru Mungu kwamba Baraka ya Ibrahimu imetujilia…. Tutafanywa tuwe na uzaomwingi sana, tutafanywa kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwetu

UZAO WAKO UWE ESTABLISHED MILELE…

Endelea kujiombea……………

Apostle Shemeji Melayeki

GLOBAL FAMILY GATHERINGS MINISTRIES

PHONE: +255 714 548 565

We are the Standards! 2017

No comments:

Post a Comment