Pages

Friday, May 31, 2013

Vitu muhimu vya kuangalia unapojiandaa kuwa au kutafuta mwenzi wa Maisha-Part V


 
Watarajiwa......

Leo tunaendelea na somo letu la tano juu ya vitu muhimu vya kuangalia unapotafuta au kijuandaa kuwa na mwenzi wa maisha.

Tunapoendelea na somo hili ambalo ni pan asana,tumelichambua vizuri sana tukiangalia vitu muhimu ambavyo mhusika anayetegemea kupata au kutafuta mwenzi anatakiwa ahakikishe anavifanyia kazi,halafu tuliendelea kuangalia sasa vitu gani muhimu uangalie kwa huyo anategemea kuwa mwenzi wako.

Hivi vipengele ni muhimu sana kwa wewe ambaye unategemea kuingia kwenye ndoa na pia hata kwa mwanandoa maana vitakusaidia kutengeneza kwa upya juu ya ndoa yako.

Ni maombi yangu somo hili likawe Baraka na kukupeleka katika lile kusudi ambalo Mungu analo juu yako juu ya mambo ya ndoa.


Tuendelee..

3.         Je huyo mtu anakupenda kwa dhati

Ni muhimu sana kuwa na uhakika wa kiasi cha  upendo alichonacho mtarajiwa wako. Mwingine anaweza kuwa na wewe kwasababu tu labda amevutiwa na umbile au vitu ulivyo navyo.

Kuna mpendwa mmoja aliingia kwenye uhusiano akifikiri kwamba huyo mtarajiwa anampenda,basin a yeye akajitoa san asana kwake,kumbe yule mtarajiwa alikuwa tu anapenda kuwa na yule mpendwa   kwasababu alikuwa ana uwezo wa kifedha. Sasa hii ilikwenda hivyo ila kitu kizuri ni kwamba yule mpendwa alikuwa na mahusiano mazuri na Mungu wake,basi akawa anaendelea kumuomba Mungu juu ya ule uhusiano ndipo siku akaja kugundua kwamba yule mpendwa ana mahusiano na mtu mwingine ambaye sasa ndio anayempenda ila yeye alikuwa anamtumia tu kwasababu ana hela. Ashukuriwe Mungu maana hakuruhusu waingine katika ndoa,maana angeteseka sana huyo mpendwa kuwa na mahusiano na mke au mume ambaye hakupendi.

Nimetoa ushuhuda huu kukupa tahadhari na kukuonyesha umuhimu wa kuwa na mahusiano na Mungu kama nilivyokwisha kutoa somo hapo Nyuma.

Upendo utasaidia mambo yafuatayo katika ndoa;

Thursday, May 30, 2013

One on One with Esther Mhembelo a Promising Gospel Artist in Tanzania


Esther Mhembelo,Promising Gospel Artist in Tanzania
 
Blogger: Praise the Lord may I know who are you? Your names and Nick Names if any
My names is Esther Hedva Mhembelo my nickname is Esti
Blogger: Wow Thanks, When did you receive Christ
I received Jesus Christ as my Lord and savior in March 2005. The day I made Jesus my Lord my life changed completely. My life story has been from glory to glory nothing less. He has made my life so beautiful. I love my Lord so much he is a wonder

Blogger: Amen, What motivate you to be involved in Gospel Music
God has blessed me with a unique voice and he has given me this gift for free. I use my voice to bring glory to his name. The everlasting love that he has for me compels me to sing for him.
You know the gospel must be preached and through singing the gospel is preached in the lyrics that we write. Jesus is made famous or known through our singing
I love to sing so much and through singing its how I express my love for Him. I was born to worship him and Him alone.
Blogger: Amen Esther, When did you started and How
I started singing gospel music in 2006. I started singing in church before I even thought of recording my album.

Blogger: How Many Albums do you have? Which are they?
I have one album with the name Nafsi Yangu (My Soul) that is already recoded which has 10 songs and right now I have already started working on my second album by God’s grace before July the album will be ready
All Nafsi Yangu Songs can be listened from here www.reverbnation.com/esthermhembelo
 

Monday, May 27, 2013

God will Do a New Thing by Pastor R Namwenje

From the Altar

 
Isaiah 43: 1-2,18-19  “ 1 But now thus saith the Lord that created thee, O Jacob, and he that formed thee, O Israel, Fear not: for I have redeemed thee, I have called thee by thy name; thou art mine. 2 When thou passest through the waters, I will be with thee; and through the rivers, they shall not overflow thee: when thou walkest through the fire, thou shalt not be burned; neither shall the flame kindle upon thee.”

In our life there are things that has happen in the past that we wish they could happen again or there are things that has happen that we don’t even want to remember them because they were terrible or heart breaking.

18 Remember ye not the former things, neither consider the things of old.

19 Behold, I will do a new thing; now it shall spring forth; shall ye not know it? I will even make a way in the wilderness, and rivers in the desert.

 This morning God is saying he is going to do a new thing, does not matter what happen in your past, our God does not consider your past, he is going to do a new thing.

There are people who have been affected by their past, they have so disappointed, stressed and heartbroken ,but God is  saying do not remember the former things neither consider the things of old he is going to do a new thing.

Isaiah 43: 3-4

3 For I am the Lord thy God, the Holy One of Israel, thy Saviour: I gave Egypt for thy ransom, Ethiopia and Seba for thee.

 

4 Since thou wast precious in my sight, thou hast been honourable, and I have loved thee: therefore will I give men for thee, and people for thy life.

 

Friday, May 24, 2013

Usikate Tamaa Songa Mbele


Usikate Tamaa
Nawasalimia katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo,

Leo nina ujumbe mfupi kwako wewe ambaye una mzigo mzitoo  sana,umelia sana ,umekata tamaa,labda huna school fees ya watoto,au hujabahatika kupata mtoto,au hujapata kazi,au watu hawakupendi wamekuzushia mambo mabaya,au unaumwa ugonjwa ambao Daktari amesema kwamba hakuna tiba,au unatamani kuwa na mwezi wako wa maisha na unaona kama  muda umeenda,au una msukosuko katika ndoa mambo sio shwari,au umeachwa mpendwa wangu,au kila uanchofanya hufanikiwi umejaribu kila biashara na kila fursa haufanikiwi kila unachoshika na mkono wako kimezaa mapooza matokeo yake vimekuacha katika madeni, mpendwa natanguliza Pole lakini siku ya leo napenda kukuambia hivi Bwana Yesu alisema katika 1Peter 5: 7 Neno  katika tafsiri ya NIV "Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni",hilo jambo ambalo unaliona Zito sana kwako mtwike Yesu na yeye atakutunza na kukupumzisha na masumbuko ya dunia hii.

Yawezekana umelia sana sana umepita vituo mbalimbali vya maombi,nakushauri leo mpendwa tulia kwa Bwana na kama neno linavyosema katika Yohana 14:1 "Yesu aliwaambia, "Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia". Yawezekana hata umesafiri nchi mbalimbali kwa watumishi wakubwa ukitafuta suluhu ya kilio chako,lakini umejikuta uko palepale..

Usifadhaike mpendwa liko tumaini,mwamini Mungu kwamba atafanya katika wakati ambao hukujua utamshangaa Bwana. Mungu anakwenda kukushangaza (Surprise) nao waliokucheka,waliokata tamaa wakaona kwamba wewe ndio basi au kukukebehi watajua kwamba unamtumikia Bwana Mwenye uwezo kuliko kitu chochote duniani na Mbinguni. Mungu anakwenda kukufunika na utukufu wake. Amen

Tena anasema katika Wafilipi 4:6-7 "Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushu kuru 7. Na amani ya Mungu, ambayo inapita ufahamu wote, italinda mioyo yenu na nia zenu kwa Kristo Yesu"

Unapokuwa katika majaribu usimtafute mwanadamu wa kukusaidia,wengine wanakimbilia wazazi wao na kuamini ndio watakao wasaidia ni kweli nafasi ya mzazi ni kubwa lakini atakupa tumaini la muda ,Mungu ndie mwenye tumaini la kweli na yeye ndio anayekujua kwasababu alikuumba kwahiyo anayo majibu juu ya maisha yako,anayo majibu juu ya afya yako,anayo majibu juu mapito yote unayopitia,Songa mbele mpendwa utayapita tuu,nakuambia utacheka tena mpendwa,utainuliwa,kila kilichokuwa kimeibiwa na Ibilisi katika maisha yako kitarudishwa kwako,Halleluya

Wednesday, May 22, 2013

Apostle Onesmo Ndegi Welcomes you to Professional Breakthrough Conference


 
 
  • Are you Professional and need God intervention in your profession
  • Are you stuck professionally
  • Do you want to receive God word for your Profession?

Then this Conference is for you, Don’t Plan to Miss

Book your Calendar


 Register Now through: 0754 26 11 82
                                            0714 12 52 36
                                Email: lwcministry@gmail.com

 

Tuesday, May 21, 2013

Maombi Ya Ulinzi – Sehemu Ya Tatu na Mchungaji Florian Katunzi


Jenga Madhabahu Ya Mungu Aliye Hai

*Kutoka 8:22-23

“ Nami siku hiyo nitatenga nchi ya Gosheni watu wangu wanayokaa ili hao mainzi wasiwe huko, ili kwamba upate kujua wewe ya kuwa mimi ndimi Bwana kati ya dunia name nitatia mpaka kati ya watu  wangu na watu wako, ishara hiyo italetwa kesho.”

-Nitatenga nchi, Nitaweka mipaka. Wakati misri wanapitia mapigo mazito  Bwana aliweka mipaka kati ya eneo la Gosheni walikokaa  Israel, eneo hilo likatengwa likawa na ulinzi wa Mungu.

-Unaposimama juu ya madhabahu ya Mungu aliye hai ndani ya nchi, Bwana anasema walikuwepo watu wanaomba na kumtumikia katika hali ya unyenyekevu, Bwana atashuka mahali hapa tuombapo na kuitenga nchi yetu na maangamizi.Tunapojenga  madhabahu ya Mungu aliyehai ndani ya nchi , tunasimama mahali hapa na kuomba Mungu aliye hai, anashuka na kuponya nchi yetu.
*2Mambo ya nyakati 7:15

“Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.”
*2Mambo ya Nyakati 7:13-14

“Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzinge kula nchi au nikiwapelekea watu wangu tauni, ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha  na kuomba na kutafuta uso , na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka  mbinguni  na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya  nchi yao”.

Monday, May 20, 2013

Waumini wapekuliwa mbele ya Rais Kikwete kushuhudia kusimikwa askofu


TISHIO la ugaidi linaloikabili Tanzania limechukua sura mpya baada ya vyombo vya ulinzi kwa kushirikiana na maofisa usalama kulazimika kukesha wakifanya doria mjini hapa kuhakikisha ibada ya kusimikwa kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dk. Jacob Chimeledya inafanyika salama.

Ulinzi huo uliendelea kutwa nzima jana kuzunguka Kanisa Kuu la Anglikana mjini hapa na maeneo jirani wakati wote wa ibada hiyo iliyohudhuriwa na Askofu Mkuu wa Cantebury nchini Uingereza, Justin Welby huku Rais Jakaya Kikwete akiwa mgeni rasmi.

Tangu juzi usiku maofisa wa polisi waliovalia sare na kiraia pamoja na wale wa usalama walikuwa wakizunguka katika mitaa mbalimbali ya mjini, kuzunguka kanisa kuu hilo huku baadhi yao wakiwa na silaha za moto na mbwa.

Wakati wote ibada ikiendelea jana, barabara ya kutoka soko kuu la Majengo kupitia hospitali ya rufaa ya mkoa ilikuwa imefungwa huku ile ya kutoka Hoteli ya Dodoma hadi Nyerere ikiwa imefurika askari waliosheheni silaha.

Thursday, May 16, 2013

Vitu muhimu vya kuangalia unapojiandaa kuwa au kutafuta mwenzi wa Maisha-Part IV



 
Haya wapendwa wangu,poleni kwanza maana wiki ijayo sikutokea nilikuwa busy kidogo na huduma,yote ni katika kuujenga mwili wa Kristo

Leo tunaendelea na vitu muhimu  vya kuangalia kwa mtu anayetarajia kuwa mwenzi wako. Tulianza na jambo muhimu juu ya Uhusiano wake na Mungu tukachambua vipengele mbalimbali katika hapo inawezekana kabisa sijamaliza vyotee maana eneo la uhusiano wa mtu na Mungu ni pana sana,ila kwa kifupi yale ni mambo muhimu ya kuzingatia.

Tuendelee...


1.      Historia yake ya nyuma ikoje

Huyu mwenza ni vizuri ukajua historia yake ya nyuma kama utakuwa na neema akuambie yeye mwenyewe au ujiweke kuwa mchunguzi wa kujitegemea katika hilo maana si ni jambo la maisha yako,kwahiyo lazima uhakikishe linakupa amani.

Nimeona vilio katika ndoa watu wanakuja kujua kwamba wenzi wao walikuwa hivi na vile wakati tayari wameshaingia,mtu anaona kama vile mwenzake amemchezea picha yaani filamu kabisa,kwasababu niambie mwenzangu umeshaingia ndio unajua hee mpendwa huyu kumbe ana watoto,au alikuwaga mwizi,jambazi,mahusiano e.t.c. Kwakweli inauma sana kujua jambo hilo kwa kuchelewa au ukiwa tayari kwenye ndoa.

Ni vizuri mtu ujue mapema halafu ujievaluate kama unaweza kuyabeba mambo hayo,ujipime mapema kabisa hivi kweli mimi jamani nitaweza kuolewa au kumuoa mtu mwenye historia ya namna hii,je nitaweza kulelea mtoto wa mtu mwingine? Je nitaweza kuibeba aibu hii ya mwenzi wangu au nitajisikia hata vibaya kutembea nae maana yeye alikuwa na historia hii.

 

Ukiona huwezi usijitese na pia sio vizuri uingie na ukaanze kumtesa mwenzako na maneno ya manyanyaso ooh ndio maana ulikuwa a,b,c...z, mpendwa kuwa muwazi mapema

Ili kuwa na amani na kutoingia katika mahusiano halafu yavunjike kwa ajili ya mambo ya historia zingatia haya;

 

a.      Uliza historia mapema

Ni vizuri katika hatua ya mwanzo kabisa ya urafiki kabla hamjafika kutambulishana kwa wazazi,ndugu na jamaa kujua kwa uwazi kabisa historia ya huyo anayetaka kuwa mwenzi wako. Hii itakusaidia kuamua kuendelea au kuachana na mahusiano hayo mapema. Itakupunguzia kama sio kukuepushia kabisa na machungu ambayo yangejitokeza huko mbeleni

b.      Kupata muda wa kutosha kuijua na kutathimini hiyo historia
Jipe muda usikimbie sana,usifanya fasta fasta,utakua mtu anakuja kwa spidi kali sana anataka aoe kumbe kuna kitu ameficha kikubwa anataka fasta usipate hata muda wa kukihisi hicho kitu kuwa makini mpendwa.

Na ujue kabisa kwa akili zako hutaweza ila Mungu atakuwezesha,na atakuwezesha tu utakapokuwa na mahusiano mazuri na yeye,Amen! Hebu tusome pamoja huu msitari kutoka katika Yeremia 33:3 “ Niite nami nitakuitikia nami nitakuonyesha mambo makubwa usiyoyajua” ukiangalia huu mstari utaona jinsi Mungu anavyosema kwamba muite na yeye atakuitikia na kisha atakuonyesha mambo makubwa usiyoyajua. Kwa hiyo hata kama kuna vitu anaficha hataki uvijue ukimwita Yesu atakuonyesha mpendwa wala usiwe na wasiwasi. Mungu ni mwaminifu sana sana yaani ninayo kila sababu ya kusema hivyo maana nimeuona uaminifu wake katika mambo mbalimbali kwangu na watu wengine walioamua kumtegemea.

Mungu anaweza mpendwa mtegemee tu yeye peke yake na uweza wake.
 

Wednesday, May 15, 2013

Vijana wa Tanzania washauriwa kuwa na Fikra Kubwa ili kuleta maendeleo katika nchi yao


Profesa Elisante Ole Gabriel Mkurugenzi Mkuu Idara ya Mendeleo ya Vijana Tanzania
Maneno hayo yalisemwa na Profesa Elisante Ole Gabriel ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa maendeleao ya Vijana katika Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo alipokuwa anaeleza Vijana juu ya Sera ya Maendeleo ya Vijana katika Ukumbi wa Nchi ya Ahadi ( The Promise Land). Semina hiyo ni mojawapo ya semina na mikutano ambayo imekuwa ikifanyika katika ukumbi huo kila wiki ili kuhamasisha vijana watanzania waweze kubadili mtazamo na kuikwamua nchi yao,mikutano hiyo inaandaliwa na Mchungaji, MC Maarufu na Mtangazaji wa Redio Clouds FM Harris Kapiga.

Katika mkutano huo Profesa Elisante aliwataka vijana wa kitanzania kuachana na dhana potofu kwamba maendeleo yanahitaji kuwa na mtaji au hela tu wakati tatizo kubwa liko katika fikra na mtazamo wa vijana kwa ujumla.

Aliendelea kusema kwamba wameweza kugundua kwamba vijana watanzania wanakabiliana na changamoto kuu nne; ambazo ni

·         Fikra,kwamba kuna watu wenye fikra Kubwa,fikra ya wastani na fikra ndogo

Ili kujikwamua ni lazima vijana waamue kuwa na fikra Kubwa.

·         Uelewa wa kuongeza thamani katika shughuli za Uzalishaji Mali (Value Addition)

·         Upatikanaji wa Mtaji kwa gharama nafuu

·         Mifumo ya kiutendaji kama leseni,lugha,rushwa e.t.c

Tuesday, May 14, 2013

Dare to Different by Pastor Yared Dondo


From the Altar


Pastor Dondo

Opening Scripture Daniel 1:18-20

“18 At the end of the time set by the king to bring them into his service, the chief official presented them to Nebuchadnezzar. 19 The king talked with them, and he found none equal to Daniel, Hananiah, Mishael and Azariah; so they entered the king’s service. 20 In every matter of wisdom and understanding about which the king questioned them, he found them ten times better than all the magicians and enchanters in his whole kingdom”.

From above scripture Daniel and his fellows made a difference in their society,they were ten times better than all magicians and enchanters of Nebuchadnezzar.

As Christians we have to ask our selves the followings questions;

          Why are we here on Earth

          Where are we going

          How will we go there

We should be transformed so that we can transform others

In this world we can experience pressure from every part like health, finance, relationship, family and many more, we will be able to stand them if we have been transformed

There are Three that we can learn from Life of Daniel;

1. He Knows he was

Though he was in captive he date to be different, he understand who he was, he knows his position that he was not ordinary.

In our society there a lot of opportunities, resources and potential we should take a advantage of them to move forward because the same spirit that was in Daniel is in us also.

Ask yourself why are you in that job, business ,school, partnership and determine to make a difference wherever you are

Monday, May 13, 2013

MAOMBI YA ULINZI – Sehemu ya Pili na Mchungaji Florian Katunzi


Rev Florian Katunzi
*CHIMBUA KIFUSI, NG’OA MAGUGU YOTE.

*Mwanzo 26:12 - 22, Hagai 2:6-9
Maisha ya ustawi wa watu wengi wa Mungu adui ameutupia kuufukia kwa kifusi.

*Mathayo 13 : 24-28               
“ Bwana Yesu Kristo akawatolea mfano mwingine akisema, ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika bonde lake lakini watu walipolala akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano akaenda zake, baadaye majani ya ngano yalipoanza kuzaa yakaonekana na magugu, watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia Bwana hukupanda mbegu njema katika bonde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawambia adui ndiye aliye tenda”

Katika maisha yetu ya wokovu, ni maisha kamili yenye mamlaka kamili ya kimungu. Hivyo lazima maisha yetu ya kiroho yastawi sambamba na maisha yetu kimwili. Yesu Kristo anatoa mfano wa mkulima aliyelima bonde akapanda ngano(mbegu ya ngano) alipolala(hakulinda shamba) akaja adui akapanda magugu katikati ya ngano.

Hivyo katika bonde moja kukawepo mbegu za aina mbili, mbegu ya ngano na mbegu ya magugu na vyote vikaota vikamea vikatoa matunda sawa sawa na mbegu yake, mbegu ya ngano ikazaa ngano na mbegu ya magugu ikazaa magugu.

Katika somo hili nataka tujifunzi juu ya kazi ya Yesu Kristo.

*Wakolosai 1:13

“Naye alituokoa toka nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza ufalme wamwana wa pendo lake”.

Kristo Yesu anafanya mambo matatu makuu pale anapoingia ndani ya mtu.

(A)  Anamwokoa toka nguvu za giza, nguvu za mauti na kuzimu.

(B)  Anatuhamisha  toka katika ufalme wa shetani.

(C)  Anatuingiza katika ufalme wa Mungu.

Wednesday, May 8, 2013

City Harvest Church Welcomes you to Career Exploration Seminar


Career Exploration is not properly understood and sometimes it has been misinterpreted in our society, this has made people to make wrong choices when it comes to career.

 
Knowing that City Harvest Church, a Church for young professional who are committed to excellence  in collaboration with Organizing Committee has prepared a Career Exploration Seminar for you a Young Professional, Student, Parent or Guardian with Questions about Career Exploration

When speaking to Dr. Tumsifu Elly the Chairman of Organizing Committee for this Seminar, he said people should expect to understand the following after the Seminar;

          Where to concentrate Career wise

          Options available towards Career Development

          In Depth assessment on Career

 
The Seminar will be conducted this Saturday 11th May,at City Harvest Church from 10:00 a.m to 3:00 p.m
Entrance : FREE
 
This is a Never Miss Seminar
 

You are All Welcome

Monday, May 6, 2013

Habari Zaidi: kutoka mlipuko katika Parokia teule ya Olasiti, Arusha


Kanisa la Olasiti lililolipuliwa

Kwa hisani ya Wavuti........

UPDATE/TAARIFA MPYA
·       Kijana mmoja anashikiliwa na Polisi kama mshukiwa wa mlipuko huo (inadaiwa alipokamatwa   alikutwa na stock nyingine ya mabomu)
·         Mtu mmoja amefariki (mwanakwaya)
·         Waliojeruhiwa jumla ni 66.
 
Majina ya waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospitali za maunt Meru, na hospitali teule ya jiji la Arusha ya St Elizabeth wametambulika kuwa ni:- John Thadei, Regina Fredirick, Joram Kisera, Novelt John, Rose Pius, John James, Anna Kessy, Joan Temba, Neema Kihisu, Gloria Tesha, Innocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, Simon Andrew, Anna Edward, Lioba Oswald, Rose Pius, Philemon Gereza, Kisesa Mbaga na Beata Cornell.

Majeruhi wengine na umri wao katika mabano, ni Consensia Mbaga (53), Christopher Raymond (10), Deborah Joachim (24), Elizabeth Isidori (24), Anna Didas (52), Bertha Cosinery (49), Edda Ndowo (77), Derick Cyprian (8), Faustine Andrea (35), Mary Okech, Mesoit Siriri (33), Clenes pius (22), Joyce yohana (15), Restituta Alex (50), Mathias Riha (74), Magreth Andrew(45), James Gabriel (16), Regina James (17), Elizabeth Masawe(15), Elizabeth Sauli (18), Njau (35), Yasinta Msafiri (16) Doreen Pancras (28), Alex Arnold, Agripina Alex (9), James Gabriel (16), Loveness Nelson (17), Amalone Pius (25), Frank Donatus (10), Alphonce Nyalandu (26), Athanasia Reginald (14), Phillemon Ceressa (49), Neema Daud (13), Sophia Kanda (72), Theofrida Innocent (21) na Regina Darnes(17).
 

Thursday, May 2, 2013

Vitu Muhimu vya kuangalia unapojiandaa kupata mwenzi wako wa maisha.......Part IV


 
Leo tutaanza kuangalia vitu unavyotakiwa kuangalia kwa mtu unayetegemea kuwa mwenzi wako wa Maisha;

Tutaanza na Jambo kubwa muhimu ambalo likikosewa linaleta matatizo makubwa kwa wanandoa,na wengi wamekuwa wakiangalia sana vitu vya mwilini wanalisahau jambo hili,twende tujifunze;

1.      Uhusiano wake na Mungu ukoje

Kitu cha muhimu sana na utakachokipa uzito angalia uhusiano wa huyo anayetaka kuwa mwenzi wako ni uhusiano wako na Mungu ukoje? Je amempokea Yesu kama Bwana wa Maisha yake,kama ndio sio uishie hapo unaendelea mbele enhee je maisha yake ya wokovu yakoje ? Je yuko makini kiasi gani na vitu vya Mungu,maana mwingine ameokoka lakini hana umakini kabisa na Mungu na maisha yake yuko busy na mambo mengine tu ya kidunia zaidi. Mwingine unakuta anakuwa busy kanisani,anaimba kwaya,ni muhudumu lakini anafanya tu kwa interest sio kwamba anafanya kwa sababu anampenda Mungu ni hobby tu sasa mpendwa usidanganike na mtu ambaye anajionyesha yuko busy tu lazima umsome ana ushirika gani na Mungu. Hili eneo la mahusiano yake na Mungu nalo lina vipengele vichache ambavyo tutataangalia;

a.      Je ana hofu ya Mungu

Mtu mwenye hofu ya Mungu anakuwa makini sana na mambo ya Mungu,na anampa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yake. Yaani kabla hajakwambia utajua huyu mtu anamuogopa Mungu.

Hili utaliona kwa jinsi anavyofanyia watu wengine kama washirika wenzake,wafanyakazi wenzake au wanafunzi wenzake na pia familia yake.

Mtu mwenye hofu ya Mungu anaogopa dhambi na hachukulii vitu vya Mungu kwa mazoea zoea tu. Kinawachowaponza watu wengi ni ile kuzoea wokovu,mtu anazoea wokovu na anaanza kuchanganya mambo ya kidunia anayaweka katika wokovu.

b.      Je ni Mcha Mungu

Tukiangalia Neno la Mungu katika Mithali 16: 6 “Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha Bwana watu hujiepusha na maovu”,katika neno hili tunaona umuhimu wa mtu kuwa mcha Mungu

Itamsaidia kujiepusha na maovu, Ule uchaji ambao uko ndani yake utamfanya aogope kutenda dhambi. Kwahiyo utakuwa na uhakika kwamba atakuwa ni mume au mke sahihi kwako kwasababu atakuheshimu wala hatakunyanyasa maana anao uchaji wa Mungu ndani yake,Haleluya! Kwahiyo mpendwa angalia sana huyo mpendwa kama anasema ameokoka je uchaji wake ukoje? Maana watu wengine wapo wapo tu nani rahisi kuzolewa na upepo wa Ibilisi na kufanya yale mambo ambayo Ibilisi anapenda.