Monday, January 7, 2013

Nyimbo za Injili zilizong`aa mwaka 2012



Tunapouanza mwaka mpya wa 2013 ningependa turudi nyuma kidogo tuangalie ni nyimbo gani za Injili zilizotesa au kung`aa mwaka uliopita wa 2012.

Rose Muhando


Utafiti huu niliufanya nikiangalia nyimbo ambazo zilipigwa sana kwenye sherehe mbalimbali kama Harusi,Send Off,Kitchen Parties,Batizo,Vipaimara na sherehe nyinginezo za wakristo.

Christina Shusho

Yaani ukienda kwenye sherehe Fulani lazima hizo nyimbo zipingwe na kwakweli watu walizipenda na wanazipenda sana maana ukumbi mzima utashangaa unasimama na kucheza tena cha ajabu unaona watu wa imani mbalimbali wakifurahia na kucheza nyimbo hizo zikipingwa,kingine nilichoshangaa ni kwamba tena unakuta mtu ni wa imani nyingine lakini anaimba wimbo wote.Hii inaonyesha kukubalika sana kwa nyimbo hizo.

Enoch Jonas katika moja ya matamasha
Nyimbo hizo ni Wema wa Mungu wa Enock Jonas,Utamu wa Yesu wa Rose Muhando,Nipe Macho wa Christina Shusho.
 


Rose Muhando



 

Wimbo wa Enock Jonas licha ya kuburudisha pia unafurahisha sana maana kuna maneno haya shetani na mama mkwe wake wanalia eenh …ha ha ha I see itabidi nimtafute huyo mtumishi anieleze huyo mama mkwe wa Devil ni nani au ni njia tu ya kufikisha ujumbe kwamba shetani na ukoo wake wanalia.

Christina Shusho


Nawapongeza sana waimbaji hawa na waimbaji wote wa Nyimbo za Injili Tanzania,Mungu awabariki na kuwaongezea maarifa zaidi mnapoendelea kuifanya kazi yake huku mkiburidisha jamii.

 

2 comments: