Rev Florian Katunzi |
*CHIMBUA KIFUSI, NG’OA
MAGUGU YOTE.
*Mwanzo 26:12 - 22, Hagai
2:6-9
Maisha ya ustawi wa watu
wengi wa Mungu adui ameutupia kuufukia kwa kifusi.
*Mathayo
13 : 24-28
“ Bwana Yesu Kristo
akawatolea mfano mwingine akisema, ufalme wa mbinguni umefanana na mtu
aliyepanda mbegu njema katika bonde lake lakini watu walipolala akaja adui yake
akapanda magugu katikati ya ngano akaenda zake, baadaye majani ya ngano
yalipoanza kuzaa yakaonekana na magugu, watumwa wa mwenye nyumba wakaenda
wakamwambia Bwana hukupanda mbegu njema katika bonde lako? Limepata wapi basi
magugu? Akawambia adui ndiye aliye tenda”
Katika maisha yetu ya
wokovu, ni maisha kamili yenye mamlaka kamili ya kimungu. Hivyo lazima maisha
yetu ya kiroho yastawi sambamba na maisha yetu kimwili. Yesu Kristo anatoa
mfano wa mkulima aliyelima bonde akapanda ngano(mbegu ya ngano)
alipolala(hakulinda shamba) akaja adui akapanda magugu katikati ya ngano.
Hivyo katika bonde moja
kukawepo mbegu za aina mbili, mbegu ya ngano na mbegu ya magugu na vyote
vikaota vikamea vikatoa matunda sawa sawa na mbegu yake, mbegu ya ngano ikazaa
ngano na mbegu ya magugu ikazaa magugu.
Katika somo hili nataka
tujifunzi juu ya kazi ya Yesu Kristo.
*Wakolosai 1:13
“Naye alituokoa toka nguvu
za giza, akatuhamisha na kutuingiza ufalme wamwana wa pendo lake”.
Kristo Yesu anafanya mambo matatu makuu pale anapoingia
ndani ya mtu.
(A) Anamwokoa toka nguvu za giza, nguvu za mauti
na kuzimu.
(B) Anatuhamisha toka katika ufalme wa shetani.
(C) Anatuingiza
katika ufalme wa Mungu.
Baadaye ya hatua hizi Yesu
anatupa mamlaka za kifalme wa mbinguni.
*Luka 9:1 “Akawapa uwezo
na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi”
*Mathayo 16: 18-19
“Juu ya mwamba huu
nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitalishinda ,Nami nakupa wewe
funguo za ufalme wa mbinguni na lolote utalofunga duniania litakuwa limefungwa
mbiguni na lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.”
FUNGUO ZA UFALME WA mbinguni
tunazo katika Kristo Yesu, Yesu anasema watu walipolala adui akaja akapanda
mbegu za magugu katikati ya mbegu njema za ngano.
Maombi ya ulinzi niya muhimu katika ustawi wa maisha
ya kiroho na kimwili, mtu wa Mungu uliyeitwa kwa jina la Bwana wewe ni mlinzi
wa maisha yako, watoto wako na mali zako.
Maisha yako lazima yawe yameunganishwa (connected) na
madhabahu ya Mungu aliyehai, funguo za Baraka ,funguo za ustawi wako , funguo
za mali ziko mikononi mwako sio nje yako.
Isaka alikuwa mbarikiwa wa Bwana, lakini baada ya kufa
baba yake mzee Ibrahim, mali za Isaka zilipukutika zote matokeo yake akajikuta
katika njaa nzito maana wafilisti walimwonea wivu wakamdhoofisha kwa kuvifukia
visima vya maji wakajaza kifusi.
*Mathayo
26:15
“Na
vile visima vyote walivyovichimba, watumwa wa baba yake siku za ibrahimu babaye
,wafilisti walikuwa wamevifukia wakavijaza kifusi.”
Lakini Isaka baada ya kukaa Gerari miaka mingi , mwisho
akamua kulima shamba pale Gerari Bwana akambariki na akamstawisha, watu wa
Gerali wafilisti wakamwonea wivu tena.
*Mwanzo 26:14
“Akawa na mali
ya kondoo na mali ya ngo’mbe na watumwa wengi”
Abimeleki mfalme wa wafilisti akamwambia Isaka utoke
kwetu, maana una nguvu sana kuliko sisi, Isaka alipoinuka katika Mungu akafanya
yampasayo kufanya mbele za Mungu na Baraka zilionekana tena kwake wale waliomdhalau
kwanza, wakatambua Isaka anazo nguvu za tofauti kuliko za wafilisti. Isaka
akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyo vichimba siku za Ibrahimu
babaye maana wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake ibrahimu.
-Katika Mungu , mtu wa Mungu anapojisahau akalala, adui utumia mwanya
huo kufukia Baraka zetu maana jukumu la kulinda(Kuomba) si la Mungu bali ni
letu. Katika huduma yangu nimekutana na watu wengi wamefungwa na nguvu nzeto za
shetani.
Dada mmoja akaja kwangu akasema, kila nikipata mchumba,
uchumba unavunjika sabababu
zisizokojulikana mchumba anasema hasikii Amani, lakini baada ya kumwombea nguvu
za majini zikajidhihirisha nguvu za giza na kudai huyu ni mke wetu tumemfunga
sisi tunataka awe Muhuni tu sio kuolewa. Baada ya mapambano makali akafunguliwa
nikamwambia sasa lazima utaolewa, lakini baada ya miezi kama sita
akaja akaniletea taarifa amepata mchumba, nikamsihi kuendelea na maombi baada
yakupata mchumba lakini hakufanya hivyo bali kwa furaha aliyokuwa nayo akaamua
kuwashirikisha marafiki zake wawili akawapa mpango mzima wa uchumba wake na
mipango ya harusi, marafiki wakamwonea wivu.
Rafiki wa kwanza(M.S) akachukua jina lake huyu binti na
la mchumba wake akaenda kwa mganga mmoja pale tandale anaitwa (Mohamed Mohamed ni mzanzibar)
akamloga yule binti akamtupia jini nuksi akamfanya awe nuksi, akamfanya yule
mchumba wa binti awe mzito awe mzito akamtupia jini farakana wakamfarakanisha na huyu binti
na mchumba wake.
Rafiki wa Pili(L.K) akaenda kwa mganga pia pale Ilala
anaitwa Aziz, huyu mganga akamtupia jini yule binti asionekane tena kwa mchumba
wake,aonekane mwenye sura ya kizee.
Ndipo huyu binti anakuja ofisini tena, akaniambia
mchungaji mambo yameharibika tena na analia kwa uchungu. Baada ya ushauri
nikataka kujua kwanini mtu niliyemuombea akafunguliwa kafungwa tena, nikamwambia piga magoti
nikamuita Yesu Kristo mwenye nguvu na ndipo pepo nuksi akapiga kelele akidai
kwanini nawafata fata sana, nikamtiisha chini ya mamlaka kuu ya
kimungu na pepo akasema yote ndipo nikamuuliza
mmerudi humu kwa kutumia mlango gani? Wakajibu yeye mwenyewe huyu binti
haombi analala tu na anakaa na marafiki zake wa zamani( kupiga story) ana
maongezi yasiyofaa, hivyo yeye tumemwingia kwa njia hiyo tu, huyu ameokoka sio
mzinzi lakini dhaifu, ndipo nikayaamuru yatoke nikadhibatilisha nguvu zote
nikachimbua na kung’oa magugu ya pepo nikaamuru na kumfungua mchumba wake yeye
mwenyewe.
Kuokoka pasipo kudumu katika maombi utafungwa na nguvu
za giza utafungikika, utaanza kuangaika kutafuta maombizi, mkristo usitegemee
upako wa kununua, usitegemee upako wa mafuta na maji, usitegemee upako wa
sabuni na chumvi hapana upako nje ya maombi, upako wa uweza wa Mungu
unapatikana ndani mwa maombi tu.
*Luka
6:12-19
“Ikawa
siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika
kumwomba Mungu.” Na makutano walikuwa
wakitaka kumgusa kwasababu uweza ulikuwa ukimtoka kiponya wote.
Wako watu wengi
wakristo maisha yao yamejaa kifusi ba magugu, adui amefukia visima vyao vya
Baraka, visima vyao vya utajiri na huduma. Bwana asema lazima tujifunge silaha
zetu tupigane vita maana ingawa tunaenenda katika mwili hatufanyi vile kwa
jinsi ya mwili. Wale waliofungwa katika madhabahu za kichawi sharti waje
wasimame na familia zao na mali zao mbele za Bwana.
* Ayubu 1:5 “ Ayubu hutuma
kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema na kusongeza sadaka za
kuteketezwa kama hesabu yao wote”
Ayubu aliomba kama mlinzi wa familia yake akatoa sadaka
kwa ajili ya watoto wake. Unaposimama mbele za Bwana tambua wewe ni mlinzi wa
taifa, watoto wako na mlinzi wa mali zako
*Mwanzo
19: 1 – 38
Ibrahimu
alisimama akaomba ulinzi juu ya kifo kwa jamaa yake Lutu akamwombea ulinzi
wakimungu.
*Mwanzo
19 : 29 “ Ikawa Mungu alipoharibu miji ya bondeni (Sodoma na Gomora) Mungu
akamkumbuka I brahim akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo ya
aliyootoka Lutu.”
Lutu aliokolewa na Mungu si kwa haki yake bali Mungu
aliyaangalia maombi ya mtumishi wake aliyesimama mchana na usiku mbele zake.
Lutu na familia yake waliishi maisha ya vugu vugu hata baada ya kuokolewa, Lutu
akawa mkulima na mlevi wa pombe , akanywa pombe na binti zake akazaa nao pia ,
uchafu mzito binti mkubwa akazaa nae mtoto akamwita Moabu na binti wa pili
akazaa mtoto akamwita Benani ndiye baba
wa Amoni.
Maombi yako mama, baba, kijana yatainua uzao wako,
jamaa zako, kazi zako, ndoa yako na ustawi wako pia. Tunakwenda kutikisa mkuu
wa anga hili, mkuu wa nchi kavu na mkuu wa majini, watu wengi wamefunikwa kwa
nguvu za mkuu wa anga hili yule kerubi afunikaye.
Nilioombea mama mmoja anasema tangu azaliwe maisha yake
niya shida na misukosuko, katika kumwombea majini yanapiga kelele kwa kilio cha
uchungu yakidai huyu ni mtu wetu usimfungue si ameokoka tu mwache usimfungue
uchumi wake maana nyota yake ndiyo tunayotumia , huyu ni mtu mkuu sisi tumepewa
na babu yake tangu akiwa mimba tuliingia kwa njia ya mtoli ambao shangazi yake
alimpikia mama yake akiwa mjamzito alipokunywa tukaingia ndani.
Wakati wewe unasubiri mtoto azaliwe ndipo uombe mapepo
yanaingia akiwa bado tumboni. Nguvu za giza nikapambana nazo kama masaa matatu,
maana zilikuwa ni nguvu za kutisha
mno maana walitaka huyu mama awe
malkia wa anga, wakapinga nisendelee
kuomba wakidai wewe unatuharibia kazi
zetu, tumekubali watu waokoke wasiende
mbinguni, hubiri hivyo lakini usiwafungue uchumi wao.Nyota ya huyu mama nikubwa
inatumiwa na kufanya biashara akiwemo na mjomba wake yuko Arusha tajiri,lakini
sasa umeharibu tulikuwa tunataka ende Arusha akafanye zinaa na mjomba
wake lakini sasa unatuchoma.
-Katika ulimwengu war oho kuna mambo mazito mno hata
mengine hayasemeke, makafara mazito
yanatolewa, damu zinamwagwa shetani anakunywa damu za watu. Mwisho nikamfungua
mama Yule kwa jina la Yesu Kristo
*Yeremia
1:5
“Kabla
sijakuumba katika tumbo nalikujua na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa
nimekuweka kuwa nabii wa mataifa”
Usifanye mzaha adui yuko kazini kinyume na ustawi wetu,
kinyume na taifa letu , imenilazimu sasa kuombea watoto wetu.
-Sasa wanauliza kwanini nimeitisha maombi ya kuombea
Taifa, wanasema lazima tunywe damu za watanzania hapa ipo madhabahu yetu,
unapinga vita mbona ni mapatano ya watu wetu waliokoka hapa na kule ili damu ipatikane ili mambo yao yawanyokee.
Nami nikasema lazima tung’oe madhabahu zote za kishetani ndani ya taifa
letu.Tunaomba mbele za Mungu kwa maombi ya siku tatu yakung’oa madhabahu
tutafunga na kuomba, tutamtolea Mungu sadaka na kujenga madhabahu ya ulinzi.
*Luka
11:21-22
“Mtu
mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake alindapo nyumba yake,vitu vyake vi salama
, lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda amnyang’anya
silaha zake zote alizokuwa akizitegemea na kuyagawanya mateka yake.”
Amina nimebarikiwa sana na hili somo Mungu azidi kutetea watenda kazi wake...
ReplyDeleteMtumishi upo JUU. Mungu akutie nguvu, ni kweli wakristu wengi tunashindwa kutumia MAMLAKA na kusoma NENO. Endelea kuturushia zaidi na zaidi masomo mengi yanatujenga. Pia maombi ya vita na kupata upenyo binafsi ningefurahia sana. Barikiwa. Emma Dismas
ReplyDeleteBaba nimefurahi sana juu ya somo lako ni kweli kabisa wakristo wengi tunaamini ukiokoka tu ndiyo umemaliza kila kitu kumbe unahitaji kupambana siyo kidogo. asante sana mtumishi wa Mungu endelea kutoa masomo.
ReplyDeletePhillip Bugobora
Shalom! MUNGU akubariki kwa somo hili zuri, mara nyingi nimekuwa nikimlaum MUNGU, pasipo kujua, ninefunguka mno! Nitafanyia kazi maarifa haya ya neno la MUNGU .
ReplyDeleteMtumish wa Mungu Mchungaji Katunzi Mungu aendelee kukuinua na kukutumia. tuko nyuma yako Baba
ReplyDeleteMtumishi wa Mungu Mchungaji Katunzi Mungu aendelee kukutumia maana kazi yako si bure atakulipa taji. Tuko nyuma yako baba. Amina
ReplyDeleteTudumu daima katika imani ya Mungu wa kweli, sala, maombi, na kujitakasa ili shetani asipate nafasi. Asante sana mtumishi wa Mungu hasa katika shuhuda. Mimi binafsi hizo shuhuda za watu ulizotueleza zimenifungua sana na zimeniongezea uchaji wa Kimungu zaidi.
ReplyDelete