Edson Mwasabwite |
Wiki iliyopita nilipata nafasi ya kufanya Interview na Muimbaji wa nyimbo za Injili hapa Tanzania,aliyeimba nyimbo zinazobariki wengi twende tuone anasemaje;
Blogger: Naomba majina yako kamili,na je unatumia
Jina tofauti la kisanii? Tungependa kulijua pia ili jamii iweze kukutambua kwa
urahisi.
Jina langu ni Edson Mwasabwite
Jina langu ni Edson Mwasabwite
Blogger:Umeokoka na unaabudu wapi
Ndio,KKKT
Kijitonyama
Blogger Historia yako kwa Kifupi ya
kuimba,yaani ulianzaje na wapi?
Tangia utoto,sana Sunday
School Mbeya-Rungwe,UWAKI-Umoja wa Watoto wa Kikristo,alivyoanza kujitambua
akagundua ana kipaji cha uimbaji.
Blogger:Katika
kuimba kwako je umeshatoa Album au single yoyote? Itaje ina nyimbo ngapi?
Ninayo
moja iko katika Audio Cassete,CD,VCD &
DVD,Inaitwa ni kwa Neema na Rehema,ina nyimbo nane ,ila
ninaandaa Albam ya pili ndio anaiandaa
Blogger: Wimbo unaoupenda katika nyimbo
zako
NI KWA NEEMA NA REHEMA
Blogger:Ni
kwanini unaupenda huo wimbo/nyimbo
Kwasababu
hakutegemea kama atafika alipo ni kwa neema tu na rehema,na pia ameishi maisha
magumu maana aliachwa Yatima. Hii ni historia ya maisha yangu. Wokovu wenyewe
ni kwa neema akiangalia vijana wengine yeye yuko salama zaidi. Amen
Blogger:Nani
anasambaza kazi zako? Je anakusaidia vizuri?
UMOJA
AUDIO VISUAL
Blogger:Kuna
mafanikio gani umeyapata katika kuimba kwako nyimbo za Injili
Mafanikio yapo,japo kwa mtu mwingine yanaweza kuonekana kama sifuri ila
mafanikio inategemea na huyo mtu yuko katika nafasi au ngazi gani. Ingawa ndio
nimeanza naona mafanikio,namshukuru Mungu.
Blogger:Umekutana
na changamoto gani katika safari yako ya kuimba
Ndio,hasa
mtu anapoanza kuimba maana kuna mtu anataka kufanya ila unakuta fedha mara
nyingine inakuwa ni kikwazo ili kuweza kuiweka uimbaji wako katika viwango vya
juu.pili,
watu wengine wanakushauri vibaya kwa makusudi ili uanguke
tatu,hakuna
ushirikiano kwa wale walio wazoefu katika muziki wa Injili,hii imesababisha
hata hasara maana huna mwongozo kutoka wazoefu
Blogger:Unaonaje Music wa Injili hapa
Tanzania?
Wanafanya vizuri
ila kuna changamoto ya utaalamu,wasikilizaji na jamii kwa ujumla hawajaupa nafasi
sana. Watu wengi wanauchukulia kama burudani tu swala la kuelimisha na
kusisimua. Ila tunashuru Mungu kwamba watu wanatuunga mkono. Na ndio maana
utakuta nyimbo zinazohit ni zile za kuburudisha zaidi. Kwa Tanzania Mungu
ameupa musiki wa Injili Neema.
Blogger:Na Unatoa Ujumbe gani kwa waimbaji
wa Nyimbo za Injili ambao kwa njia moja au nyingine wanajisahau na
kujichanganya na mambo ya dunia hii
Ujumbe
wangu kwa waimbaji wenzangu wa nyimbo za Injili,ujue kama unahubiri kwahiyo uwe
mfano na wakili,tusiwe kama vibao lakini tusiende huko. Yesu alisema itamfaa
nini mtu apate vya dunia na kuikosa mbingu.
Blogger:Zaidi ya kuimba ni kitu gani
kingine unachofanya
Mfanyabiashara,Mungu
amenipa karama hii,kwasasa niko kiutumishi zaidi.
Blogger:Je
kimaisha je uko wapi? Umeoa au Hujaoa bado? Watoto wangapi?
Niko Dar,sijaoa,namuomba Mungu anipe yule aliyekusudia maana ukosee
kujenga nyumba au kurekodi nyimbo utarejea lakini si kuoa naomba Mungu anipe
aliyenikusudia. Sina mtoto
Blogger:Una Ujumbe gani kwa Waimbaji wa
Nyimbo za Injili hapa Tanzania
Tuwe
barua mtu akituona ajue kweli huyu anamwimbia Mungu aliye hai. Tujiandae kuimba
mbinguni sio kupata sifa hapa duniani
Blogger: Una Ujumbe gani kwa Jamii
inayoburidishwa na nyimbo za Injili
Wawe tayari
kuelimishwa pia na nyimbo za Injili na si kuburudika tu,wajue tunaishi kwa
neema tu wajue Mungu ndio ametupa vyote tulivyo navyo,ambao hawajaokoka
wampokee Yesu Kiristo.Vyote tulivyo navyo bila Kiristo ni bure wajiulize
wataishi wapi baada ya maisha haya.
Hongera sana kaka..Nyimbo zako ni nzuri sana na zinagusa maisha yangu kwakweli..katika mkesha wakuingia mwaka huu wa 2013 pale Mikochen B Ilipofika saa 6 tu ulipigwa kwa neema tu na rehema..yani I was so bleced that day..keep it up and remember Jesus is Lord..
ReplyDeleteJesus is Lord! Bwana Asifiwe sana.
ReplyDeleteAlelujah! Ni ukweli usiofichika kwamba, haijalishi kama ni tajiri au masikini njia ni moja; ukiangalia waliotutangulia utajua kabisa kweli sisi binadamu humu duniani tunaishi kwa neema tu.