Wednesday, February 27, 2013

Je unajua Jacson Benti zaidi ya kuimba anafanya nini zaidi? Fuatana nami.....



Jackson Benti muimbaji wa Nyimbo za Injili

Wiki hii Rejoice and Rejoice Blog imeweza kufanya mahojiano na muimbaji mahiri sana wa  nyimbo za Injili hapa Tanzania

Blogger: Naomba majina yako kamili,na je unatumia Jina tofauti la kisanii? Tungependa kulijua pia ili jamii iweze kukutambua kwa urahisi.
Majina yangu ni Jackson Benty,jina la kikazi huwa napenda kutumia St.(Saint)Jackson Benty

Blogger:Umeokoka na unaabudu wapi
Nimeokoka,naabudu katika kanisa liitwalo Jerusalem,liko hapa Majengo,Arusha

Blogger Historia yako kwa Kifupi ya kuimba,yaani ulianzaje na wapi?
Nilianza kuimba nikiwa mtoto kabla ya kuanza shule ya msingi,lkn nilianza kuifanya huduma kama kazi mwaka 2001 nikiwa na marehemu Fanuel Sedekia.



 Blogger:Katika kuimba kwako je umeshatoa Album au single yoyote? Itaje ina nyimbo ngapi?
Nimeshatoa album tano,kati ya hizo kuna video mbili ambazo ni Mwanangu na Nataka Nifanane Nawe.Zingine ni Ndiwe Mungu,Kwako Mpenzi yenye nyimbo za aina ya taarab lkn ya injili na U wa Thamani ambayo ina nyimbo za vitabuni.

Blogger: Wimbo unaoupenda katika nyimbo zako
Kila album ina nyimbo zaidi ya mbili ninazopenda

Blogger:Ni kwanini unaupenda huo wimbo/nyimbo
Kila wimbo una kitu cha pekee kinachonitia nguvu

 Blogger:Nani anasambaza kazi zako? Je anakusaidia vizuri?
Albums zote ziko kwa wasambazaji tofauti,na kila mmoja anafanya kwa sehemu na uwezo wake.
 
Blogger:Kuna mafanikio gani umeyapata katika kuimba kwako nyimbo za Injili
Mafanikio ya kwanza ni kusaidika kiroho,maana kadiri ninavyotaka kupiga hatua ya kufanya vizuri inanilazimu kupiga hatua ya kiroho pia.Namshukuru Mungu kwa kuzitumia nyimbo hizo kugusa na kubalisha maisha ya wengi wanaozipata.Vile vile kazi hii inanisaidia kupata mtandao mkubwa kadiri ninavyoendelea,hivyo kufanya maisha yangu ya kimwili kubadilika na kuwa bora zaidi.Kwa sasa Mungu ametuwezesha kuishi kwa kufanya kazi hii ya injili hata kuwa na studio yetu ya Audio Recording.

 Blogger:Umekutana na changamoto gani katika safari yako ya kuimba
Changamoto zimekuwepo na zipo,lakini Mungu Mkuu kuliko changamoto zote anayetupa kushinda na zaidi ya kushinda anakaa ndani yetu na anatenda kazi.Ziko nyingi,baadhi ni namna ya kufanikisha kukitoa kile kilichiko ndani yangu ili kiwafikie watu kama kinavyotakiwa,ikiwa ni pamoja na recording ya audio na video.mazingira ya mazoezi ili kutuwezesha kufikia hatua ya kufanya muziki ambao ni live.

Blogger:Unaonaje Music wa Injili hapa Tanzania?
Muziki wa Nyimbo za Injili Tanzania naona unakua,waimbaji wanaongezeka kwa kasi na Mungu ni Mwema,wanaoongezeka sehemu kubwa wanafanya vizuri sana.Pamoja na kukua kwake bado mafanikio yake sio makubwa kimauzo ambayo ni pamoja na ufikaji wa huduma hiyo kwa watu kwa wakati na katika hali inayotakiwa.

 Blogger:Na Unatoa Ujumbe gani kwa waimbaji wa Nyimbo za Injili ambao kwa njia moja au nyingine wanajisahau na kujichanganya na mambo ya dunia hii
Ujumbe kwa waimbaji wenzangu,kwanza wamebarikiwa.Kuweza kufanya kazi kwa hatua ya kwanza tayari ni baraka.Mungu tunayemtumikia yu hai anatuona na anajishughulisha na mambo yetu,hajatusahau,hivyo tuwe waangalifu tusije tukamsahau huku tukiendelea kufanya kazi yake.Pamoja na kuwa watumishi wa Mungu,tutunze sana kubaki tukiwa wana wa Mungu.

Blogger:Zaidi ya kuimba ni kitu gani kingine unachofanya
Zaidi ya muziki wa injili nafanya huduma nyingine ya kufundisha neno la Mungu,mimi ni mwalimu.

 Blogger:Je kimaisha je uko wapi? Umeoa au Hujaoa bado? Watoto wangapi?
Nimeoa,nina mke mmoja na Mungu ameshatujalia mtoto mmoja wa kiume.



Jackson Benti,Rejoice and Rejoice Blog inakutakia Baraka tele unapoendelea kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji,Mungu aendelee kukuinua kutoka hatua moja hadi ya juu zaidi,uendelee kuwa taa na chumvi kwa kupitia huduma yako. Amen

 

 

 

 

 

 

4 comments:

  1. Hongera Jack..Mungu wa mbinguni na akubariki kwa baraka zote za Rohoni na mwilini..

    ReplyDelete
  2. nakupenda sana Mungu akupe nguvu

    ReplyDelete
  3. Hakika namtukuza Mungu kwa ajili yako.Ubarikiwe zaidi na zaidi.

    ReplyDelete
  4. naupenda sana wimbo wa "u wa thamani" lakini cjauona niupate wapi??

    ReplyDelete