Watarajiwa...... |
Leo tunaendelea na somo letu la tano juu ya vitu muhimu vya kuangalia unapotafuta au kijuandaa kuwa na mwenzi wa maisha.
Tunapoendelea na somo hili ambalo ni pan
asana,tumelichambua vizuri sana tukiangalia vitu muhimu ambavyo mhusika
anayetegemea kupata au kutafuta mwenzi anatakiwa ahakikishe anavifanyia
kazi,halafu tuliendelea kuangalia sasa vitu gani muhimu uangalie kwa huyo
anategemea kuwa mwenzi wako.
Hivi vipengele ni muhimu sana kwa wewe ambaye
unategemea kuingia kwenye ndoa na pia hata kwa mwanandoa maana vitakusaidia
kutengeneza kwa upya juu ya ndoa yako.
Ni maombi yangu somo hili likawe Baraka na kukupeleka
katika lile kusudi ambalo Mungu analo juu yako juu ya mambo ya ndoa.
Tuendelee..
3. Je huyo
mtu anakupenda kwa dhati
Ni muhimu sana kuwa na uhakika wa kiasi cha upendo alichonacho mtarajiwa wako. Mwingine
anaweza kuwa na wewe kwasababu tu labda amevutiwa na umbile au vitu ulivyo
navyo.
Kuna mpendwa mmoja aliingia kwenye uhusiano akifikiri
kwamba huyo mtarajiwa anampenda,basin a yeye akajitoa san asana kwake,kumbe
yule mtarajiwa alikuwa tu anapenda kuwa na yule mpendwa kwasababu alikuwa ana uwezo wa kifedha. Sasa
hii ilikwenda hivyo ila kitu kizuri ni kwamba yule mpendwa alikuwa na mahusiano
mazuri na Mungu wake,basi akawa anaendelea kumuomba Mungu juu ya ule uhusiano
ndipo siku akaja kugundua kwamba yule mpendwa ana mahusiano na mtu mwingine
ambaye sasa ndio anayempenda ila yeye alikuwa anamtumia tu kwasababu ana hela.
Ashukuriwe Mungu maana hakuruhusu waingine katika ndoa,maana angeteseka sana
huyo mpendwa kuwa na mahusiano na mke au mume ambaye hakupendi.
Nimetoa ushuhuda huu kukupa tahadhari na kukuonyesha umuhimu
wa kuwa na mahusiano na Mungu kama nilivyokwisha kutoa somo hapo Nyuma.
Upendo utasaidia mambo yafuatayo katika ndoa;