Showing posts with label Uchumba hadi Ndoa. Show all posts
Showing posts with label Uchumba hadi Ndoa. Show all posts

Wednesday, November 23, 2016

MWENENDO WAKATI WA UCHUMBA

Mambo ya kufanya na yasiyofaa kufanya kabla na wakati wa uchumba

Mhandisi Lucas & Happiness Mgalula (TAG City Harvest Church)


Kila mtengenezaji huweka kitabu cha maelekezo ili kuelezea namna ya utumizi wa kitu husika.

Mungu ametupa nguvu na twaenda kwake kujifunza kuhusu udhibiti wa nguvu hizo, Power & Control

Mara nyingi huwa tunaangalia uchumba lakini kuna mahali umeanzia, mahusiano ya urafiki. Tunaangalia namna vijana waliookoka wanavyopaswa kuenenda katika mahusiano kuelekea ndoa.

Umri huu ni kipindi muhimu ambacho hakirudi tena, ni cha muhimu kwako, kwa familia, wazazi, kanisa, jamii nzima na Mungu. Wote wanakutegemea upite salama na kufanikisha kusudi la Mungu.

Kabla ya Uchumba

Kipindi unachojiuliza ikiwa utapata mtu sahihi na ikiwa moyo wako utamkubali. Hata usipoijua njia, hautapotea

I.      Mahusiano na wenzako

-  Fanya ni utaratibu wako kuomba juu ya mahusiano uliyonayo na wenzako ili ule utakaopelekea ndoa ushamiri zaidi na yale yatakayoleta vurugu yafe! Mwanzo 24:12-14 aliyetumwa kumtafutia Yakobo mke alikuwa makini kuomba hivyo
-  Mwambie Mungu akusaidie ili ule uhusiano ulio makini uuone.
-  Anaweza kutokuwa na vigezo vyote unavyovidhania lakini akawa ndiye hasa. Isaya 30:21 Hii ndiyo njia, ifuate

II.  Tafuta ushauri wa wenye hekima wa Mungu

-  Unapoona kama uhusiano mmoja unashamiri na unaweza kupelekea kwenye uchumba, tafuta ushauri wa wenye hekima waliookoka hasa wanandoa.
-  Kuna mambo mengi njiani ambayo utahitaji maombi na msaada wao.
-  Mungu hukupa mwanamke/mwanaume, kazi kwako kumjenga awe mke/mume
-  Hakuna anayekuwa amekamilika, maana hakuna aliyekuwa mume au mke kabla hamjatangazwa hivyo na kuanza kuishi pamoja. Hakuna anayenunuliwa sokoni akiwa kamili
-  Hekima huja kwa kusikia au kupitia, hakuna aliyekuwa amepitia ndoa kabla, hivyo ni vema kupata wanandoa wenye hekima wakusaidie
-  Usiufiche uhusiano wako unaoelekea kwenye uchumba, ni hatari

III.    Kuwachukulia wote kuwa ndugu zako

-  Watu wote unaohusiana nao kanisani na kwingineko, wachukulie kama dada au kaka. Mvulana usiwadharau wadada na msichana usiwachukulie wakaka kama watu waonevu
-  Kuna aina hii ya heshima ambayo kaka na dada wanakuwa nayo kwa kila mmoja. 1Timotheo 5:1-2 Kwa usafi wote, nia, kimawazo, maneno na matendo
-  Sote tu wa damu moja, tumenunuliwa kwa damu ya Kristo
-  Kwa kuhusika katika shughuli nyingi za kanisa zinazoweza kuwaleta pamoja na mkafahamiana, ndipo waweza kujua namna ya kuamua ikiwa tabia zenu zitaendana na mtachukuliana. "Birds of feathers flock together"
-  Baada ya kumfahamu, heshima iendelee, hapa ni kabla ya kuwa “Mr. Special” au “Ms. Special”
-  1Wakorintho 13:4-8 (Sifa za Upendo)
-  Linda moyo wako kuliko vyote ulindavyo, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima
-  Kama kuna kitu "special" baina yenu ni bora ukiseme na siyo kuficha ficha. Acheni kung'ang'aniana kama kumbikumbi kila uendako naye yupo halafu mnasema hakuna kinachoendelea baina yenu. Hiyo ni mbaya na hatari na unaweza kukosa "opportunity" na hata kumkosea Mungu.

NOTE: Don't treat anyone special! Don't single her out! Avoid over-clinging to one person when there is nothing-marital material!

Kabla ya Ndoa

-  Usimtembelee mtu wa jinsia tofauti (mchumba) kwake mkiwa peke yenu.
-  Usimfulie, kumpikia au kumsafishia nyumba. Kwa nini upate privileges za ndoa kabla? Una haraka gani?
-  Inaweza kuanza vizuri na kwa nia njema lakini mkaangukia kwenye "premarital sex and pregnancies" ambayo italeta majuto, uchungu na chuki

Wakati wa mahusiano/uchumba

-  Usichochee mapenzi kabla ya wakati wake. Ni mchumba wako lakini haimaanishi unao uhuru wa kufanya lolote utakalo. Huwezi kuwa Rais kabla ya kuapishwa
-  Mwili wako unatambua tayari kwamba huyu ni mtu maalumu, nao unajiandaa na kuitikia hivyo. Kuwa makini.
-  Avoid physical touches, as they will result into premarital sex and unplanned pregnancies
-  Uchumba unaweza kuvunjika. Mungu atakupa amani ndani yako kuendelea mbele, isiwe mzigo kwako ukatumia nguvu nyingi kumridhisha au kumweka kwako halafu mwitikio ukiwa mdogo unaanza kujiuliza kwa nini. Usijilazimishe au kukubali kwa kumhurumia. Ikiwa haiwezekani sema kwa upendo na upole. Ikiwa ana shida, ndiyo maana Mungu akakufunulia wewe ili uchukue hatua za Kikristo kumsaidia

Swali: Vipi kuhusu kutoa zawadi kwa mtu uliye kwenye mahusiano naye/mchumba?
-  Zawadi inaweza kuwa aina fulani ya rushwa, inaufunga moyo wa mtu. Anaweza kukukubali kwa hizo kwa kuwa umeuteka moyo wake na utalazimika kuwa unafanya vitu kwa ajili yake ili aendelee kukukubali

-  Ni bora ukilazimika au kujisikia kutoa zawadi, utoe ambayo haitaumiza moyo wako mambo yakienda kombo. Usianze kununua naye vitu vya thamani, kuwekeza pamoja, kujenga, viwanja na kadhalika.


-  Ni vema upendo ukaja kawaida, zawadi zitafuata kwa nafasi yake

Wednesday, October 15, 2014

Uchumba hadi Ndoa: Do you want your Spouse to change



Wengi wanataka kuona madadiliko kwa wenzi wao lakini hawako tayari kubadilika kwanza, hebu mpendwa wangu chukua hatua ya kubadilika leo.
Utakapobadilika na mwenzi wako utashangaa anabadilika

Muombe Mungu akuonyeshe ni eneo gani unatakiwa kubadilika na ukabadilike leo
Hata kama unaona hiyo tabia ni ngumu, mkabidhi Mungu yeye anaweza yote hakuna jambo gumu asiloliweza.


Mungu atusaidie na akakusaidie pia, Amen

Thursday, October 9, 2014

City Harvest welcomes you to Couples Seminar

You are all invited to Couples Seminar which will be held at City Harvest






Venue: Victoria Service Station Building, 2nd Floor along Mandela Road

Time: 9:30 to 5pm

Contribution:  5,000/= per person for bites and logistics

 

 

Successful Couples will make a Successful Family which will make Successful Society hence having Successful Nation

 

You are Warmly Welcome

Wednesday, August 6, 2014

Uchumba hadi Ndoa: Usifikiri utaweza kubadilisha tabia ya mwenzi wako baada ya kuolewa naye au Kumuoa

 

Bwana Asifiwe watu wazuri wa Mungu, namshukuru Mungu kwa siku hii nzuri aliyonipa maana kwakweli muda nao umekuwa mali.

Natamani sana kila wiki niendeleze Makala haya lakini mara nyingine tunabanwa na muda lakini pia Mungu ana makusudi kwa kila jambo.

Leo naomba tuzungumze jambo hili muhimu sana katika mahusiano, linalohusu pale mtu anapokuwa na matarajio kwamba mwenzi wake atakuja kubadilika tabia yake mbaya au isiyombariki baada ya kuingia kwenye Ndoa

Hii inakuwa hivi inawezekana watu wamekaa katika uchumba wanavyoendelea kuna tabia unaziona kwa mwenzi wako ambazo unaona kwamba ni ngumu yaani hazibebeki, lakini unaamua kwamba utaendelea maana unajua kwamba ukimuoa au akikuoa utakuwa na Mamlaka ya Kuweza Kumbadilisha au Kukomesha hiyo tabia.

Sisemi kwamba watu wenye udhaifu fulani hawawezi kubadilika,HAPANA mtu yoyote yule anaweza kubadilika ila Mabadiliko yatatokea tu pale mtu ANAAMUA kubadilika na sio kung`ang`anizwa kubadilishwa.

Hakuna aina ya ubabe ambao wewe mke au mume unaweza kutumiakwenye Ndoa ili kubadilisha tabia yake, sio pesa, sio chochote kitakachoweza kubadilisha mtu

Unaweza kuwa na mchumba ambaye ana mahusiano mengi mengi, leo umemkuta na meseji za Joyce, Kesho za Jane,mara umesikia jana alikuwa na mwingine sijui KFC au Steers pale, wengine tena wanakutumia labda meseji za kejeli au wengine wanakupigia simu kwamba huyo ni cha Wote, lakini wewe unang`ang`na kwamba eti huyu mtu wangu atabadilika pale tu Nitakapomuoa….

Kuna kisa nilikisikia hivi karibuni kaka alikuwa mchumba, kumbe huyo dada alikuwa anaendeleza mahusiano ya zamani kisirisiri, sasa kibaya sana siku mbili kabla ya harusi kuna mtu alimuona huyu mwanadada akiwa ametoka kwa yule mtu wake wa zamani, huyu kaka aliambiwa lakini akasema huyo mimi nikimuoa nitamkomesha hataweza kutoka hata ndani nitamfungia, NITAMBADILISHA.

Je Ndugu yangu unafikiri kweli kwa tabia hii huyo dada yetu ataacha mahusiano hayo, kama kweli anashindwa kuheshimu ndoa yake kabla hajaingia maana hapo hata huyo mume hajamjua vizuri je akishaishi naye kweli ndio ataiheshimu hiyo Ndoa. Hebu tafakari hili mpendwa wangu....

Neno katika Mathayo 6: 24“Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Maana atamchukia mmoja na kumpenda huyo wa pili; au ataambatana na mmoja na kumdharau huyo mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.”

Ukisoma Maneno ya Mungu hapo juu neno liko wazi Kabisa kwamba mtu huwezi kutumikia mabwana wawili yaani huwezi kushika mambo mawili lazima kuna moja utalidharau na kuzingatia lingine.

Thursday, June 19, 2014

Uchumba hadi Ndoa: Jiepushe na Mahusiano ya Zamani


 
Bwana Asifiwe wapendwa karibu tena katika Masomo yenu ya Uchumba hadi Ndoa yanatoletwa kwenu na Mshauri wako.

Leo tutazungumzia jambo muhimu sana ambalo limesumbua mahusiano mengi ya uchumba na Ndoa pia, jambo lenyewe ni Mahusiano ya nyuma ambayo mtu alikuwa nayo. Mahusiano hayo ni kama mkaka au mdada alishakuwa na mchumba mwingine huko nyuma lakini ikashindikana kuendeleza mahusiano ikabidi wavunje uhusiano. Hayo ndio mahusiano hasa nitakayozungumzia leo.

Mahusiano ya nyuma mara nyingi huvunjika pale mnaposhindwana tabia, mitazamo, maamuzi na kadhalika na kadhalika.

Mpendwa wangu yamkini huko nyuma kabla ya kukutana na huyo mtarajiwa wako ulishakuwa na Mahusiano, ni muhimu sana kuhakikisha unachukua maamuzi thabiti kuhakikisha kwamba hayo mahusiano ya nyuma yanaisha na hakuna kingine kinaendelea kati yenu zaidi ya salamu tena tu ikitokea tu mmekutana uso kwa uso sio unaanza kumpigia simu enhee unaendeleaje hiyo ni hatari na dhambi ya kutokuwa muaminifu. 

Siku hizi ndoa zina shida kubwa ya Cheating kwasababu watu hawakuachilia mahusiano ya nyuma. Au unakuta mtu anampigia Simu yule mwenzi wa zamani na kumuelezea jinsi anavyopata matatizo labda na uhusiano wa sasa wenyewe wanaita a sholder to cry.

Nasikitika sana maana hayo mambo yako makanisani pia siku hizi ni jambo la hatari sanaaa.     Sasa wengine wataendeleza huo uhusiano kwa siri mpaka wanafunga Ndoa unaendelea hivyo hivyo kwahiyo utashangaa Ndoa mwezi imevunjika kumbe shida ni Mahusiano ya Zamani jamani hiyo Roho ishindwe naikemea kwa Jina la Yesu.

Nilisoma mahali kuna dada alikuwa anakwenda kuolewa ile siku moja kabla ya ndoa eti akaenda kuagana na mtu wake wa zamani basi yaliyomkuta huko ikawa ni mauti na dunia nzima kujua siri na uchafu huo alikuwa anaufanya.

Unaweza kuona labda leo hujakamatwa lakini unatakiwa ujue mpendwa wangu Mungu hapendi vuguvugu kama umeamua mimi ni wa Yesu mfuate umeamua kurudi nyuma kaa nyuma lakini usijifishe kanisani ukajifanya kondoo kumbe wewe ni mbwa mwitu unamfanyia mwenzako ubaya anakuamini sana anafikiri amepata mwenzi mwaminifu kumbe wewe unafanya uasherati ndugu kuna malipo, Jihadhari ndugu yangu.

Mahusiano ya zamani ndio chanzo cha nyumba ndogo tunachoona katika jamii watu wamegeuza fashion.. Siku hizi mtu haogopi kama huyo mtu ameoa au ameolewa ni Hatari mpendwa Jihadhariii.

Madhara ya Mahusiano ya Zamani:      

Tuesday, June 3, 2014

Uchumba hadi Ndoa: Sababu Kumi zinazofaa kumfanya mtu aamue Kuoa au Kuolewa


Karibu tena katika Makala haya yanayoletwa kwenu na Mshauri wako wa Ndoa na Mahusiano, Leo tunaendelea na Sababu Kumi zinazofaa kumfanya mtu aamue kuoa au kuolewa , tukimalizia sababu tano zilizobaki
 
Tuendelee

 

6.      Kuambatana na Urafiki kweli

Lengo kubwa la Ndoa ni wanandoa kuwa na mahusiano ya yaliyojengwa ndani ya urafiki na kuambatana

Rafiki ni mtu ambaye mnashirikiana katika mambo mengi, ni mtu unayependa kumuona na kuzungumza naye mambo yako, ni mtu ambaye ukiwa na huzuni utapenda awe wa kwanza kumwambia, ukiwa na furaha pia utamshirikisha furaha yako. Hata ikitokea mmetofautiana na kugombana na rafiki hutajisikia vizuri utatamani tu utafute njia ya kutatua mgogoro na urafiki uendelee.

Na marafiki wengi wa kweli ambao wamekuwa marafiki wa muda mrefu wamepita katika vipindi vingi, kuna kipindi wamegombana, wamekwazana na wamefurahi sana kwa pamoja lakini wameendelea kuchukuliana na dio maana urafiki wao unaendelea.

Hivyohivyo ndoa inapaswa kujegwa katika urafiki wa dhati na wa kweli, ili kuweza kuchukuliana pale mnapopishana

Kwahiyo ukitaka kuingia katika ndoa uwe Tayari kumfanya mwezi wako kuwa Rafiki hapo utafurahi sana katika ndoa, maana utakuwa huru kwa mwenzako, kumtania, kumweleza chochote, na hata kama hujafurahi utamwambia nay eye pia, na pale mnapokwazana kwasababu ni rafiki itakuwa rahisi sana kusulihisha mgogoro. Kwahiyo kijana na binti yangu ingia katika ndoa na mtazamo huu utakusaidia sana

Usije ukamfanya mwenzako baba au mama yako, mama na baba wana nafasi zao tunaziheshimu, mfanye mwezi wako kuwa rafiki, Haleluyaaaaaaaaaaaa

 

Hata Neno katika Mwanzo 2 : 21- 24 “Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,

na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.

Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”

 

Mungu aliona ni vyema wana ndoa kuwa Mwili mmoja na kuambatana, hamwezi kuambatana pia kama sio marafiki ndio maana leo tumeona ndoa nyingi wameshindwa kuambata kwasababu mahusiano yao hayana urafiki, Mungu akusaidie wewe unayetegemea kuingia katika ndoa ujifunze hili na wewe uliyeko katika Ndoa basi anza leo kuwa na urafiki na mwezi wako ili muweze kuambatana, yaani mkifanya mambo yenu kwa pamoja

 

7.      Ushirika

Ndoa ni nafasi nzuri sana ya kuweka ushirika katika matendo,yamkini umelelewa katika mazingira ya ubinafsi mpendwa wangu ambapo chako ni chako, hakuna mtu anavaa hata ndala zako, au hata anayegusa kitu chako, sasa ukiingia katika ndoa ujue mambo yatakuwa tofauti, kama Neno la Mwanzo 2: 21-24 Ndoa ni kuambatana inabidi ufungue moyo wako kuwa Tayari kushirikiana na mwenzi wako katika mambo yote, katika huzuni, changamoto, hali ya kupungukiwa, furaha na raha, sio kwa vile leo umeolewa na mwenzako anavitu basi unashirikiana naye akiishiwa tu au wanavyosema wana dotcom akifulia unamkimbia si sawa, hiyo sio ndoa mpendwa. Jiweke Tayari kushirikiana na mwenzako hapo utaona maisha mazuri utakuwa unaimba haleluyaaaa

 

8.      Kusaidiana mahitaji ya kila mmoja

Wednesday, May 21, 2014

Uchumba hadi Ndoa: Sababu Kumi zinazofaa kumfanya mtu aamue Kuoa au Kuolewa


Mpendwa wangu Shalom,
 
Karibu tena katika Makala haya ya Uchumba hadi Ndoa, yanayoletwa kwenu na Washauri Wenu wa Ndoa na Mahusiano.

Wiki mbili zilizopita tuliangalia sababu 10 zisizofaa kuamua kuoa au kuolewa, ambapo tulipata nafasi ya kuchambua mambo mengi na ya muhimu.


Basi leo Karibu tena tuendelee na Somo lingine, Leo tutazungumzia Sababu Kumi(10) zinazofaa kumfanya mtu aamue Kuoa au Kuolewa;


1.      Ndoa ni Mpango wa Mungu

Mungu ndiye Mwanzilishi wa Ndoa, tunasoma katika Mwanzo 2: 18 “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”

Mungu aliona si vema mtu awe peke yake na ndipo akamfanyia msaidizi(MKE) wa kufanana naye. Kwahiyo unaona kabisa Ndoa ilikuwa ni mpango wa Mungu na sio kwamba baba yetu Adamu alijiamulia tu kwa msukumo wake mwenyewe. Na hii muhimu sana kwa Wakristo kujua kwamba Mungu anatuwazia mawazo mema, yeye bila kuombwa na Adamu anaona huyu ngoja nimpatie mwezi wake ambaye anafanana naye, Mungu alijua akimpa ambaye hawafanani itakuwa kasheshe. Mungu ni Mpangaji Mzuri sana kwakweli Uzuri wake haulezeki nikiangalia jinsi amefanya mambo yake huwa namshangaa na kumsifu tu.

Katika maisha yako ya kila siku najua umekuwa na mahitaji mbalimbali ambayo unayapeleka mbele za Mungu kwa njia ya maombi, kwa mfano Kufaulu mitihani, kupata kazi, kupona magonjwa , kupata kazi nakadhalika nakadhalika, Sasa kama umemuomba Mungu akakujibu juu ya hivyo vitu vingine kwanini kwenye swala la Ndoa usimwamini Mungu hivyohivyo.

Kabla ya kupata mwezi na baada ni vizuri kuwa katika hali ya maombi ili mapenzi ya Mungu yatimizwe, ili Mungu akupe mtu yule aliyemkusudia ambaye unafanana naye. Kwasababu ukipata unayefanana nae mtaishi kwa upendo na kuchukuliana.

Kwahiyo ni ombi langu kwako ndugu yangu mpendwa kwamba Mungu akupe neema ya kukaa katika maombi katika hatua yoyoye ambayo uko, iwe hujapata mwenza , au umeshampata au uko ndani ya Ndoa.

Hiyo itakusaidia sana kuwa na maisha ambayo Mungu amekukusudia kwasababu utakuwa unatembea katika mpango wa Mungu


2.      Kuonyesha Upendo wa Mungu kwa Mwenzi wako

Mungu wetu ni Upendo na upendo wake ni wa Agape, yeye alitupenda wakati sisi tuko katika dhambi na wala hatuna chochote ambacho tumempa.

Upendo wa Mungu sio kama ambao baadhi ya watu wanao, hauna masharti, watu wengi wana upendo wa masharti ule wa Nipe Nikupe, nakupenda kwasababu ya Pesa, au nakupenda kwasababu ya najua nitapata upendeleo fulani fulani, na siku hizi imekuwa hatari sana vijana wengi wanaoa au kuolewa na watu kwasababu hao watu wana vitu fulani kama magari, nyumba, hela, au vyeo

Lakini Upendo wa Kweli ni ule wa Mungu ambao hauna masharti, tunapaswa kuingia katika Ndoa ikiwa ni njia nzuri ya kuonyesha Upendo wa Mungu kwa wenzi wetu.

Ndoa ni sehemu sahihi kabisa ya wenzi kuonyesha upendo wa Agape kwa kila mmoja,kumpenda mwenzako akiwa mzima au mgonjwa, akiwa na fedha ua hana, akiwa na cheo au asipokuwa nacho, kumuonyesha mwenzako upendo bila kusubiri kupata chochote kama Mungu na Kristo walivyotupenda kwanza.

 

3.      Kuonyesha Upendo wa Kweli kwa Mwezi wako

Ndoa ni sehemu muhimu sana ya kuonyesha upendo kwa mwezi wako, kwahiyo ni vizuri kuoa  au kuolewa kwa makusudi ya kutaka kuonyesha upendo kwa mwenzi wako

Katika Ndoa kunatakiwa kuonyesha aina tatu za Upendo;

·         Phileo ambao ni ule upendo wa Kimahaba kwa mpenzi wako, kwahiyo unapooa au kuolewa ndugu mpendwa ujue una jukumu la kuonyesha upendo wa kimahaba kwa mwenzi wako

·         Eros ni vizuri kuingia kwenye ndoa kwa shauku ya kutaka kuonyesha upendo wa kimapenzi kwa mwenzako, kuwa Tayari na furaha kwa ajili ya ile zawadi kubwa ya Tendo la Ndoa Mungu aliyoiandaa

·         Agape wanandoa pia wana jukumu la kuonyesha upendo wa Mungu kwa kila mmoja kama nilivyokwisha kuelezea hapo juu

              Kwa hiyo Upendo kwa mwenzi wako ni jambo la msingi sana nan i msukumo unaoruhusiwa kufanya maamuzi ya kuingia katika Ndoa, kwahiyo mpendwa kama hujaingia hebu jichunguze je kuna upendo , ni nini  

             Msukumo wako?


4.      Shauku ya kuazisha familia pamoja

Wednesday, May 14, 2014

Uchumba hadi Ndoa: Usioe au Kuolewa kwa msukumo wa Sababu hizi kumi zisizofaa


 
Habari mpendwa wangu, Karibu tena wiki hii nyingine nzuri Mungu ametupa tuzungumze na kushauriana

Leo tunaendelea na somo letu zuri tuliloanza wiki iliyopita la Usioe au Usiolewe kwa Msukumo wa Sababu hizi Kumi zisizofaa

Halleluya nasikia furaha sana kupata kibali cha kuzungumza na wewe siku ya leo.

 

Haya tuendelee na zile sababu tano zingine;

 

6.      Hofu ya kujitegemea

Kuna watu wengine ni tegemezi sana kwa wazazi wao,utegemezi huu unaweza ukawa umesababishwa na malezi wazazi waliwalea au yeye mwenyewe tu ni mvivu.

Utakuta mzazi anamfanyia mtoto kila kitu, atamtafutia chuo, atampeleka chuo, atamtafutia kazi, atamtafutia kiwanja,kupikiwa, kufuliwa etc,yaani mtoto anafanyiwa kila kitu kiasi kwamba yeye mwenyewe hana nafasi ya kuwaza na kufanya vitu peke yake. Sasa hapo pia inategemea na mtoto mwenyewe kama anapenda hiyo hali ndio atabweteka hivyohivyo.

Sasa basi akiona amekaa kwao na umri unaenda sana na wazazi labda wanamshauri apange nyumba na kujitegemea yeye anapata woga kwasababu alizoea kufanyiwa kila kitu ili kukwepa hayo anaamua aolewe au aoe na yeyote anayejitokeza ili tu apate pa kutegemea.

Sasa ndugu yangu kama umemuoa mtu au umeolewa na mtu kwasababu ya huo woga unafikiri kweli utaiweza ndoa, na je huyo uliyemtegemea akashindwa kufikia hayo matarajio yako ya utegemezi si utakimbia, nakuomba leo badili mtazamo usichukua uamuzi wa kuingia kwenye ndoa kama sehemu ya kumtegemea mwenzio akufanyie fanyie, badilika leo ndugu yangu, kuolewa ni kuzuri pale tu panapofanyika vile Mungu anataka na kama nilivyosema mwanzo kuna sababu nzuri tu za kuoa au kuolewa lakini sio hofu ya kujitegemea.

 

7.      Hofu ya kumuumiza mwenzako

 

Inawezekana ulikuwa kwenye mahusiano ya uchumba, lakini muda ulivyoendelea ukaona kwamba huwezi tena kuendelea na huo uhusiano inawezekana kwa sababu nzuri tu

Sasa labda ukiangalia muda ambao mlikaa katika huo uhusiano, mambo mliyoahidiana na kufanya pamoja, labda jinsi jamii inavyowatambua, ukaingiwa na hofu kwamba kwakweli sitaweza kumwambia huyu kaka au dada kwamba siwezi kumuoa au kuolewa naye kwasababu nitamuumiza sana. Matokeo yake unamuoa au unaolewa na mtu ambaye kiukweli hukupenda ila ni kwasababu uliogopa kumuumiza.

Sasa vile vitu vilivyokusababisha utake kufanya uamuzi wa kuachana nae na wewe ukashindwa kwasababu uliogopa kumuumiza, ujue kwenye Ndoa ndio utaviona vizuri sana tena clear, sasa sijui utamlaumu nani unaanza kukosa raha na mwisho kama hutakuwa makini na Mungu kuingilia kati hiyo ndoa inaweza kuvunjika kabisaa.

Au mwingine anaamua kabisa kumwambia mwenzake kwamba kutokana na jinsi huu uhusiano unavyoenda naona tuvunje kabla hatujaenda kupata matatizo katika ndoa, sasa mwingine hasa wakina dada Analia hapo mawiki na mawiki, na mwingine anatishia kujiua, sasa mkaka akiona hivyo anaogopa kwamba mwenzake atapoteza maisha kwasababu yake kwahiyo analazimika kuendelea na mahusiano hadi ndoa.

Je unategemea akimuoa huyo aliyetishia kujiua na bado ulikuwa na sababu za msingi za kuvunja uhusiano unafikiri maisha ya ndoa yatakuwaje? Hebu tafakari

Nakumbuka kuna kijana aliniambiaga namuoa fulani kwasababu unajua nimekaa nae miaka mingi sasa nimempotezea muda japo simpendi lakini namuonea Huruma,hiyo si sawa bora uchumba uvunjike kwa machozi kuliko Ndoa jamani naomba kusisitiza, Haleluya bado unanipenda jamani maana kuna watu wanapenda kung`ang`ania wee kama kakukataa jamani sio mwisho wa Safari na wala hutakufa kwa kumkosa tena baadae ukijam kutafakari  kwanini nilikuwa napoteza muda kwa mtu kama huyu utajicheka sanaaaaa cause they don’t deserve you, Wewe ni mtoto wa Mfalme Bwana, Ambassador of Christ why worries enhee! Aminaaaa!

Tuesday, May 6, 2014

Uchumba hadi Ndoa: Usioe au Kuolewa kwa msukumo wa Sababu hizi kumi zisizofaa






Karibu tena katika Makala haya ya Mahusiano na Ndoa, leo Washauri wenu tuko Tayari kabisa kuwaletea somo zuri kabisa la kujiepusha kuingia katika ndoa kwasababu tu ya misukumo isiyofaa

Leo tutaanza kuongea juu ya kuolewa au kuoa kwa msukumo wa sababu tano zisizofaa, sababu tano zingine tutamalizia wiki ijayo, Karibu Sana

 

Tunaposema sababu zisizofaa ina maana kuna sababu Nzuri tu zinazofaa za kwa mtu kuamua kuoa au kuolewa sasa hizo tutaleta baada ya kumaliza hili

 

1.      Kuwa huru na ulinzi au kufuatiliwa na Wazazi

Vijana wengi wameamua kuoa au kuolewa kwasababu labda wazazi wao wamekuwa wanaingilia sana uhuru wao kwa mtazamo wao

Kama tunavyojua maana pia hata sisi tulikuwa vijana, kijana anakuwa anatamani sana kuwa huru kujipangia maisha yake labda afanye hivi na vile au arudi nyumbani usiku au saa ingine asirudi kabisa, sasa mzazi anakuwa mkali atamuuliza maswali kwanini unafanya hivi, kwanini umechelewa, kwanini unachelewa kazini, nakadhalika nakadhalika, au labda ana mahusiano mzazi anayatilia mashaka, sasa kijana mwingine anaona wazazi wanaingilia uhuru wake, Kwahiyo sasa anaamua ili kuondokana na hiyo adha hawa wazazi wananizingua sana ngoja niolewe tuone watanifuatilia huko kwa mume au nyumbani kwangu.

Sasa ni kweli utakuwa umeoa au kuolewa kama huo tu msukumo wa kuoa kwakweli ndugu yangu sio sahihi, kwasababu baada ya muda maswali na ufuatiliaji ule unaweza kuanza tena kwa mwezi wako atataka kujua ratiba zako sasa kwasababu wewe ndicho ulikimbia kwenu huoni kama hapa utakimbia tena, Hebu tafakari kabla hujaamua hiyo ni sababu kweli ya msingi ya wewe kuolewa…

 

2.      Kukimbia matatizo ya nyumbani kwenu

Kila familia ina changamoto zake, wengine uchumi unayumba, nyingine baba mlevi na mkorofi labda, au magomvi yasiyoisha, wengine kusakamwa, wengine ukaa uswahilini sana hupapendi kwakweli, sasa kwa kuona hivyo na labda wanakataa usipange unaamua kuoa au kuolewa ili uwe mbali na kero hizo za nyumbani.

Ina maana wewe huwezi kuvumilia mawimbi ndugu yangu, kama umeshindwa kuvumilia changamoto za wazazi wako hivi huyo unayemuona kwamba anakuambia anakupenda sasahivi je kweli akipata au changamoto utaweza kukaa kweli, maana leo anaweza kukosa kazi, hela ukajikuta uko katika maisha ambayo hata uliyokimbia kwa wazazi wako ni mazuri Zaidi, eenhe tuambie utakimbia tena au? Ndio maana leo tuko hapa kukusaidia na kukushauri lazima utafakari kabla hujaamua ili usije ukaamua kuingia katika ndoa kwasababu ambazo hata hazina tija, zipo sababu zenye tija tutakuja kuzifundisha.

Tafakari ndugu, mdogo na mwanangu, je kuna lingine linalokufanya uamue uchukue huo uamuzi.

 

3.      Unajiona mnyonge na hufai wala hustahili na huna sifa sasa akitokea mtu anasema anakupenda unaamua fasta

Kuna watu labda mazingira waliokulia au ufahamu walionao juu ya maisha umewafanya wawe wanyonge na kujiona hawafai, hawastahili, hawana sifa ya kuoa au kuolewa

Inaweza kuwa labda wazazi waliwalelea katika mazingira ya unyongee sana wakiwaambia kwamba hawafai, wamekuwa wakijidharau sana, wakijishusha sana

Na hii hata wanapokuwa na marafiki wanaendeleza hii tabia , kwahiyo hata mashuleni wanajulikana ni watu wasiofaa, wanyongee sanaa sana, hawana sifa na kibaya wao wenyewe wanajitambulisha hivyo

Labda mwingine anavyojiona na umbile lake anaweza kujidharau au kudharauliwa

Sasa mtu ambaye yuko katika mazingira hayo akatokea tu mtu akawambia anampenda anaweza kuamua haraka sana kwasababu labda hakuwahi kupata mtu anayemdhamini, lakini hiyo tu haitoshi kuwa sababu ya kuoa au kuolewa

Wednesday, April 30, 2014

Uchumba hadi Ndoa: Jihadhari na matarajio potofu kuhusu Ndoa




Habari ya leo mpendwa wangu, Karibu sana katika Makala haya ya Uchumba hadi Ndoa yanayoletwa kwako na Mshauri wako kila wiki.

 
Leo tutazungumzia kipengele muhimu cha Kujihadhari na matarajio potofu kuhusu Ndoa, au yaliyojengwa kuhusu Ndoa.

Matarajio potofu ni ile hali ya kuamini kwamba kuna vitu fulani vitatokea au vitakuwa hivi halafu wala havitatokea na wala haviko hivyo unavyotarajia.

Matarajio potofu kuhusu ndoa yako sana katika jamii zetu sio za Kiafrika tu hata mabara ya Ulaya, yako katika jamii za dini mbalimbali, kabila na mila mbalimbali

Najua hata wewe kuna matarajio potofu kuhusu Ndoa ambayo utakuwa umeyaamini kwasababu ulizaliwa katika jamii ambayo yaligeuka kuwa sehemu ya hiyo jamii.
 
Katika jamii zetu na mazingira yanayotuzunguka matarajio potofu yanaweza kuwa na sehemu kubwa inayofanya Ndoa nyingi ziwe katika shida ambazo zimekuwa nazo leo.

Kitu kibaya ni kwamba hata sisi Wakristo tumeyaamini na tunayakiri maratajio hayo matarijio potofu, ndio maana leo nimekuja kukuambia kwamba hayo ni potofu labda ulikuwa hujui.

 

Tuangalie Aina Tano za Matarajio Potofu kuhusu Ndoa;

1.      Ndoa Ndoano au Ndoa si Lelemama

Mara nyingi kwenye sherehe mbalimbali za Harusi utakuta pande mbili ya Bibi Harusi na Bwana Harusi wanapewa nafasi ya kutoa nasaha sasa hapo ndio utasikia haya maneno yakisemwa katika nasaha na tena cha kushangaza utakuta watu ukumbini wananapiga makofi.

Sasa wewe mzazi au mlezi mwenzangu unaposubiri ile sherehe pale ndio uje kumwambia mtoto Ndoa si Lelemama au Ndoa ni Ndoano kwanini umechelewa si ungemkataza au ungekataa mahari jamani, Ili basi kumuepusha na hiyo lelemama unafikiri ipo.

Maana kwa kusema pale ina maana unakiri kabisa kwa mdomo wako Mwanangu Ndoa Ndoano au si Lelemama kwahiyo ukavumilie, pale unamfanya huyo mratajiwa awe na hofu kubwa kwahiyo atakaa kimtegomtego ili tu akiona tu kaugomvi kidogo anakumbukaa anhaa hii ndio ileee lelemama niliambiwa na baba au mama siku ile pale Kibada Skyline Hall…Ohh mwisho wa siku anaanza tu kuhesabu makosa siku anakurudia na mizigo ooh Baba na Mama ile Lelemama yangu anhaa hukuwahi kuiona imekuwa lelemama kwelikweli Nimeshindwa na Nimerudi, Utajibu nini mzazi mwenzangu au mlezi mwenzangu.

 
Haimaanishi kwamba kama wewe mzazi au mlezi ulipata shida katika Ndoa yako na mtoto wako lazima apitie ulichopita, hata kidogo , na jaribu ulilopitia je umetafuta Kusudi maana nimejifunza kila Jaribu ulilopitia katika maisha lina kusudi sasa kwasababu tunashikilia sana Uchungu inakuwa Ngumu kuliona Lile Kusudi ambalo ndilo hasa Mungu anataka tulifanye, Haleluyaaaaaaaaa

Sasa na wewe kijana au binti haya na wewe hata hujaolewa unaanza kukaa barazani ooh unajua Bwana wanaume siku hizi wasanii tuu Ndoa hamna, hakuna zote Ndoa Ndoano, unajua kinachotokea katika Ulimwengu wa Roho, tusome pamoja Mithali 18: 21 “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”

Haya kijana na Binti yangu umeona Maneno ya Mungu yanavyosema,kuwa makini unaongea nini wewe ni mtoto wa Mfalme wa Wafalme usiishi kama watu wa mataifa ambao hawana Tumaini,badili Maneno ya Kinywa chako leo, Sema mimi ndoa yangu itakuwa nzuri itabariki watu, itasimama kama Ushuhuda na utapata hicho unachokisema.Aminaaaaaa


Tuesday, April 15, 2014

Uchumba hadi Ndoa: Jifunze kuchukuliana na Mwenzi wako



Hata Mungu anafurahi ndoa inapokuwa na furaha na raha
 
Karibu katika masomo haya ya Uchumba hadi ndoa ,yanayoletwa kwenu na Mshauri wako wa Mahusiano na Ndoa.

Kwanza nikuombe sana radhi kutorusha masomo haya kwa muda mrefu lakini sasa kwa uwezo wa Mungu tutakuwa tunaendelea na masomo yetu kila wiki.

Kwahiyo uweke katika kalenda na kumbukumbu zako kila siku ya Jumanne tutakuwa na masomo haya….Karibu tuendelee..

Leo naomba nizungumzie kitu ambacho ni muhimu sana kwa mahusiano na ndoa pia. Unapojiandaa kuingia katika ndoa unapaswa kujiandaa jinsi utakavyokwenda kuishi na mwenzi wako. Maana uhusiano unaouendea sio kama ule uliokuwa nao na Baba, Mama, kaka, dada au bibi yako ni Zaidi sana mpendwa, unaingia katika uhusiano wa karibu wa ndani mtu ambaye utalala naye kitanda kimoja kila siku na wakati.
Mwenzi wako wa ndoa ni mtu wa karibu hata kama hujisikii kumuona

Mtu ambaye iwe jua iwe mvua utakuwa unamuona.

Mtu ambaye hata kama hujisikii kuongea na mtu siku hiyo atakuongelesha

Mtu ambaye hata kama hujisikiaa kumuona atakuwepo hapo na utamuona

Ni mtu ambaye lazima uwe naye karibu hata kama siku hiyo amekukwaza sanaa

Ndio maana nikaona kuna umuhimu wa kuwa na masomo haya maana mengi yametokea kama tunavyoona katika jamii sasa, talaka sasa inatolewa tu kirahisi rahisi tu, zamani nilipokuwa mdogo kiukweli kabisa nilikuwa sijui kama kuna talaka huo ndio ukweli wangu. Mungu alinipa neema ya kuwa katika mazingira hayo, sasa nilipokuwa na nikawa mjini ndipo nikasikia hiyo sentensi lakini bado niliona kama ni ya kundi fulani tu lakini nakuambia sasa inaogopesha maana imeingia kanisani. Katika kutafakari haya Mungu akanipa mzigo huu niseme na nyie watu wake kwamba NDOA BILA TALAKA INAWEZEKANA,Amen..

Haya tuendelee na Somo letu sasa, kuhusu kuchukuliana ni hali ya kumuelewa mwenzako pale anapofanya kitu ambacho hakikufurahishi au usichokipenda. Lakini kuchukuliana sio kupuuzia au kudharau naomba nitofautishe maana wengi wanapuuza au kudharau mambo wenzao wanayoyafanya hiyo nayo yaweza kuleta shida.