Karibu
tena katika masomo haya ya uchumba hadi Ndoa,tunaendelea na mtiririko wa Vitu
muhimu vya kufanya au kuangalia kabla hujaoa au kuolewa.
Somo
letu la leo tutaangalia upande wetu wenyewe tukiangalia kama wewe mwenyewe
unayetegemea kuoa au kuolewa Je Unaweza Kusamehe?
Najua
utaniuliza sasa mimi nitajuaje kama naweza kusamehe au Lah, Kwani nimeolewa au
kuoa?
Ni
Kweli hujaolewa bado au hujaoa lakini maisha unayoishi sasa iwe ni na ndugu
zako, na rafiki, wanafunzi wenzako,majirani zako, wafanyakazi wenzako,wanakwaya
wenzako n.k yanatoa picha kubwa kwamba wewe ni mtu unayeweza kusamehe au lah.
Kama
wewe pale nyumbani mdogo wako akikukosea wewe ni mtu wa kushika bango kubwa
kutaki kabisa kusamehe mpaka ukoo ukae chini kuwapatanisha inaonyesha kabisa
wewe si mtu wa Kusamehe kwa urahisi na tabia hii utaipeleka kwa urahisi sana
kwenye ndoa.
Au
wewe pale shule au Chuoni ni mtu ambaye huwezi kusamehe kabisa kwasababu labda
mwanachuo mwenzako amekukwaza akakuomba msamaha lakini wewe hukumsamehe na hadi
mmemaliza chuo au shule umeuendeleza ule uadui , hiyo ni dalili kubwa kwamba
siku huyo mwenzako akija kukukosea kuna uwezekano mkubwa sana wa kutomsaheme.
Kuna
mtu nakumbuka alikuwa shuleni akagombana na mwenzake yaani huo ugomvi haukuisha
na hakuna hata mmoja aliyetaka kusamehe kwahiyo mpaka leo Zaidi ya miaka kumi
hao watu wameendelea kuwa maadui na kitu kilichowafanya wagombane kilikuwa
kidogo sana.
Sasa
hao watu unategemea kwamba kwenye ndoa kama mwenzao atawakwaza watasamehe kweli
kama sio msaada wa Kristo Yesu tu.
Watu
wengine wameokoka kabisa lakini utasikia anasema yaani I am so delicate mimi
ukinigusa nakaa mbali na wewe hiyo ina maana huwezi kusamehe au kuchukuliana na
mwenzako.
Unatakiwa
kujua kwamba vitabia fulani ulivyo navyo ambavyo ama kwa kujua kutokujua hutaki
kuvishughulikia vina madhara makubwa sana katika ndoa maana vitakuja tu
kujitokeza hasa pale ambapo mtakuwa mmeshazoeana na mwenzako, tena ndio
vitakuwa dhahiri kabisaaaa.
Neno
la Mungu katika Mathayo 6: 14 – 15 “Maana
mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi pia. 15 Lakini
msipowasamehe watu makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.”
Kwahiyo
nakushauri amua leo kujifunza kusamehe kwanza maana kama umeokoka au ni
Mkiristo na husamehi na wewe Mungu hatakusamehe makosa yako. Kwahiyo utakuwa
Mkristo Jina.
Ndugu
zangu Msamaha sio Rahisi, lakini hatuna Budi Kumuomba Mungu kutupa neema na
uwezo wa kusamehe hata kama mtu ametukosea mara nyinge kiasi gani.