Karibu katika mafundisho haya yanayoletwa kwenu na Mwalimu Samwel Mkumbo
|
Mwalimu Samwel Mkumbo |
Utangulizi:
Maana hapa
hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. (Waebrania 13:14)
Mtu huweza
kutoka asubuhi kwenda katika shughuli mbalimbali wengine huenda mashambani
wengine maofisini na wengine kwenye shughuli za aina nyingine, biashara lakini
ifikapo jioni au usiku HURUDI NYUMBANI, inawezekana kama ni watoto au ni wazazi
waliachana asubuhi wengine wakienda kazini wengine shuleni lakini jioni
WATARUDI NYUMBANI.
Mtu anapotoka
mji mmoja na kwenda mji mwingine kwa ajili ya kuishi huko aidha kwa sababu za
kikazi au hata biashara, akafanikiwa na akaanzisha maisha huko akawa na familia
huko na akajenga na makazi yake huko, lakini siku akifariki mara nyingi wengi
HURUDISHWA kuzikwa NYUMBANI.
Katika kitabu
hiki ambacho kitakusaidia kukueleza mambo kadhaa juu ya wokovu ulioupokea
katika maisha yako, utajifunza mambo mengi na ni maombi yetu ya kwamba kitabu
hiki kiwe msaada mkubwa sana kwako.
Mambo
utakayojifunza:
Sura ya
Kwanza: katika sura
ya kwanza utajifunza namna ambavyo dunia hii si mahali pa kupategemea na ya
kwamba si mahali pa kudumu, na pia utajua kama dunia si mahali pa kupategemea
je hatma yako ni nini, na ni nini mwisho wa maisha yako.
Sura ya
Pili: itakusaidia
kujua ni nini unachotakiwa kufanya kama dunia si mahali pa kudumu ili uweze
kufika unakotakiwa kwenda, utajifunza kuwa unahitaji sana maandalizi ya
kuelekea mahali unapotakiwa kwenda.
Sura ya
Tatu: mambo ya
msingi ikiwa ni mwendelezo wa sura ya pili ni kujua ya kwamba unakokwenda
hutakiwi kwenda mikono mitupu, kuna mambo unayotakiwa kuyabeba, hivyo kwanza
utajikuta kuna maswali unatakiwa kuyajibu ya ulichobeba kwanza na kisha utajua
ni nini unatakiwa kubeba.
Sura ya
Nne: sura hii
itakuelekeza mambo ambayo ni muhimu uyafahamu katika safari hii, mambo
yatakayotokea njiani, mambo ambayo yanapotokea usishangae, lakini pia utapata
tumaini kwa kujua ya kwamba hauko peke yako.
Nimalizie
utangulizi huu kwa kusema JIANDAE KURUDI NYUMBANI.
Sura ya kwanza.
DUNIANI
SIO KWETU
Nataka niweke
wazo hili kwanza kwako wakati unaendelea kusoma sehemu hii, ni kwamba DUNIANI
SIYO KWETU, ndio! Namaanisha hata wewe hapo ulipo, Duniani siyo Kwako,
haijalishi umeweka nini duniani, au unaipendaje dunia, au dunia inakupendaje.
Si kitu unawapendaje watu wa dunia na vitu vya dunia lakini nataka ujue, na
siyo utani kabisa kwamba hapa DUNIANI SIYO KWETU.
Waebrania
13:13-14 imeandikwa
hivi;
13 Basi
na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutumu lake. 14 Maana hapa hatuna
mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.