Showing posts with label Teaching. Show all posts
Showing posts with label Teaching. Show all posts

Thursday, April 9, 2015

CITY HARVEST WELCOMES YOU TO THE GREAT SERVICE EVENT


You are all invited you to a terrific Gospel Event of MAKING THE GREAT SERVICE (MGS) with a monthly theme of GET WELL to be presented at City Harvest Church, Mabibo Garage this Sunday on 12 April, starting at 3 p.m.

Speaker: Pastor Harris Kapiga, Motivational Speaker and Clouds TV Presenter will give intellectual and inspirations to young professionals.

City Shakers praise and worship team will perform live alongside well known gospel singers Mirium Kasula and Phillip Rupia.


It will be great event of hand clapping and joyful praise n worship event accompanied by cultural presentations, interactive discussions, interviews, inspirational talks, prophetic dance, G-Talent, games and many more.


COME AND HAVE SOME FRESH MOMENTS AND GAIN GREATER ENERGY IN THE PRESENCE OF THE LORD

ENTRANCE: FREE

Thursday, March 12, 2015

Wewe ni Mshindi Ishi kama Mshindi

Anza siku yako Leo kwa ushindi Maana wewe ni mshindi Kumbuka kuzaliwa kwako tu ni ushindi

Kulikuwa na mashindano makubwa ya mbegu za uzazi lakini ya kwako ndio ilishinda zingine zikafa

Usijidharau maana asili yako ni ushindi, hata kama mazingira yako ya sasa hayafanani na ushindi yasikutishe hayo yatapita wewe ni mshindi songa mbele ukashinde

Amini kwamba utafanikiwa na kila utakachokifanya Kitafanikiwa

Nenda sasa ukashinde Leo ndio siku yako ya kufanikiwa na kushinda

Wednesday, February 4, 2015

MAOMBI YA KUFUNGUA MALANGO NA MILANGO -1 na Mchungaji Florian Katunzi



Mchungaji Florian Katunzi

Karibu katika mfufulilizo wa somo hili jipya linalofundishwa na Mchungaji Florian Katunzi wa EAGT City Centre, ambalo naamini ukilifuatilia kwa makini hautatoka kama ulivyo. Pia napenda kukwambia ya kuwa jiandae kukipokea kitabu hiki ambacho bado kipo jikoni na kitakuwepo mtaani hivi punde.
 
Leo tunaanza na Sehemu ya Kwanza
 
Zipo aina nyingi za maombi yanayotajwa kwenye Biblia takatifu, na yenye matokeo dhahiri yenye kudhihirisha uweza wa ki-Mungu wenye nguvu za kuangusha ngome zote za giza.  Katika kitabu hiki nitafundisha aina ya maombi ya kufungua  malango na milango.

 

KUOMBA maana yake ni Kumwita Mungu. “Katika shida yangu nalimwita BWANA, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.” Zaburi  18:6

 

Ndani mwa maombi haya  BWANA  atakufungulia milango, na hakuna malango yatakayofungwa mbele yako tena. Neno la Mungu linatuambia:

 

 “Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafame; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa. Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.”  (Isaya 45:1-3)

 

Kipindi hiki wana wa Israeli walikuwa uhamishoni Babeli, kumbuka walitekwa na kuchuliwa uteka mpaka nchi ya Babeli na Jemadari Nebukadreza, mnamo mwaka 605 KK, baada ya kuwashinda wamisri  katika vita ya Karkameshi. Wakati huo kulikuwa na makundi mawili yaliyopelekwa uhamishoni Babeli, kundi la pili lilikuwa ni lile lililochukuliwa mwaka 586 KK.

 

Huyu Nebukadneza, ni mtoto wa kiume wa Nabopolasa, aliyemridhi baba yake kuwa mtawala wa dola ya Wakaldayo mwaka 605 KK. Hii ni kwa mujibu wa kitabu cha  The Cambridge Acient history  III Uk. 212.  Nebukadireza alikuwa  jemadari kijana aliyekuwa ana misuli ya vita na tena shujaa na mwerevu wa mapigano, hivyo alikuwa na sifa zote za kurithi kiti cha baba yake.

 

Wachambuzi wa mambo ya kale wanamuelezea kuwa alikuwa ni askari na mwanasiasa aliye heshimiwa sana kutokana na uwezo wake wa kuongoza mapigano na kujenga hoja katika uwanja wa kisiasa.

 

Baada ya kutwaa madaraka, mfalme huyu mpya alihusika kujenga  vyema himaya na alama za Babeli katika maeneo mbali mbali ya dunia, tena alijiongezea sifa kwa kumuoa Malkia wa Media  Amyhiya, binti wa Cyaxareas, aliyekuwa na utawala wa Kaskazini.

 

Neno la Mungu katika kitabu cha Daniel 2:36-43, linatuonyesha kuwa baada ya Nebukadreza aliyekuwa kiongozi wa dola yenye nguvu sana ya Ukaldayo kiasi cha  ufalme wake unafananishwa na kichwa cha dhahabu kwa  thamani yake, hata hivyo, alipojiinua kiasi cha kutaka kuabudiwa, ufalme wake, ulikomeshwa na Dola ya Ukaldayo iliingia hatua ya mwisho pamoja na kuchaguliwa kwa Nabondus mnamo mwaka 556 KK.

 

Baada ya kufa kwa Nebukadreza kinafuata kipindi kifupi cha kupinduana na kuchinjana kwa watawala na mwisho kabisa utawala wa Dola ya Ukaldayo unafutika kabisa na unaibuka utawala wa Wamedio, Umedi na Uajemi (Medionapersia) chini ya Mfalme Koreshi Mwajemi na Dario wa wamedi, walioungana pamoja na kuangusha Dola ya Ukaldayo mwaka 538. Utawala wa wabanabe ulidumu kwa kipindi cha miakamia mbili (200), mpaka 331 KK.  Ndani ya kipindi hiki cha utawala wa Wamedi na Wajemi, tunamuona Koreshi, tuliyemsoma katika andiko letu la msingi akitimiza unabii uliotolewa kwa kinywa cha Nabii Isaya miaka mia moja hamsini (150) kabla ya kutimizwa kwake  katika mwaka 538.

 

Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya wakaldayo. Katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Daniel, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka ambayo Neno la BWANA lilimjia Yeremia Nabii, kutimiza ukiwa wa Yerusalem, yaani, miaka sabini. nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwake maombi na dua, pamoja na kufunga na kuvaa nguo za magunia na majivu.” (Daniel 9:1-3).

Wednesday, November 12, 2014

JIANDAE KURUDI NYUMBANI Sehemu ya Kwanza na Mwalimu Samwel Mkumbo


Karibu katika mafundisho haya yanayoletwa kwenu na Mwalimu Samwel Mkumbo

Mwalimu Samwel Mkumbo
Utangulizi:
 
Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. (Waebrania 13:14)

Mtu huweza kutoka asubuhi kwenda katika shughuli mbalimbali wengine huenda mashambani wengine maofisini na wengine kwenye shughuli za aina nyingine, biashara lakini ifikapo jioni au usiku HURUDI NYUMBANI, inawezekana kama ni watoto au ni wazazi waliachana asubuhi wengine wakienda kazini wengine shuleni lakini jioni WATARUDI NYUMBANI.

Mtu anapotoka mji mmoja na kwenda mji mwingine kwa ajili ya kuishi huko aidha kwa sababu za kikazi au hata biashara, akafanikiwa na akaanzisha maisha huko akawa na familia huko na akajenga na makazi yake huko, lakini siku akifariki mara nyingi wengi HURUDISHWA kuzikwa NYUMBANI.

Katika kitabu hiki ambacho kitakusaidia kukueleza mambo kadhaa juu ya wokovu ulioupokea katika maisha yako, utajifunza mambo mengi na ni maombi yetu ya kwamba kitabu hiki kiwe msaada mkubwa sana kwako.

Mambo utakayojifunza:

Sura ya Kwanza: katika sura ya kwanza utajifunza namna ambavyo dunia hii si mahali pa kupategemea na ya kwamba si mahali pa kudumu, na pia utajua kama dunia si mahali pa kupategemea je hatma yako ni nini, na ni nini mwisho wa maisha yako.

Sura ya Pili: itakusaidia kujua ni nini unachotakiwa kufanya kama dunia si mahali pa kudumu ili uweze kufika unakotakiwa kwenda, utajifunza kuwa unahitaji sana maandalizi ya kuelekea mahali unapotakiwa kwenda.

Sura ya Tatu: mambo ya msingi ikiwa ni mwendelezo wa sura ya pili ni kujua ya kwamba unakokwenda hutakiwi kwenda mikono mitupu, kuna mambo unayotakiwa kuyabeba, hivyo kwanza utajikuta kuna maswali unatakiwa kuyajibu ya ulichobeba kwanza na kisha utajua ni nini unatakiwa kubeba.

Sura ya Nne: sura hii itakuelekeza mambo ambayo ni muhimu uyafahamu katika safari hii, mambo yatakayotokea njiani, mambo ambayo yanapotokea usishangae, lakini pia utapata tumaini kwa kujua ya kwamba hauko peke yako.

Nimalizie utangulizi huu kwa kusema JIANDAE KURUDI NYUMBANI.

Sura ya kwanza.

DUNIANI SIO KWETU

Nataka niweke wazo hili kwanza kwako wakati unaendelea kusoma sehemu hii, ni kwamba DUNIANI SIYO KWETU, ndio! Namaanisha hata wewe hapo ulipo, Duniani siyo Kwako, haijalishi umeweka nini duniani, au unaipendaje dunia, au dunia inakupendaje. Si kitu unawapendaje watu wa dunia na vitu vya dunia lakini nataka ujue, na siyo utani kabisa kwamba hapa DUNIANI SIYO KWETU.

Waebrania 13:13-14 imeandikwa hivi;

13 Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutumu lake. 14 Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.

Tuesday, August 26, 2014

Kuna Uhusiano Mkubwa kati ya Usalama na Ubora wa Nafsi yako na Uhai wa Kanisa -III na Mwalimu Samwel Mkumbo

 

 Mwalimu Samuel Mkumbo pichani
Karibu atika mifululizo yote ya somo hili kutoka mwanzo mpaka sasa imekuwa ni suala la kuangalia ni kwa jinsi gani nafsi zetu zinahusika sana katika Uhai wa Kanisa. Sehemu ya mwisho nitasema nawe kwa kifupi sana kuhusu Uhusiano wa nafsi ya Kanisa.

Karibu tujifunze pamoja…..

Luka 12:15 inasema hivi;

Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.

Ni heri kila mmoja akahakikisha ya kwamba Nafsi yake iko na furaha kila wakati, kwa ajili ya uhai wa kanisa lako, lakini pia kwa ajili ya uhai wa nyumba yako kama msingi wa kanisa, kwa ajili ya ofisi yako, kwa ajili ya ukoo wako.

Lakini pia ni vema kila mmoja akahakikisha anafanya bidii kumfurahisha mwingine na kuifanya nafsi ya mwingine isiwe na jeraha hata moja, kuifanya nafsi ya mwingine isitende dhambi, kila mmoja acheze karibu na mwenzake, kama kucheza basi tucheze peke yetu, hakikisha unamlinda mwenzake asipate shida wala asipotee.

1 Wakorintho 8:12 tunasoma hivi;

Hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri iliyo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo

Kuna Uhusiano Mkubwa kati ya Usalama na

Ubora wa Nafsi yako na Uhai wa Kanisa

Sasa labda tutazame kwa nafasi nyingine uhusiano wa Nafsi yako ikiwa na Usalama na ubora wa nafsi yako na Uhai wa Kanisa ikiwa ni la nyumbani au ni mahali unapoabudu au ofisini kwako au hata shuleni kwako unakosoma.

Labda niweke jambo hili la msingi, tunapozungumzia kanisa ni lazima tukajua ya kwamba si suala la dhehebu moja tu au suala la watu wanaosali kwa pamoja lakini suala la Kanisa ni jambo linalohusu watu wote waliookoka na wanaomkubali BWANA YESU kuwa ni mwokozi wa maisha yao na Mfalme wa Ulimwengu wote.

Sasa kuna shida ambayo ni muhimu tukaishughulikia vizuri kidogo ili tusipate shida tunapoangalia utekelezaji wa Somo hili, na jambo lenyewe ni lazima akili zetu na fahamu zetu zifunguke tukajua mambo kadhaa ili tuone Umuhimu wa kuona Nafsi ya kila mmoja inakuwa salama na bora ili Kanisa liweze kuwa Hai.

1 Wakorintho 3:16-17 tunasoma hivi;

Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.

Sasa kuna jambo la msingi hapo natamani tulitazame kwa makini sana sana, maana kama tusipolitazama kwa makini tunaweza tusielewe vizuri, na hilo jambo linatuonesha Uhusiano uliopo kati ya Usalama na Ubora wa Nafsi yako inavyohusiana na Uhai wa Kanisa la Tanzania, Kanisa la Ulimwengu mzima lakini pia kuanzia na Kanisa la Nyumbani kwako na mahali unapoabudu.

Basi tuutazame huo mstari kwa makini sana sana, kuna maneno kadhaa ya huo mstari natamani tuyatazame kwa makini …..Hamjui ya kuwa NINYI mmekuwa hekalu la Mungu….. na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani YENU?....... Kama MTU akiliharibu hekalu la Mungu,… Mungu atamharibu MTU huyo….. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo NINYI.

Maneno niliyoyaweka kwa herufi kubwa yana maana kubwa sana, Paulo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu anawaandikia Wakorintho akitaka kuwaonesha ni jinsi gani Uhusiano wa Kanisa unavyotengenezwa na unavyotegemea mtu mmoja mmoja. Anapozungumzia Hekalu la Mungu anasema ni NINYI au ndilo SISI kama tukijiweka kwenye nafasi ya Wakorintho na ambayo ni nafasi muhimu lazima tujiweke hapo ili hiyo nafasi tuichukue kwa Umuhimu mkubwa sana.

Jambo amabalo ni la kulitazama kwa makini kwenye mistari hiyo ni kwamba inapozungumziwa kanisa basi tunatazama kama Muunganiko wa watu,. Maana HEKALU LA MUNGU (moja) linajengwa na NINYI (wengi), lakini pia inawezekana hilo Hekalu la Mungu ambalo ni watu wengi likaharibiwa na MTU yaani mmoja. Sasa basi kuna jambo la kulitazama tena hapo kwa makini Zaidi, kwamba kama Hekalu la Mungu linalojengwa na SISI linaweza kuharibu na YULE au WEWE basi pia linaweza kujengwa na WEWE- Nitalielezea hilo baadae kwa undani.

Tuesday, August 5, 2014

USALAMA NA UBORA WA NAFSI YAKO UNAVYOHUSIANA NA UHAI WA KANISA na Mwl Samwel Mkumbo -Sehemu ya Kwanza

Karibuni katika makala haya yanayoletwa kwani na Mwalimu Samwel Mkumbo
 
Mwalimu Samwel Mkumbo

Uhai wa kitu chochote kile unategemea namna au jinsi mwenye huo uhai au aliyekabidhiwa dhamana yuko katika hali gani, unaweza kulaumu juu ya uharibifu wa jambo au mambo Fulani lakini kabla ya kulaumu angalia kwanza yeye aliyeharibu au aliyekabidhiwa mikononi mwake yuko katika hali gani.

MATENDO 20:28 inasema hivi;

Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

Sasa kabla sijaendelea Zaidi nataka niseme jambo la msingi sana hapa, kichwa cha Somo letu kinatuhitaji tuwe na ufahamu wa kuhakikisha kwamba kila tunachokiongea katika somo hili ni mambo makubwa mawili, NAFSI YAKO NA KANISA LAKO. Wewe ni nafsi moja katika kanisa, Je unayo kazi gani wewe kama Nafsi?

Unaweza usijue wala usiliangalie kwa uzito, lakini inapasa kuelewa tafsiri hii;

KANISA ni Nafsi za watu zilizounganishwa kwa kunia mamoja katika Imani yao na hiyo Imani wameijenga katika msingi wa YESU KRISTO, hivyo kanisa bila ya nafsi zilizokubaliana za watu wengi wa aina mbalimbali si kanisa maana ili wawe kanisa lazima nafsi zao ziungane kwa kunia mamoja na kuwa na Imani moja ambayo hiyo Imani ndiyo inatengeneza nia moja.

TAZAMA NAMI:

Ili kanisa liwe na Nguvu na likae katika mstari unaotakiwa ni lazima nafsi za watu ndani ya Kanisa ziwe ziko salama kabisa, yaani ziwe zimetunzwa katika hali ambayo uhakika wa kundi kuishi kwa Amani utakuwepo kwa uhakika.

Labda tuunganishe vipande viwili vya huo mstari wetu wa msingi ili uone jambo la msingi kidogo….. Jitunzeni nafsi zenu,,.,.. mpate kulilisha kanisa lake Mungu,.,.,..

Mfano wa Mtumwa Mwaminifu

Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo. Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini (LUKA 12:42-46)

Sasa hapo ninataka nikufundishe jambo ambalo kimsingi ambalo halipo kwenye Mistari hiyo hapo juu, na lenyewe ni juu ya adhabu aliyopewa huyo wakili. Ona mtari huu;,..,.. akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, AKILA NA KUNYWA NA KULEWA;,.,….

Maana suala sio kusema bwana wake anachelewa ila baada kuona bwana wake anachelewa alifanya nini? Na wala sio kuwapiga watumwa ila baada ya kuwapiga watumwa alifanya nini? Yeye alichokifanya ni KULA NA KUNYWA NA KULEWA,..,..

Biblia inaposema yeye ALIKULA NA KUNYWA NA KULEWA, maana yake aliacha kufanya alichotakiwa kufanya lakini pia aliiharibu nafsi yake kwa MVINYO yaani kwa Ulevi. Maana suala si kula na kunywa kwa sababu hayo ni mahitaji ya mwili wa kila mtu, lakini suala ni KULEWA na biblia inasema KILEO HUDHIHAKI,. Na pia HUPOTOA HUKUMU ZA HAKI.

Friday, July 25, 2014

JE UMEKATALIWA

                 
 

Mara Nyingi utasikia mtu akisema yule jamaa Ana Roho ya kukataliwa au mimi jamani kila ninachokifanya nakataliwa au kila ninapoenda nakataliwa.                         
 
Inawezekana umekataliwa mambo mengi katika maisha tena kibaya zaidi umekataliwa na watu wako wa karibu kama ndugu, jamaa na marafiki au pia waweza.kujikuta umekataliwa na wafanyakazi wenzako au wafanyabiashara wenzako au watumishi wenzako, wanafanya maamuzi makubwa lakini hawakihusishi labda wanakudharau wanaona kwamba hustahili kujua.     
Mara nyingi familia zimekuwa na tabia ya kuwakataa na kuwatenga wenye kipato kidogo katika familia, yamkini wewe ni mzaliwa wa kwanza lakini familia haikudhamini IMEKUKATAA kwasababu hawaoni mchango wako na.kwakweli hujafanya makusudi ni kwamba huna tu cha kutoa, wameuza uzaliwa wako wa kwanza kwa mdogo wako ambaye ndio Tajiri wa familia, wanaamua maamuzi makubwa ya familia hawakushirikishi kwasababu tu huna kitu.     Ndugu yangu watu wamekudharau ,wamekucheka, wamekung'ong'a kwasababu huna kitu au huna elimu au huna mtoto au huna mwenzi wa maisha, labda hali yako ya kukataliwa imesababisha huna hata pa kukaa wala huna wa kukupa chakula Ndugu yangu nimekuja kuongea na wewe siku ya Leo waliokukataa ni wanadamu tu ila Mungu hajakukataa wala hana mpango wa kukutaa unayo sababu ya kufurahi siku ya Leo kwasababu mfalme wa wafalme ,Mungu Mkuu,Jehova,Yahweh,HAJAKUTAKAA.                 
 
Ukisoma 1 Petro 2: 4-9, utaona jinsi hata Yesu alikataliwa lakini maandiko yanasema katika mstari wa 4 "Mmwendee yeye jiwe lililo hai lililokatakiwa na wanadamu lakini kwa Mungu ni TEULE LENYE HESHIMA".                         
 
Yesu alikataliwa na wanadamu, alipigwa, alidhihakiwa, alitemewa mate,alidharauliwa , ALIKATALIWA tena kwa watu wake wenyewe wakimkejeli huyu si mtoto wa fundi seremala tu iweje Leo a anatuletea wokovu kwasababu wao walikuwa na madaraja kwamba labda katika ukoo Fulani tu au watu wa aina Fulani ndio tu wanaweza kuwa wazuri wakasahau Yuko Mungu ambaye njia zake hazichunguziki,anayejua Mwanzo na Mwisho wake, Leo ndugu yangu ukumbuke Mungu ni yeye yuleyule hajabadilika anakuon tofauti na watesi wako wanavyokuona, hali ya sasa isikufanye ukakata tamaa ukakosa Baraka na Miujiza Mikubwa iliyo mbele yako, hivi unajua ndugu yangu wewe ni Uzao mteule,kuhani wa kifalme, taifa takatifu, mtu wa Milki ya Mungu? Usisikilize kelele zao Mungu anakuwazia mawazo Mema, hakuna mwanadamu mwenye usemi wa mwisho juu ya mustakabali wako aliyekuumba ndio anajua mustakabali wako yeye ndio anakujua, wao wakiona maskini, Mungu anakuona Tajiri, wakikuona huzai Mungu anaona hakuna tasa katika Israel, wakiona wewe wa mwisho Mungu anakuona kichwa wala si mkia, Wewe ni Mshindiiii.                          
 
 Inuka Mungu HAJAKUKATAA.........Haleluyaa

Tuesday, July 15, 2014

TAMBUA BARAKA ZINAZOKUJIA ZINATOKA WAPI na Mwalimu Samwel Mkumbo

Bwana Yesu asifiwe mpendwa karibu sana katika makala haya yanayoletwa kwenu na Mwalimu Samwel Mkumbo.

Mwalimu Samwel Mkumbo
Hakika Baraka ni jambo mojawapo la msingi sana kwa  watoto wa Mungu na ni jambo la Faraja tuonapo mwana wa Mungu akifanikiwa katika mambo yake yote. Kama inenwavyo;

..,….Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli. Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo…,… (3Yoh 1:1-2)

Sasa basi ni vema ukafahamu  ya kuwa kubarikiwa ni jambo la msingi sana na tena ni moja ya ushuhuda kwa watoto wa Mungu. Lakini pia Baraka ni kutukuka sana katika Ukuu wa Mungu na pia juu ya haya yote tunaweza kuona ni kwa jinsi gani uweza  wa Mungu unajidhihirisha katika mambo yetu ya mwilini naam katika kutuma mema katika Tumaini jipya la imani yetu.

Lakini pia Biblia inatupa maelezo kadhaa juu ya kupata Baraka au mafanikio maana si kila mafanikio (Baraka) zina mkono wa Mungu ndani yake, au ni utukufu wa Mungu mingine ni mitego ya shetani katika kutuangusha katika imani yetu katika KRISTO YESU, naam! Maandiko matakatifu yanatupa mifano kadhaa ya Baraka zitokazo kwa Mungu na zile zinazoletwa na mwovu kama mtego kwetu.

Vielelezo!!

-Habari za Elisha na Naamani.

2 Wafalme 5:1-14 tunaona kisa kizuri na cha kutufundisha juu ya Baraka.

Nabii Elisha alipata nafasi ya kufanya muujiza wa uponyaji kwa Naamani (Yule jemadari wa Shamu) juu ya ukoma wake, na baada ya muujiza huo, mtu huyo, huyo Naamani alitaka kumpa zawadi Elisha, lakini Elisha hakukubali,. 2 Wafalme 5: 15-16 inasema;

Akamrudia Yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa  tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako. Lakini akasema, Kama BWANA aishivyo ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee, lakini akakataa.

Katika maandiko hayo utaona ya kuwa Elisha hakupokea Baraka kutoka kwa Yule Jemadari naam, huyo  Naamani, lakini ni vema tukafahamu ya kuwa si kwa sababu Elisha alikuwa na tabia ya kutopokea zawadi na Mbaraka kutoka kwa watu aliowahudumia, la hasha! Bali ipo sababu nyingine, maana  ni Elisha huyu huyu alipokea msaada kutoka kwa mama Mshunami! Tazama hapa;  2Wafalme 4:8

Kwa hiyo si kila tunuku unayopewa ni ya kukubali lakini pia si zote ni za kukataa maana kila jambo lina maana yake na matokeo yake ambayo kwa hayo twaweza kutambua kusudi na mapenzi ya Mungu kwetu lakini pia hila na mitego ya shetani.


-Mfano wa Yesu.

Monday, June 23, 2014

NAFSI ILIYONASWA na UZINZI na Frank Philip



Mtumishi Frank Philip
Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani …Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika” (Mithali 6:26 & 32,33).

Nimeona jambo hili, nami nikatafuta kujua kama kuna hekima ndani yake “men’s hearts can be shared, but women’s hearts replaces”. Maana yake: Moyo wa mwanaume ukipenda, waweza kupenda tena kwa wakati mmoja, ila moyo wa manamke ukipenda, humwondoa wa kwanza na kumpenda mwingine.

Ukitaka kuona kwa njia ya urahisi, jiulize ni kwanini mwanaume mmoja anaweza kuoa wake zaidi ya mmoja na maisha yakaenda? Na jiulize tena, je! Mwanamke anaweza kuwa na mpenzi wa nje ampendaye sana, na maisha yake ya ndoa/mahusiano yakawa sawa? Wote wawili: mwanamke na mwanaume, wana hatari ya kuingiliwa mioyoni mwao, japo kwa madhara tofauti.

Hii hali sio rahisi kuikubali katika mahusiano ya kawaida ambapo mtu anatoka nje ya ndoa/uhusiano kwa siri. Mara nyingi mtu afanyaye mambo hayo, hudhani yuko sawa, kumbe ameathirika kabisa. Ukitaka kujua ninachosema, angalia mambo ya kawaida kabisa ya kwenye ndoa/uhusiano kwa watu ambao mmoja au wote wamenaswa nafsi na kahaba. Mambo ya kawaida kabisa kwenye uhusiano/ndoa yanaanza kuwa kero, mzigo na ya kuchosha. Ukiona hii shida, usipambane na mtu kwa jinsi ya mwilini, shughulika na nafsi kwa sababu hapo ndipo penye shida.

Nitasema na wanawake sasa. Hii hali ya “replacement”, huwa haianzi mara moja. Huenda kwa awamu, na hatua mbali mbali, kuanzia hisia, matendo kisha ngono. Ndio maana mwanamke akitoka nje ya ndoa watu husema “amefika mbali”. Mara zote huanza na “nafsi kunaswa” na kahaba. Kama kuna mtego mbaya, ni kuacha nafsi yako inaswe. Kwenye nafsi ndiko kuliko na mawazo na maamuzi. Kama nafsi imenaswa, mara ZOTE mtu ataanza kuwaza tofauti, na kisha kufanya maamuzi mabaya. Ndio maana tunaonywa sana kwamba “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima” (Mithali 4:23). Ukitaka kuona uzima kwenye ndoa/uhusiano wako, linda sana moyo wako; ukitaka kuona mauti kwenye ndoa/uhusiano wako, achilia moyo wako uingiliwe.

Thursday, June 5, 2014

KIVULI cha NAKALA HALISI na Mwalimu Frank Philip

Karibu katika makala haya ya Mafundisho ya Neno la Mungu yanayoletwa kwenu na Mtumishi wa Mungu Frank Philip.


Mwalimu Frank Philip
Katika maisha ya kila siku, tumekuwa na utaratibu wa kutumia KIVULI (copy) cha nakala HALISI (original), kwa matumizi mbali mbali. Mara nyingi, kama sio zote, kivuli cha nakala halisi huweza kutumika kama nakala halisi, hadi kuwe na ulazima wa kuonesha nakala halisi. Kwa mahali pengine, kivuli cha nakala halisi hakiwezi kusaidia kitu, hadi nakala halisi iwepo. Kwa matumizi ya kuanzia (preliminary use), kivuli cha nakala, huwa ni kitu cha msaada; kwa matumizi mengine maalum, kivuli hakimfai mtu kitu. Kwa mfano, huwezi kusafiri na kuingia nchi nyingine kwa kutumia vivuli vya nyaraka za kusafiria. Ndiyo ilivyo hata kwa nchi tunayoiendea baada ya maisha haya, jina lake ni Yerusalem mpya, ushukao kutoka juu. Huwezi kuingia na kivuli cha wokovu, unahitaji vazi halisi. Wokovu ni vazi jeupe, limeoshwa kwa Damu ya Mwana-kondoo. Huwezi kuingia kwenye karamu ya Mwana-kondoo bila vazi halisi.

Sifa moja kubwa ya kivuli cha nakala halisi ni kufanana sana, hasa kwa kubeba taarifa muhimu. Mara nyingi, kama sio zote, kulingana na kinakilishi (photo copier), ni vigumu kubainisha kati ya kivuli na halisi, hadi kwa kutumia vifaa maalum (counterfeit detectors). Bwana Yesu akasema, “acheni msing’oe, msije mkang’oa na ngano pia”! Hii inaonesha mfanano wa hali ya juu kiasi kwamba unaweza kung’oa ngano ukidhani ni gugu. Hivi ndivyo ilivyo hata kwa watu wenye majina ya kuwa hai, kumbe! Wamekufa. Tunadhani tuko na wenzetu, kumbe ni kivuli tu! Dhambi huleta mauti. Atendaye dhambi ni wa Ibilisi, japo anaishi, amekufa. Kweli hatuokolewi kwa matendo ya sharia, ila matendo yako yatakufanya kuwa kivuli au halisi.

Kwa kuelezea jambo hili, Bwana Yesu alitumia mfano wa magugu na ngano (Mathayo 13:24-30). Kwa bahati mbaya, kila shamba la ngano huwa na magugu, tena mengi. Ndipo wanafunzi wake waliposhangaa, kwanini Bwana hakutoa kibali cha kung’oa magugu mara moja? Bwana Yesu alisema “acheni magugu na ngano vikue pamoja”. Angalia neno hili, wakati ngano inakua, na magugu yanakua pia. Laiti kimoja kingekua zaidi ya kingine, ndipo tofauti ingekuwa dhahiri. Lakini ona sasa, kila ngano ikuapo, magugu hukua pia!

Nikitizama mfano wa magugu na ngano najifunza mambo mengi. Kwanza, magugu na ngano yanaweza kuwa kiwakilishi cha jamii ambayo hapa naita “shambani mwa Bwana”, kwa lugha nyepesi, mkusanyiko wa waaminio. Sasa najua shambani mwa bwana ni zaidi ya mkusanyiko wa waaminio, lakini kwa sasa, nachukua kundi la wana wa Mungu kama ngano, na kundi la wana wa giza kama magugu. Ona jambo hili, wote wanakaa katika shamba moja; na Bwana anasema, usiwatenganishe, waache wakue pamoja! Pili, nikaona jambo hili kuwa la msingi sana, Je! Kama ngano ingetengwa kabisa na magugu, tungejuaje sifa za ngano fulani katika kupambana na mazingira yake? Nani angejua tofauti ya ngano bora na mbovu, dhaifu na njema? Kwa maana, kama ngano ikizidiwa na magugu, basi kila mmoja atajua udhaifu wake. Kumbuka imeandikwa “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo” (Ufunuo 21:17). Lakini kukiwepo na ngano ambayo itastahimili magugu, na kuzaa kati ya magugu hayo, na kuonekana kwa dhahiri tofauti yake baina ya magugu, hiyo itakuwa ngano njema na yakusifiwa. Naam, yafaa kutunzwa ghalani, kwa maana ni ngano njema. Kwa ngano dhaifu, mara ipandwapo, hukua ila ilitingwa sana na magugu, na yamkini kushindwa kuzaa, na hatimaye kufanana na magugu kabisa. Ngano dhaifu namna hii, isiyozaa, haina tofauti na gugu, kwa maana imefanana sana, japo kwa jina, inaitwa ngano, hiyo ni gugu tu.

Tuesday, May 13, 2014

When the Little is Much by Pastor Yared Dondo


Pastor Yared Dondo
Lead Pastor,City Harvest Church
Opening Scripture 1 King 17 : 8-16

 “And the word of the Lord came unto him, saying,

 

9 Arise, get thee to Zarephath, which belongeth to Zidon, and dwell there: behold, I have commanded a widow woman there to sustain thee.

 

10 So he arose and went to Zarephath. And when he came to the gate of the city, behold, the widow woman was there gathering of sticks: and he called to her, and said, Fetch me, I pray thee, a little water in a vessel, that I may drink.

 

11 And as she was going to fetch it, he called to her, and said, Bring me, I pray thee, a morsel of bread in thine hand.

 

12 And she said, As the Lord thy God liveth, I have not a cake, but an handful of meal in a barrel, and a little oil in a cruse: and, behold, I am gathering two sticks, that I may go in and dress it for me and my son, that we may eat it, and die.

 

13 And Elijah said unto her, Fear not; go and do as thou hast said: but make me thereof a little cake first, and bring it unto me, and after make for thee and for thy son.

 

14 For thus saith the Lord God of Israel, The barrel of meal shall not waste, neither shall the cruse of oil fail, until the day that the Lord sendeth rain upon the earth.

 

15 And she went and did according to the saying of Elijah: and she, and he, and her house, did eat many days.

 

16 And the barrel of meal wasted not, neither did the cruse of oil fail, according to the word of the Lord, which he spake by Elijah.”

 

When Elijah request a help from a widow she replied that have nothing but a handful meal in a barrel and little oil in a cruse.

May be there is someone here who think he has little but I want to assure you God has different plan, the little you have can be much in the Kingdom of God

If God want to do something is doesn’t matter what you have, whether it is much or little, educated or not,rich or poor, ministry accepted or rejected, he will fulfill his word regardless of who is standing.

In the above story the country was devastated , there are several things that we can learn from this story;

1.      Poverty

The country was in Poverty.

Sometimes we complained that we are poor but we are not fair because our condition is better compared to others.

Some they don’t have place to live, the whole family( father, mother, grandmother, grandfather and kids) are working as servants to rich people

Elijah was poor even the brook that he depended for water dried. He has nothing.

As he was speaking to God, God told him to go to Zeraphat to meet a widow who will feed him.

In Verse  9 Arise, get thee to Zarephath, which belongeth to Zidon, and dwell there: behold, I have commanded a widow woman there to sustain thee.

In those days widows where poor than other people but still God commanded him to go widow.

The widow has nothing and she has given up with her life, she was waiting to die

She believes in God but has no hope to live again.

To believe in God is not sufficient we have to put into action what we Believe

 

2.      Promise

Wednesday, April 23, 2014

DAMU ICHORAYO MIPAKA na Pastor Sayuni Mngodo


Tusome kwa pamoja Yohana 5: 5-9

“5 Basi, hapo palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa muda wa miaka thelathini na minane. 6 Naye alipomwona huyo mtu amelala hapo, akatambua kwamba alikuwa amekaa hapo kwa muda mrefu, akamwuliza, "Je, wataka kupona?" 7 Naye akajibu, "Mheshimiwa, mimi sina mtu wa kunipeleka majini wakati yanapotibuliwa. Kila nikijaribu kuingia, mtu mwingine hunitangulia." 8 Yesu akamwambia, "Inuka, chukua mkeka wako utembee." 9 Mara huyo mtu akapona, akachukua mkeka wake, akatembea. Jambo hili lilifanyika siku ya Sabato.”

Yesu alipita katika birika lililokuwa likitibuliwa watu wa kwanza kudumbukia wanapata unafuu.

Akamkuta mtu amekuwa mgonjwa kwa miaka 38 amekaa pale eneo la birika akiwa amelala na kwenye ya godoro.

Yesu alipofika pale akamuuliza unataka nikufanyie nini, akasema hakuna mtu wa kunipeleka katika birika.

Jibu lake linafanya tujiulize hivi kweli hakuwahi kuona mtu wa kumsaidia.

Dunia haitafuti mtu wa kumpa msaada wa chakula au malazi bali inatafuta mtu atakayewanganisha na MUUJIZA wao.

Warumi 8: 19

“Viumbe vyote vinatazamia kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto wake”

Watu wana nia, shauku na njaa ya kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Ina maana kuna kitu hakiko sawa mahali fulani, kinasubiri udhihirisho wa wana wa Mungu.

Kutumika kama daraja kati ya dunia na utatuzi wa matatizo yao.

Najua utaniuliza nani ni mwana wa Mungu, hebu tusome mistari ya Biblia hapo juu

Yohana 1:11-12

“Alikuja katika nchi yake mwenyewe, nao walio wake hawakumpokea. 12 Lakini wale wote waliompokea na kumwamini, hao aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu”

 

Warumi 8: 14

“Wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni watoto wa Mungu”

 

Kama umempokea Yesu wewe ni mwana wa Mungu

Katika Ofisi yako, biashara yako na majirani wajue wewe ni mwana wa Mungu.

Sasa hiyo ilikuwa msingi, tuingie katika somo la PASAKA sasa..

Fungua na mimi Kutoka 12: 1-13

Monday, April 14, 2014

Mambo ya Msingi Kanisa linayoweza kupata kwa kujua/ kufahamu asili yake Sehemu ya II na Mwalimu Samwel Mkumbo

Mwalimu Samwel Mkumbo
Wiki iliyopita tulitazama kwa sehemu kama Utangulizi tu unaotupeleka kwenye Kujua kulingana na Somo hili juu ya MAMBO YA MSINGI KANISA LINAYOWEZA KUPATA KWA KUJUA/KUFAHAMU ASILI YAKE. Karibu tuendelee mtu wa Mungu,

 
Upo umuhimu sana wa kufahamu Asili ya Kanisa, na kama nilivyosema hapo mwanzoni ni kwamba si kwamba ninazungumzia Asili ya Kanisa kwa mtazamo wa Historia yake au mpangilio wa matukio yaliyotokea kwenye Kanisa tangu lilivyozaliwa, la hasha! Lakini nazungumzia Asili ya Kanisa kwa kutazama Uzao na Nafasi yake.

Hebu tutazame mifano michache itakayonisaidia kukuelekeza mambo ambayo ninataka nikuoneshe mtu wa MUNGU, katika mifano hii utaona mambo kadhaa ambayo yatafungua ufahamu wako umuhimu wa kujua Asili ya Kanisa kwa kutazama Uzao na Nafasi yake.

Habari za Wana wa Skewa.

Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.  (Matendo 19:13-16)

Sasa lengo kubwa si kukuonesha hadithi hiyo nzima, lakini kuna kipengele ambacho hakipo hapo kwenye hiyo mistari na si kwamba kimesahaulika kwenye hiyo mistari lakini hakipo kabisa,  lakini nataka nikitumie hicho hicho kipengele ambacho ukiangalia kwa undani hakipo ndicho nataka nitumie kukufundisha hapo. Kipengele chenyewe ni MAJIBU YA WANA WA SKEWA.

Wednesday, April 9, 2014

Nilichojifunza kuelekea Maadhimisho ya Miaka 75 ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God(TAG)


Kanisa la Tanzania Assemblies of God liko katika maandalizi ya kusherekea miaka 75 tangia kuanzishwa kwake. Kanisa hilo lilianzishwa mwaka 1939 na Mmishenari aitwaye Paul Deer ambaye alitokea katika uamsho wa Kipentekoste wa Azusa uliotokea kule Los Angeles, California nchini Marekani miaka ya 1906 hadi 1915.


Askofu Emmanuel Lazaro, Askofu wa Kwanza wa Kanisa la TAG


Paul Deer alifikia mkoani Mbeya ndipo akaanzisha Kanisa la TAG akishiriakiana na watu wengine.

Maadhimisho hayo yamesaidia tukaweza kujua mambo muhimu sana ambayo Wakristo wenzetu waliyafanya ili kuhakikisha kanisa linakuwepo na kuenea duniani.

Jambo kumbwa sana lililonifanya nijifikirie mara mbilimbili juu ya maisha yangu ya Ukristo ni jinsi wamishenari hao walivyotembea miles 120 ili tu kuhakikisha sehemu mbalimbali za Afrika zinapata Injili ya Kweli ya Yesu Kristo.
 
Askofu Dr Barnabas Mtokambali, Askofu Mkuu wa sasa wa Kanisa la TAG

Sasa nikiangalia kizazi cha sasa tulivyozoea kupanda bajaji, pikipiki na tax katika umbali mfupi ilimradi tu tusitembee maana ni wavivu watoto wa dotcom, je kweli tunaweze kutembea mpaka Tandahimba kupeleka Injili ya Yesu Kristo? Kwani hao waliotutangulia walisukumwa na nini hasa? Na sisi tutafanyaje basi ndugu yangu ili tuweze kuacha historia ya Injili hapa duniani.

Tujue kwamba kule Mbinguni kutakuwa na taji je kwa unavyojiangalia utavikwa taji kwa jambo gani hasa ulilolifanya la KUJITOA HASWAA kwa ajili ya Injili………….Tujichunguze na kumuomba Mungu atusaidie ni wapi anataka tumtumikie ili na sisi tubaki katika Historia kwamba tulifanya a,b,c kwa ajili ya Injili.

Kwa kifupi Maadhimisho yatafikia Kilele mwezi wa saba kule Mbeya.

 

Endelea kutembelea Rejoice and Rejoice Blog mambo mazuri yanakuja

 

Ubarikiwe na Bwana Yesu Kristo, Amen

Tuesday, April 1, 2014

Mambo ya Msingi Kanisa linayoweza kupata kwa Kujua au Kufahamu Asili yake na Mwalimu Samwel Mkumbo


 Amani ya Kristo iwe pamoja nawe mtu wa Mungu, Karibu katika makala haya yanayoletwa kwenu na Mwalimu Samwel Mkumbo ambaye ni Graduate wa Chuo Kikuu Dar es Salaam na alikuwa Coordinator wa Fellowship ya God Kingdom Business (GKB)
 
Mwalimu Samwel Mkumbo
UTANGULIZI...

Lengo kubwa la somo hili ni kutazama ni vitu gani ambavyo kanisa la Tanzania na Ulimwengu kwa ujumla linakosa kwa sababu tu Kanisa halijachukua maamuzi ya kujua Asili yake na namna ambavyo MUNGU analitazama Kanisa.

Na labda niweke wazi jambo hili ya kwamba si azimio kubwa katika Somo hili kusema ASILI ya Kanisa kwa namna ya Historia ya kuzaliwa kwake kwa kutaja miaka au labda matukio ya muhimu, la hasha! Japo tunaweza kuangalia Historia kwa sehemu kidogo tu ikibisi kufanya hivyo ili kujua mambo mengi zaidi.

Maana ninajua wapo wazee wetu wa Imani na wenye kuijua Historia ya Kanisa la Tanzania na Ulimwengu kwa ujumla na wanafundisha hayo hivyo basi Azimio kubwa ndani ya Somo hili ni kutaka Kanisa lijue Asili yake kwa namna ya Uzao na Nafasi yake! Ndio! ASILI YAKE kwa kuangalia UZAO na NAFASI yake.

SEHEMU YA KWANZA

Moja ya jambo ambalo MUNGU analitaka ni sisi watu tuliookoka Kujua Asili yetu ndani ya Asili tuliyokuwa nayo. Yaani inapasa tufahamu kuwa sisi ni kina nani tunatoka wapi na tunakwenda wapi, naam ni watu wa shina na chipukizi gani?

Na mara kadhaa kwenye Biblia Mungu anataka na watumishi wake wanafanya juhudi kutaka kutujulisha asili ya Kanisa, maana tunapoijua asili ya Kanisa kuna mambo ya msingi tunayapata ndani yake na ambayo tusipojua asili ya Kanisa hatuwezi kuyapata, na hayo mambo si kama ni ya ziada kwamba tukiyapata sawa na tukiyakosa sawa, HAPANA! Ni mambo ya MSINGI na ni Muhimu sana Kanisa likafahamu kwa upana wake hasa vijana ambao kesho na keshokutwa ndio watakaokuja kuliongoza na kulilea Kanisa, ndio! Ni muhimu sana sana.

1 Petro 1:18 inasema hivi;

Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;

Thursday, March 13, 2014

Moyo wa Mwanamke 2014: Wanawake wajifunza Umuhimu wa Nguvu ya Maarifa katika maisha yao

 
Kongomano hilo la siku tano lililofanyika katika kanisa la Living Water Kawe (Makuti) ambako ndio Kanisa la mbeba maono hayo ya Moyo wa Mwanamke Mama Mchungaji Lilian Ndegi liliwafanya wanawake waingie katika viwango vingine vya juu baada ya kujifunza Umuhimu wa Maarifa katika maisha ya Mwanamke.
 
 

Mchungaji Lilian Ndegi akifungua kwa maombi, kwakweli Mungu alimtumia sana huyu mama katika njia ya tofauti. Hapo unaweza kuona karama za Roho Mtakatifu zinavyofanya kazi hasa pale unapoamua kumtafuta Mungu kwa bidii.

 
Mchungaji Lilian Ndegi pamoja na watumishi wengine kutoka sehemu mbalimbali za Afrika walikuwa wanenani katika Kongomano hilo. Baadhi ya Wanenani hao ni mbeba maono mwenyewe Pastor Lilian Ndegi, Esimy Kabeya (Afrika ya Kusini) ,Prophetes Jeanne Kiratu (Mombasa Kenya), Pastor Jael (Nairobi Kenya),Pastor Florence (Gloryland Arusha) na Mchungaji Naomi Mhamba ( Living Water Kawe)
Mungu aliwatumia sana hawa watumishi wake kuleta ujumbe wa Nguvu ya maarifa katika wanawake.
Wanawake walipata nafasi ya kujifunza jinsi ambavyo Mwanamke asipokuwa na maarifa nyumba na maisha yake yataharibika kama ilivyoandikwa katika Hosea 4: 6 "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako"

 
Mchungaji Naomi Mhamba(Prof.) alifundisha juu ya Uponyaji wa Uzao wa Mwanamke Vs Nguvu ya maarifa alifundisha vizuri sana akitoa mifano halisi ya kulea kizazi hiki na maarifa yamekuwa mengi ambapo Ibilisi analeta maarifa mengi katika jamii na yanavizia watoto na jinsi ya kukabiliana na hila hizo za Ibilisi kwa kumlea mtoto kama Mungu alivyokusudia


Wamama wakisikiliza kwa makini kwakweli ungeangalia nyuso zao kila mmoja aliweza kupokea kitu kipya cha kumsadia yeye, maisha na familia yake. Na kama tunavyojua ukimfundisha Mwanamke umefundisha jamii.



Mtumishi Esimy Kabeya kutoka Afrika Kusini na yeye alifundisha juu ya Nguvu ya Uelewa katika maisha ya mwanamke.


Picha ya Watumishi/ Wananaji wa Kongomonano hilo la Moyo wa Mwanamke



Wanawake wakiwa chini ya Uvuvio wa Roho Mtakatifu


 
Siyo kama mama alifungisha Harusi siku hiyo jamani ni style ya kufundisha ya mama huyu ambayo inamfanya mtu unaelewa kwa kiwango cha juu, hapa anaonyesha mfano wa wanawake wawili tofauti mwenye Hekima na asiye na Hekima. Kwa nje anaweza kuonekana mdada mrembo lakini kumbe ndani hana hekima na mwingine anaweza akaonekana kwa nje labda havutii sana lakini ndani akawa na hekima
 
 

 
Pastor Lilian Ndegi akifundisha kwa kutumia mfano wa wacheza Karata waliokuwa wanacheza kwa kutumia Almasi ,ikiwa na maana kwamba usipokuwa na maarifa utafanya kitu cha thamani kikose uthamani wake na ni rahisi kukupoteza
 
Prophetess Jeanne Kiratu kutoka Mombasa Kenya alifundisha juu ya Jinsi Mungu anavyokwenda kufanya Turn Around (Mageuzi) katika maisha ya mwanamke pale atakapotumia Maarifa yaliyoko katika Neno la Mungu katika maisha yake
 
Pastor Jael kutoka Nairobi na yeye alifundisha Nguvu ya Hekima katika maisha ya Mwanamke, alifundisha kwa njia ya shuhuda za wanawake mbalimbali ambao zamani hawakuwa na hekima katika maisha yao lakini walipopata maarifa wakaishika Hekima na maisha yao na familia yakabadilika hadi watu wakashangaa
 
 

 

Pastor Florence kutoka Gloryland Arusha alifundisha juu ya Nguvu saba za Maarifa, akafafanua kwamba wengi wanaomba tu bila kuwa na maarifa lakini mara nyingine maombi bila maarifa ni kama kelele mbele za Bwana. Mchunangaji huyu alifanya wanawake wacheke sana kwa style yake ya kufundisha kwa umaridadi. Alifundisha wanawake umuhimu wa kuishi kama Malkia na Wafalme.


Neema Baraka na yeye alikuwepo kumwimbia na kumtukuza Bwana, wanawake walipata nafasi ya kumsifu na kumtukuza Bwana Yesu.




Kusifu na Kuabudu



 

Upendo Nnkone alikuwepo katika huduma yake ya kumsifu na kumwabudu Bwana Yesu





Ritha Chuwalo akimchezea Bwana Yesu, twendeeeee


Chezea Bwana...



Wow Wow kulikuwa na mambo mengine mazuri pia katika Kongomano hilo ambapo siku ya Tarehe sita ilikuwa ni Birthday ya mama Pastor Lilian Ndegi ambapo wamama walikuwa wameandaa Cake na wanawake waliweza kushiriki kwa pamoja. Happy Belated Birthday Mchungaji..


Caaaaaake...




 
Kata Cake tuleeee..


Pastor Lilian Ndegi akilisha wengine Cake



Pia mama Mchungaji Lilian Ndegi alizindua Kitabu chake cha Thamani Maneno ya Kinywa Changu, nakushauri Mwanamke mwenzangu utafute hicho kitabu maana kinachotuponza wanawake ni Maneno :) . Haleluyaaaaaaaaaaaaaaa