Neno Yuda 1: 3-4
“Wapendwa, ingawa nilikuwa na hamu kubwa kuwaandikieni kuhusu wokovu
wetu, nimeona ni muhimu niwaandikieni nikiwasihi mwendelee kuipigania
kwa nguvu imani ambayo Mungu amewakabidhi watakatifu mara moja tu kwa
wakati wote. 4 Hii ni kwa sababu watu wasiomcha Mungu ambao tangu
zamani wamekwisha kuandikiwa hukumu hii, wamejiingiza miongoni mwenu
kwa siri. Hawa ni watu ambao wanapotosha neema ya Mungu wetu na
kuitumia kama kisingizio cha kutenda maovu. Wao wanamkana Yesu Kristo
ambaye pekee ndiye Mkuu na Bwana wetu.”
Kanisa limevamiwa na watu ambao sio wa kweli au wasanii, wamejiingiza
kwa siri na nia zao za kupotosha Imani ya Ukiristo.
Hawana nia ya kumtumikia Mungu wala kwenda mbinguni wana mipango ya
siri. Hawana nia ya Wokovu.
1 Timotheo 4: 1-2
“Roho anasema wazi wazi kwamba katika siku za mwisho watu wengine
wataiacha imani yao na kusikiliza roho za udanganyifu na mafundisho ya
mashetani. 2 Mafundisho hayo yanaletwa na wanafiki waongo ambao
dhamiri zao zimekufa kama vile zimechomwa kwa chuma cha moto. “
Mambo ambayo yamelikumba Kanisa la sasa
1. Kuna mambo mengi yamelikumba Kanisa la sasa kama mafundisho potofu
na manabii wa uongo.
1 Yohana 4:1
“Wapendwa, msiamini kila roho bali zipimeni roho zote kwa makini muone
kama zinatoka kwa Mungu. Kwa maana manabii wengi wa uongo wametokea
duniani.”
Sio kila mtu anasema Bwana Asifiwe ni mtumishi wa Mungu
Kuna watu wamejiingiza hawana nia njema na wokovu, ni wapotoshaji wa
Neno la Mungu
Kuwa makini na mafundisho unayoyapata
Kuna maombezi yanaendeshwa sasahivi watu wanakuwa kama walivyozaliwa
na jinsia tofauti
Kuna watu wamejiingiza makanisani hawana nia nzuri na kanisa
1 Timotheo 4: 3-4
Itakuja wakati watageukia mafundisho ya uongo na kuacha mafundisho ya uzima.
Usiamini kila roho zipime roho
Kuna waumini wengine ni watafiti ,kila siku anabadili kanisa ,
wamekuwa kama helikopta kila siku kutafuta poa kutua
Wachungaji wanapata shida na waumini watoro, wanawapa wachungaji
stress maana wanarandaranda makanisani
2. Mwenendo wa Kanisa unabadilika ukilinganisha na tulikotoka hasa
kwasababu ya utandawazi kukua kwa kasi
Waumini wengi hawataki kukemewa wanataka wachungaji wahubiri
wanachotaka wao na sio kile Mungu anataka. Na ndio maana
wanarandaranda wakitafuta wachungaji watakaoubiri wanachotaka,
wakisikia mahubiri ya kukemewa tu wanahama kanisa wanaenda kutafiti
kwingine.
Lakini inabidi kumuomba Mungu akutane na wewe, Mungu akuguse
,akutembelee na kukufinyanga
3. Badala ya dunia kufuatisha Kanisa , Kanisa linafuatisha namna ya Dunia
Turudi kwenye misingi ya wokovu, turudi kwa Mungu
Mathayo 6: 33
“ Lakini uta futeni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya
yote mtaongezewa.”
Mungu ameahidi mtu akikaa na Mungu basi Baraka zitamfuata,basi tukae
na Mungu kwanza, tumtafute Mungu kwanza hayo mengine yote yataongezwa
kwetu
Wengine wanakimbilia kuwekewa mikono na kila aina ya watumishi ili
wafanikiwe, wengine wananyeshwa maji , mafuta, chumvi ili wabarikiwe.
Waumini wa leo wamegeuza baadhi ya watumishi kama waganga wa kienyeji
ili kuwatabiria maisha yao na mustakabali wao. Wengi wanataka miujiza
lakini hawamtaki mtenda miujiza.
Kaa ulipo na simama katika Imani, Mungu atakutokea
Imani yetu ni ya muhimu sana yapasa KUILINDA
Mambo yatupasayo kufanya kulinda Imani
1. Jihakiki kama kweli umezaliwa mara ya pili
Je mwenendo wako ukoje
Wokovu sio kitu cha kisanii ni kitu halisi na ukifanya vibaya utaishia pabaya
Lazima uwe na mahali unapolelewa maisha yako ya Ukiristo sio
kurandaranda kwenye makanisa mbalimbali
2. Kuishi maisha Matakatifu
1 Peter 1: 15-16
“Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, kadhalika ninyi muwe
watakatifu katika mwenendo wenu; 16 maana imeandikwa: “Muwe watakatifu
kwa sababu mimi ni mtakatifu.”
Tusiwe watu wenye nia mbili
Mathayo 23: 27
“Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnafanana
na makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa juu yanaonekana maridadi
lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu.”
Wengine ni wanafiki wanaishi maisha ya wokovu wakiwa karibu na
Wachungaji tu au watu waliookoka,au wakiwa kanisani lakini wakiwa nje
wala hakuna anayejua kwamba wameokoka maana wanajichanganya na namna
ya dunia hii.
Marko 7: 6
Ufunuo 3: 15- 16
Msimamo wa wokovu lazima ujulikane
3. Tuishi maisha yenye ushuhuda
1 Peter 2: 11-12
“Wapendwa, ninawasihi, mkiwa kama wageni na wapi taji njia hapa
duniani, epukeni tamaa mbaya za mwili ambazo hupi gana vita na roho
zenu. 12 Muwe na mwenendo mwema kati ya watu wasiomjua Mungu, ili kama
watawasema kuwa wakosaji, wayaone matendo yenu mema na wamtukuze Mungu
siku ile atakapotujia.”
Majirani zako wanasemaje kuhusu wewe ,mtaani ,kazini wanasemaje
Sisi ni ladha, chumvi na mwanga ,tusilitukanishe Jina la Mungu
Maisha yetu yanatakiwa yabariki na yainue na yawavutie wengine kwa Yesu
1 Timotheo 4:12
Kuwa kielelezo, watu waige kutoka kwako, wamuone Yesu.
Watu wamtukuze Yesu kwa maisha yako
Yohana 12: 26
Ukimtumikia Mungu naye atakuheshimu
Ukikaa na Mungu , Miujiza Itakufuata
Mungu atusaidie ndugu zangu tuilinde IMANI yetu ya KIKRISTO,Amen