GET YOUR COPY NOW
Philipian 4:4
Philipian 4:4 "Rejoice in the Lord always. I will say it again: Rejoice!"
Showing posts with label Maombi. Show all posts
Showing posts with label Maombi. Show all posts
Thursday, May 25, 2017
Monday, December 26, 2016
MAOMBI YA FUNGUA MALANGO NA MILANGO - SEHEMU YA 7
Na Mchungaji Florian Katunzi -EAGT City Center
SILAHA NANE ZA KUFUNGUA MILANGO NA MALANGO YALIYOFUNGWA MBELE YAKO
Bwana apewe
sifa. Bado naendela na mfululizo wa somo hili ambapo katika makala zilizopita
nilikufundisha aina TANO za funguo za kufungua malango na milango. Nilizitaja
funguo hizo ambazo ni Neno la Mungu, Toba, Imani, maombi na Nguvu za Roho za
roho Mtakatifu. Kimsingi kama utazisoma na kuzielewa basi ni imani yangu ya
kuwa utafika mbali kiimani sanjari na kujua ni kwa jinsi gani unatakiwa
kupambana na adui shetani.
Leo nitahamia
katika kipengele kingine cha silaha nane za kufungua milango na malango,
Endelea….
Maombi yetu ya
Kufungua Milango na Malango yaliyofungwa inahitaji Uhodari na Uthabiti katika
Imani, hivyo lazima silaha hizi zitumike ndipo Milango na Malango yaliyofungwa
yatafunguliwa. Kufungua kilichofungwa si kazi rahisi. Maandiko matakatifu
yanasema; “Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani; kwa maana
kushindana kwetu si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya
wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa Roho, kwa
sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kushindana siku ya uovu,
na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.” Waefeso 6:10-14
Maisha yetu ya
Kristo yapo katika mgongano wa kiroho na shetani na huu mgongano unaitwa VITA
VYA IMANI. Ambavyo vinaendelea hadi atakapokuja mara ya pili Yesu Kristo
kuvikomesha. Lakini ushindi wa mtu wa Mungu umehakikishwa na Kristo mwenyewe
kwa njia ya kifo chake pale msalabani. Alipokufa na kufufuka ametangaza ushindi
kwa kila amwaminiye tangu wakati ule hata sasa tunashinda na zaidi ya kushinda.
Palipo na neno “KUSHINDA” maana yake pana neno “KUSHINDANA”.
Maisha yetu ya
imani ni ya kushindana na kushinda. Wengine kwa kutokujua, adui alipokuja
kushindana nao wakaogopa, wakaona Mungu amewaacha na kujiuliza maswali mengi
KWANINI BWANA AMEYARUHUSU HAYA? Kumbe maisha ya ukristo halisi ni vita sio
lelemama ndiyo maana BWANA anasema tuwe hodari na moyo wa ushujaa. “Uwe
hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakaye warithisha watu hawa… uwe
hodari tuu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote… usiache
kwenda mkono wa kuume au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.”
Yoshua 1:6-7
BWANA umtumia
mtu hodari na mwenye moyo wa ujasiri sio mtu legelege na dhaifu. Ndiyo maana
alimtumia Daudi kumpiga Goliati kwa sababu alikuwa na moyo wa uhodari na
ujasiri mwingi. Daudi hakwenda vitani kubahatisha bali alikwenda ksuhindana na
kushinda ndivyo ilivyotokea. Maandiko yanasema; “Mtu mwenye nguvu aliyejifunga
silaha zake alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama lakini mtu mwenye nguvu
kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang’anya silaha zake zote
alizokuwa akizitegemea na kuyagawanya mateka yake.” Luka 11:21-22
Yesu Kristo
anahimiza kujifunga silaha zetu na kuyalinda Malango na Milango yetu. Pasipo
kujifunga silaha hatuwezi kumshinda yule adui shetani. Lazima uzivae hizi
silaha ndipo zitakazofanya Ushinde Falme za giza, Wakuu wa giza hili na
kuyashinda Majeshi ya pepo wabaya. Maandiko yanasema; “Maana ingawa tunaenenda katika
mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili, maana silaha za vita vyetu si za mwili
bali zinauwezo katika Mungu hata kuangusha ngome.” 2Wakorinto 10:3-4
Vita vyetu vya
kiroho sharti vipiganwe kwa silaha za rohoni – pasipo kuvaa hizi silaha za
kiroho hatuwezi kuziangusha ngome zilizojengwa kinyume na zenye kuhakikisha
Malango hayafunguliwi.
SILAHA
YA KWANZA
Zipo silaha nane za kiimani zenye nguvu za kufungua malango na
milango iliyofungwa katika maisha yetu ya kiroho na kimwili. Silaha hizo ni:-
(i)
KATAA
Imani ni kuwa na hakika katika Mungu na
mwenye haki ataishi kwa imani. Maandiko matakatifu yanaonyesha waziwazi ya kuwa
msingi wa wokovu ni imani. Yatupasa kuyakataa yale tusiyoyaamini katika imani
yetu, mfano wa Musa alivyokataa kuitwa mtoto wa binti Farao, japo kuitwa mtoto
wa binti Farao kulikuwa na faida nyingi za kimwili lakini akachagua ufalme wa
Mungu na haki yake kuliko ufalme wa Farao ambao mwisho wake ni kutupwa jehanamu
ya moto. Hivyo Musa akatumia silaha hii ya kwanza ya KUKATAA matokeo yake BWANA
akamtumia kama shujaa na mkombozi wa wana wa Israeli toka utumwani Misri.
Maandiko matakatifu yanathibitisha; “Kwa Imani Musa alipozaliwa alifichwa miezi
mitatu na wazazi wake kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri wala hawakuogopa
amri ya mfalme KWA IMANI MUSA
ALIPOKUWA MTU MZIMA ALIKATAA KUITWA MWANA WA BINTI FARAO. Akaona afadhali
kupata mateso kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo akihesabu
kushutumiwa kwake Kristo ni UTAJIRI MKUU kuliko hazina za Misri kwa kuwa
aliyatazamia hayo malipo. Kwa Imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme,
maana alistahimili kama amuonaye yeye asiyeonekana kwa Imani alifanya Pasaka,
na kule kunyunyiza damu ili yule mwenye kuangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse
wao” Waebrania 11:23-28
Musa alikataa kuitwa mtoto wa binti
Farao, ukawa ndio mlango wa ukombozi wa wana wa Israel kutoka katika milango ya
kuzimu ya Farao. Hii ni silaha kubwa sana ambayo lazima tuivae kabla ya mambo
yote. Ni lazima kwa Moyo wako wote na Roho yako yote na kwa Akili zako zote Kataa hali uliyonayo
katika ulimwengu wa Roho ama katika Mwili. Maandiko matakatifu yanasema; “Tumbo
la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake. Mauti
na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”
Mithali 18:20-21
Ukiri katika
ulimi una nguvu ya kuangusha malango na milango ya kuzimu hivyo ulimi wa imani
ni mti wa uzima. Ni vema kutumia ndimi zetu kujitamkia mema sisi wenyewe,
kutamka mema kwa watoto wetu na juu ya mali zetu maana BWANA Mungu alitamka iwe
na ikawa. “Ulimi wa mwenye haki ni kama fedha teule; Moyo wa mtu mbaya haufai
kitu” Mithali 10:20
Dada
mmoja pale Morogoro eneo la Forest aliokoka akiwa na miaka kumi na mitano
(Miaka 15), siku moja akiwa anatoka shule pale Morogoro mjini, alikutana na
mvulana mmoja kumbe ni mjumbe wa shetani (mtu jini) lakini yeye aliona ni
mvulana, wakasalimiana, lakini kumbe huyu binti amevamiwa na nguvu za yule
jinni kwa sababu alimwambia dada nimekupenda naye akasema asante kama utani
lakini ndo ukiri wa kinywa. Baada ya hapo huyu binti alianza kuota ndoto mbaya,
anafanya mapenzi; hiyo hali iliendelea kwa muda mrefu akiwa ndani ya wokovu.
Huyu binti alipokuwa anakuja kwangu kuniona alikuwa na umri wa miaka thelathini
na sita (Miaka 36) akiwa bado hajaolewa, hiyo ilikuwa mwaka 2012, akisema;“Mchungaji
nimefunga na kuomba na nimetoa sadaka sana lakini sipati mpenyo, ee Mtu wa
Mungu niombee.”
Wakati naanza
kumpa ushauri ili nipate kumwombea, nikaitiisha ile nguvu iliyo mfunga
kwa jina lenye nguvu la Yesu Kristo. Ndipo nguvu ya pepo jinni dume likapiga
kelele likidai huyu binti ni mke wake, limemuoa akiwa na umri wa miaka kumi na
mitano kule Morogoro. Nikaipinga ile nguvu ya pepo, nikasema huyu ameokoka,
ninyi mnawezaje kukaa ndani yake? Nikahoji
tena ni mlango gani mliotumia
kumfunga huyu binti; yule jini akasema waziwazi huyu binti ni mvumilivu na
mwaminifu sana kwa huyo Mungu wenu, lakini mimi ninammiliki kwa sababu yeye mwenyewe hajawahi kunikataa na
kuitengua ndoa yetu, kwani hujui imeandikwaje katika Warumi? “Kwasababu
ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya
kuwa Mungu alimfufua katika wafu, Utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata
kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.” Warumi 10:9-10
Yule kijana
(Jini) alimwambia binti nakupenda naye akakubali lakini hawakuonana tena na ni
miaka zaidi ya kumi na sita ndoa ipo katika ulimwengu wa roho. Ukiri una nguvu
ya Uzima ama Mauti. Ni lazima ukatae na
utengue kila mkataba na maagano yote ya giza sawasawa na kuamini kwako. Ndiyo
maana Musa alikataa kwanza kabla ya wito wake. Tendo la kukataa kuitwa binti
Farao ndilo likamfanya Mungu amuite kwa kazi yake.
Wakristo wengi
wanataka kufunguliwa Milango na Malango lakini bado hawajakataa kabisa Mizimu
ya ukoo, Mizimu ya mababu na mabibi zao, maagano mbalimbali walioungamanishwa
kwayo kabla ya wokovu. Usikiri
Udhaifu juu yako, juu ya watoto wako, juu ya mume wako, juu ya mke wako, juu ya
kazi yako, juu ya ndoa yako wala juu ya maisha yako.
“Neno BWANA lilinijia, kusema, kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua,
na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; Nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Ndipo niliposema, Aa, Bwana Mungu! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.
LAKINI BWANA akaniambia, USISEME, Mimi ni mtoto maana utakwenda kwa kila
nitakayekutuma kwake, nawe UTASEMA KILA NENO NITAKALOKUAMURU. Usiogope
kwasababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana” Yeremia 1:4-8
Usiseme kinyume na Neno la Mungu juu yako maana BWANA anakuwazia mema naye
ulituma Neno kwako lipate kukuponya na kukufungulia milango na malango ya
Baraka na Ustawi.
Angalia Musa
pamoja na BWANA kumtumia katika kutenda maajabu na miujiza mingi, lakini Musa
alikufa akiwa na utasi (kigugumizi) kwa
sababu hakuukataa udhaifu huo bali aliukubali kuwa sehemu ya maisha yake.
Maandiko yanathibitisha;
“Musa
akamwambia BWANA, Ee Bwana, mimi si msemaji tokea zamani, wala tokea hapo
uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni
mzito. Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani
afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi,
BWANA? Basi sasa, enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha
utakalolinena. Akasema, Ee Bwana nakuomba, tuma kwa mkono wake huyo
utakayemtuma. HASIRA YA BWANA ikawaka juu ya Musa, akasema, je! Hayuko
Haruni, ndugu yako, Mlawi? Najua ya kuwa yeye aweza kusema vizuri. Pamoja na
hayo, tazama, anakuja kukulaki, naye atakapokuona, atafurahi moyoni mwake. Nawe
utasema naye, na kuyatia maneno kinywani mwake; nami nitakuwa pamoja na kinywa
chako, na pamoja na kinywa chake, na kuwafundisheni mtakayofanya. Naye atakuwa
msemaji wako kwa watu, hata yeye atakuwa mfano wa kinywa kwako, nawe utakuwa
mfano wa Mungu kwake. Nawe utatwaa fimbo hii mkononi mwako, na kwa hiyo
utazifanya zile ishara.” Kutoka
4:10-17
Mungu
alimkasirikia Musa kwa kitendo cha kukataa Uponyaji wa kinywa chake. Matokeo
yake mtumishi wa Mungu Musa mpaka anakufa, alikufa akiwa na utasi (kigugumizi).
Pia tunajifunza kwa YABESI; alikataa maisha
ya huzuni, Bwana akageuza huzuni zake kuwa heshima. Kabla ya kupokea hicho
unachotaka lazima uvae Silaha hii ya kukataa utaona mlango unafunguka
mbele yako.“Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze, na mamaye akamwita
jina lake Yabesi, akasema, Ni kwasababu nalimzaa kwa huzuni. Huyo Yabesi
akamlingana Mungu wa Israeli, akasema, Lau kwamba ungenibarikia kwelikweli, na
kunizidishia hozi yangu na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na
uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu!
Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.” 1Nyakati 4:9-11
Pamoja na jina
lake kuitwa huzuni, Yabesi alipomjua Mungu alikataa kuitwa huzuni, akakataa
maisha ya huzuni. Ndani mwa Maombi haya ya Kufungua Milango na Malango ni
lazima tukatae malango yote yaliyotupwa juu yetu au tumezaliwa nayo, maana katika ukiri wa Imani mna nguvu ya
kufungua Milango na Malango.
Tunajifunza kwa AYUBU; Pamoja na
mateso ya zaidi ya miaka kumi na saba (miaka 17), Kuugua, Kufilisika na Misiba,
lakini bado mtumishi huyu wa Mungu alikataa
kutamka kinyume cha Imani yake katika Mungu. Katika mambo yote Ayubu
hakufanya dhambi wala kumuwazia Mungu kwa upumbavu. “Lakini mimi najua ya kuwa
Mteteaji wangu yu hai, Na yakuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi. Lakini,
pasipokua na mwili wangu nitamuona Mungu; Nami nitamuona mimi nafsi yangu, Na
macho yangu yatamtazama, wala si mwingine, Mtima wangu unazimia ndani yangu.”
Ayubu 19:25-27
Haya maneno
yalifungua Mlango na Milango ya Ayubu tena akainuliwa toka kwenye shimo la uharibifu. Baada ya hayo yote, BWANA aligeuza uteka wa
Ayubu.
“Basi huyo BWANA akaubarikia mwisho wa Ayubu
zaidi ya mwanzo wake, naye alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia efu
sita, na jozi za ng’ombe elfu, na punda wake elfu. Tena alikuwa na wana waume
saba, binti watatu. Akamwita huyo wa kwanza jina lake Yemima; na wa pili
akamwita jina lake Kesia; na wa tatu akamwita jina lake Keren-hapuhu. Katika
nchi hiyo yote hawakuwapo wanawake waliokuwa wazuri kama hao wa Ayubu; na baba
yao akawapa urithi kati ya ndugu zao wana waume. Kisha baada ya mambo hayo Ayubu
akaishi miaka mia na arobaini, nae akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hata
vizazi vinne. Basi Ayubu akafa, mzee sana mwenye kujawa na siku.” Ayubu 42:12-16
Ayubu alikataa Kukiri udhaifu, Kukiri misiba, Kukiri mateso
japo alikua kwenye mateso. Alisema, nalitoka tumboni kwa mama yangu ni uchi
nitarudi nikiwa uchi. Maandiko matakatifu yanasema; “Maana mwenye kuangalia upepo
hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna. Kama vile wewe usipojua njia ya
upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadharika
huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.” Muhubiri 11:4-5
Kwa imani
katika Kristo Yesu yatupasa kukataa yaliyokinyume na imani na tukiri yakuwa
anaweza kufanya mambo yote; Aweza
Kufungua Milango na Malango yaliyofungwa. Bwana Yesu Kristo anamtumia mtu aliye
tayari kutumika na si vinginevyo. Acha kujiua kwa maneno ya kinywa chako. Maana
yeye Kristo Yesu ni mwaminifu. Vaa na ujifunge SILAHA yako itakusaidia. “Basi
atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au
tuyawazayo kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.” Waebrania 3:20
Labels:
EAGT City Center,
malango,
Maombi,
milango,
Rev Florian Katunzi
Monday, December 19, 2016
MAOMBI YA KUFUNGUA MALANGO NA MILANGO - SEHEMU YA 6
AINA TANO ZA FUNGUO ZA KUFUNGUA MALANGO NA MILANGO
Na Mchungaji Florian Katunzi - EAGT City Center
UFUNGUO WA TANO
NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU
Neno
“Nguvu” kwa lugha ya Kigiriki ni (dunamis) ina maana ya zaidi ya Nguvu au Uwezo
wa kawaida. “Inaashiria hasa nguvu iliyo katika utendaji wa ki-Mungu, hii ni
nguvu zaidi ya nguvu.
(Dunamis
is not just any power; it is miraculous power or marvelous works. Dunamis can also
refer to “Moral power and excellence of soul according to the Greek lexicon).
Nguvu ya Roho mtakatifu inajumuisha mamlaka ya kutoa pepo wachafu na upako wa
kuponya magonjwa. Roho mtakatifu ndiye ufunguo wa kumshinda adui shetani na
kazi zake. Roho mtakatifu ni zaidi ya nguvu ama uweza. Katika maandiko
matakatifu, Yesu kristo alionyesha unafsi wa Roho mtakatifu kwa kumwongelea
kama nafsi ambapo alisema; “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli
yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia
atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.” Yohana 16:13
Kimsimgi
tunajifunza kwa Yesu Kristo kabla ya kuanza huduma yake hapa ulimwenguni,
alipokwisha kubatizwa na Yohana mbatizaji, wakati anaomba mbingu zilifunguka
Roho mtakatifu akashuka juu yake kwa Nguvu tangia hapo maandiko matakatifu
yanathibitisha “Ikawa watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye
anaomba, mbingu zilifunuka; Roho mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa
kiwiliwili, kama hua, sauti ikatoka mbinguni wewe ndiye mwanangu mpendwa wangu
ninyependezwa nawe.” Luka 3:21-22
Tunajifunza
katika maandiko haya yakuwa Nguvu ya Roho mtakatifu haishuki kwa mtu hivihivi
mpaka awe anaomba. Lakini wako wakristo wengi wanaotaka kujazwa Roho mtakatifu
wakati hawana maombi katika maisha yao. Maombi ufungua mbingu zimfungukie
mwombaji. Baada ya Yesu kristo kujazwa Roho mtakatifu, maandiko matakatifu
yanashuhudia wazi yakuwa aliongozwa na Roho muda wa siku arobaini katika maombi.
“Naye
Yesu, hali amejaa Roho mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho
muda wa siku arobaini nyikani.”
Luka 4:1
Pia
yunajifunza ili milango na malago ya ukombozi wa mwanadamu yapate kufunguliwa
ilibidi Roho mtakatifu ashuke kwa nguvu na uweza mkuu ili kumfunika mwanamwali
bikra apate uwezo wa kubeba mimba pasipo kukutana na mwanamume kwa jinsi ya
kibinadamu.
“Mwezi
wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina
lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake
Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. Akaingia
nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. Naye
akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna
gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yesu.
Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha
enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme
wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili,
maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, ROHO MTAKATIFU ATAKUJILIA JUU
YAKO, na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu ya hicho
kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, mwana wa Mungu.”
Roho
mtakatifu akishuka kwetu huja na nguvu zake aliye juu katika Uwezo na nguvu za
Roho Mtakatifu, tunavishwa uwezo wa kuangusha ngome zote zilizofunga Malango na
Milango yetu ya Baraka za kiroho na kimwili, ndiyo maana Bwana Yesu kristo
alisema, Mtapokea nguvu akisha kuwajilia Roho Mtakatifu. Mkristo nguvu yako
haimo katika vitu vya upako kama vile; mafuta ya upako, maji ya upako, sabuni
za upako, chumvi ya upako, kitambaa cha upako, udongo wa upako, kiganja cha
nabii wa upako nambo yafananayo na hayo yanayoibuliwa kila kukicha katika ibada
zilizotungwa kwa akili za binadamu. Ndugu mpendwa katika kristo yachunguzeni
maandiko vema; mpate kuijua kweli inayoweza kuwawekeni huru mbali na mateso.
Tukiwa na msimamo thabiti wa kiimani yatupasa kuliamini Neno la Mungu sio
maneno ya watu, watawaijieni kwa mfano wa wanakondoo lakini ndani ni mbwa mwitu
wakali. Maagizo ya Yesu Kristo aliye mwanzilishi wa huduma hii iliyokubwa na bora
anasema; “Lakini mtapokea nguvu, akiisha
kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika
Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” Matendo
1:8
Yesu
kristo aliwaambia wanafunzi wake msitoke Yerusalemu bali mwingojee nguvu ya
Roho mtakatifu, ambayo kwa hiyo watatenda kazi ya kufungua waliofungwa. Maana
pasipo huyo Roho mtakatifu hakuna atakayeweza. Tunaona akina Petro na Yohana
baada ya kupokea Nguvu ya Roho mtakatifu waliweza kunena habari za Kristo Yesu
na ufalme wake kwa ujasiri na nguvu. Hata wengi walistaajabu walipoona ujasiri
wao. “Ndipo Petro akijaa Roho mtakatifu, akawaambia, enyi wakubwa wa watu na
wazee wa Israeli … wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana
hapana jina jingine katika mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa
kwalo. Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na wakajua ya kuwa ni watu
wasio na elimu, wasio na maarifa wakastaajabu wakatambua ya kwamba walikuwa
pamoja na Yesu.” Mdo 4:8-13
Kwa
hiyo Roho mtakatifu akiwa kwa mtu hujidhihirisha kwa madhihiriho ya ishara,
miujiza na maajabu ambayo huwastaajabisha wengi wayaonapo. Roho mtakatifu
uhuisha nafsi zetu na miili yetu toka kwenye mafungo ya giza kwa kutufungulia
malango na milango. Tunajifunza kwa Lazaro alipougua, akafa, akazikwa kwa muda
wa siku nne alikuwamo kaburini lakini kwa nguvu za Roho mtakatifu Yesu alipaza
sauti yake akamwita Lazaro toka kwa wafu akawa hai tena. Hata sasa Roho
mtakatifu bado anatenda kazi kwa wote waaminio maana tukimwita katika Kristo
Yesu ushuka kuokoa na kuponya wengi. Hata kama lipo kaburi limefunga maisha
yako ya kiroho na kimwili kwa uweza na nguvu za Roho mtakatifu sharti
ufunguliwe. (Through Power of Holy Ghost we Force out evil spirit). Maandiko
yanasema katika injili ya Yohana; “Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa
Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake. Ndie Mariamu yule
aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye
alikuwa hawezi. Basi wale waumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye
umpendaye hawezi. Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali
ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo. Naye
Yesu alim,penda Martha na umbu lake na Lazaro. Basi aliposikia ya kwamba
hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo. Kisha, baada ya hayo,
akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena. Wale wanafunzi wakamwambia,
Rabi, juzi juzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe
unakwenda huko tena? Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu
akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu. Bali akienda
usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake. Aliyasema hayo; kisha baada
ya hayo, akawaambia, Rafiki yrtu, Lazaro amelala, lakini ninakwenda nipate
kumwamsha. Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona.
Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena
habari ya kulala usingizi. Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa.
Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini; lakini na
twendeni kwake. Basi Tomaso, aitwaye pacha, akawaambia wanafunzi wenziwe,
twendeni na sisi, ili tufe pamoja naye. Basi
Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne. Na Bethania
ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadri ya maili mbili hivi, na watu wengi katika
Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya
ndugu yao. Basi Martha aliposikia kwamba yesu anakuja, alikwenda kumlaki, na
mariamu alikuwa akikaa nyumbani. Basi Martha akamwambia Yesu, bwana, kama
ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Lakini hata sasa najua ya kuwa yo
yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa. Yesu akamwambia, ndugu yako atafufuka.
Martha akamwambia, najua yakuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. Yesu
akamwambia, mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa,
atakuwa anaishi, naye kila aishie na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je!
Unayasadiki hayo? Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe
Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimmwenguni. Naye alipokwisha kusema hayo,
alikwenda zake, akamwita umbu lake Mariamu faraghani, akasema, Mwalimu yupo
anakuita. Naye aliposikia aliondoka upesi, akamwendea. Na Yesu alikuwa hajafika
ndani ya kijiji, lakini alikuwa akalipo palepale alipomlaki Martha. Basi wale
Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wamfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka
upesi na kutoka, walimfuata, huku wakidhani ya kuwa wanakwenda kaburini ili
alie huko. Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka
miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu
hangalikufa. Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye
wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, akasema, Mmemweka wapi?
Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. Yesu akalia machozi. Basi Wayahudi wakasema,
angalieni jinsi alivyompenda. Bali wengine wao wakasema, je! Huyu aliyemfumbua
macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife? Basi Yesu, hali akiugua
tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe
limewekwa juu yake. Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki,
akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. Yesu akamwambia,
Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? Basi wakaliondoa
lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, baba, nakushukuru kwakuwa
umenisikia. Name nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya
mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kukusadiki kwamba ndiwe
uliyenituma. Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku
nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso
wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.” Yohana 11:1-44
Roho
mtakatifu huleta uzima badala ya mauti; akatoka nje maana yake, akahuwishwa
Lazaro toka kwa wafu japo alikuwa amekufa na ameoza. Ijapokuwa alikuwa ananuka,
nguvu ya Roho Mtakatifu iliposhuka juu yake aliyekuwa katika hali ya kufa
ikamwinua Lazaro toka kwa wafu akawa hai tena. Ni vema kila mmoja aliyeamini
kutambua kuwa Roho mtakatifu ni Ufunguo unaotoa nafsi nyingi katika mafungo ya
giza. Kwa nguvu za Roho mtakatifu hata kazi zetu za kimwili zaweza kuhuishwa
inaweza kuwa Biashara, Kazi, Elimu vyote vilivyozikwa na kufishwa kuwa hai
tena. Kama BWANA alivyonena kwa kinywa cha nabii Ezekieli na kusema; “Nanyi
mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa
ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu. Nami nitatia roho yangu ndani
yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya kuwa
mimi, BWANA, nimesema hayo, na kuyatimiza, asema BWANA.” Ezekieli
37:13-14
Kwa
nguvu za Roho mtakatifu sharti malango na milango vifunguliwe ndani mwa maombi
sio nje ya maombi kwa kuwa tunapomlilia Mungu na kumwita, yeye hushuka na
kutufungua mafungo yetu yote. “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa
nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama pazia la hekalu likapasuka vipande viwili
toka juu hata chini, nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka, makaburi yakafunuka;
ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala, nao wakiisha kutoka makaburini
mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.”
Mathayo 27:50-57
Nchi
ilitetemeka
Wakuu
wa anga lazima watetemeke maana Roho Mtakatifu ni nguvu iliyo juu ya yote
lazima Wakuu wa nchi washushwe, Wakuu wa giza washushwe, Wakuu wa majini
washushwe katika viti vyao kwani Kila goti lazima lipigwe mbele ya Kristo Yesu
Mwokozi.
Miamba
ilipasuka
Wako
watu wamefungwa nafsi zao katika miamba na majabali mazito, lazima ipasuke ili
wote waachiliwe waliofungwa vifungo kwenye miamba kupitia nguvu ya Roho
mtakatifu.
Makaburi
yakafunuliwa
Kaburi
ni kifuniko kibaya sana kinachotesa wengi. Wengi wanafunikwa makaburini kupitia
makafara ya tambiko. Kwa nguvu za Roho Mtakatifu miili mingi ya watakatifu
waliofungwa na nguvu ya kaburi watainuka.
Kama
pazia la hekalu lilivyopasuka, ndivyo kila kizuizi kilichowekwa katika maisha
yako ya kiroho na kimwili kitapasuka toka juu mpaka chini. Huu ndio ulikuwa
mwisho wa Agano la kale na kuwa mwanzo wa Agano jipya. Katika Kristo Yesu
yakale sasa yamepita tazama yamekuwa mapya. Katika ulimwengu wa Roho watu wengi
wamefungwa na mapazia ya mabibi na mababu zao, mapazia ya kiganga na kichawi,
mapazia ya mizimu na matambiko, lazima tuwafungue watu wa Mungu mapazia hayo
ndani mwa maombi haya ya kufungua milango na malango. Yesu akasema mfungueni
sanda mwache aende zake. Ikiwa na maana Lazaro alipofufuka alitoka kaburini
akiwa amevaa sanda (vazi la wafu) ndiyo maana Kristo Yesu aliagiza avuliwe hilo
vazi yaani sanda ndipo aachwe huru aende zake. Hapa tunapata siri nzito ya
kiroho ya kuwa wako wakristo wengi waliookolewa toka katika mafungo ya giza
lakini hawajahamishwa na kuingizwa katika ufalme wa mwana wa pendo lake. Ni jukumu
letu watumishi wa Mungu kufanya maombi na maombezi ya kuwafungua watu baada ya
kuamini. Maana KWELI ya Mungu kupitia Neno ndiyo inayomuweka mtu huru mbali na
mateso. Ni muhimu sana tukafundisha na kuombea sawasawa na Neno la Mungu. Maana
wako wanaodhania ya kuwa baada ya kuokoka vita vyao vimeisha kumbe wokovu ndio
mwanzo wa vita vya kiroho na kimwili. Kwa mantiki hiyo ndiyo maana Bwana Yesu
akawaambia wanafunzi wake; “Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni,
roho i radhi ila mwili ni dhaifu.”
Marko 14:38
Hata
wana wa Israaeli walipokwisha kuokolewa toka utumwani Misri kwa nguvu na uweza
mkuu, tunajifunza kwao jinsi walivyokutana na vipingamizi ambavyo viliwafanya
wamlilie Mungu na kupigana vita. Walipigana kiroho, wakapigana kimwili. Mfano
halisi ni vita vyao na Waamaleki “Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana
na Israeli huko Refidimu. Musa akamwambia Yoshua, tuchagulie watu, ukatoke
upigane upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo
ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua akafanya kama Musa
alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya
kile kilima. Ikawa, Musa alipoinua mkono wake, Israeli waliposhinda; na
aliposhusha mkono wake, Amaleki walishinda. Lakini mikono ya Musa ilikuwa
mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri
wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake
ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake
kwa ukali wa upanga. BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe
ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa
Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. Musa akajenga madhabahu, akaiita
jina lake Yehova-nisi; akasema, BWANA ameapa; BWANA atakuwa na vita na Amaleki
kizazi baada ya kizazi.” Kutoka
17:8-16
Wanadamu
kwa jinsi ya ubinadamu wao wanaweza kufanya jitihada zao za kiganga na kichawi
au za kawaida katika mwili wakakuwekea vipingamizi ili wewe mtu wa Mungu
usiinuke. Lakini katika nguvu za Roho mtakatifu tutashinda na zaidi ya
kushinda. Angalia mfano, Yesu Kristo walijaribu kumzuia asifufuke toka
kaburini kwa kulilinda kaburi kwa kutumia askari wenye silaha na kuweka jiwe
kubwa juu ya kaburi. “Hata siku ya pili, ndiyo iliyo baada ya
Maandalio, wakuu wa makuhani, na Mafarisayo wakamkusanyikia Pilato, wakasema,
Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa akali hai, Baada ya
siku tatu nitafufuka. Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya
tatu; wasije wanafunzi wake wakamiba, na kuwaambia watu, amefufuka katika wafu,
na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza. Pilato akaawaambia, mna askari,
nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyo. Wakaenda, wakalilinnda kaburi salama,
kwa kulitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi.” Mathayo
27:62-66
Lakini
ilipofika saa ya Roho mtakatifu kudhihirisha nguvu zake, walinzi pamoja na
silaha zao walikuwa kama wafu. Maandiko yanathibitisha; “Hata sabato ilipokwisha,
ikapambazuka siku ya kwanza ya juma, mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa
pili, walikwenda kulitazama kaburi. Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la
nchi, kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja
akaliviringisha lile jiwe akalikalia. Na sura yake ilikuwa kama umeme na mavazi
yake meupe kama theluji. Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa
kama wafu. Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi, kwa maana
najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa. Hayupo hapa, kwani amefufuka kama
alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa. Nanyi nendeni upesi, mkawaambie
wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda galilaya;
ndiko mtakakomwona. Haya nimekwisha waambia.” Mathayo 28:1-7
Roho
Mtakatifu ni Nguvu ya Mungu na ni Pumzi ya Mungu yenye kuleta uhai tena. Kama
Kristo alihamishwa toka kwa wafu nasi tutahamishwa kiroho na kimwili kwa nguvu
za Roho Mtakatifu.
ROHO MTAKATIFU UFUNGUA VIFUNGO VYA
UTASA;
Kwa
nguvu za Roho Mtakatifu na uweza wake Sara alipokea uwezo wa kuwa na
mimba alipokuwa amepita wakati wake. Milango na malango ya utasa yaliyomfunga
Sara muda wa miaka wa ishirini na mitano, kwa imani ilifunguliwa.
“Kwa
imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita
wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.” Waebrania 11:11
Hata
sasa kwa uwezo wa nguvu za Roho
Mtakatifu, wako wakristo wengi watafunguliwa ndani mwa maombi ya kufungua
milango na malango ya UTASA yasiwafunge tena maana yeye aliyeahidi ni
mwaminifu na kusema, hatakuwepo mwenye kuharibu mimba wala aliye tasa katikati
yetu.
Roho
Mtakatifu akufunike kama kivuli wewe uliyekuwa umefunikwa na roho chafu za
mashetani. Roho Mtakatifu na nguvu zake zikufunike kama kivuli, ili Vuli la
uchawi na uganga litoke kwako. Kwa nguvu za Roho mtakatifu tumevishwa uweza na
Kristo Yesu wa kufungua na kufunga na tutakachokifungua kitafunguliwa katika
Mungu aliye hai. Na tutakachokifunga kitafungwa katika Mungu aliye hai. Maana
maandiko yanasema;
“Na ufungua wa nyumba ya Daudi nitauweka
begani mwake; yeye atafungua wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala
hapana atakayefungua.” Isaya 22:22
Nguvu
zake Roho mtakatifu zitakapokufunika, Utatenda makuu kwa uwezo wake. Katika
yeye Roho Mtakatifu, Wagonjwa wanapokea uponyaji, wanaosumbuliwa na nguvu za
mapepo wanawekwa huru mbali na mateso, walioshushwa chini na kudharauliwa
wanainuliwa tena. “Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na
kuponya maradhi.” Luka 9:1
Ni
lazima tuhamishwe kwa Maombi yenye Imani. Usikubali kuteswa na kugandamizwa,
Mtwike Yesu fadhaha zako, mizigo yako, taabu zako, vilio vyako naye atakuhamisha tu. Bwana atazitangua ishara zao wachawi na
waganga, Maana kwa nguvu za Roho Mtakatifu hakuna uchawi wala uganga kusimama
mbele yako tena. BWANA wa majeshi anasema; “Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala
hapana uganga juu ya Israeli.” Hesabu 23:23
Ushuhuda wa dada mmoja
Dada
mmoja toka pale Kilimanjaro; alinijia akiwa na mateso ya magonjwa yaliyomkumba
alipopigwa na upepo njia panda akiwa anakwenda dukani pale kijijini kwao. Baada
ya kupigwa na upepo alianguka na kuzimia, alipozinduka alijikuta yuko hospitali
akiwa amelazwa. Baada ya miaka miwili kupita tangu apigwe na upepo wa ajabu,
ndipo alipokuja kwenye Ibada ya Maombezi ya kufungua Milango na Malango. Ndipo
nilipomwombea kwa kuziita nguvu za Roho mtakatifu zenye kung’oa kila aina
ya mapando yaliyopandikizwa kwa watu wa
Mungu. Hapa tunaona wachawi wanatumia upepo kumloga na kumwingia dada huyu.
BWANA anatuma nguvu ya Roho mtakatifu katika kanisa la kwanza kama uvumi wa
upepo. Maandiko yanathibitisha kwamba; “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste
walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa
upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja
wao.” Matendo ya Mitume 2:1-4
Upepo
wa kichawi na kiganga uliokuwa unamtesa huyu dada ulimalizwa nguvu zake na
kubatilishwa kwa Nguvu za Upepo wa Roho Mtakatifu, nikatengua kila aina ya
upepo mchafu ulio mpitia kwa jina la Yesu Kristo.
Labels:
EAGT City Center,
malango,
Maombi,
milango,
Rev Florian Katunzi
Monday, December 12, 2016
MAOMBI YA KUFUNGUA MALANGO NA MILANGO - SEHEMU YA 5
Na Mchungaji Florian Katunzi - EAGT City Center
Bwana asifiwe mtu wa Mungu. Bado tunaendelea na mfululizo wa somo hili ambapo katika matoleo yaliyopita nilikufundisha juu ya funguo tatu na nikakwambia faida na namna ya kuzitumia. Na leo tunaendela na ufunguo wa nne …
Bwana asifiwe mtu wa Mungu. Bado tunaendelea na mfululizo wa somo hili ambapo katika matoleo yaliyopita nilikufundisha juu ya funguo tatu na nikakwambia faida na namna ya kuzitumia. Na leo tunaendela na ufunguo wa nne …
Endelea….
UFUNGUO WA NNE
MAOMBI
Maombi: maana yake ni kusemezana na MUNGU au kutafuta
uso wa BWANA; katika hali ya unyenyekevu na kicho “Toka mbinguni BWANA
aliwachungulia wanadamu, AONE KAMA YUKO MTU mwenye akili, Amtafutaye Mungu.” Zaburi
13:2
Katika
kipengele hiki tunakwenda kujifunza maombi kama ufunguo wa kufungua milango na
malango yaliyofungwa.
“BWANA akamtokea Sulemani usiku, akamwambia, Nimesikia uliyoyaomba, na
mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya dhabihu. Nikizifunga mbingu isiwe
mvua, tena nikamuru nzige kula nchi, na nikiwapelekea watu wangu tauni; ilkiwa
watu wangu walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na
kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi nitasikia toka mbinguni, na
kuwasamehe dhambi yao, na kuponya nchi yao. Sasa macho yangu yatafumbuka, na
masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. Maana sasa
nimeichagua nyumba hii na kuitakasa ili kwamba jina langu lipate kuwako huko
milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima.” 2Mambo ya
Nyakati 7:12-16
Tunajifunza kwa
mfalme Sulemani jinsi alivyo jinyenyekeza na kusimama madhabahuni pa BWANA
ikiwa ni ishara iliyowazi ya kuwa BWANA ndiye mfalme wa wafalme astahiliye
kuabudiwa na kutukuzwa. Hivyo tunajifunza mambo manne yafuatayo:-
(1) “Ikiwa watu wangu watajinyenyekesha” watu
wa Mungu lazima watambue ushindi wao dhidi ya malango ya giza unapatikana ndani
mwa maombi sio nje ya maombi. Mtu akijinyenyekesha sawasawa na Neno la Mungu
hakika atashinda na zaidi ya kushinda. “…
Ikawa, Musa alipoinua mkono wake, Israeli walishinda; na aliposhusha mkono wake
Amaleki walishinda. Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe,
wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake,
mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua
lilipokuchwa Yoshua akaangamiza amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga…” Kutoka
17:8-16
Kwa kuinua
mikono yake kwa BWANA Musa anaonyesha wazi jinsi anavyomtumaini na kumwamini
Mungu. Waamaleki walipotokea kupigana na Israeli lengo lao ni kuwazuia wasipite
walifunga malango na milango kwa njia ya kuanzisha vita. Nguvu ya ushindi ya
Israeli ilitegemea kudumu katika Maombi, Imani na utii kwa Mungu. Wakati maombi
ya Musa yalipokoma (aliposhusha mikono) mtililiko wa nguvu za Mungu ulikoma kwa
watu wa Mungu. Hii ikiwa dhahiri kwamba tunapoomba nguvu ya Mungu hushuka na
kinyume chake tusipoomba hakuna nguvu ya Mungu inayoshuka.
Pia tunajifunza
ya kwamba Baraka za Mungu na Ulinzi wa Mungu havishuki hivhivi kwetu mpaka tuvishushe
kwa njia ya Maombi. “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtaona; bisheni, nanyi
mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea naye atafutaye huona naye abishaye
atafunguliwa.” Mathayo 7:7-8
(2) “Na Kuomba” maana yake, watu wa Mungu lazima
waombe kwake bila kukoma kwa ajili ya kupata rehema na neema zitokazo kwa Mungu
na lazima wamtegemee moja kwa moja na kumwamini yeye aingilie kati. Bwana Yesu
Kristo anasema; “…imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tamaa.”
Luka 18:1-
Katika maisha
ya imani yako mapito mbalimbali yenye magumu, vita, dhiki, njaa, magonjwa na
adha mbalimbali ambazo mtu wa Mungu anakabiliana nazo (changamoto za maisha).
Pamoja na changamoto zote hizi hatukati tamaa bali tunatiwa nguvu katika yeye
Kristo Yesu. Maandiko matakatifu yanasema “Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu
wa n je unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana
dhiki yetu nyepesi iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele
uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana bali visivyoonekana. Kwa
maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.”
2Wakorintho 4:16-18
(3) “Kutafuta uso wa Mungu” Watu wa Mungu
ni lazima wamrudie Mungu kwa bidii na kwa moyo wote na kutamani uwepo wake na
sio tu kujaribu kukimbia shida ndipo milango yao na malango yao
yatakapofunguliwa siku zote za maisha yao. Katika maisha ya huduma ya Yesu
Kristo hapa duniani aliutumia ufunguo huu wa kuutafuta uso wa Mungu aliye hai
na maombi yake yalisikiwa na uweza wa Mungu ulikuwa ukimtoka na kuponya watu.
Alianza kwa maombi (Luka 4:1-14), akadumu katika maombi (Luka 6:12-19) na kumalizia katika maombi (Luka
22:39-46). Tofauti sana na maisha ya
wakristo walio wengi ambao huomba wakati wa shida na majaribu. “Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea
yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia
sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; na ingawa ni
mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokwisha
kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu ya milele kwa watu wote wanao mtii; kisha ametajwa na Mungu kuwa
kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki” Waebrania 5:7-10
(4) “Kuziacha njia zao mbaya” Watu wa Mungu
ni lazima watubu kwa kweli ya Mungu na kuziacha njia zao mbaya ndipo maombi yao
na dua zao zitasikiwa. Bwana Yesu Kristo alisema “… amin, amin, nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
Wala mtumwa hakai nyumbani siku zote; mwana hukaa siku zote. Basi mwana
akiwaweka huru mtakuwa huru kwelikweli.” Yohana 8:34-36
Hivyo BWANA
anataka kabla ya mambo yote katika maisha yetu tufanye maombi kwa sababu ndiyo
ufunguo unaofungua njia. Pasipo kufungua milango na malango kwanza hatuwezi
kupenya kiroho na kimwili. Tukisoma maandiko matakatifu yanaonyesha dhahiri
hakuna mtu wa Mungu aliye shinda pasipo maombi tangu baba zetu wa imani mpaka
manabii walishika sana ufunguo huu wa maombi. “Basi, kabla ya mambo yote, nataka
dua, na sala, na maombezi, na shukurani, zifanyike kwa ajili yua watu wote; kwa
ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na imani,
katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu
Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.
Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja,
Mwanadamu Kristo Yesu; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya
wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake.” 1Timotheo 2:1-6
Haya ni Maombi
yenye kujengwa katika Msingi wa Neno la Mungu,
Imani itokanayo
na Neno la Mungu. Mwombaji ni lazima Aombe sawa sawa na Neno la Mungu.
Yesu baada ya
kubatizwa kabla ya Huduma alianza kwa Maombi, ambayo yalifanya mbingu
zimfungukie. Kwa mantiki hiyo tunajifunza yakuwa Maombi ufungua malango na
milango ya mbingu. Tunaona mfano wa Kristo Yesu kama kielelezo;
“Ikawa, watu
wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu
zilifunuka; Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua,
sauti ikitoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu, nimependezwa nawe.”
Luka 3:21-22
Katika maisha
yetu ya ukristo tukitaka kufungua milango na malango kwa ajili yetu wenyewe,
kwa ajili ya watoto wetu, kwa ajili ya mali zetu sharti tutumie kwa bidii
ufunguo huu wa Maombi, sawasawa na ushahidi wa Neno la Mungu lilivyonenwa kwa
kinywa cha mtumishi wa Mungu Ezra alipokuwa anaongoza watu wa Mungu toka
uahamishoni Babeli kwenda kujenga na kufungua milango na malango ya Yerusalemu.
pamoja na kuwa na kilakitu cha kujengea kama vile dhahabu, fedha na vitu vingi
vya thamani. Ezra hakuvitegemea hivyo bali aliutegemea mkono wa BWANA ulio
hodari ndio maana aliitisha mbiu ya kufunga na kuomba ili kujitafutia njia iliyonyooka
itokayo kwa Mungu kabla ya kuanza safari. “Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto
Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia
iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa
mali yetu yote. Maana naliona haya kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapanda
farasi, ili kutusaidia juu ya adui njiani, kwa maana tulikuwa tumesema na
mfalme, tukinena, Mkono wa Mungu u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea
mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni kinyume cha wote wamwachao. Basi
tukafunga, tukamsihi Mungu wetu kwa ajili ya hayo; naye akatutakabali.” Ezra
8:21-23
Yako mema toka
kwa Mungu aliye hai kwa Mwombaji. MBINGU ZIKIFUNGUKA ndani mwa Maombi, Magonjwa
yataondoka katika miili ya watu, Maana Maombi hushusha Uweza wa Ki-Mungu wenye
nguvu ya kufungua Mafungo yote. Yesu Kristo baada ya Kuomba, Mbingu
zilifunguka, kilichotokea ni Udhihirisho wa nguvu za Ki-Mungu zenye kuponya
watu.
“Lakini yeye
alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba. Ikawa siku zile
mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa
wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Uyahudi, na
Yerusalemu, na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya.” Luka 5:16-17
UWEZA WA BWANA
ndio unaofungua Malango na Milango kwa Mwombaji. Pasipo Maombi hakuna kitakacho
tendeka katika maisha ya mkristo anaye mtegemea Mungu. “Ikwa siku zile aliondoka akaenda
mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. Hata kulipokuwa
mchana aliwaita wanafunzi wake, akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao
aliwaita mitume, Simoni, aliyemwita jina pili, Petro na Andrea nduguye, na
Yakobo na Yohana, na Filipo na Bartolomayo, na Mathayo na Tomaso, na Yakobo wa
Alfayo, na Simon aitwaye Zelote, na Yuda wa Yakobo, na Yuda Iskariote, ndiye
aliyekuwa msaliti. Akashuka pamoja nao, akasimama mahali tambarare, pamoja na
wanafunzi wake wengi, na makutano makubwa ya watu waliotoka Uyahudi wote na
Yerusalemuu, na Pwani ya Tiro na Sidoni, waliokuja kumsikiliza na kuponywa
magonjwa yao na wale waliosumbuliwa na pepo wachafu waliponywa. Na makutano
yote walikuwa wakita kumgusa, kwa sababu uweza
ulikuwa ukimtoka ukiwaponya wote.” Luka
6:12-19
Yesu Kristo,
anafanya Maombi usiku kucha maana yake anakesha katika Maombi. Matokeo yake ni
Udhihirisho wa nguvu na uweza wa ki-Mungu unashuka kwa watu na kuwaponya. Ndani
mwa maombi ndimo tunamovishwa Uweza na Nguvu za ki-Mungu aliye hai zenye
kuangusha malango na ngome za kuzimu.
Yesu Kristo alikuwa na uwezo katika Kutenda na Kunena, lile Neno
alilolisema kwa watu liliambatana na Uwezo na Nguvu.
Maana wako watumishi wengi wa Mungu ambao wananena tu lakini neno lao halina
nguvu matokeo yake kondoo wa BWANA wanaingia na mizigo yao kwenye ibada na
wanatoka na mizigo yao. Kukosa funguo za ufalme wa Mungu ni jambo la hatari kwa
mtumishi wa Mungu.
Unapomwendea
Mungu sharti ujue unasimamia Neno gani la Mungu, maana Mungu hulituma Neno na
ndani yake ndimo ulimo Uzima. Katika maisha yetu ya wokovu tunaweza kukutana na
watu wengi wenye wivu na nia ovu, kama hawa makuhani wa kisadukayo kwa wivu wao
waliwakamata mitume wakawatupa gerezani lakini kwa mkono wa BWANA wenye nguvu
alituma malaika wake akawafungua mafungo yao;
sawasawa na Neno la Mungu. Toka kitabu cha Matendo ya Mitume 5:18-20
Neno linasema; “Wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza, lakini malaika wa
Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema, Enendeni mkasimame
hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu.”
Hapa
tunajifunza ya kuwa hatuko peke yetu katika mapito yetu yuko asiyeshindwa.
Wajapofunga magereza yao, wajapofunga ndoa zetu, wajapofunga watoto wetu
wasiolewe, wajapofunga uchumi wetu yatupasa tumwite Mungu aliye hai naye hakika
atatufungua maana kwa msaada wa BWANA tutatenda makuu, na maadui zetu
tutawakanyaga kwa nguvu zake. Japo gereza liliendelea kulindwa na walinzi na
malango yake na milango yake kufungwa BWANA aliposhuka ndani ya gereza
alifanyika mlango wa kutokea. “Hata watumishi walipofika hawakuwaona
gerezani, wakarudi wakatoa habari, wakisema, gereza tumeikuta imefungwa salama,
nao walinzi wamesimama mbele ya mlango; lakini tulipoufungua hatukukuta mtu
ndani.” Matendo 5:22-23
Kila kilicho
kamatwa kikawekwa ndani ya Gereza la Kiganga na Kichawi, gereza la magonjwa,
gereza la nyumba ndogo, gereza la kuzaa kufa kufa na mapooza, gereza la kufeli
katika masomo/ kutokufaulu katika mitihani, gereza la uchumi, Lazima
VITAFUNGULIWA.
“Basi watu wote wakulao wataliwa, na adui zako wote watakwenda
kufungwa, kila mmoja wao, na hao walio kuteka nyara watatekwa, na wote
waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. Maana nitakurudishia afya, nami
nitakuponya jeraha zako, asema BWANA” Yeremia 30:16-17
BWANA
akufungulie Mlango na Milango sawa sawa na Kuomba kwako. Mungu analiangalia Neno
lake apate kulitimiza, hivyo Omba sawa sawa na Neno utapata jawabu lako.
Usiogope, Maana hutapatwa na aibu tena; Tunayo mamlaka ya kugeuza kila hali
sawasaw na Neno la Mungu alilonena kwa kinywa cha nabii Isaya na kusema; “Nimeziona
njia zake; nami nitamponya, nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye
na hao wanaomlilia.” Isaya 57:18
Maombi
yanafungua Malango na Milango ya Mbingu. Naye BWANA humwongoza daima mtu
Mwombaji na Kuishibisha nafsi yake mahali pasipokuwa na maji na kumtia nguvu.
Sawasawa na Neno la Mungu lililonenwa na kinywa cha nabii Isaya“Naye
BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na
kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama
chemchemi ambayo maji yake hayapungui.” Isaya 58:11
AYUBU aliomba Ustawi kwa ajili yake, kwa ajili ya watoto wake na mali
zake. Akatoa Sadaka za kuinuliwa mbele za Mungu aliye hai akiziambatanisha na
Maombi yake. Naye BWANA akamwitikia na kumstawisha katika hayo aliyoyaomba na
kuyatolea sadaka.
“Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao
zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na
mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa;
kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru
Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote. Ilikuwa, siku moja
ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye
akaenda kati yao. BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani
akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika
kutembea huku na huku humo. Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia
huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu
mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani
akamjibu BWANA, na kusema, je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure? Wewe hukumzingira
kwa UKINGO pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi
za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.” Ayubu 1:5-10
Katika fungu
hili la Neno la Mungu tunapata kielelezo cha mtu wa imani, mchaji wa Mungu,
mwelekevu na aliyejiepusha na uovu. Tunapata taswira ya maisha yake ya kiimani
jinsi alivyo yajenga katika msingi wa maombi, hata wakati wa mapito yake BWANA
aliendelea kuwa Ukingo kwake. Ndiyo maana alisema “Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, nay a kuwa hatimaye
atasimama juu ya nchi. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, lakini,
pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu; nami nitamwona mimi nafsi yangu, na
macho yangu yatamtazama wala si mwingine…” Ayubu 19:25-27
Ayubu alifanya
maombi maalumu kwa ajili ya watoto wake hakuwaacha wajiendeendee bali alisimama
kama kuhani wa familia yake, akawainua mbele za Mungu kwa maombi na sadaka.
Nasi katika maisha yetu tumepewa ukuhani usioondoka katika Kristo Yesu.
Yatupasa kusimama imara katika maombi kuyafungua malango na milango, kwa ajili
yetu sisi, watoto wetu na mali zetu. Kwa kuwa Mungu anamtafuta mtu miongoni
mwetu atakayesimama mbele zake mahali palipo bomoka na kujenga boma. “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao,
atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili
ya nchi nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.” Ezekieli 22:30
Labels:
EAGT City Center,
malango,
Maombi,
milango,
mlango,
Rev Florian Katunzi
Monday, December 5, 2016
MAOMBI YA KUFUNGUA MALANGO NA MILANGO - SEHEMU YA 4
Na Mchungaji Florian Katunzi - EAGT City Center
Mpendwa
msomaji bado naendelea na somo hili la maombi ya kufungua malango na milango,
ambalo pia utaweza jipatia nakala ya kitabu chako hivi punde.
Wiki
jana nilikugusia juu ya ufunguo wa pili wa kufungua milango na malango ambapo
nilikufundusha juu ya imani. Bado tunaendelea na aina hizi tano za funguo na
leo nitakufundisha juu ya ufunguo wa tatu…..Endelea.
UFUNGUO WA TATU;
TOBA
Toba
ni tendo la kiimani la kuungama dhambi na maovu yote yaliyokwisha kufanyika kwa
nia ya kujenga upya mahusiano na Mungu aliye hai sawasawa na Neno lake. Maana
dhambi ni uasi hivyo atendaye dhambi hujitenga na rehema za Mungu. “Afichaye
dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”
Mithali 28:13
Yako
malango na milango iliyofungwa kwa watu wa Mungu kwa sababu ya dhambi. Maana
wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Palipo dhambi na
makosa panahitaji toba si vinginevyo. Watu wengi wameruka ufunguo huu matokeo
yake wamefunga na kuomba hawakupata majibu kwa kuwa Mungu hadhihakiwi,
apandacho mtu ndicho atakacho vuna. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali
karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”
Warumi 6:23
Tunajifunza
kwa mtumishi wa Mungu Danieli baada ya kuvisoma vitabu vyenye maneno ya Mungu
alipata ufahamu utokanao na Neno, akaamini sawasawa na Neno la Mungu jambo la
tatu akachukua hatua ya kutubia maovu na dhambi zake na za Taifa lake. Ili kwa
njia ya toba BWANA awafungulie milango na malango yaliyokuwa yamefungwa kwa
nguvu za miungu ya Babeli.
“Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa
Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya
Wakaldayo; katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma
vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia
nabii, yaani, miaka sabini. Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka
kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.
Nikamwomba BWANA, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu,
mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri
zake; tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, kwa
kuyaacha maagizo yako na hukumu zako; wala hatukuwasikiliza watumishi wako,
manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba
zetu, na watu wote wa nchi. Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna
haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na
kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote
ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa. Ee Bwana, kwetu sisi kuna
haya ya uso, kwa wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, kwa sababu tumekutenda
dhambi. Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi, wala
hatukuitii sauti ya BWANA, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake,
alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii. Naam, Israeli
wote wameihalifu sheria yako, kwa kugeuka upande, wasiisikilize sauti yako;
basi kwa hiyo laana imemwagwa juu yetu, na uapo ule ulioandikwa katika sheria
ya Musa, mtumishi wa Mungu; kwa sababu tumemtenda dhambi. Na ye ameyathibitisha
maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuziwetu waliotuamua, kwa
kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama
hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu. Kama ilivyoandikwa katika sheria ya
Musa, mabaya haya yote yametupata lakini hata hivyo hatukumwomba BWANA, Mungu
wetu, atupe fadhili zake, ili tugeuke na kuyaacha maovu yetu, na kuitambua
kweli yake. Basi BWANA ameyavizia mabaya hayo, akatuletea; maana BWANA, Mungu
wetu ni mwenye haki katika kazi zake zote azitendazo; na sisi hatukuitii sauti
yake. Na sasa, Ee Bwana Mungu wetu, uliyewatoa watu wako hawa katika nchi ya
Misri kwa mkono hodari, ukajipatia sifa, kamailivyo leo; tumefanya dhambi,
tumetenda maovu. Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na
ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu;
maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu, Yerusalemu na watu wako
wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka. Basi sasa, Ee Mungu wetu,
yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya
patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana. Ee Mungu wangu, tega sikio
lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa
kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini
kwa sababu ya rehema zako nyingi. Ee Bwana, usikilize, ukatende, usikawie; kwa
ajili yako wewe, Ee Mungu wangu; kwa sababu ya mji wako na watu wako wanaitwa
kwa jina lako. Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi
yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za BWANA,
Mungu wangu, kwa ajili yam lima mtakatifu wa Mungu wangu; naam, nilipokuwa
nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo
kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.
Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe
akili upate kufahamu. Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja
kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na
kuyafahamu maono haya. Muda wa majuma sabini umuamuriwa juu ya watu wako, na
juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na
kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na akuleta haki ya milele, na kutia
muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu. Basi ujue na
kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu
hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba, na katika majuma
sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam,
katika nyakati za taabu. Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi
atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja
watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika , na
hata mmwisho ule vita vitakuwepo; ukiwa umekwisha kukusudiwa. Naye atafanya
agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo
ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu;
na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye
kuharibu.” Danieli 9:1-27
Danieli
anaanza kwa Kuungama ili apate kufungua Malango na Milango iliyofungwa.
Unapotubu
dhambi na kuziacha ni Mlango wa kuinuliwa, Hata kama umetupwa chini, Maandiko
yanasema wazi Mtu mwaminifu atakuwa na Baraka tele na Malango yake yatafunguliwa
daima.
“Haya
njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa
nyeupe kama theruji, zijapokuwa nyekundu kama bendera zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali
na kutii mtakula mema ya nchi, bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa
upanga maana kinywa cha BWANA kimenena haya.” Isaya
1:18-19
Angalia
pia watu wa Ninawi, walivyofungua Malango yao kwa nguvu ya TOBA, maana
Walilisikia Neno, Wakaliamini na Kutubu, Naye Yehova akawafungua. Walibatilisha
lango la mauti kwa njia ya toba. Hivyo toba ina nguvu katika Mungu hata
kuangusha ngome za mauti na kuzimu. Mfalme wa Ninawi aligeuza hasira ya Mungu
juu yake na watu wake pale alipoomba rehema za Mungu kwa njia ya toba. Nasi
tukiomba rehema kwa ajili yetu na watoto wetu hakika BWANA ni mwingi wa rehema
si mwepesi wa hasira, yeye husamehe wote wanao jinyenyekeza kwake.
“Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye
akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za
magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu akatangaza habari katika
mji wa Ninawi kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema mwanadamu asionje kitu,
wala mnyama wala makundi ya ng’ombe, wala makundi ya kondoo, wasile wala
wasinywe maji bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao
wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya,
na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na
kughairi na kuiacha hasira yake kali ili msiangamizwe? Mungu akaona matendo yao
ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akaghairi neno lile baya ambalo
alisema atawatenda, asilitende.” Yona
3:6-10
TOBA
ilirejesha upya uhai kwa watu wa Ninawi.
Nasi
Kanisa hatuwezi kufunguliwa Malango na Milango pasipo kufanya TOBA ya kweli.
“Tazama mkono wa BWANA haukupunguka, hata
usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu
yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake
msiuone, hata hataki kusikia.” Isaya
59:1-2
Lazima
uiondoe dhambi katikati yako kwa Kutubu na Kuungama mbele za Mungu. Ufunguo huo
wa TOBA ndio unaotupa Uwezo na Ujasiri wa kupaingia Patakatifu pake Mungu aliye
hai kwa jinsi ya Imani. Ni lazima MKRISTO UZAE MATUNDA YAPASAYO TOBA.
“Basi zaeni matunda yapasayo toba.” Mathayo 3:8”
Wokovu
maana yake ni Kutengwa mbali na dhambi.
Hatuwezi kufunguliwa Milango ya Baraka na Ustawi kama
hatutajitenga na maovu.
“Ndipo Yona akamwomba BWANA Mungu wake,
katika tumbo la yule samaki, akasema, Nalimlilia BWANA kwa sababu ya shida
yangu, naye akaniitikia; katika tumbo la kuzimu naliomba. Nawe ukaisikia sauti
yangu. Maana ulinitupa vilindini, ndani ya moyo wa bahari, gharika ya maji
ikanizunguka pande zote, Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu
yangu. Nami nikasema nimetupwa mbali na macho yako, lakini nitatazama tena
kukabili hekalu lako takatifu. Maji yalinizunguka hata nafsini mwangu, Vilindi
vilinizunguka, mwani ulikizinga kichwa
changu, Nalishuka hata pande za chini za milima, Huyo nchi na mapingo yake
yalinifunga hata milele. Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee
BWANA, Mungu wangu, Roho yangu ilipozimia ndani yangu, nalimkumbuka BWANA;
maombi yangu yakakuwasilia katika hekalu lako takatifu. Watu waangaliao mambo
ya ubatili na uongo, Hujitenga na rehema zao wenyewe; lakini mimi nitakutolea
sadaka kwa sauti ya shukurani, nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa
BWANA. BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.” Yona 2:1-10
Nabii
Yona alipo Omba toba na Rehema akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, BWANA
akamwinua tena, akamfungulia Milango na Malango ya Utumishi. Angalia pia
Samsoni pamoja na kumkosea Mungu kwa kiwango kikubwa kwa uzinzi mpaka
akatobolewa macho, Lakini alipo Omba TOBA, Jehova Elshadai, Mungu anayetenda
zaidi ya tarajio akamwinua tena.
“Samsoni akaenda Gaza, akaona huko mwanamke
kahaba, akaingia kwake. Watu wa Gaza wakaambiwa yakwamba, huyo Samsoni amekuja
huku, wakamzingira wakamvizia usiku kucha penye lango la mji, wakanyamaza kimya
usiku kucha, wakisema, na tungoje mpaka mapambazuko, ndipo tutamwua. Basi
Samsoni akalala hata usiku wa manane, akaondoka katikati ya usiku, akaishika
milango ya lango la mji na miimo yake miwili, akaing’oa pamoja na komeo lake,
akajitwika mabegani, akavichukua hata kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.
Ikawa baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika bonde la Soreki, jina lake
akiitwa Delila. Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze,
upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda,
tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.
Delila akamwambia Samsoni, Tafadhali uniambie asili ya nguvy zako nyingi, na
jinsi uwezavyo kufungwa, ili uteswe. Samsoni akamwambia, wakinifunga kwa kamba
mbichi saba ambazo hazija kauka bado, hapo ndipo nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama
wanadamu wenzangu. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamletea kamba mbichi saba
zisizokauka, naye akamfunga nazo. Na yule mwanamke alikuwa na watu katika
chumba cha ndani, wakimwotea. Basi akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakuja.
Ndipo akazikata zile kamba kama vile uzi wa pamba ukatwavyo ukiguswa na moto.
Basi hiyo asili ya nguvu zake haikujulikana. Delila akamwambia Samsoni, Tazama,
umenidhihaki na kuniambia uongo; sasa tafadhali, niambie, wawezwa kufungwa kwa
kitu gani? Akamwambia wakinifunga tu kwa kamba mpya ambazo mtu hakufanya kazi
nazo, hapo ndipo nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. Basi Delila
akatwaa kamba mpya akamfunga nazo, akamwambia, Wafilisti wanakuji, Samsoni, na
wale wenye kuotea walikuwa katika chumba cha ndani. Naye akazikata, akazitupa
kutoka mikononi mwake kama uzi. Delila akamwambia Samsoni, hata sasa
umenidhihaki, umeniambia maneno ya uongo; niambie sasa, waweza kufungwa kwa
kitu gani? Akamwambia, ukivifuma hivi vishungi saba vya nywele za kichwa changu
katika mtande wa nguo. Basi akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni,
Wafilisti wanakujia. Naye akaamka usingizini, akaung’oa ule msumari, na ule
mtande. Mwanamke akamwambia, Wawezaje
kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu,
wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi. Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa
maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa. Ndipo
alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, wembe haukupita juu ya
kichwa change kamwe; maana mimi nimekuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni mwa
mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu,
nitakuwa kama wanadamu wenzangu. Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote
yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema,
Njoni huku nmara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo
wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao. Naye
akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi
saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka. Kisha
akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema,
nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA
amemwacha. Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakatelemka naye mpaka
Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika
gereza. Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa
kwake. Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu
wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi
mwetu. Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu
wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua
watu wengi miongoni mwetu. Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, mwiteni
Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze
mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili. Samsoni akamwambia yule kijana
aliyemshika mkono, niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate
kuzitegemea. Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote
wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume
kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza. Samsoni akamwita
BWANA, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba,
mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili
ya macho yangu mawili. Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za katikati ambazo
nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake wa kuume na moja
kwa mkono wake wa kushoto. Samsoni akasema; na nife pamoja na hawa Wafilisti.
Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote
waliokuwa ndani yake. Basi wale watu waliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa
wengi kuliko wale waliowaua wakati wa uhai wake. Ndipo ndugu zake, na watu wote
wa nyumba ya baba yake wakatelemka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya
Sora na Eshtaoli, katika kiwanja cha
kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka
ishirini.” Waamuzi 16:1-31
TOBA
ilimfanya Samsoni ahesabiwe kuwa miongoni mwa Mashujaa wa Imani maana wokovu
aliouleta siku ya kufa kwake ulikomesha ufalme wa Wafilisti kwa kuwa
aliwaangamiza kuanzia mdogo mpaka mfalme wao. “Nami niseme nini tena? Maana
wakati usingetosha kuleta habari za Gidioni na Baraka na Samsoni na Yefta na
Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme,
walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya samba, walizima nguvu za
moto, waliokoka na makali ya upanga, walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu,
walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.” Waebrania
11:32-34
Israeli
wakafanya dhambi kwa kukosa uaminifu katika kitu kilichowekwa wakfu.
Walipokwisha kuangusha mji wa Yeriko na kuta zake na wakauingia mji wa Ai.
Akani mwana wa Zabdi mwana wa Zera wa kabila la Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa
wakfu, hasira ya BWANA ikawaka juu ya wana wa Israeli kutokana na kutokuwa
waaminifu katika maagizo ya Mungu aliye hai.
“Lakini
wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani,
mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda, alitwaa
baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya BWANA ikawaka juu ya wana wa
Israeli. Kisha Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko mpaka mji wa Ai, ulio karibu
na Bethaveni, upande wa mashariki wa Betheli, akawaambia, akisema, pandeni juu
mkaipeleleze nchi, basi wakapanda juu wakaupeleleza Ai. Wakarejea kwa Yoshua
wakamwambia, wasiende watu wote, ila waende watu kama elfu mbili, tatu,
wakupige Ai; usiwataabishe watu wote kwa kuwaendesha huko; maana watu hao ni
wachache tu. Basi watu wakaenda huko wapata elfu tatu tu; nao wakakimbia mbele
ya watu Ai. Watu wa ai wakawapiga watu kama thelathini na sita; wakawafuatia
kutoka mbele ya mlango mpaka Shebarimu, wakawapiga huko kwenye matelemko; mioyo
ya watu ikayeyuka, ikawa kama maji. Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka
kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA hata jioni, yeye na wazee wa Israeli;
wakatia mavumbi vichwani mwao. Yoshua akasema, Ee Bwana MUNGU, kwa nini
umewavusha watu hawa mto wa Yordani, ili kututia katika mikono ya Waamori, na
kutuangamiza? Laiti tungelikuwa radhi kukaa ng’ambo ya Yordani Ee Bwana, niseme
nini baada ya Israeli kuwapa visogo adui zao? Maana Wanaani na wenyeji wote wan
chi hii watasikia habari hii, naowatatuzingira, na kulifuta jina letu katika
nchi. Nawe utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu? BWANA akamwambia Yoshua,
Haya! Inuka, mbona umeanguka kifudifudi hivi? Israeli wamefanya dhambi, naam,
wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu
vilivyowekwa wakfu, tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao
wenyewe. Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa
visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena,
msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu. Haya! Inuka, uwatakase
watu, ukaseme, Jitakaseni, mwe tayari kesho; maana BWANA, Mungu wa Israeli,
asema hivi; kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako, Ee, Israeli; huwezi
kusimama mbele ya adui zako, hata mtakapokiondoa kile mlicho nacho kilichowekwa
wakfu. Basi asubuhi mtaletwa karibu nami kabila kwa kabila; kisha itakuwa ya
kwamba kabila ile atakayoitwaa BWANA itakaribia jamaa kwa jamaa; na jamaa ile
atakayoitwaa BWANA itakaribia nyumba kwa nyumba; na nyumba ile atakayoitwaa
BWANA itakaribia mtu kwa mtu. tena itakuwa ya kwamba yeye atakayetwaliwa, naye
anacho kitu kile kilichowekwa wakfu, akateketezwa kwa moto, yeye na vitu vyote
alivyo navyo; kwa sababu amelivunja agano la BWANA, na kwa sababu ametenda
upumbavu katika Israeli. Basi Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, akawasogeza
Israeli kabila kwa kabila; kabila ya Yuda ikatwaliwa. Akazisogeza jamaa za
Yuda, akitwaa jamaa ya Wazera; akaisogeza jamaa ya Wazera mtu kwa mtu; Zabdi
akatwaliwa. Akawasogeza watu wa nyumba yake mmoja mmoja; na Akani, mwana wa Karmi,
mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda akatwaliwa. Yoshua akamwambia
Akani, mwanangu, nakusihi, umtukuze BWANA, Mungu wa Israeli, ukaungame kwake;
uniambie sasa ulilolitenda; usinifiche. Akani akamjibu Yoshua, akasema, kweli
nimefanya dhambi juu ya BWANA, Mungu wa Israeli, nami nimefanya mambo haya na
haya. Nilipoona nyara katika joho nzuri ya Babeli, na shekel mia mbili za
fedha, na kabari ya dhahabu, uzani wake shekel hamsini, basi nalivitamani
nikavitwaa; tazama vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha
chini yake. Basi Yoshua akatuma wajumbe wakapiga mbio mpaka hemani; na tazama,
vile vitu vilikuwa vimefichwa hemani mwake, na ile fedha chini yake. Wakavitoa
kutoka hapo katikati ya hema, wakavileta kwa Yoshua, na kwa wana wa Israeli
wote, nao wakaviweka chini mbele za BWANA. Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja
naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na lile joho, na ile kabari
ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo
zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde
la Akori. Yoshua akasema, mbona umetufadhaisha hivi? BWANA atakufadhaisha wewe
leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na
kuwapiga kwa mawe. Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa yam awe hata leo;
naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale
likaitwa, Bonde la Akori hata hivi leo.”
Yoshua 7:1-26
Kitu
kilichowekwa wakfu maana yake ni cha Mungu.
Mfano:
ZAKA
ni sehemu ya kumi ya mali, mazao, mifugo, fedha n.k
BWANA
ametoa maagizo na sheria maalumu katika vitu vitakatifu, nayatupasa kupambanua
kati ya vitu vitakatifu (wakfu) na vya siku zote. Maandiko matakatifu
yanasema;
“Usiache
kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba
mwaka baada ya mwaka.” Kumbukumbu
14:22
Inasisitizwa
kuwa makini na kuvitenga vitu vitakatifu kwa Mungu visiwe au kuliwa katika
malango ya nyumba zetu maana kufanya kinyume na maagizo ya neno la Mungu ni
kukaribisha laana na ukaufu katika kazi zetu za mikono. Maandiko matakatifu
yanasema;
“Usile
ndani ya malango yako zaka ya nafaka zako, wala divai yako, wala mafuta yako,
wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng’ombe wala ya kondoo, wala
nadhiri zako uwekazo zo zote, wala sadaka zako za hiari, wala sadaka ya
kuinuliwa ya mkono wako;” Kumbukumbu
12:17
Jilinde
nafsi yako usile zaka siku zote za maisha yako; maana ukila zaka umekula kitu
kilichowekwa wakfu ni dhambi. “Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi
hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo. Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande,
mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, name nitawarudia
ninyi, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani? Je!
Mwanadamu atamwambia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema,
Tumekuibia kwa nanmna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa
laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani,
ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA
wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, nakuwamwagieni
Baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu; wala
mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba,
asema BWANA wa majeshi. Na mataifa yote watawiteni heri; maana mtakuwa nchi ya
kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.” Malaki 3:6-12
Kutokutoa
zaka ni kwenda kinyume na maagizo ya Mungu hivyo mtu uliyeokoka ukila zaka
utapigwa mbele ya adui zako;
·
Biashara yako itapigwa.
·
Ndoa yako itapigwa.
·
Elimu ya watoto wako itapigwa.
·
Ustawi wako utapigwa.
“Je
mwanadamu utamwibia Mungu? Lakini ninyi; mnaniibia mimi lakini ninyi mwasema
tumekuibia kwa namna gani”
Kutokutoa
zaka ni kumpora Mungu haki yake katika kazi zako za mikono (sehemu ya kumi ya
mapato yako) ni sehemu takatifu kwa Mungu. BWANA anasema;
“Tena
zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, NI YA
BWANA; NA KAMA MTU AKITAKA kukomboa cho chote cha zaka yake, ATAONGEZA SEHEMU
YAKE YA TANO juu yake.” Mambo ya
Walawi 27:30-31
Sehemu
ya kumi ni takatifu kwa Mungu. Hivyo kutoa
zaka sio swala la hiari bali ni lazima kama kulivyo kuokoka ni lazima, nje
ya hapo utatupwa Jehanamu. Kumwacha Mungu siyo lazima unywe pombe au ufanye
uzinzi lakini kwa tendo la kukosa uaminifu ni dhambi na Kristo anasema TUBUNI
NA MREJEE, tafuteni ufalme wa Mungu na haki yake na mengine yote
mtazidishiwa. BWANA Yesu Kristo akasema;
“Ole
wenu waandishi na mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na
bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema,
na imani; hayo IMEWAPASA KUYAFANYA, WALA YALE mengine msiyaache.” Mathayo 23:23
Yesu
Kristo aliunga mkono utoaji wa fungu la kumi alipowakemea Mafalisayo waliotilia
mkazo fungu la kumi tu huku wakiwa wamesahau mambo ya adili na sheria. Wengine
hudhani alipinga utoaji wa fungu la kumi, lakini sivyo, yeye alikuwa anaweka
uwiano.
Wako
wanaodhani kuwa fungu la kumi sio lazima wakidai ni kwaajili ya waumini wa
agano la kale. Wao hudhani fungu la kumi ni agizo la torati. Lakini sivyo.
Fungu la kumi liliamriwa kabla ya torati unaweza kusoma “Abramu aliporudi kumpiga
Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka
amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni bonde la mfalme. Na Melkizedek mfalme wa
Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sana…
Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.” Mwanzo 14:17-20
Kwa
kuwa Imani tu pasipo matendo ya haki ya kiimani, ufalme wa Mungu hauwezi kuwa
kwako. Ili malango na milango ifunguke sharti kuwa mwaminifu. Maana BWANA
ameahidi kwa ajili yetu atamkemea yeye alaye:
·
Asile tena Kazi zetu.
·
Asile tena Ndoa zetu.
·
Asile tena Familia zetu.
Maana
Kristo Yesu “Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo
kubwa pia; na aliye dhalimu katika dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.”
Luka
16:10
Ukishindwa
kutoa zaka ya hicho kidogo unachopata, huwezi kupewa kikubwa. BWANA anasema
angamiza vyote lakini wewe kwa tamaa unaficha, matokeo yake unaleta
mauti katika familia yako badala ya Baraka na ustawi.
BWANA
Yesu Kristo anasema “Akawaambia, Ninyi ndinyi mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini
Mungu awajua mioyo yenu; kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo
mbele za Mungu. Luka 16:15
Maana
vyote vitapita lakini Neno la Mungu halitapita kamwe katika maisha yetu. Ufalme
wa Mungu umo ndani yetu pale tunaposhika Neno lake kwa uaminifu.
AKANI
kwa tamaa ya joho tu na shekeli mia mbili za fedha (Akani anasema NALITAMANI
MKAVITWAA katika hema yangu na ile fedha. Akani na familia yake waliangamizwa “Kisha
Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile
fedha, na lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na
ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote
alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori. Yoshua akasema, Mbona
umetufadhaisha hivi? BWANA atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote
wakampiga kwa mawe, kisha wakateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe. Kisha
wakakusanya juu yake chungu kubwa yam awe hata leo; naye BWANA akauacha ukali
wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde ka Akori,
hata hivi leo.” Yoshua 7:24-26
Baada
ya TOBA ya wana wa Israeli BWANA akasema “…Inukeni mwende Ai; angalia mimi nimeutia
Ai na watu wake; mji wake na nchi yake mikononi mwenu na hawatasimama tena
mbele yenu.”
Ushindi
wetu wa ki-Mungu hutoka kwa Mungu hivyo afichaye dhambi zake HATAFANIKIWA bali
yeye aziungamaye atapata rehema mbele za Mungu.
Ufunguo
huu ni wa muhimu sana katika maisha yetu “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali
yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema” Mithali 28:13
Kukosa
uaminifu huleta kupigwa. Lazima tuchunguze mwenendo wetu na tuyatubie matendo
yetu mafu.
“[Ikiwa
siku zile Wafilisti walikusanyika ili kupigana na Israeli], nao Waisraeli wakatoka juu ya Wafilisti
kwenda vitani; wakatua karibu na Ebenezeri, nao Wafilisti wakajipanga juu ya
Israeli wakapigwa mbele ya Wafilisti; wakauawa watu wa jeshi lao lililokuwa
uwandani wapata watu elfu nne. Hata watu walipofika kambini, wazee wa Israeli
wakasema, mbona BWANA ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende tukalilete
sanduku la agano la BWANA toka Shilo hata huku, lije kati yetu, na kutuokoa
katika mikono ya adui zetu. Basi wakatuma watu kwenda Shilo, nao wakalileta
toka huko sanduku la agano la BWANA wa majeshi, akaaye juu ya makerubi; na
Hofni na Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwako huko pamoja na sanduku la
agano la Mungu. Na sanduku la agano la BWANA lilipoingia Kambini, Israeli wote
wakapiga kelele kwa sauti kuu, hata nchi ikavuma. Nao Wafilisti waliposikia
mshindo wa zile kelele, walisema, Maana yake nini mshindo wa kelele hizi kubwa katika
kambi ya Waebrania? Wakatambua ya kuwa sanduku la BWANA limefika kambini.
Wafilisti wakaogopa, maana walisema, Mungu ameingia kambini. Wakasema, Ole
wetu! Kwani halijawa jambo kama hili tangu hapo. Ole wetu! Ni nani
atakayetuokoa na mkono wa miungu hawa walio hodari? Hawa ndio miungu
waliowapiga Wamisri kwa mapigo ya kila namna jangwani. Iweni hodari, na kufanya
kiume enyi Wafilisti, msije mkawa watumwa wa Waebrania, kama wao walivyokuwa
watumwa wenu; fanyeni kiume, mkapigane nao. Wafilisti wakapigana nao, Israeli
wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana
katika Israeli walianguka watu thelathini elfu wenye kwenda vitani kwa miguu.
Hilo sanduku la Mungu likatwaliwa; na Hofni na Finehasi, wale wana wawili wa
Eli, wakauawa. Basi, mtu mmoja wa Benyamini akapiga mbio kutoka mle jeshini
akafika Shilo siku ile ile, hali nguo zake zimeraruliwa, na mavumbi kichwani
mwake. Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia,
akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule
mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia. Naye Eli aliposikia
kelele za kile kilio, akasema, maana yake nini kelele za kishindo hiki? Yule
mtu akafanya haraka, akaenda, akamwambia Eli. Basi Eli umri wake umepata miaka
tisini na minane; na macho yake yamepofuka hata asiweze kuona. Yule mtu
akamwambia Eli, Mimi ndimi niliyetoka jeshini, nami leo hivi nimekimbia toka
jeshini. Naye akasema, Yalikwendaje, mwanangu? Yeye aliyeleta habari akajibu,
akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa,
hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu
limetwaliwa. Ikawa walipotaja sanduku la Mungu, Eli akaanguka kitini pake kwa
nyuma, kando ya mlango, shingo yake ikavunjika, akafa; maana alikuwa mzee, tena
mzito. Naye alikuwa amewaamua Israeli miaka arobaini. Tena mkwewe, mke wa huyo
Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia habari ya
kutwaliwa sanduku la Mungu, nay a kwamba mkwewe na mumewe wamekufa,
akijiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia. Hata alipokuwa katika
kufa, wale wanawake waliohudhuria karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana
umezaa mtoto mwanamume. Walakini hakujibu, wala hakumtazama. Akamwita mtoto,
Ikabodi, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la
Mungulilikuwa liketwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe.” 1Samweli 4:1-21
Israeli
walipopigwa hawakuangalia kwa makini sababu ya kupigwa kwao matokeo yake badala
ya kufanya toba wakaanza kusaka vitu vya upako viwasaidie katika vita vyao,
matokeo yake wakapigwa navyo, wakafa watu wengi sana na sanduku la BWANA Mungu
wa majeshi likatekwa.
Ndivyo
walivyo wakristo wengi siku za leo, milango na malango yao yanapofungwa badala
yakutengeneza njia zao mbele za Mungu, matokeo yake wanasaka vitu vya upako,
kama vile maji, mafuta chumvi, vipande vya sabuni matokeo yake wamefarakana na
Mungu kwa kufuata ibada ziliotungwa kwa namna ya wanadamu. Maana Mungu ni Roho
na wale wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli, kwa mantiki
hiyo mtu wa Mungu zingatia kweli ya Mungu ndani ya Neno lake si vinginevyo,
mahali pa toba fanya toba. BWANA anasema; “Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu,
haitupasi kudhani ya kuwa uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu
vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu. Basi zamani zile za ujinga
Mungu alijifanya kama hazioni bali sasa amewaagiza watu wote wa kila mahali
watubu.” Matendo17:29-30
Nasi
yatupasa tutengeneze mienendo yetu maana pasipo kuwa na matendo ya haki
tukakimbilia kulitaja jina la Kristo Yesu tu, malango na milango havitafunguka.
“Bali
mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka
agano langu kinywani mwako? Maana wewe umechukia maonyo, na kuyatupa maneno
yangu nyuma yako. Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye, ukashirikiana na
wazinzi. Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, na ulimi wako watunga hila.
Umekaa na kumsengenya ndugu yako, na mwana wa mama yako umemsingizia. Ndivyo
ulivyofanya, nami nikanyamaza; ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe. Walakini
nitakukemea; nitayapanga hayo mbele ya macho yako.” Zaburi 50:16-21
Dhabihu
ya Mungu ni Roho iliyopondeka na kutubu.
“Dhabihu
za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu,
hutaudharau.”
Zaburi 51:17
Anania
na mkewe Safira walikufa kwa sababu ya kutokuwa waaminifu katika kitu
kilichowekwa wakfu mbele za Mungu.
“Lakini mtu mmoja jina lake Anania pamoja na
Safira mkewe, aliuza mali, akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye
akijua haya akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. Petro akasema,
Anania, kwanini shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na
kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali
yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani haikuwa katika uwezo wako?
Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu bali
Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa.ofu nyingi ikawapata watu
wote walioyasikia haya. Vijana wakamchukua nje, wakamzika. Hata muda wa saa
tatu baadaye mkewe akaingia naye hana habari ya hayo yaliyotokea. Petro
akamjibu, niambie mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani
hiyo. Petro akamwambia imekuaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia
miguu yao ya waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe.
Mara akaanguka miguuni pake akafa. Wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa,
wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mume wake.” Matendo 5:1-10
Usituppe
neno la Mungu nyuma yako, maana mshahara wa Dhambi ni Mauti.
“Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi
ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawata urithi ufalme wa Mungu, wala
waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala
watamanio, wala walevi wala watukanaji, wala wanyang’anyi. Na baadhi yenu
mlikuwa watu wa namna hii lakini MLIOSHWA, LAKINI MLITAKASWA, lakini
mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu
wetu.” 1 Wakorintho 6:9-11
Lazima
kuoshwa kwa Damu ya Yesu Kristo kwa njia ya TOBA, hapo ndipo Malango na Milango
yako itakapofunguliwa mbele yako.
Lazima
Kristo amiliki na kutawala maisha yako, hivyo hatulegei bali tunapiga mbio
katika Maombi; ijapokuwa Utu wetu wa nje unachakaa lakini Utu wetu wa ndani
sharti ufanywe upya siku kwa siku.
Lazima
tuyavue matendo yote maovu na Tumvae Kristo.
“Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye
kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika
wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.” 1Petro
1:17
Kwa
hiyo tujifunge viuno vya nia zetu tukitumainia kwa utimilifu ile neema
inayoletwa katika ufunuo wake Yesu Kristo. Kama watoto wa kutii tusijifananishe
na tamaa zetu za kwanza za ujinga wetu, bali kama yeye aliyetuita alivyo mtakatifu, sisi nasi yatupasa tuwe
watakatifu katika mienendo yetu wote. Kwa
maana imeandikwa mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
~~~~~ Usikose sehemy ya 5 wiki ijayo ~~~~~
Labels:
EAGT City Center,
malango,
Maombi,
milango,
Rev Florian Katunzi
Subscribe to:
Posts (Atom)
