|
Mwerezi ukiwa umefunika sakafu na kupendezesha Jengo |
Fungua na mimi Biblia
Kitabu cha 1 Wafalme 6 :13-18
“13Nami nitakaa miongoni mwa Waisraeli, nami sitawaacha
watu wangu Israeli.’’
14Basi Solomoni akajenga hekalu na kulikamilisha.
15Akazifunika kuta zake za ndani kwa mbao za mierezi, akizipigilia ukutani
kuanzia sakafuni mwa hekalu hadi kwenye dari na kufunika sakafu ya hekalu kwa
mbao za misunobari. 16Akagawa dhiraa ishirini sehemu ya nyuma ya hekalu kwa
mbao za mierezi kuanzia kwenye sakafu hadi darini ili kufanya sehemu ya ndani
ya patakatifu, yaani Patakatifu pa Patakatifu. 17Ukumbi mkubwa uliokuwa mbele
ya chumba hiki ndio ulikuwa na urefu wa dhiraa arobainif. 18Ndani ya hekalu kulikuwa
na mierezi, ilionakishiwa mfano wa maboga na maua yaliyochanua. Kila kitu
kilikuwa cha mwerezi, hakuna jiwe ambalo lilionekana.”
Mwerezi ulifatwa Lebanon na Solomoni
Wakati wa Kipindi cha Mfalme Solomoni miti ya mwerezi ilitumika kufunika mawe yaliyoko
kwenye Jengo lililokuwa linajengwa
Wakristo tunatakiwa kufunika mawe yote katika Kanisa
Kanisa tumeitwa kama mwerezi kufunika mawe yote
Mawe ni madhaifu yote ambayo yako katika Kanisa,
Familia,Kazi, Watoto, Ndoa n.k
Tunatakiwa kufunika mawe ya kuvunja moyo, kukata tamaa
ili watu wakutane na Uwepo wa Mungu
Unatakiwa ufunike mambo ya Ndoa yako maana wewe ni
Mwerezi
Siku hizi utakuta vyombo vya Habari vya Kikristo kama
Magazeti, Blogs, TVs,Radio n.k vinatumika kuwasema Watumishi wa Mungu Vibaya
Roho ya Kuchafuana imeingia Makanisani, tumesahau
kabisa kwamba tumeitwa Kuhubiri Habari Njema na sio kutangaza Mabaya ila Mabaya
tunashughulikia ndani kwa Utaratibu uliowekwa.
Kama uko Katika Ndoa na mwenzako ana udhaifu fulani,
sio uanze sasa kupita kwa ndugu na marafiki zako ukisema eeenhe jamani usimuone
vile mume au mke wangu ana udhaifu a, b,c,d ,Funika mawe mpendwa
Mfunike mwenzako kama ni la Kumrekebisha umrekebishe
mkiwa wenyewe kama la kumsaidia umuombeee Mungu hashindwi kitu atamrekebisha,
Haleluyaaaaaaaaaaaaaaa!
Sasa una mtoto unafikiri labda tabia yake ni ngumu na
imekushinda, uwe mwerezi funika mama , funika ewe Baba, si unaanzia kwa
shangazi, then mjomba, then Bibi, Babu, Ukoo hapana funika maweee kama Mwerezi
Mrekebishe kwa Upendo, muonyeshe Upendo, Muombeee
hakuna linalomshinda Mungu.
Haya mambo nimejifunza maana kuna mahali nilipita
ninaye mdogo wangu nampenda sana lakini katika utaratibu ambazo Mungu na labda
Shetani wanajua akakengeuka Imani, kwakweli mwanzoni sikuwa mwerezi
nililalamika ila Roho Mtakatifu alinifundisha Siri Nzito ya kufunika, sio
Rahisi ila kwa uweza wake Mungu tutayaweza yoteee maana yeye anatutia nguvu,
Aminaaaaaaaaaa!
Ukijua Siri ya mtu basi sio unaanza kuitangaza, from
point a,b,c,d, funika kama la kurekebisha kwa upendo muite mpendwa hapa haikuwa
sawa au muombee, Mungu atashughulika nae.
Haleluya, Basi Mungu akubariki sana na akuwezeshe
katika kila hatua ya maisha yako na akuwezeshe kuwa na tabia ya mwerezi
tukifunika mawe katika kila mahali tunapokuwa.
Endelea kutembelea Rejoice and Rejoice Blog maana Bwana
anafanya mambo makubwa na tuko tayari kutumika na kuleta vile vitu yaani
vyakula vya Kiroho na Kuinuliwa ambako Mungu amepanga uvipate, Sema Amina mtu
wa Mungu.
Mungu Akubariki sanaaaaaa