Karibuni katika makala haya yanayoletwa kwani na Mwalimu Samwel Mkumbo
|
Mwalimu Samwel Mkumbo |
Uhai wa kitu
chochote kile unategemea namna au jinsi mwenye huo uhai au aliyekabidhiwa
dhamana yuko katika hali gani, unaweza kulaumu juu ya uharibifu wa jambo au
mambo Fulani lakini kabla ya kulaumu angalia kwanza yeye aliyeharibu au
aliyekabidhiwa mikononi mwake yuko katika hali gani.
MATENDO
20:28 inasema hivi;
Jitunzeni
nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa
waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu
yake mwenyewe.
Sasa kabla
sijaendelea Zaidi nataka niseme jambo la msingi sana hapa, kichwa cha Somo letu
kinatuhitaji tuwe na ufahamu wa kuhakikisha kwamba kila tunachokiongea katika
somo hili ni mambo makubwa mawili, NAFSI YAKO NA KANISA LAKO. Wewe ni nafsi
moja katika kanisa, Je unayo kazi gani wewe kama Nafsi?
Unaweza
usijue wala usiliangalie kwa uzito, lakini inapasa kuelewa tafsiri hii;
KANISA ni Nafsi za watu zilizounganishwa
kwa kunia mamoja katika Imani yao na hiyo Imani wameijenga katika msingi wa
YESU KRISTO, hivyo kanisa bila ya nafsi zilizokubaliana za watu wengi wa aina
mbalimbali si kanisa maana ili wawe kanisa lazima nafsi zao ziungane kwa kunia
mamoja na kuwa na Imani moja ambayo hiyo Imani ndiyo inatengeneza nia moja.
TAZAMA
NAMI:
Ili kanisa
liwe na Nguvu na likae katika mstari unaotakiwa ni lazima nafsi za watu ndani
ya Kanisa ziwe ziko salama kabisa, yaani ziwe zimetunzwa katika hali ambayo
uhakika wa kundi kuishi kwa Amani utakuwepo kwa uhakika.
Labda
tuunganishe vipande viwili vya huo mstari wetu wa msingi ili uone jambo la
msingi kidogo….. Jitunzeni nafsi zenu,,.,.. mpate kulilisha kanisa lake
Mungu,.,.,..
Mfano wa
Mtumwa Mwaminifu
Bwana
akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana
wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri
mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo. Kweli nawaambia,
atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake,
Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake,
akila na kunywa na kulewa; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na
saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na
wasioamini (LUKA
12:42-46)
Sasa hapo ninataka nikufundishe jambo ambalo kimsingi
ambalo halipo kwenye Mistari hiyo hapo juu, na lenyewe ni juu ya adhabu
aliyopewa huyo wakili. Ona mtari huu;,..,.. akaanza kuwapiga wajoli wake,
wanaume kwa wanawake, AKILA NA KUNYWA NA KULEWA;,.,….
Maana suala
sio kusema bwana wake anachelewa ila baada kuona bwana wake anachelewa alifanya
nini? Na wala sio kuwapiga watumwa ila baada ya kuwapiga watumwa alifanya nini?
Yeye alichokifanya ni KULA NA KUNYWA NA KULEWA,..,..
Biblia
inaposema yeye ALIKULA NA KUNYWA NA KULEWA, maana yake aliacha kufanya
alichotakiwa kufanya lakini pia aliiharibu nafsi yake kwa MVINYO yaani kwa
Ulevi. Maana suala si kula na kunywa kwa sababu hayo ni mahitaji ya mwili wa
kila mtu, lakini suala ni KULEWA na biblia inasema KILEO HUDHIHAKI,. Na pia
HUPOTOA HUKUMU ZA HAKI.