Tuesday, March 14, 2017

Mahusiano kuelekea Ndoa - 1

Sir Azgard Stephen
Na Sir Azgard Stephen

Shalom wana wa Mungu. Leo natamani niseme nanyi kidogo, kwa njia ya maswali, juu ya mahusiano yanayopelekea ndoa. Mimi sio mtaalamu sana wa eneo hili, lakini naamini naweza ku-share kitu kwenu na pengine kikawa cha msaada.

Maandiko, katika kitabu cha Mwanzo, yameainisha swala la mahusiano kwa mifano.

1. Mfano wa kwanza tunauona kwa Adamu. Anapewa choice ya kujichagulia companion miongoni mwa wanyama wote. Aliwapitia wote, lakini akakosa. Mungu akamtengeneza Eva, akamleta kwa Adam, for the first time Adam akafall kwa Eva, na akaweka msingi wa mahusiano, Love at first sight

2. Isaka alitafutiwa mke na baba yake, kama ambavyo inatokea katika tamaduni nyingi za kiafrika. Isaka anapokutana na yule dada aitwaye Rebeka, maandiko yanasema "...Isaka akamuingiza Rebeka nyumbani mwa Sara mama yake, akampenda, naye akawa mkewe. Akajenga msingi mwingine wa mahusiano, love at experience.

3. Bingwa wa kupenda, Yakobo, ambaye alikutana na Raheli nyumbani kwa mjomba wake Rabani. Yeye kwake mapenzi nigaragaze, alikuwa tayari si kutoa vitu tu, bali muda wa miaka 14 kumpata mrembo yule (kama maandiko yalivyomuita). Yeye kwa upendo aliokuwa nao, miaka saba ilikuwa kama kufumba na kufumbua, akahamia ukweni kabisaaa. Hili na lenyewe likaweka msingi wa ule upendo uitwao LOVE IS BLIND

Sasa maswali haya ni basic:

1. Upendo ni nini hasa?

2. Hivi ni swala la mimi kupenda au ni swala la Mungu kunipa mke?

3. Inakuwaje unamtokea mdada anakumwaga? Ni makosa yako mkaka, ni upendo, au ni makosa ya mdada?

4. Inakuwaje tumeingia katika mahusiano halafu baadaye tukagombana na hata kuachana? Shida ni sisi au mahusiano yenyewe?

5. Hivi katika kupenda, beauty inahusika au tabia tu inatosha? 

6. Ni ipi sasa njia sahihi ya kuchumbia (proposing?)
Yatafakarini hayo.

Blessings

No comments:

Post a Comment