Na Sir Azgard Stephen
Azgard na mkewe |
Shalom wana wa Asafu.
Leo nataka nizungumzie swali la 3 linalohusu kukataliwa, au kibuti kama
wahusika wanavyoita.
Hili ni miongoni mwa
mambo mabaya kwa vijana, kupeleka proposal kisha kukataliwa.
Nianze kwa kusema,
kibuti ni ishara ya "premature
proposal." Kunaweza kukawa na
sababu nyingine, lakini kwa kweli hii ndio main.
'Premature proposal, ni pale unapopeleka hoja kwa mdada bila
kumuandaa vya kutosha.
Yaani unamuona mdada,
unampenda, unatamani awe mkeo baadae. Unachofanya unafanya unachokiita uchunguzi,
kisha ukijiridhisha unaenda kuomba. Unamkamata kwenye ulimwengu wa Roho,
unajiwekea na ishara huko. Eti nikienda kumwambia aseme ndio, akisema hapana au
nipe muda huyo sio wangu!!! Unaenda dada anakutolea macho, hakuelewi. Unamuona
shetani mkuuubwa.
Well, sikosoi juhudi za
watu katika hilo, kama nilivyosema awali kuomba ni muhimu tena sana kuliko
ambavyo wengi tunafanya, lakini nasisitiza kutumia njia sahihi.
Proposing is an art, sio kupelekeana vitisho na mistari. Kuna
mpendwa mmoja, kaoa sasa, alimkuta huyo dada yuko kwenye mahusiano. Akamtisha
huyo dada kuwa yuko kwenye wrong relationship, yule dada akamuacha kaka wake, ndio wakaoana
na huyo mpendwa. Sorry but to me this is
intimidation. Inaweza kuwa kweli yule dada
alikuwa kwenye wrong relationship, lakini njia aliyotumia kwa mtazamo wangu
haikuwa nzuri. However, sometimes the
end justifies the means.
Nikirejea kwenye mada,
vibuti vingi vinatokea kwa sababu kaka hakujipanga. Najaribu kukaa kwenye
nafasi ya mdada. Kwa mfano, Baraka (sorry kukutumia hapa, just example) unakuja
kwangu nakuita kaka, unaniamsha kila siku 11 niende prayers, na kunihimiza
fellowship. Nakuheshimu tu kama baba Jemadari, kwa miezi miwili uliyochukua
namba yangu ya simu. All of a sudden unaniambia una maongezi nami, tukutane Talma
cafeteria. Mimi najiandaa, naweka na kabiblia kangu kwenye pochi, nakuja
nikijua kuna vitu unataka unielekeze nikue kiroho zaidi (kumbuka kuhimiza
fellowship na maombi). Nafika unaleta vistori viwili vya uwongo, alafu unadondosha
agenda unataka niwe mkeo
In actual sense,
nitakutolea macho, "because I didnt expect that, it was very
premature." "I mean how" nikuelewe, sijawahi hata siku moja
kuwaza utatokea upande huo. Kwa akili zangu, na "understanding"
yangu, nitakumwaga tu
'Guys' nilishawahi
kufanya hii 'mistake', nilim-propose mdada very prematurely, nikamuweka kwenye 'hard time' sana. When I came to realize nikamwambia awe na amani, like it never happened. Alikuwa ananiheshimu sana, na maamuzi sahihi
ilikuwa ni kunimwaga. Lakini sasa anawaza akinimwaga atakuwa kanikosea heshima
na akinikubali atakuwa hajajitendea haki, she don't feel me. Akawa "so down", akakosa amani sana. Ikabidi
ni-withdraw proposal yangu. It was real
embarrassing.
Katika hili nashauri
yafuatayo;
1. Establish a relationship with a person,
communicate. Huyu dada akujue,
akuzoee, akufahamu japo kwa uchache. Yaani "don't be formal, but
casual." Hii haimaanishi uwe comedian, lakini kuwe na casual relationship between you.
2. Win her heart. Hapa ndio kuna shughuli hapa, winning someone's heart. This will stay forever. Sasa you dont win her heart
by money or gifts, but by affections. Ukiamka asubuhi wish her good morning. Usiku don't go to sleep without telling good night. Siku moja moja mtegee uone kama una-win kwa yeye
kukutafuta. Akiwa na tukio show concern, be there
if possible. Sio unatuma maandiko
tu. Maandiko yana-win Roho, ila kinachopenda ni moyo
Wish her happy birthday,
send her a birthday card. Hivi vyoote ni vya
kawaida tu, anyone can do to anybody, lakini ile "frequency" ya kuvifanya
vinamfanya huyu dada akuwaze, akufikirie, na akuone kila wakati. Hapa ndio
utaskia "yule kaka ana care". When u hear that, somehow u have won somebody's heart. She dont
want to see how intelligent and God fearing you are, she want to see how much
you care!
3. Muoneshe kuwa
unampenda. Sijasema mwambie, nimesema muoneshe! Yaani huyu dada kabla hata
hujamwambia kuwa unampenda, anatakiwa ajue unampenda, angalau awe na hiyo
"clue". Katika hatua hii, fanya vitu vichache vinavyoonesha u-special
kwake, na ajue kuwa that is special for her. Kama hakupendi, basi utaona ata-retreat.
Ikitokea hiyo ama urudi kwenye #2 hapo juu au usepe, ukijua kuwa hii
"mission" haina matunda. Hii itaepusha "embarassment" za
kibuti, mtaachana mkiwa hamjaambiana.
Ukifanya hiyo #2 vizuri,
hii ya #3 itakuja vizuri sana. Kabla hata hujaanza kumuonesha unampenda utaona
response yake, badala ya wewe kumtafuta sana utaona mnatafutana. Ukiingiza #3
hapo utaona tu mambo yanaweka tick ✅
Jambo la msingi hapa ni
kwamba, huyu dada akikukubali hapo #2 basi chukua hatua umuoneshe unampenda,
mfanyie vitu ambavyo bila chenga atajua huyu kaka ananipenda. Mara nyingi hapa
wadada wanashindwa kujizuia, usipomwambia atakwambia. Hii itakuwa na maana
umeremba sana mwandiko mpaka peni ikatapika.
4. Sasa njia nyeupe,
kupeleka proposal au kukimbia mission. Hii ina maana, kama #1
imekuruhusu kwenda #2, na #2 imetengeneza njia ya #3 vizuri, basi njia ni
nyeupe kwenda kuweka hoja, na wala hutakuwa na wasiwasi kwasababu unajua
matokeo, Chelsea vs Yanga
Kama nilivyosema awali,
proposing is an art, kwahiyo ukicheza vizuri hapa kamwe hutakaa ukione kibuti
kinafananaje.
Pamoja na ufundi wote
huu, ni muhimu SANA kuomba in the process, kwani hii sio guarantee
ya kupata mke mwema. Kumbuka, sikuwa nazungumzia jinsi ya kupata mke mwema,
bali nazungumzia how to do it right.
Kuna watu wamepishana na
wake zao kwa kufanya proposal zao vibaya, very bad. Yaani ukweli ni kwamba
mdada ni mzuri (right), na wewe ni mzuri, na together you can make good couple. Lakini kwa sababu tu hukumu-affect (love is
affection), mnapishana. Maskini hajui kwamba you are the right guy for her, wewe unajua she is the right girl
for you, mnapishana. It is your responsibility to let her know, by
process.
Nitoe
"caution" hapa, mkaka ukimu-entertain mdada yeyote katika njia hiyo she will fall in the trap, na kama huna mpango naye utamuumiza sana.
Kwa kumalizia niseme tu
kuwa, your wife is going to be your best friend, a
soul-mate. Hiyo
"process" hapo ni muhimu sana kumfanya awe hivyo. Yaani mke wako
lazima akutofautishe wewe na kaka zake. Na wewe lazima umtofautishe na dada
zako. It is not by responsibility, but by affection. Yaani kuna vile mke wangu akitokea moyo
unaruka, tofauti kabisa na mdada yeyote. Na kuna vile namuona mke wangu
nikiwepo, I am the only person no
matter how many are in the place. Hii haitokei "naturally", inatengenezwa.
I had to propose to my
wife 2 months before plan kwa sababu niliona
nisipofanya hivyo she will break the ice, na wengine hatupendi wadada ndio watuambie
wame-fall.
Love surpass all, upendo ndio humfanya mtu ku-move mountains. What makes your woman to choose u instead of her job (sometimes),
you instead of her relatives, you instead of the movie superstars, you instead
of high profile MPs, etc, is how much you invested in her heart. Maandiko yanasema, palipo na mapendo vinono
vinakaa pembeni, mboga ya majani inatosha kabisaa.
Nimezungumza sana upande
wa wakaka, ikimpendeza Mungu nitazungumza upande wa wadada, hasa kwanini
wanakaa kwenye relationship muda mrefu bila kuwa na uhakika kama huyo kaka
atamuoa au la
Mungu awabariki
Sir Azgard
No comments:
Post a Comment