Showing posts with label Women. Show all posts
Showing posts with label Women. Show all posts

Monday, May 19, 2014

Kongomano la Mwanamke wa Thamani lawa Baraka kwa Wanawake wa Moshi


Kongomano la Mwanamke wa Thamani lililofanyika Moshi mjini, lilimalizika wiki iliyopita likiwaacha wanawake wengi wakiwa wamepata maarifa ya Neno la Mungu na kufunguliwa.


Pastor Neema Shoo mwandaaji wa Kongomano la Mwanamke wa Thamani akifungua rasmi Kongomano hilo
Upendo Kilahiro alikuwepo akimsifu na kumwabudu Bwana Yesu

Watu wakisifu na Kuabudu
 
 
Kongomano hilo liliandaliwa na Pastor Neema Shoo ambaye alifungua na utangulizi kutoka  Mithali 31:1 alisema mwanamke au mke mwema nani awezaye kumuona nikaonyesha kipo kitu ndani ya mwanamke ambacho ni cha thamani 

Mambo manne yaliyofichika ndani ya Mwanamke             

1. Hekima Ayubu 28:18b naam Kima cha Hekima chapita marijani, Kama hekima inapita marijani basi na Mithali 31:1 inasema mwanamke mwema uthamani wake unapita marijani basi hicho cha thamani ndani ya mwanamke ni Hekima       Mithali 14:1 inaonyesha ukiwa na hekima unajenga nyumba yako bali mpumbavu anaibomoa                                                                   

2. Ufahamu kilichofichika ndani ya mwanamke ni ufahamu Ufahamu ni uwezo wa kupambanua jema/baya.  Ufahamu ni Akili Mwanamke mpumbavu asiye na akili hubomoa nyumba kwa mikono yake ukiwa na Akili utajenga utajua nini nifanye wapi na saa ngapi kwalugha nyepesi Utajitambua.                                         



Pastor Neema akitambulisha Mchungaji wake na Baba na Mama wa kiroho Pastor Dickson Mtalitinya na Mke wake pia alifundish​a

Thursday, May 8, 2014

Kongomano Kubwa la Mwanamke wa Thamani kufanyika mjini Moshi

 

 
Wote Mnakaribishwa Katika Kongomano Kubwa La Mwanamke wa Thamani litakalofanyika Moshi mjini.
 
Mada:  Uthamani wa Mwanamke
            Uhusiano wa Mungu na Mwanamke
 
Wahubiri: Pastor Neema Shoo -Host
                 Pastor Lilian Ndegi
                 Pastor Dickson Mtalitinya- MTBC Moshi
 
Lini: Tarehe 10/ 05/2014 siku ya Jumamosi kuanzia saa 4 Asubuhi hadi saa 9 Mchana
 
Wapi: Ukumbi wa Lutheran Bookshop Stand ya Moshi Mjini
 
Waimbaji: Upendo Kilahiro
                MTBC Praise Team
 
Nikiongea na mwandaaji wa Kongomano hilo Pastor Neema Shoo, amesema kwamba wanawake watakaohudhuria Kongomano hilo wategee Kufunguliwa na Kupata Maarifa ya Neno la Mungu, hawataondoka kama walivyokuja, Amen!
 
Kwakweli mwanamke mwenzangu usikose maana vitu Mungu ameweka ndani ya hawa watumishi vitakupeleka kiwango kingine kabisa.
Kwa ninavyomjua Pastor Lilian Ndegi lazima wanawake wa Moshi wapate urejesho.... Haleluyaaaaaa
 
 
 

Thursday, March 13, 2014

Moyo wa Mwanamke 2014: Wanawake wajifunza Umuhimu wa Nguvu ya Maarifa katika maisha yao

 
Kongomano hilo la siku tano lililofanyika katika kanisa la Living Water Kawe (Makuti) ambako ndio Kanisa la mbeba maono hayo ya Moyo wa Mwanamke Mama Mchungaji Lilian Ndegi liliwafanya wanawake waingie katika viwango vingine vya juu baada ya kujifunza Umuhimu wa Maarifa katika maisha ya Mwanamke.
 
 

Mchungaji Lilian Ndegi akifungua kwa maombi, kwakweli Mungu alimtumia sana huyu mama katika njia ya tofauti. Hapo unaweza kuona karama za Roho Mtakatifu zinavyofanya kazi hasa pale unapoamua kumtafuta Mungu kwa bidii.

 
Mchungaji Lilian Ndegi pamoja na watumishi wengine kutoka sehemu mbalimbali za Afrika walikuwa wanenani katika Kongomano hilo. Baadhi ya Wanenani hao ni mbeba maono mwenyewe Pastor Lilian Ndegi, Esimy Kabeya (Afrika ya Kusini) ,Prophetes Jeanne Kiratu (Mombasa Kenya), Pastor Jael (Nairobi Kenya),Pastor Florence (Gloryland Arusha) na Mchungaji Naomi Mhamba ( Living Water Kawe)
Mungu aliwatumia sana hawa watumishi wake kuleta ujumbe wa Nguvu ya maarifa katika wanawake.
Wanawake walipata nafasi ya kujifunza jinsi ambavyo Mwanamke asipokuwa na maarifa nyumba na maisha yake yataharibika kama ilivyoandikwa katika Hosea 4: 6 "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako"

 
Mchungaji Naomi Mhamba(Prof.) alifundisha juu ya Uponyaji wa Uzao wa Mwanamke Vs Nguvu ya maarifa alifundisha vizuri sana akitoa mifano halisi ya kulea kizazi hiki na maarifa yamekuwa mengi ambapo Ibilisi analeta maarifa mengi katika jamii na yanavizia watoto na jinsi ya kukabiliana na hila hizo za Ibilisi kwa kumlea mtoto kama Mungu alivyokusudia


Wamama wakisikiliza kwa makini kwakweli ungeangalia nyuso zao kila mmoja aliweza kupokea kitu kipya cha kumsadia yeye, maisha na familia yake. Na kama tunavyojua ukimfundisha Mwanamke umefundisha jamii.



Mtumishi Esimy Kabeya kutoka Afrika Kusini na yeye alifundisha juu ya Nguvu ya Uelewa katika maisha ya mwanamke.


Picha ya Watumishi/ Wananaji wa Kongomonano hilo la Moyo wa Mwanamke



Wanawake wakiwa chini ya Uvuvio wa Roho Mtakatifu


 
Siyo kama mama alifungisha Harusi siku hiyo jamani ni style ya kufundisha ya mama huyu ambayo inamfanya mtu unaelewa kwa kiwango cha juu, hapa anaonyesha mfano wa wanawake wawili tofauti mwenye Hekima na asiye na Hekima. Kwa nje anaweza kuonekana mdada mrembo lakini kumbe ndani hana hekima na mwingine anaweza akaonekana kwa nje labda havutii sana lakini ndani akawa na hekima
 
 

 
Pastor Lilian Ndegi akifundisha kwa kutumia mfano wa wacheza Karata waliokuwa wanacheza kwa kutumia Almasi ,ikiwa na maana kwamba usipokuwa na maarifa utafanya kitu cha thamani kikose uthamani wake na ni rahisi kukupoteza
 
Prophetess Jeanne Kiratu kutoka Mombasa Kenya alifundisha juu ya Jinsi Mungu anavyokwenda kufanya Turn Around (Mageuzi) katika maisha ya mwanamke pale atakapotumia Maarifa yaliyoko katika Neno la Mungu katika maisha yake
 
Pastor Jael kutoka Nairobi na yeye alifundisha Nguvu ya Hekima katika maisha ya Mwanamke, alifundisha kwa njia ya shuhuda za wanawake mbalimbali ambao zamani hawakuwa na hekima katika maisha yao lakini walipopata maarifa wakaishika Hekima na maisha yao na familia yakabadilika hadi watu wakashangaa
 
 

 

Pastor Florence kutoka Gloryland Arusha alifundisha juu ya Nguvu saba za Maarifa, akafafanua kwamba wengi wanaomba tu bila kuwa na maarifa lakini mara nyingine maombi bila maarifa ni kama kelele mbele za Bwana. Mchunangaji huyu alifanya wanawake wacheke sana kwa style yake ya kufundisha kwa umaridadi. Alifundisha wanawake umuhimu wa kuishi kama Malkia na Wafalme.


Neema Baraka na yeye alikuwepo kumwimbia na kumtukuza Bwana, wanawake walipata nafasi ya kumsifu na kumtukuza Bwana Yesu.




Kusifu na Kuabudu



 

Upendo Nnkone alikuwepo katika huduma yake ya kumsifu na kumwabudu Bwana Yesu





Ritha Chuwalo akimchezea Bwana Yesu, twendeeeee


Chezea Bwana...



Wow Wow kulikuwa na mambo mengine mazuri pia katika Kongomano hilo ambapo siku ya Tarehe sita ilikuwa ni Birthday ya mama Pastor Lilian Ndegi ambapo wamama walikuwa wameandaa Cake na wanawake waliweza kushiriki kwa pamoja. Happy Belated Birthday Mchungaji..


Caaaaaake...




 
Kata Cake tuleeee..


Pastor Lilian Ndegi akilisha wengine Cake



Pia mama Mchungaji Lilian Ndegi alizindua Kitabu chake cha Thamani Maneno ya Kinywa Changu, nakushauri Mwanamke mwenzangu utafute hicho kitabu maana kinachotuponza wanawake ni Maneno :) . Haleluyaaaaaaaaaaaaaaa